Nakala ya karatasi na mwandiko wa Lwakatare wakati anatoa maelekezo hii hapa

Hahahahahahahahahaha
yani karatasi lenyewe lililotumika linaonekana kabisa ni jipya ukilinganisha na clip inavyosemekana kuchukuliwa!
Daaa wamechemsha sana hapa!

Hili karatasi utafikiri hii statement imetoka kuandikwa muda si mrefu hahahahah
 
Kama Mwigulu na Nape walikuwa na huo mkanda kwa zaidi ya miezi miwili, wakashindwa kuuwakilisha Police, nao pia ni watuhumiwa.
 
LUDOVICK ni kijana mtaalamu wa IT, ndiye moderator wa blog ya Maggid Mjengwa. Tayari kuna uzi unaomzungumzia huyu mtu. Tayari wanaanza kuumbuka mmoja baada ya mwingine. Maggid anaweza sahidia hili.
 
Habari wanajukwaa;

Kama alivyoahidi BUKOBA BOY kwenye maelezo yake yaliyoambatana na video ya LWAKATARE kwamba atakuwa anatupa ushahidi mmoja baada ya mwingine, Amesharusha karatasi aliyokuwa anaitumia Lwakatare kuchukua Note/Summary wakati anatoa maelekezo kwa kijana wake kwenda kuandaa mazingira ya utekaji.

Inayoonekana juu kulia kwenye karatasi ni namba ya MSACKY, Mwandishi wa habari wa mwananchi ambaye ni target mojawapo katika kutekwa. Wale waliosema kwamba ile video ni ya uongo wajiridhishe sasa kwamba BUKOBA BOY ana full data na amejiimarisha.

Wakubali sasa kwamba huu ni mwandiko wa LWAKATARE NA HAYO NI BAADHI YA MANENO ALIYOYATAMKA KWENYE VIDEO YAKE.

Zaidi unaweza kutembelea youtube japo haionekani vizuri.. NAOMBA MODS WAIKUZE HAPA JF ILI WASOMAJI WASIPATE SHIDA. KARATASI YENYEWE HII HAPA CHINI

attachment.php


Kijana wenu Ludovic tumeishamjua tayari, ndiye aliyetengeneza ile clip.
 
Wewe ni mtupu sana upstairs
* hivi uoni hilo karatasi lilivyo jipya kabisa? Hivi umeprint baada ya kuandika au umepiga copy baada ya kuandika?

* kwa nini tusiseme mmeforg muandiko?
*hivi unajua huu ni ushahidi dhaifu sana ndio maana hujaupeleka polisi?
*hivi unajua kwanini polisi walikuwa wanapekua kwa lwakatare?
*hivi unajua kama hata wakikuta barua kama hii kwa lwakatare haito aminika? Maana wewe umesha haribu ushahidi watakuwa wana kazi kuthibitisha kama sio planted!

You have done nothing my dear!

huu ndio mwandiko halisi wa LWAKA. TUJADILI HILO KWANZA
 
This is what I can say about Magamba-"Cito maturum cito putridum" means-early ripe early rotten!
 
Habari wanajukwaa;

Kama alivyoahidi BUKOBA BOY kwenye maelezo yake yaliyoambatana na video ya LWAKATARE kwamba atakuwa anatupa ushahidi mmoja baada ya mwingine, Amesharusha karatasi aliyokuwa anaitumia Lwakatare kuchukua Note/Summary wakati anatoa maelekezo kwa kijana wake kwenda kuandaa mazingira ya utekaji.

Inayoonekana juu kulia kwenye karatasi ni namba ya MSACKY, Mwandishi wa habari wa mwananchi ambaye ni targ

Akika wew umelaniwa huwo siyo mwandiko wa rwakatare wadanganye wajinga wenziyo hao hao ccm.
 
Hii ameandika mwana JF mwenzetu de'levis

============================== ========

Nilikuwa sina nia ya kuandika sana humu lakini baada ya kusoma comment yako nimelazimika kusema kitu...jambo lolote unaloambiwa , kuliona au kulisikia ni lazima ushughulishe akili kufikili ili ujiridhishe kama ni la kweli au la vinginevyo utakuwa unakubaliana na jambo ambalo si la kweli...jaribuni kuipa nafasi akili yenu kufikiri.... bahati mbaya sana katika siku za hivi karibuni imeonekana watanzania wengi sana wana tatizo la kutoipa akili nafasi ya kufanya maamuzi na kung'amua na mmoja wao ni Pasco....wachache wanaipa akili nafasi ya kufikiri.

