Nakala ya karatasi na mwandiko wa Lwakatare wakati anatoa maelekezo hii hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nakala ya karatasi na mwandiko wa Lwakatare wakati anatoa maelekezo hii hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hugochavez, Mar 15, 2013.

 1. hugochavez

  hugochavez JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2013
  Joined: Mar 1, 2013
  Messages: 1,724
  Likes Received: 497
  Trophy Points: 180
  Habari wanajukwaa;

  Kama alivyoahidi BUKOBA BOY kwenye maelezo yake yaliyoambatana na video ya LWAKATARE kwamba atakuwa anatupa ushahidi mmoja baada ya mwingine, Amesharusha karatasi aliyokuwa anaitumia Lwakatare kuchukua Note/Summary wakati anatoa maelekezo kwa kijana wake kwenda kuandaa mazingira ya utekaji.

  Inayoonekana juu kulia kwenye karatasi ni namba ya MSACKY, Mwandishi wa habari wa mwananchi ambaye ni target mojawapo katika kutekwa. Wale waliosema kwamba ile video ni ya uongo wajiridhishe sasa kwamba BUKOBA BOY ana full data na amejiimarisha.

  Wakubali sasa kwamba huu ni mwandiko wa LWAKATARE NA HAYO NI BAADHI YA MANENO ALIYOYATAMKA KWENYE VIDEO YAKE.

  Zaidi unaweza kutembelea youtube japo haionekani vizuri.. NAOMBA MODS WAIKUZE HAPA JF ILI WASOMAJI WASIPATE SHIDA. KARATASI YENYEWE HII HAPA CHINI
  lwakatare.jpg
  [​IMG]
   
 2. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2013
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,373
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Tutajuaje kama huo mwandiko ni mwa Lwakatare na siyo wa Riz au Mwingulu na kundi lake
   
 3. B

  Baba mtata JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2013
  Joined: Dec 6, 2012
  Messages: 280
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acha uwongo
   
 4. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2013
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,967
  Likes Received: 6,661
  Trophy Points: 280
  Hii ameandika mwana JF mwenzetu de'levis

  ============================== ========

  Nilikuwa sina nia ya kuandika sana humu lakini baada ya kusoma comment yako nimelazimika kusema kitu...jambo lolote unaloambiwa , kuliona au kulisikia ni lazima ushughulishe akili kufikili ili ujiridhishe kama ni la kweli au la vinginevyo utakuwa unakubaliana na jambo ambalo si la kweli...jaribuni kuipa nafasi akili yenu kufikiri.... bahati mbaya sana katika siku za hivi karibuni imeonekana watanzania wengi sana wana tatizo la kutoipa akili nafasi ya kufanya maamuzi na kung'amua na mmoja wao ni Pasco....wachache wanaipa akili nafasi ya kufikiri.

  Kuna matukio mengi sana na mengine wengi hamuyafahamu ambayo yanalenga kuichafua image ya taifa na kwa kuwa matumizi ya technolojia nchini yamekuwa yakikuwa kwa kasi hasa matumizi ya simu na intanet na kwa kuwa techolojia inakuwa kwa kasi na hivyo wengi wanashindwa kwenda sambamba na ukuaji wake na hivyo wanajikuta wanakubaliana na kila kitu wanachokiona ama kusikia..

  katika mkanda huo ambao wewe pasco unauita ni ''bonafide and genuine'' nimefanikiwa kuuona jana mchana na mimi na wenzangu tumekaa na kuupitia kwa makini kabisa na kwa njia za kisasa zilizotusaidia kujua uhalisia wake... mkanda huo ni fake na tayari taarifa imeshatolewa....hata wewe pasco ukijipa mda wa kukaa na kuipa akili yako nafasi utagundua kuwa mkanda ule ni fake vinginevyo utakuwa unasumbuliwa na '' invincible ignorance''

  Chini hapa nitakusaidia kidogo ili walau upate picha ya kuwa mkanda ule ni fake...

  00:01 ------Sauti inaanza kwa kutamka ''MIKE'' na kisha kuuliza '' HAPO?'' maana yake watu hawa wanajiandaa kuanza kujirekodi na wakati wa nafanya editing waliyaacha maneno hayo

  00:15 ..........sauti ya mtu wa pili inasikika ikisema '' TUTANOTE TENA HAPO'' ...inaelekea watu hawa kuna mahali walikosea na kusema watarudia mahali hapo...

  00:28 .......Binti anaonekana akija dirishani na kisha anaondoka baada ya maongezi mafupi na mwenzake aliyoko upande wa pili wa dirisha.

