Nakata undugu huu wa mizinga....

Nakata undugu huu wa mizinga....

Hahaha wewe c ulikua supporter wa wanawake kupiga mizinga wapenz wao ni fresh eenhh..toa hela hizo wacha roho mbaya..pesa makaratasi tu hayo
 
Mimi bwana nachoamini ni kuwa Aliekupa wewe upeo na akili nyingi za maisha na kutafuta pesa ndo kamnyima huyoo ndugu yako upeo mkubwa na kumpa ule alionao!

Na yule ni mtihani wako wa maisha! Mungu anakupima tu kwa yule kiumbe wake. Kakupa uwezo wa kumsaidia kwa makusudi kabisaa, na hakuna mzinga atakaokupiga uncle ulio nje ya uwezo wako! La hasha uwezo wa kumsaidia unao labda tu ni priority ndo inagomba!

Binadamu tujifunze kuishi na mitihani yetu, misalaba yetu tusichoke kuibeba asilani. Ukishajua flani ni msalaba wangu basi wajitahidi usikerekwe nae, na kumzoea kumsaidia na kumfanya part ya maisha yako. Kwani pesa ngapi twalewea bar na hazituumi? na zaidi tunaunguza maini tu?

Mimi nina ndugu zangu wasumbufu ila nimewazoea na namshukuru sanaaa Mola, tena sanaaa kwa kunipa msalaba mwepesi, kuna watu ndugu zao Vichaaa kabisa, wengine walemavu, wengine wagonjwa! Mungu tuipushie mbali ila kumkimbia ndugu yako anaejielewa, hakuaibishi, anaenda chooni mwenyewe anachokubebesha mzigo ni pesa ndogo ndogo tu?????????? Ni kumkufuru Mungu kulaumu kwa na ndugu kama huyo!

So find uncle, be nice to him, na umpe uwezacho Gog will bless your hustles kila anachopunguza uncle atakurudishia mara 10. Uncle ile ndo destiny yake alio andikiwa!

Asante
 
Back
Top Bottom