Nakupenda sana baby ila kila mwezi utanipa laki tatu (3)

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,830
Huyu dem napishana nae kila mara hapa mtaani kwetu na kwa kuwa mimi si mtu wa story sana na washikaji hapa kitaa yaani nikitoka nimetoka nikiingia nimeingia hivyo sijazoeleka sana na watu wengi.

Sasa huyu dem kila nikirudi hua namkuta kibarazani kwao (sijui kakariri muda wangu wa kurudi home) yeye ndo huwa wakanza kunisalimu, yeye anaishi nyumba jirani.

Siku moja nikiwa kwa daladala narudi home nikakutana nae kwenye gari tukakaa siti moja, story zikaanzia hapo hadi kubadilishana no za simu.

Baada ya wiki mambo yakawa moto, mitoko ya hapa na pale n.k, hana kazi yoyote yupo yupo tu mtaani na sikutaka kumdadisi sana kujua maisha yake.

Sasa leo tukiwa tunachati kanambia kuwa ananipenda sana muda mrefu alitamani kuwa na mimi.

Nikamuuliza sababu ya kuachana na ex wake (mana alikuwa anamponda sana) akasema wameachana sababu jamaa alikuwa hamjali kwa mahitaji yake yoyote yani kifupi hamthamini.

Nikamuuliza unadhani mimi naweza kukujali na kukupa mahitaji yako yote. Akasema hapana huwezi kuwa na yote ila kwa kiasi fulani nitashukuru.

Nikamuuliza ni kipi hasa unakihitaji akasema anataka apate angalau laki 3 kwa mwezi.

Nikamuuliza kazini kwako unalipwa sh ngapi kwa mwezi hadi udai laki tatu kwa mwanaume?

Bado hajanijibu hadi sasa.

Dada zetu naona sasa mapenzi wameyageuza kuwa ajira wanadai mpaka mishahara sasa!!
 
Huyu dem napishana nae kila mara hapa mtaani kwetu na kwa kuwa mimi si mtu wa story sana na washikaji hapa kitaa yaani nikitoka nimetoka nikiingia nimeingia hivyo sijazoeleka sana na watu wengi.
Hawa ndio madem wakuoa sasa mana wana mipangilio mizuri ya pesa ukimweka ndani atakuwa anafanya mambo ya msingi

Sio hawa wadangaji wengine atakuomba kila siku pesa asione toleo jipya la simu au nguo mpya dukani mwisho utajikuta pesa zinatumika bila mpangilio nakufanya matumizi kuwa makubwa. Laki tatu ni pesa ya madafu nitumie kila wiki pesa afanye mambo yake.
 
58 Reactions
Reply
Back
Top Bottom