Nakata undugu huu wa mizinga....

Nakata undugu huu wa mizinga....

Ujue "mtaka nyingi nasaba, hupata mingi misiba".Lakini pia,"tenda wema wende zako, usingoje shukurani" na ingawa "damu nzito kuliko maji" ukweli utabaki "chombo cha kuzama hakina usukani" ilhali "sikio la kufa halisikii dawa" na usishangae kabisa kupata "fadhila ya punda mateke". Ikiwa "jina jema hung'ara kizani" ujue pia "la kuvunda halina ubani".

Wasema "maji yakijaa hupwa" kama "mpanda ngazi hushuka" kwa vile "hakuna marefu yasiyo na tama"

"Mpanda farasi wawili hupasuka msamba" amua kama unataka kumsaidia umsaidie bila kero, na kama hutaki umuache bila kuona nuksani.
nilifikiri mbeba maboksi kumbe mwalimu wa lugha!!
hahahahahahha!
 
Lara ushauri wako uko sawa kabisa lakini kuna mazingira mengine no,

I will not believe over 1000 years kwamba this is kind of life uncle ameandikiwa, no bana...at 46 maisha ya kutanga tanga, mtu anaamua kuwa tayari kukusaidia kwenye eneo ambalo life can be something ppositive kwako lakini bado hutaki we unachotaka ni kukata miguu kwenye nyumba moja baada ya nyingine ya ndugu ili "ulelewe" ilhali u mzima kabisa na nguvu zako zote ni umeamua tu kufunga utashi wako kuishi hivyo

Ana mtoto mmoja wa kike ambae anashindwa kumhudumia kwa sababu ya maisha ya kutanga tanga....nimeona kuliko kupoteza resources zangu kwa uncle bora nizitumie kuhakikisha mtoto wake (mdongo wangu) anapata fursa ya kusoma mpaka atakapofikia kuwa na miguu yake

Ni kweli kwa tunaoamini katika Biblie (na hata Waislamu pia) asietunza watu wa kwao ni mbaya kabisa na ni mbaya kuliko hata asiyeamini....lakini katika kesi kama hii ya uncle kwa kweli no na naamini kama ungekuwa unamfahamu vizuri (maana kuhadithiwa sio sawa na uhalisia halisi) ungeona nilichofanya ni sahihi maana sasa ndugu wote ni kama tunaelekea kukubaliana sasa huyu mtu namna pekee ya kumchangisha akili ni kuahca ujinga wa kumlea na ujinga wake

Kuna ile ya mara moja chache mtu anakuambia ana tatizo umsaidie, lakini sio hiyo ya kuwa 100% dependant.........akuuuu, ngoja hiyo hela ambayo ningempa iende imsaidie binti yake ajikwamue kimaisha

Bwana Cathod rudisha moyo nyuma! Kama nilivokwambia huo ni Mtihani wako! Ushafeli mtihani ujue? Ila muda wa kubadili majibu unao.

Kama nilivokwambia uncle ni Destiny yake hiyo! Kapewa umwezo mdogo wa kufikiri, na Mola ni mwenye huruma, coz kaona kampa uwezo mdogo wa kufikiri basi ili asiteseke mja wake kawagea nyinyi nduguze uwezo wa kutosha kumu accomodate comfortably!

Maisha bwana ili ushinde mihani wa dunia hii yakupasa kufikiri na moyo wala si logic!

Mimi na wazazi wangu wote 2, wazima, wanafanya kazi, nilienda kuishi kwa ndugu yangu wa mbali sanaaa, Mama mjane, ana watoto wake 5, 2 walemavu, kuna watoto wa ndugu yake 4, ndugu wa marehemu mumewe 2, na sie ndugu wa kuvuta manati 3 na wote kwetu kuna uwezo wa kuishi hoteli au hostel ila ndo Udugu huo! Sikuwahi kutoa hata 100 miaka yote likizo nimeishi pale! MUNGU AMZIDISHIE YULE MAMA KWA MAANA NI NDUGU WA KWELI! Sina cha kumlipa. Kuna watu roho zao sio za dunia hii!.
 
..wiki takatifu hili.. Unatenda dhambi kubwa.

Kumbuka hujafa hujaumbika..

Usitukane mamba kabla hujavuka mto..
Mkuu pamoja sana tena ana takiwa aache roho mbaya, ndugu yako usipo kulilia shida aende kum lilia nani?
 
Bwana Cathod rudisha moyo nyuma! Kama nilivokwambia huo ni Mtihani wako! Ushafeli mtihani ujue? Ila muda wa kubadili majibu unao.