  01:45......Sauti ya mtu mwingine ambaye baadae alikuja kutambulika kama ''RICH'' anasikika akiwasalimia lakini aliyesalimiwa(lwakatare) kulingana na picha na mdomo wake inaonekana si yeye aliyeitikia '' marahaba''..kuthibitisha hilo mara baada ya salamu msalimiwa hakugeuka kumwangalia anayesalimia ila aliendelea na shughuli zake na papo hapo kijana anayeonekana na kupewa maelezo mara moja anaanza mazungumzo na kijana (rich) aliyekuwa anasalimia na ndipo anamwita jina hilo ''rich'' na wanapeana pole za matatizo na habari za sikukuu nk. katika mazungumzo mtu anayeonkena kwenye clip(lwakatare) bado haeguki kumwangalia huyo rich badala yake anaendela kutoa maelezo namna ya kudhuru watu.... hapa kuna abrakadara katika clip hii......

  03: 15......wakati mazunguzo na melekezo toka kwenye clip ya lwakatare yakiendelea kwa mbali anasikika binti anayemkaribisha mtu mwingine na pia anasikika akisema '' napanda maua'' na anamalizia na neno ''karibu ingia ndani''..( ili kumsikia binti umakini unahitajika kidogo)

  03:20.....inasikika sauti mtu akikoroga chai kwenye meza yalipokuwa yanafanyika mazungumzo na anarudisha kijiko kwa kugonga meza lakini picha inayoonekana haimuoneshi mtu huyo na wala hakuna dalili za kuwa kwenye meza ya lwakatare kulikuwa na kikombe cha chai na kuwa chai ile ilikorogewa pale.. ...na pia kwa kufatilia kwa makini mtu anayekoroga chai si yule aliyekuwa anapewa maelekezo.... kitu kingine ni kwamba clip nzima quality ya sauti ya lwakatare haisikiki sawa sawa kama sauti ya mtu wa pili (kijana anayepewa maelekezo) ...

  05:35 .....sauti inasikika ikitamka '' UNAELEWA LAKINI?'' lakini ukiangalia kwa makini mdomo wa lwakatare hakutamka neno hilo badala yake mdomo unaonyesha ametamka '' UMELIONA HILI?'' ni sawa na pale alipokuwa akisalimiwa na ‘RICH'' hakutamka neno ''marahaba '' na badala yake neno alilotamka kulingana na mdomo ulivyoonekana alitamka '' YOTE MUHIMU'' na ndio maan hakugeuka kumwangalia yule aliyekuwa anasalimia kama ilivyoelezwa hapo juu..

  05:57... Sauti inasikika ikitamka kuwa ''kama tulivyofanya hii ya morogoro kisha kwenda igunga'' swali la kujiuliza hapa ni mauaji yapi yalitangulia? Ya morogoro au igunga?..... bado ushahidi unaonyesha video hii ni ya kupika..

  07:36.....Sauti inasikika ikisema '' dawa aina mbali mbali vidonge, unga ama liquid form fanya utafiti ujue zinapatikana wapi na ni bei gani; ni rahisi mno kama tulivyofanya utafiti wa mgongolwa tukapata ile kitu'' hapa pia kunachanganya inawezekanaje kijana anapewa jukumu la kutafuta bei na upatikanaji wa madawa wakati huo huo akikumbushwa namna walivyopata '' ile kitu'' kwa mgongolwa ambapo kijana alishiriki ...maana yake kijana anajua bei na wapi yanapatikana...( who is mgongolwa by the way?)

  15:59 ...sauti inasika ikisema '' unamuweka kwenye dilemma hajui adui ni nani yaani anakuja hapa anakukuta wewe ''LUDOVICK'' ndiye unamfatilia''...huyu Ludovick ni nani?( some dots needs to be collected and connected here ) yawezekana ni mmoja wa vijana waliokuwa wanajirekodi na hili ni jina lake halisi na wametajana pasi kujua au ni code name?..

  17:10 kijana anayepewa maelekezo (''Ludovick) anauliza '' kwa hiyo kama kila kitu kitaenda well inakwenda mpaka lini?'' lakini katika kujibu clip inayomuonyesha lwakatarea akijibu swali hilo akisema '' Bahati mbaya umekuja na majibu yasiyojitosheleza'' ....katika majibu haya kuna mkanganyiko mkubwa maana hakuna uhusiano wa swali lililoulizwa na jibu lililotolewa....tangu dakika ya 15 ya clip hii maelezo ya sauti zinazosikika hayana mpangilio wa manaa... mengi yalilenga kufuatisha ishara na vitendo vya lwakatare alivyokuwa akiongea na ukitizama kwa makini hakuna uhusiano kati ya maneno yenyewe na mdomo wa lwakatare.............

  19:20...Lwakatare anaonekana akiongea kwa mdomo na vitendo(kuchezesha mikono) huku kichwa chake na macho vikielekea kwa kijana(ludovick) aliyesimama/ kukaa mbele yake ..mara gafla kitu kinadondoka chini na kijana anainama kukiokota lakini bado lwakatare akiongea kichwa na macho vikiangalia juu alipo kijana na kijana anaitikia mmmh, mmmh mara gafla clip inakatwa na kuishia hapo... hapa pia kunamkanganyiko mkubwa... na hakuna uhusiano wowote wa maneno yale na picha inayoonekana na tukio la kudondoka kitu chini..... binafsi naamini clip ingeendelea kuanzia hapo sura ya mtu wa pili ingeonekana hasa mara baada ya kuokota kitu kilichodondoka na ndio maana clip imeishia hapo.......


