mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,286
- 6,729
Eti unasema nini wewe Mshana!? Nyumba ndogo ni msingi imara wa ndoa nyingi!? Acha kupotosha wanaume wenzio hivi hiyo michepuko ni misingi au mipasuko!? Hiyo ndio chanzo cha migogoro isiyokwisha kwenye familia nyingi maana moyo ni mmoja hauna nguvu ya kupenda kuwili sawa sawia, wanaume wengi mkishakua na nyumba ndogo dharau kwa wake zenu huzidi Mara dufu. Ogopeni magonjwa hivi huwa mnajiulizaga kipindi unalala kwa mkeo yule hawala yako huwa analala na nani? Sasa hivi kuna gonjwa lisilokingwa na kinga ya condom mnatuletea homa za Ini ndani ya nyumba,tulieni wapuuz nyie
Sent using Jamii Forums mobile app
LadyAJ, kwa lugha uliyotumia, hapo juu, ni dhahiri wewe ni mtata. Umejaza pekepeke na shutuma tu, na siyo ushauri.
Hakuna ugonjwa unaoua wanaume sana, kimawazo na kimwili, kama hiyo lugha uliyotumia kuwasilisha hisia zako.
Mwanaume anahitaji kuheshimiwa na kubembelezwa hata kama kafanya kosa dhahiri. Pekepeke na shutuma za mwanamke, kama zako, ni adui mkubwa wa mahusiano katika ndoa.
mshana jr, kawasilisha hoja mwafaka kwa upande wa akina baba, akiwatahadharisha matokeo hasi ya nyumba ndogo. Kwa falsafa, anawahasa akina mama ndoani, kuwa makini na ndoa zao.
LadyAJ, mpira uko uwanjani kwako.