Nakazia, viongozi chukueni tahadhari ya Corona

Feb 18, 2019
34
400
Naombeni kuwakumbusha viongozi wetu pamoja na wasaidizi wa viongozi, MSIICHUKULIE POA CORONA, CHUKUENI HATUA MADHUBUTI KIPINDI HIKI CHA MKUSANYIKO WA MSIBA WA KUMUAGA HAYATI JPM.

Nanyi wasaidizi wa Rais mteule wa sasa Mh. Samia Suluhu, hakikisheni mnamlinda kwa gharama zozote na maambukizi ya corona. Nyie wasaidizi mna mchango mkubwa sana kwenye kifo cha Hayati JPM kwani hasahasa wewe Waziri wa Afya na Naibu wako kwani mliamua kuvilinda vibarua vyenu zaidi badala ya kusimamia ukweli wa mambo ulivyo kulingana na viapo vyenu.

Narudia tena MKINGENI MAMA SAMIA na exposure yoyote ya huu ugonjwa. Nimesikitika sana kuona leo kwenye hafla ya kuapishwa kwake akiwa hajavaa barakoa, wameenda kwenye baraza la mawaziri pia hamna aliyevaa barakoa. Inasikitisha sana kuona viongozi wetu wakubwa wakiwa wanashindana na sayansi.

Ni hayo tu.
 

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
2,773
2,000
Inashangaza sana kwamba wananchi wametakiwa kukusanyika uwanja wa UHURU na barabarani kwa wingi bila maelekezo na tahadhari za kujikinga na maambukizi ya covid-19!

Kuna uwezekano watu wataitikia kwa wingi kutokana na upendo wao kwa marehemu JPM hadi kuwepo na misongamano, huku wengine wakilia na kuanguka nk.

Bila tahadhari za kujikinga na maambukizi ya covid-19 tuombe mwenyzi Mungu atupishe na majanga kutokana na kupuuza maelekezo ya WHO kuhusu jambo hili.
 

Makuku Rey

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
2,661
2,000
Inashangaza sana kwamba wananchi wametakiwa kukusanyika uwanja wa UHURU na barabarani kwa wingi bila maelekezo na tahadhari za kujikinga na maambukizi ya covid-19!....
Ugonjwa huu Tanzania haupo, tuendelee KUCHAPA KAZI au naongea uongo ndugu zangu😆😆😆

Tutakufa kwa jeuri yetu.
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,185
2,000
Narudia tena MKINGENI MAMA SAMIA na exposure yoyote ya huu ugonjwa. Nimesikitika sana kuona leo kwenye hafla ya kuapishwa kwake akiwa hajavaa barakoa, wameenda kwenye baraza la mawaziri pia hamna aliyevaa barakoa. Inasikitisha sana kuona viongozi wetu wakubwa wakiwa wanashindana na sayansi
Hiyo sayansi yako ni shiiiiiida
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom