Nakala ya karatasi na mwandiko wa Lwakatare wakati anatoa maelekezo hii hapa

Mmemsikia mwanasheria Tundu Lisu nyie mawakala wa magamba mnaoropokaropoka humu?
 
Wewe umejiunga hapa JF kuleta upumbavu hapa. Kawaambie waliokutuma kwamba JF kuna watu wana akili zao na wala hatudanganyikiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Hayo maandishi kwa nini usiyapeleke polisi ambao tayari wanamshikiria Lwakatare.

Umejiunga hapa tarehe 8 mwezi huu ili kusaidia kuleta huu ujinga. Namshangaa pia Mwema na akili zake anamkamata mtu kwa ujinga huu wakati kina Sheikh Ilunga wako mtaani wanakata mitaa hata baada ya kuwaamrisha wenzake wawaue viongozi wa dini ya kikiristo!!

Join Date : 8th March 2013

Posts : 16
Rep Power : 305
Likes Received43
Likes Given4


Wewe unawajua walio waua viongozi wa kikristo? Ngoja report ya polisi itakapotoka kama hujasema imepikwa maana inaweza kuja na sababu nyingine kabisa kuliko uli uliyoitarajia. Drug deals!
 
Wataelewa nini hawa wanchojua kila kitu ni ushahidi! Angalia karatasi ilivyo mpya kama imeandikwa leo!
Mmemsikia mwanasheria Tundu Lisu nyie mawakala wa magamba mnaoropokaropoka humu?
 
Acha majungu, MoDs hawatoi ban kwa sasabu wanamjua mtu au hawamjui mtu bali sheria, kanuni ndiyo muongozo. Hayo ni maneno katika clipp ya Ilunga labda uwe haujaisikiliza?

Vile vile kama unahisi mtu katoa post yenye element ya abuse, tumia kitufe cha abuse report atashughulikiwa na siyo kulalamika hapa jukwaani. Huko MoDs watapima uzito wa kosa alilofanya mhusika na kupewa chakula yake.

Ndio umechangia nini sasa? Nawewe kama hiyo clip ya Ilunga imekutach si upeleke polisi? Unalialia nini sasa jukwaani?
 
Ninachoomba kwa mwenyezi ni atunusuru ili vita yenu isiendelee kutuua sisi tusiohusika!!jamani ccm mbona bado mna nafasi ya kukubalika tu?hata kama kuna makosa yaliyofanyika huko nyuma si ya kurekebisha tu?munavyoua wananchi masikini munaona ndiyo njia sahihi ya kuwafanya nyie muwe binaadam zaidi? Hakika hakuna ubinaadam zaidi ya huu mulionao,hamutaenda popote nje ya ardhi hii tunayoikanyaga!!hata mukituua wote! Naenda kupiga magoti nimuombe Mwenyezi Mungu anionyeshe haki ya mnyonge wa nchi hii alipoificha,nimuombe ayaainishe makosa tuliyomkosea yeye au ccm ili tuweze kuyatubia!!tumewaamini ccm kwa miaka yote,tumewapa kila kitu,na bado wanatoa roho zetu,Ee Mwenyezi Mungu ugeuze uso wako sasa!!!.
 
Habari wanajukwaa;

Kama alivyoahidi BUKOBA BOY kwenye maelezo yake yaliyoambatana na video ya LWAKATARE kwamba atakuwa anatupa ushahidi mmoja baada ya mwingine, Amesharusha karatasi aliyokuwa anaitumia Lwakatare kuchukua Note/Summary wakati anatoa maelekezo kwa kijana wake kwenda kuandaa mazingira ya utekaji.

Inayoonekana juu kulia kwenye karatasi ni namba ya MSACKY, Mwandishi wa habari wa mwananchi ambaye ni target mojawapo katika kutekwa. Wale waliosema kwamba ile video ni ya uongo wajiridhishe sasa kwamba BUKOBA BOY ana full data na amejiimarisha.

Wakubali sasa kwamba huu ni mwandiko wa LWAKATARE NA HAYO NI BAADHI YA MANENO ALIYOYATAMKA KWENYE VIDEO YAKE.

Zaidi unaweza kutembelea youtube japo haionekani vizuri.. NAOMBA MODS WAIKUZE HAPA JF ILI WASOMAJI WASIPATE SHIDA. KARATASI YENYEWE HII HAPA CHINI

attachment.php


Hapa ndipo mlipoharibu ..uongo wenu kwa ile video ulikuwa uko uchi sasa na kwa hii ndio mmepyeeeeeeeeeee!!!!!!!!!! kwa hiyo hili ni desa wauaji wameze au ni kwa ajili ya kusoma wakariri watafaulu mtihani wa utekaji na mauaji? au ni kwa ajili ya kwenda kununua hizo bidhaa hapo Spray,Dawa za usingizi maana wanaweza kusahau!! Bwaaahhhh! Yaani Lwakatare anapanga mauaji kwa mama ntilie,anarekodiwa na pia maneno anayoyaandika yanapatikana...Sasa naelewa kwa nini zero zinaongezeka!!
 
Hii ameandika mwana JF mwenzetu de'levis

============================== ========

Nilikuwa sina nia ya kuandika sana humu lakini baada ya kusoma comment yako nimelazimika kusema kitu...jambo lolote unaloambiwa , kuliona au kulisikia ni lazima ushughulishe akili kufikili ili ujiridhishe kama ni la kweli au la vinginevyo utakuwa unakubaliana na jambo ambalo si la kweli...jaribuni kuipa nafasi akili yenu kufikiri.... bahati mbaya sana katika siku za hivi karibuni imeonekana watanzania wengi sana wana tatizo la kutoipa akili nafasi ya kufanya maamuzi na kung'amua na mmoja wao ni Pasco....wachache wanaipa akili nafasi ya kufikiri.

Kuna matukio mengi sana na mengine wengi hamuyafahamu ambayo yanalenga kuichafua image ya taifa na kwa kuwa matumizi ya technolojia nchini yamekuwa yakikuwa kwa kasi hasa matumizi ya simu na intanet na kwa kuwa techolojia inakuwa kwa kasi na hivyo wengi wanashindwa kwenda sambamba na ukuaji wake na hivyo wanajikuta wanakubaliana na kila kitu wanachokiona ama kusikia..

katika mkanda huo ambao wewe pasco unauita ni ''bonafide and genuine'' nimefanikiwa kuuona jana mchana na mimi na wenzangu tumekaa na kuupitia kwa makini kabisa na kwa njia za kisasa zilizotusaidia kujua uhalisia wake... mkanda huo ni fake na tayari taarifa imeshatolewa....hata wewe pasco ukijipa mda wa kukaa na kuipa akili yako nafasi utagundua kuwa mkanda ule ni fake vinginevyo utakuwa unasumbuliwa na '' invincible ignorance''

Chini hapa nitakusaidia kidogo ili walau upate picha ya kuwa mkanda ule ni fake...

00:01 ------Sauti inaanza kwa kutamka ‘’MIKE’’ na kisha kuuliza ‘’ HAPO?’’ maana yake watu hawa wanajiandaa kuanza kujirekodi na wakati wa nafanya editing waliyaacha maneno hayo

00:15 ..........sauti ya mtu wa pili inasikika ikisema ‘’ TUTANOTE TENA HAPO’’ ...inaelekea watu hawa kuna mahali walikosea na kusema watarudia mahali hapo...

00:28 .......Binti anaonekana akija dirishani na kisha anaondoka baada ya maongezi mafupi na mwenzake aliyoko upande wa pili wa dirisha.

01:45......Sauti ya mtu mwingine ambaye baadae alikuja kutambulika kama ‘’RICH’’ anasikika akiwasalimia lakini aliyesalimiwa(lwakatare) kulingana na picha na mdomo wake inaonekana si yeye aliyeitikia ’’ marahaba’’..kuthibitisha hilo mara baada ya salamu msalimiwa hakugeuka kumwangalia anayesalimia ila aliendelea na shughuli zake na papo hapo kijana anayeonekana na kupewa maelezo mara moja anaanza mazungumzo na kijana (rich) aliyekuwa anasalimia na ndipo anamwita jina hilo ‘’rich’’ na wanapeana pole za matatizo na habari za sikukuu nk. katika mazungumzo mtu anayeonkena kwenye clip(lwakatare) bado haeguki kumwangalia huyo rich badala yake anaendela kutoa maelezo namna ya kudhuru watu.... hapa kuna abrakadara katika clip hii......

03: 15......wakati mazunguzo na melekezo toka kwenye clip ya lwakatare yakiendelea kwa mbali anasikika binti anayemkaribisha mtu mwingine na pia anasikika akisema ‘’ napanda maua’’ na anamalizia na neno ‘’karibu ingia ndani’’..( ili kumsikia binti umakini unahitajika kidogo)

03:20.....inasikika sauti mtu akikoroga chai kwenye meza yalipokuwa yanafanyika mazungumzo na anarudisha kijiko kwa kugonga meza lakini picha inayoonekana haimuoneshi mtu huyo na wala hakuna dalili za kuwa kwenye meza ya lwakatare kulikuwa na kikombe cha chai na kuwa chai ile ilikorogewa pale.. ...na pia kwa kufatilia kwa makini mtu anayekoroga chai si yule aliyekuwa anapewa maelekezo.... kitu kingine ni kwamba clip nzima quality ya sauti ya lwakatare haisikiki sawa sawa kama sauti ya mtu wa pili (kijana anayepewa maelekezo) ...

05:35 .....sauti inasikika ikitamka ‘’ UNAELEWA LAKINI?’’ lakini ukiangalia kwa makini mdomo wa lwakatare hakutamka neno hilo badala yake mdomo unaonyesha ametamka ‘’ UMELIONA HILI?’’ ni sawa na pale alipokuwa akisalimiwa na ‘RICH’’ hakutamka neno ‘’marahaba ‘’ na badala yake neno alilotamka kulingana na mdomo ulivyoonekana alitamka ‘’ YOTE MUHIMU’’ na ndio maan hakugeuka kumwangalia yule aliyekuwa anasalimia kama ilivyoelezwa hapo juu..

05:57... Sauti inasikika ikitamka kuwa ‘’kama tulivyofanya hii ya morogoro kisha kwenda igunga’’ swali la kujiuliza hapa ni mauaji yapi yalitangulia? Ya morogoro au igunga?..... bado ushahidi unaonyesha video hii ni ya kupika..

07:36.....Sauti inasikika ikisema ‘’ dawa aina mbali mbali vidonge, unga ama liquid form fanya utafiti ujue zinapatikana wapi na ni bei gani; ni rahisi mno kama tulivyofanya utafiti wa mgongolwa tukapata ile kitu’’ hapa pia kunachanganya inawezekanaje kijana anapewa jukumu la kutafuta bei na upatikanaji wa madawa wakati huo huo akikumbushwa namna walivyopata ‘’ ile kitu’’ kwa mgongolwa ambapo kijana alishiriki ...maana yake kijana anajua bei na wapi yanapatikana...( who is mgongolwa by the way?)

15:59 ...sauti inasika ikisema ‘’ unamuweka kwenye dilemma hajui adui ni nani yaani anakuja hapa anakukuta wewe ‘’LUDOVICK’’ ndiye unamfatilia’’...huyu Ludovick ni nani?( some dots needs to be collected and connected here ) yawezekana ni mmoja wa vijana waliokuwa wanajirekodi na hili ni jina lake halisi na wametajana pasi kujua au ni code name?..

