Nakupenda sana baby ila kila mwezi utanipa laki tatu (3)

Laki tatu kila mwezi ina TV ndani au?
Unaweza kumpa lakini sio kwa kujiombea tena mwanzoni kabisa.
Kumpa hata million sio tatizo, inategemea uwezo na hadhi, viwango vya mahusiano plus ubora wa binti.

Ubora wa binti ni hekima na busara, hatangulizi pesa mbele, anaonyesha uthamani wako kwake, binti akionyesha kuwa wewe ni bora zaidi kwake utampa hata nyumba.

Lakini binti anayetanguliza maslahi yake binafsi mpe 30,000 apite hivi.

Dunia hii kuna wanawake wenye akili na ndio wanaofaidi nyumba, magari na pesa.
Binti anaipandisha thamani yako balaa.
Kila wakati anataka kuwa nawe, ukipita muda kidogo anakujulia hali, mara hivi mara vile na anaonyesha amezama kwako balaa.

Anajifanya hataki chochote kwako zaidi ya wewe na penzi lako.
Si kuwa hataki pesa zako laah hasha bali amechagua FUNGU JEMA nalo ni kumpata mwenye vyake kwanza na mengine atazidishiwa.

Yaani anakuonyesha amezuzuka nawe kama vile duniani umebaki mwanaume peke yako

Mwanamke wa hivi si tu utampa laki 3 bali utampa maisha yako.
Hii siri nimewaibiwa .
Heaven Sent
Sky Eclat
Joannah
 
Sasa si ukadate wa 1285 kwa mwezi?

Fresh tu.
Wewe ni wa kike au me?
Ishu sio kuomba pesa, hapa ni timing.
Huyu dem inaonyesha hawana muda tayari anajimbea pesa, kwa kifupi anauza uchi.

Mapenzi hayanaga bei.
Yaani utajikuta kwa mwezi umempa hata 2 million na hujuti.

Hapo juu nimesema "mapenzi ni sawa na uwekezaji"

Ukiwekeza sana utavuna faida kubwa.
Duniani watu hulipia vyenye thamani bora.

Onyesha upendo kwanza, sahau pesa.
Ikiwa mimi nafaidi "upendo wako"
Na "sio uchi wako" pesa yoyote nitakupa..
Narudia pesa yoyote nitakupa.
Lakini kama unakuja kwangu kunifanya mradi utaumia.
 
Unaweza kumpa lakini sio kwa kujiombea tena mwanzoni kabisa.
Kumpa hata million sio tatizo, inategemea uwezo na hadhi, viwango vya mahusiano plus ubora wa binti.

Ubora wa binti ni hekima na busara, hatangulizi pesa mbele, anaonyesha uthamani wako kwake, binti akionyesha kuwa wewe ni bora zaidi kwake utampa hata nyumba.

Lakini binti anayetanguliza maslahi yake binafsi mpe 30,000 apite hivi.

Dunia hii kuna wanawake wenye akili na ndio wanaofaidi nyumba, magari na pesa.
Binti anaipandisha thamani yako balaa.
Kila wakati anataka kuwa nawe, ukipita muda kidogo anakujulia hali, mara hivi mara vile na anaonyesha amezama kwako balaa.

Anajifanya hataki chochote kwako zaidi ya wewe na penzi lako.
Si kuwa hataki pesa zako laah hasha bali amechagua FUNGU JEMA nalo ni kumpata mwenye vyake kwanza na mengine atazidishiwa.

Yaani anakuonyesha amezuzuka nawe kama vile duniani umebaki mwanaume peke yako

Mwanamke wa hivi si tu utampa laki 3 bali utampa maisha yako.
Hii siri nimewaibiwa .
Heaven Sent
Sky Eclat
Joannah
Huyo binti unaemzungumzia wewe sio anaezungumziwa kwenye mada na sote tunajua unaemzungumzia wewe anastahili unayoyasema na pengine zaidi ila anaezungumziwa kwenye mada ni kinyume chake.
 
Huyu dem napishana nae kila mara hapa mtaani kwetu na kwa kuwa mimi si mtu wa story sana na washikaji hapa kitaa yaani nikitoka nimetoka nikiingia nimeingia hivyo sijazoeleka sana na watu wengi.

Sasa huyu dem kila nikirudi hua namkuta kibarazani kwao (sijui kakariri muda wangu wa kurudi home) yeye ndo huwa wakanza kunisalimu, yeye anaishi nyumba jirani.
Toa pesa mkuu acha kuli alia.
 
Huyo binti unaemzungumzia wewe sio anaezungumziwa kwenye mada na sote tunajua unaemzungumzia wewe anastahili unayoyasema na pengine zaidi ila anaezungumziwa kwenye mada ni kinyume chake.
Mkuu hapa nimejibu hoja ya mjumbe.
Lakini pia nimejibu kinyume na anayezungumziwa.
Tatu ninajaribu kuwaonyesha wanawake wa humu wenye kumtetea au kuwa na mtazamo sawa na binti kwenye uzi.
Wanawake wanamuona mleya uzi analalamikia laki 3 kumbe sivyo.
 
Huyu dem napishana nae kila mara hapa mtaani kwetu na kwa kuwa mimi si mtu wa story sana na washikaji hapa kitaa yaani nikitoka nimetoka nikiingia nimeingia hivyo sijazoeleka sana na watu wengi.

Sasa huyu dem kila nikirudi hua namkuta kibarazani kwao (sijui kakariri muda wangu wa kurudi home) yeye ndo huwa wakanza kunisalimu, yeye anaishi nyumba jirani.

Siku moja nikiwa kwa daladala narudi home nikakutana nae kwenye gari tukakaa siti moja, story zikaanzia hapo hadi kubadilishana no za simu.

Baada ya wiki mambo yakawa moto, mitoko ya hapa na pale n.k, hana kazi yoyote yupo yupo tu mtaani na sikutaka kumdadisi sana kujua maisha yake.

Sasa leo tukiwa tunachati kanambia kuwa ananipenda sana muda mrefu alitamani kuwa na mimi.

Nikamuuliza sababu ya kuachana na ex wake (mana alikuwa anamponda sana) akasema wameachana sababu jamaa alikuwa hamjali kwa mahitaji yake yoyote yani kifupi hamthamini.

Nikamuuliza unadhani mimi naweza kukujali na kukupa mahitaji yako yote. Akasema hapana huwezi kuwa na yote ila kwa kiasi fulani nitashukuru.

Nikamuuliza ni kipi hasa unakihitaji akasema anataka apate angalau laki 3 kwa mwezi.

Nikamuuliza kazini kwako unalipwa sh ngapi kwa mwezi hadi udai laki tatu kwa mwanaume ?

Bado hajanijibu hadi sasa.

Dada zetu naona sasa mapenzi wameyageuza kuwa ajira wanadai mpaka mishahara sasa!!
Kwa hiyo unakula mkate wa marehemu?
 
Back
Top Bottom