Kama nilivokwambia uncle ni Destiny yake hiyo! Kapewa umwezo mdogo wa kufikiri, na Mola ni mwenye huruma, coz kaona kampa uwezo mdogo wa kufikiri basi ili asiteseke mja wake kawagea nyinyi nduguze uwezo wa kutosha kumu accomodate comfortably!

Maisha bwana ili ushinde mihani wa dunia hii yakupasa kufikiri na moyo wala si logic!

Mimi na wazazi wangu wote 2, wazima, wanafanya kazi, nilienda kuishi kwa ndugu yangu wa mbali sanaaa, Mama mjane, ana watoto wake 5, 2 walemavu, kuna watoto wa ndugu yake 4, ndugu wa marehemu mumewe 2, na sie ndugu wa kuvuta manati 3 na wote kwetu kuna uwezo wa kuishi hoteli au hostel ila ndo Udugu huo! Sikuwahi kutoa hata 100 miaka yote likizo nimeishi pale! MUNGU AMZIDISHIE YULE MAMA KWA MAANA NI NDUGU WA KWELI! Sina cha kumlipa. Kuna watu roho zao sio za dunia hii!.

Ahsante kwa darasa la leo....

Kwa kweli niliamua kuwekeza zaidi kwa binti yake baada ya kuomba hana muelekeo pamoja na zile behavioral challenges na ya kuwa sio mtu wa kuonesha muelekeo wowote

Wakati mwingine huwa natamani nipate dawa ya kumfanya kuwa responsible being
 
lara 1, asante kwa mchango wako. Najua umuhimu wa undugu na yote mliosema. Nasema tena sasa ikiwa ndugu huyu hana ulemavu, mzima wa akili na afya, angekuwa hata anauza karanga ningeamini ndio mungu amejaliwa rizki yake itoke hapo. Lakini hata wazo la kuuza hizo karanga hana, kama ni hoja ya kusaidia kuna watoto yatima, nafikiri wao wanapasa zaidi kupata msaada wangu na sio kulea huyu mtu mzima.

Nimeamua kufanya hivi naona dunia inaweza kumfunza zaidi, kuliko kuzidi kumsadia maana inawezakana haioni ugumu wa hali ya maisha, na naendelea kulea ujinga. Sio kwamba nina kipato kikubwa, la hasha bali nimekuja gundua anachukua advantage ya huruma yangu juu yake. Kuna watu wengine they need to learn the hard way

Kama sitofanya hivi msalaba kama huu nitaubeba mpaka lini?
 
Nashindwa ko coment machozi yana nitoka. Ulicho kie leza (kusimbulia) mimi kisha nikuta. Ndugu zangu walini dharau nakuniona kama kituko flani hivi kila nilie muomba msaada alini onyesha watoto wake yani hana uwezo wa kuni saidia mungu si asumani nika zamia kwa Madiba nashukuru nilipata safali ya kwenda Brazil (kubeba poda) nime ishi maisha hayo kama miaka tano bila kurudi home. Mwaka jana nilivyo rudi nilishangaa kuya kuta maisha jinsi yalivyo change ndugu wote hawana muelekeo wengine hata pakuishi tabu, uwezi amini ivi sasa mimi ndio lulu ya familia. Maovu yao yote nime ya sahau shada zao wana malizia kwangu tena bila haibu wengine huniita bwana mkubwa. Nasindwa kuandika vizuli dada ume ugusa mtima wangu. Nakuomba usivunje udugu sababu ya pesa, pesa sio kitu mbele ya udugu. Kisicho faaleo kitafaa kesho
 
Angekuwa na akili ya kubeba poda pia ningemwona ana dalili ya kujitegemea. Nafikiri hali hii ilikukuta ukiwa kijana, sasa kwa umri wa huyu wa kwangu je? Maana za mtaji tulishatoa zaidi ya 2x, nilishamtoa rumande 3x kwa kesi ta utapeli. jamani eeh....undugu mwengine mtihani.

Zaidi ya yote, hata ka asante hakuna maana jamaa anaona its his birthright.
 
kusaidia kuna kiasi. Msaidie mtu nae ajisaidie. Mwingine unaweza hata kumwanzishia mtaji anakula. Au anakwambia yeye hawezi kufanya kazi ngumu sio type yake. Kila leo anakunyonya acha kumsaidia dunia imfunze.

Hata mnaposaidia msaidie kwa kiasi. Mnapogeuza ndugu zenu kuwa walemavu wa misaada,hapo mnakuwa hamuwasaidii!

Kama umemsaidia lakini mwenyewe hasaidiki kata msaada. Atachakarika na kupambana.

Kuna ndugu mmoja alimpa mimba binti na akajifungua. Ikawa timbwili. Ndugu wakamsaidia na kumchukua yeye na binti. Mwanaume akapelekwa kozi veta. Binti akalelewa maana mtoto alikuwa bado mchanga. Na akaonywa asije beba mimba ya pili.