17:10 kijana anayepewa maelekezo (‘’Ludovick) anauliza ‘’ kwa hiyo kama kila kitu kitaenda well inakwenda mpaka lini?’’ lakini katika kujibu clip inayomuonyesha lwakatarea akijibu swali hilo akisema ‘’ Bahati mbaya umekuja na majibu yasiyojitosheleza’’ ....katika majibu haya kuna mkanganyiko mkubwa maana hakuna uhusiano wa swali lililoulizwa na jibu lililotolewa....tangu dakika ya 15 ya clip hii maelezo ya sauti zinazosikika hayana mpangilio wa manaa... mengi yalilenga kufuatisha ishara na vitendo vya lwakatare alivyokuwa akiongea na ukitizama kwa makini hakuna uhusiano kati ya maneno yenyewe na mdomo wa lwakatare.............

19:20...Lwakatare anaonekana akiongea kwa mdomo na vitendo(kuchezesha mikono) huku kichwa chake na macho vikielekea kwa kijana(ludovick) aliyesimama/ kukaa mbele yake ..mara gafla kitu kinadondoka chini na kijana anainama kukiokota lakini bado lwakatare akiongea kichwa na macho vikiangalia juu alipo kijana na kijana anaitikia mmmh, mmmh mara gafla clip inakatwa na kuishia hapo... hapa pia kunamkanganyiko mkubwa... na hakuna uhusiano wowote wa maneno yale na picha inayoonekana na tukio la kudondoka kitu chini..... binafsi naamini clip ingeendelea kuanzia hapo sura ya mtu wa pili ingeonekana hasa mara baada ya kuokota kitu kilichodondoka na ndio maana clip imeishia hapo.......


Pasco unaweza kuishabikia clip hii kama bonafide genuine kama na wewe ni mmoja wa washiriki wake au basi ni ushabiki wa kipuuzi ...anyway hata hivyo taarifa juu ya uhalilisia wa clip hii imetolewa....

Very good observation! Critical analysis maintained.
 
Kwa uelewa wangu mdogo wa sheria nadhani mtu unayezuia haki kutendeka nawe ni mualifu...sasa una ushahidi wa jinai halafu unakaanao na wewe ni mhalifu
 
Kwa mwenye busara ni ku-reserve comment mpaka ukungu uliotanda katika hii issue uondoke ili kuweza kupata picha kamili.., unless otherwise unaweza ukatoa comment ambazo in hindsight usingezitoa
 
kwanini watu wengi wanakataa kama Lwakatare hawezi fanya hivyo, mnaijua nafsi yake, kuna vyombo vya dola watashughulikia na ukweli utajulikana tu, watu mnajiita makamanda, sasa ndiyo ukamanda gani wa upande mmoja tu, muwe makamanda wa nchi siyo wa vyama bana

SHIDA YENU MUMEIBUKA KUIPIGANIA DINI BADALA YA KUSIMAMIA UKWELI!... BAADA YA mafundisho ya kuwagawa watanzania waislamu kama wewe mmebeba DINI na kuacha ukweli.
Kweli nchi hii imepasuka kidini!... Kwakuwa Lwakatare ni mkristo BASI HUGO na waislamu wenzako mmelivalia njuga suala la kumzushia Lwakatare kesi zisizo na kichwa wala miguu!... Inaumiza saaana wakristo kuona mtu aliyepanga njama za mauaji ya MAASKOFU, MAPADRI, WALEI NA WACHUNGAJI na kutimiza azma yake kwa miezi sita (6) hakamatwi lakini tuhuma za uzushi jeshi zima la polisi linavalia njuga na kumkamata kwa vitu vya mtandaoni!...

HIVI MANENO YOOOOTE ALIYOSEMA ILUNGA YANGEELEKEZWA KWA WAISLAMU, ... MKRISTO HUYO ANGEKUWA NJE MPAKA LEO?