Kuna matukio mengi sana na mengine wengi hamuyafahamu ambayo yanalenga kuichafua image ya taifa na kwa kuwa matumizi ya technolojia nchini yamekuwa yakikuwa kwa kasi hasa matumizi ya simu na intanet na kwa kuwa techolojia inakuwa kwa kasi na hivyo wengi wanashindwa kwenda sambamba na ukuaji wake na hivyo wanajikuta wanakubaliana na kila kitu wanachokiona ama kusikia..

katika mkanda huo ambao wewe pasco unauita ni ''bonafide and genuine'' nimefanikiwa kuuona jana mchana na mimi na wenzangu tumekaa na kuupitia kwa makini kabisa na kwa njia za kisasa zilizotusaidia kujua uhalisia wake... mkanda huo ni fake na tayari taarifa imeshatolewa....hata wewe pasco ukijipa mda wa kukaa na kuipa akili yako nafasi utagundua kuwa mkanda ule ni fake vinginevyo utakuwa unasumbuliwa na '' invincible ignorance''

Chini hapa nitakusaidia kidogo ili walau upate picha ya kuwa mkanda ule ni fake...

00:01 ------Sauti inaanza kwa kutamka ‘’MIKE’’ na kisha kuuliza ‘’ HAPO?’’ maana yake watu hawa wanajiandaa kuanza kujirekodi na wakati wa nafanya editing waliyaacha maneno hayo

00:15 ..........sauti ya mtu wa pili inasikika ikisema ‘’ TUTANOTE TENA HAPO’’ ...inaelekea watu hawa kuna mahali walikosea na kusema watarudia mahali hapo...

00:28 .......Binti anaonekana akija dirishani na kisha anaondoka baada ya maongezi mafupi na mwenzake aliyoko upande wa pili wa dirisha.

01:45......Sauti ya mtu mwingine ambaye baadae alikuja kutambulika kama ‘’RICH’’ anasikika akiwasalimia lakini aliyesalimiwa(lwakatare) kulingana na picha na mdomo wake inaonekana si yeye aliyeitikia ’’ marahaba’’..kuthibitisha hilo mara baada ya salamu msalimiwa hakugeuka kumwangalia anayesalimia ila aliendelea na shughuli zake na papo hapo kijana anayeonekana na kupewa maelezo mara moja anaanza mazungumzo na kijana (rich) aliyekuwa anasalimia na ndipo anamwita jina hilo ‘’rich’’ na wanapeana pole za matatizo na habari za sikukuu nk. katika mazungumzo mtu anayeonkena kwenye clip(lwakatare) bado haeguki kumwangalia huyo rich badala yake anaendela kutoa maelezo namna ya kudhuru watu.... hapa kuna abrakadara katika clip hii......

03: 15......wakati mazunguzo na melekezo toka kwenye clip ya lwakatare yakiendelea kwa mbali anasikika binti anayemkaribisha mtu mwingine na pia anasikika akisema ‘’ napanda maua’’ na anamalizia na neno ‘’karibu ingia ndani’’..( ili kumsikia binti umakini unahitajika kidogo)

03:20.....inasikika sauti mtu akikoroga chai kwenye meza yalipokuwa yanafanyika mazungumzo na anarudisha kijiko kwa kugonga meza lakini picha inayoonekana haimuoneshi mtu huyo na wala hakuna dalili za kuwa kwenye meza ya lwakatare kulikuwa na kikombe cha chai na kuwa chai ile ilikorogewa pale.. ...na pia kwa kufatilia kwa makini mtu anayekoroga chai si yule aliyekuwa anapewa maelekezo.... kitu kingine ni kwamba clip nzima quality ya sauti ya lwakatare haisikiki sawa sawa kama sauti ya mtu wa pili (kijana anayepewa maelekezo) ...