  Pasco unaweza kuishabikia clip hii kama bonafide genuine kama na wewe ni mmoja wa washiriki wake au basi ni ushabiki wa kipuuzi ...anyway hata hivyo taarifa juu ya uhalilisia wa clip hii imetolewa....
   
 5. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2013
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,730
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Mtahangaika sana, lakini kama mnajua uongo na ukweli ni kama maji na mafuta, mngepunguza speed.
   
 6. o

  obeid666 JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2013
  Joined: Nov 19, 2012
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mjomba naona huko Lumumba mumemuazimia Lwakatare au mbinu yenu ni kuipaka CDM matope?
   
 7. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,101
  Likes Received: 1,714
  Trophy Points: 280
  Hii inazidi kutudhihirishia ukweli wa mambo..tupe zaidi mkuu
   
 8. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2013
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,360
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  mtaruka ruka mpaka muote vigimbi! CHADEMA FOR LIFE! hata Mdhikiri mkiwa uchi hakuna wa kutufanya tusiunge CDM mkono. Maccm Mtataga mwaka huu tena mayai ya Mbuni.
   
 9. A

  Akamba Member

  #9
  Mar 15, 2013
  Joined: Mar 13, 2013
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watu wanaweza kufoji saini iweje maneno ya kawaida
   
 10. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,101
  Likes Received: 1,714
  Trophy Points: 280
  wanaoujua watasema wewe kaa kimya
   
 11. o

  obeid666 JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2013
  Joined: Nov 19, 2012
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NasDaz na KING ILUNGA semeni umbea wenu
   
 12. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2013
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Tukisema hiyo ni script ya muandaaji wa ile clip tutakuwa tumekosea?? Hiv mbona unahangaika si uvipeleke tu Polisi aisee huku hasa unakutakia nini?? Huoni kuwa ndio unazidi kuonekana ni mwanapropaganda na sio mtu mwenye lengo la kuisaidia nchi iwakamate waarifu???

  Pia karatasi aliyokuwa anaandika hizo points kwenye hiyo clip haikuwa plain,, ilikuwa kuna vitu vimeshaandikwa na kuthibitisha hilo mwanzo tu wa clip, inaonekana kuna kitu alikuwa anasoma kabla ya kuanza kuongea na akataka kuongea kisha akasita kuonyesha kuwa hakuelewa kilichoandikwa au lah amekosea kukisoma. Katika hii karatasi yenu inaonekana kama vile Lwakatare ndiye mtu wa kwanza kuandika wakati clip yenu inaonyesha kulishaandikwa kitu flan kilichokuwa kinamguide Lwaka.????????????????? Mmepasukia hapo!Kweli kwenye ukweli uongo hujitenga.
   
 13. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2013
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 44,372
  Likes Received: 13,991
  Trophy Points: 280
  Kwa hili haliwezi kuwa ushahidi kabisa.

  Hapa mnaendelea kudhihirisha mnavyopika na kupakua wenyewe!
   
 14. C

  Concrete JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2013
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mleta mada mbona unaleta mambo ya kitoto sana.
  Kuna nini cha maana hasa unachotaka tujadili.

  Vijana wa Lumumba bado kabisa hamjakomaa katika kufanya propaganda.
  Watu tayari wana upeo mkubwa sana wa kujua mbichi na mbivu.

  Nendeni tu mkajipange upya, this issue will back fire you.
   
 15. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2013
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,486
  Likes Received: 1,354
  Trophy Points: 280
  nikianza na aliyepost hii kitu since the 1st day amejiunga jf this month/year,naona ilikuwa mahususi kwa ajili ya hii issue!
  Ila magamba mmechemsha
   
 16. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2013
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,700
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  mmh,video clip na maelezo mmeona haviendani sasa mmekuja na summary,haya bana.
   
 17. Adolph

  Adolph JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2013
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 884
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  upuuzi mtupu hata mimi hapa naweza kuandika huo utumbo uliouandika hata nikiwa nimelala
   
 18. Lisa Rina

  Lisa Rina JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2013
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 1,838
  Likes Received: 2,207
  Trophy Points: 280
  Nape banaaa!dah!una siasa za kizamani!!bukoba boyyy chezeaaaa!!
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2013
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,504
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  huo wa nape kabisa huo
   
 20. mkada

  mkada JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2013
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,019
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Hizi pesa mnazotumia kuwamaliza watu kisiasa mngewekeza kwenye maendeleo,tungekuwa mbali sana,ni aibu eti hata makongo juu hamna rami,mbezi beach kuna nyumba mpaka za mil 800 lkn barabara hazina lami,kazi kuwatengenezea watu kesi tu.
   
Loading...