KWAKUWA SAFU YOOTE YA VIONGOZI WA JUU WA SERIKALI NA JESHI LA POLISI BASI ILUNGA ANALINDWA!...
 
ukitafakari kwa makini katika hali ya kawaida si rahisi mtu akawa anaongea halafu anaandika notice za maongezi yake mwenyewe ila kwa kawaida yule anayepewa maagizo ndio kawaida huwa anachukua notice. hii pia inaonyesha uwongo wenu, mmechemsha an mtazidi kuharibu kabisa kwa sababu mshauri kaenda chaka.
 
Mimi sihitaji muandiko.

Nilivyosikiliza maneno na kuangalia lips zinavyoenda tu tayari.

Next mtasema wametumia software kumfanya mdomo wake ufuatishe maneno yao.

Wamekuwa Pixar?

kiranga umeshawahi jiuliza in a video unaweza just chop maneno anayoongea mtu na kuunganisha to make new clip ??suppose hawa watu walikua wanajadili mambo mengi tu ikiwa siasa na hata mambo ya biashara,mi ndio maana sikutaka to conclude koz lwakatare haongei continuous kama anavoongea huyu mwenzake very clear.sijui utasema nini ikiwa hii video itakuwa proved fake.
 
Ndio umechangia nini sasa? Nawewe kama hiyo clip ya Ilunga imekutach si upeleke polisi? Unalialia nini sasa jukwaani?

Mpo jamvini kupigania dini.. WEWE si mwana CCM. LOWASSA akigombea 2015 kupitia CCM utahama na wenzako.

Kweli nchi hii imepasuka kidini!... Kwakuwa Lwakatare ni mkristo BASI HUGO na waislamu wenzako mmelivalia njuga suala la kumzushia Lwakatare kesi zisizo na kichwa wala miguu!... Inaumiza saaana wakristo kuona mtu aliyepanga njama za mauaji ya MAASKOFU, MAPADRI, WALEI NA WACHUNGAJI na kutimiza azma yake kwa miezi sita (6) hakamatwi lakini tuhuma za uzushi jeshi zima la polisi linavalia njuga na kumkamata kwa vitu vya mtandaoni!...

HIVI MANENO YOOOOTE ALIYOSEMA ILUNGA YANGEELEKEZWA KWA WAISLAMU, ... MKRISTO HUYO ANGEKUWA NJE MPAKA LEO?

KWAKUWA SAFU YOOTE YA VIONGOZI WA JUU WA SERIKALI NA JESHI LA POLISI BASI ILUNGA ANALINDWA!...
 
Hiyo pepa wapime finger print na watafute other rough paper za lwakatare walinganishe tuondoe mzizi wa Fitna, akigundulika basi ashughulikiwe kwa nguvu za dola kwa kadri inavyowezekana pamoja na Mabos wake walomtuma bila ya kujali vyeo vyao, umaarufu wao.
 
Nimesema CHADEMA lazima tu imutoe kafara Lwakatare au kumtosa kama kweli wanataka kuwa active na damage control. Kuendelea kumbeba kwenye mbeleko ya chama Lwakatate ni kuzidi kujisogeza kwenye tukio. Who knows, labda kuna video na makabrasha mengine ambayo ni more incriminatory out there.

Angalia, mpaka namba ya mtu ya simu ameandika. This guy is really bogus. Hata maswala ya ulinzi na usalama wake hayajui achilia mbali kulinda chama.

Hakufanya hata vetting ya watu aliokuwa anaongea nao na anawapa maelekezo nyeti kama haya. Mpaka note yake amewapatia.

kuna watu watakataa kuwa huu siyo mwandiko wake, lakini kugundua hand writing ni rahisi sana zaidi ya sauti ya mtu.
Hivi unaufahamu mwandiko wa Rwakatare?
 
Back
Top Bottom