05:35 .....sauti inasikika ikitamka ‘’ UNAELEWA LAKINI?’’ lakini ukiangalia kwa makini mdomo wa lwakatare hakutamka neno hilo badala yake mdomo unaonyesha ametamka ‘’ UMELIONA HILI?’’ ni sawa na pale alipokuwa akisalimiwa na ‘RICH’’ hakutamka neno ‘’marahaba ‘’ na badala yake neno alilotamka kulingana na mdomo ulivyoonekana alitamka ‘’ YOTE MUHIMU’’ na ndio maan hakugeuka kumwangalia yule aliyekuwa anasalimia kama ilivyoelezwa hapo juu..

05:57... Sauti inasikika ikitamka kuwa ‘’kama tulivyofanya hii ya morogoro kisha kwenda igunga’’ swali la kujiuliza hapa ni mauaji yapi yalitangulia? Ya morogoro au igunga?..... bado ushahidi unaonyesha video hii ni ya kupika..

07:36.....Sauti inasikika ikisema ‘’ dawa aina mbali mbali vidonge, unga ama liquid form fanya utafiti ujue zinapatikana wapi na ni bei gani; ni rahisi mno kama tulivyofanya utafiti wa mgongolwa tukapata ile kitu’’ hapa pia kunachanganya inawezekanaje kijana anapewa jukumu la kutafuta bei na upatikanaji wa madawa wakati huo huo akikumbushwa namna walivyopata ‘’ ile kitu’’ kwa mgongolwa ambapo kijana alishiriki ...maana yake kijana anajua bei na wapi yanapatikana...( who is mgongolwa by the way?)

15:59 ...sauti inasika ikisema ‘’ unamuweka kwenye dilemma hajui adui ni nani yaani anakuja hapa anakukuta wewe ‘’LUDOVICK’’ ndiye unamfatilia’’...huyu Ludovick ni nani?( some dots needs to be collected and connected here ) yawezekana ni mmoja wa vijana waliokuwa wanajirekodi na hili ni jina lake halisi na wametajana pasi kujua au ni code name?..

17:10 kijana anayepewa maelekezo (‘’Ludovick) anauliza ‘’ kwa hiyo kama kila kitu kitaenda well inakwenda mpaka lini?’’ lakini katika kujibu clip inayomuonyesha lwakatarea akijibu swali hilo akisema ‘’ Bahati mbaya umekuja na majibu yasiyojitosheleza’’ ....katika majibu haya kuna mkanganyiko mkubwa maana hakuna uhusiano wa swali lililoulizwa na jibu lililotolewa....tangu dakika ya 15 ya clip hii maelezo ya sauti zinazosikika hayana mpangilio wa manaa... mengi yalilenga kufuatisha ishara na vitendo vya lwakatare alivyokuwa akiongea na ukitizama kwa makini hakuna uhusiano kati ya maneno yenyewe na mdomo wa lwakatare.............

19:20...Lwakatare anaonekana akiongea kwa mdomo na vitendo(kuchezesha mikono) huku kichwa chake na macho vikielekea kwa kijana(ludovick) aliyesimama/ kukaa mbele yake ..mara gafla kitu kinadondoka chini na kijana anainama kukiokota lakini bado lwakatare akiongea kichwa na macho vikiangalia juu alipo kijana na kijana anaitikia mmmh, mmmh mara gafla clip inakatwa na kuishia hapo... hapa pia kunamkanganyiko mkubwa... na hakuna uhusiano wowote wa maneno yale na picha inayoonekana na tukio la kudondoka kitu chini..... binafsi naamini clip ingeendelea kuanzia hapo sura ya mtu wa pili ingeonekana hasa mara baada ya kuokota kitu kilichodondoka na ndio maana clip imeishia hapo.......


