Ni kweli. Mwenye wajibu wa kuitunza na kuhakikisha usalama ni manispaa. Mbona beach maarufu kama Copacabana wanaweza?
Na nani ana wajibu wa ku control hao beach boys? Nani anatoa vibali kwa hao wauzaji omba omba? Ukiangalia beach zote maarufu haziruhusu biashara holela holela. Kitu ninachokubaliana na Chalamila ni umuhimu wa uwazi. Kuruhusu migahawa, vibanda, majengo ya ibada n.k. yanayozuia beach kuonekana kutoka barabarani ni makosa makubwa. Kunatakiwa kuwa na lifeguards ambao watahakikisha usalama wa wanaogelea sio kuwaachia beach boys kufanya kazi hiyo.
Inategemea aina ya uboreshaji. Kuhusu kipindupindu angalau unaona namna hiyo mihogo inavyotengenezwa kuliko kuletewa tu mezani bila kujua jikoni kukoje. Ila mambo ya kukaanga mihogo, samaki beach ni hatari kwa usalama wa watu na mazingira (moto, moshi, majivu n.k.) na inabidi yawe controlled.
Beach nyingi Dar hazifikiki kirahisi kwa sababu Manispaa zimegawa viwanja vinavyopakana na beach hivyo vinavyozuia mtu kufika beach kirahisi. Coco beach imepakana na barabara hivyo ni rahisi kufikiwa na kila mtu.
Manispaa izuie uendeshaji wa magari na pikipiki beach. Manispaa iongeze patrol za polisi katika eneo hilo. Na zifungue beach nyingine ziwe wazi kama Coco beach.
Amandla...