Baada ya kuhitimu mwanaume akapewa mtaji tena mtaji wa mbao afanye biashara. Kodi ililipwa. Mashine ya kuranda ilifungwa. na akaambiwa akae hapo kwa ndugu angalau miez 6 ajipange. Gues what? Akamdunga mwanamke mimba ya pili. Mtaji akala too bad ikagundulika mbao zenyewe kahonga kwa mahawara!
Alichofanya nduguye ni kumtimua yeye na familia yake yote.
Leo hii kijana anajua kufanya kazi za ujenzi, anatunza mwanamke wake na wanae na fujo za ujana kazipunguza.

Angekuwa na akili ya kubeba poa pia ningemwona ana dalili ya kujitegemea. Nafikiri hali hii ilikukuta ukiwa kijana, sasa kwa umri wa huyu wa kwangu je? Maana za mtaji tulishatoa zaidi ya 2x, nilishamtoa rumande 3x kwa kesi ta utapeli. jamani eeh....undugu mwengine mtihani.

Zaidi ya yote, hata ka asante hakuna maana jamaa anaona its his birthright.
Dada amini kua huo ndio msalaba wako ambao mungu kakupa uangaike nao. Hakika huyo ndugu yako anaji tambua ndio maana haishi kukuomba msaada kwanni aendi kumuomba mtu asie ndugu yake.
 
Angekuwa na akili ya kubeba poa pia ningemwona ana dalili ya kujitegemea. Nafikiri hali hii ilikukuta ukiwa kijana, sasa kwa umri wa huyu wa kwangu je? Maana za mtaji tulishatoa zaidi ya 2x, nilishamtoa rumande 3x kwa kesi ta utapeli. jamani eeh....undugu mwengine mtihani.

Zaidi ya yote, hata ka asante hakuna maana jamaa anaona its his birthright.

mtumwz namna hiyo mwache dunia imfunze ndo akili itamkaz sawa ..... la sivyo hatojifunza anajua akiwekwa selo kuna wztu watamtoa... anajua lolote atakalofanya mtamwangaikia....

Dawa mnamwacha kwanza dunia imfundishe akitoka huko atajua kuwz maisha ni kuhangaika na si kuhangaisha watu.
 
Angekuwa na akili ya kubeba poda pia ningemwona ana dalili ya kujitegemea. Nafikiri hali hii ilikukuta ukiwa kijana, sasa kwa umri wa huyu wa kwangu je? Maana za mtaji tulishatoa zaidi ya 2x, nilishamtoa rumande 3x kwa kesi ta utapeli. jamani eeh....undugu mwengine mtihani.

Zaidi ya yote, hata ka asante hakuna maana jamaa anaona its his birthright.

Mlishakosea wewe na wazazi wako kumdekezxa huyu mtu
wanaitwa 'free loader with self sense of entitlement'
ni watu hatari sana...ndio wanao dhulumu watoto yatima mali zao
ukifa leo watajaribu kudhulumu watoto wako mali zako

usimsaidie hata shilingi moja
but wasaidie watoto wake ya msingi mfano ada za shule
 
jamani huyu ni ndugu yangu tunashare mmoja wa wazazi, ni mtu wa matatizo sana. Mpaka leo hii yuko 40+ lakini ni mtu wa drama, from case to case za aina ya utapeli. Huwa pia anatabia ya uzushi na tabia nyingine nzito. Sasa naona umebaki undugu wa maslahi, kila siku ni mtu wa kutaka asaidiwe, yani hata changamoto za kupambana na maisha hana, siku akikujulia hali ujue kuna mzinga unakuja

nimeamua kukata mahusiano sitaki zaidi ya salamu, naaanza na kublock number yake. Naombeni ushauri na busara zenu kwa uamuzi huu.

mpeleke shule inaweza kusaidia!!
 
Jamani huyu ni ndugu yangu tunashare mmoja wa wazazi, ni mtu wa matatizo sana. Mpaka leo hii yuko 40+ lakini ni mtu wa drama, from case to case za aina ya utapeli. Huwa pia anatabia ya uzushi na tabia nyingine nzito. Sasa naona umebaki undugu wa maslahi, kila siku ni mtu wa kutaka asaidiwe, yani hata changamoto za kupambana na maisha hana, siku akikujulia hali ujue kuna mzinga unakuja

Nimeamua kukata mahusiano sitaki zaidi ya salamu, naaanza na kublock number yake. Naombeni ushauri na busara zenu kwa uamuzi huu.

We mbOna unapiga mizinga mabwana zako?
 
Back
Top Bottom