Pasco unaweza kuishabikia clip hii kama bonafide genuine kama na wewe ni mmoja wa washiriki wake au basi ni ushabiki wa kipuuzi ...anyway hata hivyo taarifa juu ya uhalilisia wa clip hii imetolewa....
duh mpaka 2015 tutashuhudia vituko sijawahi kuamini kwamba nchi yetu itaharibika namna hii
 
Jamani ccm!hii si njia sahihi ya kutawala nchi!!!kama mmefikia kuua raia wenu kwa kuwa tu wengi wao hawajui lolote kuhusu teknolojia haitakuwa hekima,munatuua kirahisi namna hii kwa kuwa tu muna kompyuta ya kututengenezea picha feki ya kutudanganyia?tuwaamini muendelee kutuua?roho inatuuma kweli,hamuna tofauti yoyote na ma drug dealers wa mexico,munatumia UHAI wetu kujipatia power?kama chadema ni ya kufa basi muiache ife kwa muda wake,yaani mnatutoa kafara kwa kosa la chadema kuwasema tu?ccm ni binaadamu wanaopumua,mutaishi na mutakufa pia,munazaa na kuzaliana!chadema vilevile,munatengeneza mauti ya watoto na wajukuu zetu kwa mikono yenu wenyewe,muna pesa,muna kila kitu cha fahari ambacho kwa sisi ni ndoto ya mchana kuweza kuwa navyo,kwa nini hamridhiki?damu yetu watanzania masikini ina utamu gani midomoni mwenu?ccm imeamua kutumia roho zetu kama jukwaa la siasa????ee Mungu uko wapi?kwa nini umeuweka uso wako mbali na wanyonge sisi?maisha yetu ya kila siku ni hukumu tosha,bado umewapa nguvu maadui zetu ccm kutu
 
Habari wanajukwaa;

Kama alivyoahidi BUKOBA BOY kwenye maelezo yake yaliyoambatana na video ya LWAKATARE kwamba atakuwa anatupa ushahidi mmoja baada ya mwingine, Amesharusha karatasi aliyokuwa anaitumia Lwakatare kuchukua Note/Summary wakati anatoa maelekezo kwa kijana wake kwenda kuandaa mazingira ya utekaji.

Inayoonekana juu kulia kwenye karatasi ni namba ya MSACKY, Mwandishi wa habari wa mwananchi ambaye ni target mojawapo katika kutekwa. Wale waliosema kwamba ile video ni ya uongo wajiridhishe sasa kwamba BUKOBA BOY ana full data na amejiimarisha.

Wakubali sasa kwamba huu ni mwandiko wa LWAKATARE NA HAYO NI BAADHI YA MANENO ALIYOYATAMKA KWENYE VIDEO YAKE.

Zaidi unaweza kutembelea youtube japo haionekani vizuri.. NAOMBA MODS WAIKUZE HAPA JF ILI WASOMAJI WASIPATE SHIDA. KARATASI YENYEWE HII HAPA CHINI

attachment.php


Kweli nchi hii imepasuka kidini!... Kwakuwa Lwakatare ni mkristo BASI HUGO na waislamu wenzako mmelivalia njuga suala la kumzushia Lwakatare kesi zisizo na kichwa wala miguu!... Inaumiza saaana wakristo kuona mtu aliyepanga njama za mauaji ya MAASKOFU, MAPADRI, WALEI NA WACHUNGAJI na kutimiza azma yake kwa miezi sita (6) hakamatwi lakini tuhuma za uzushi jeshi zima la polisi linavalia njuga na kumkamata kwa vitu vya mtandaoni!...

HIVI MANENO YOOOOTE ALIYOSEMA ILUNGA YANGEELEKEZWA KWA WAISLAMU, ... MKRISTO HUYO ANGEKUWA NJE MPAKA LEO?

KWAKUWA SAFU YOOTE YA VIONGOZI WA JUU WA SERIKALI NA JESHI LA POLISI BASI ILUNGA ANALINDWA!...
 
Bungeni walifoji sahihi ya mh.PINDA itakua Lwakatare?narudia tena mfa maji haishi kutapatapa..siku za huyu mdudu anaeitwa 'ccm'zinahesabika,.
 
Wakina Nape bana yani hawa vijana watatu wanadhani wanaweza kutuchanganya akili na huu utoto
 
Nimesema CHADEMA lazima tu imutoe kafara Lwakatare au kumtosa kama kweli wanataka kuwa dactive na damage control. Kuendelea kumbeba kwenye mbeleko ya chama Lwakatate ni kuzidi kujisogeza kwenye tukio. Who knows, labda kuna video na makabrasha mengine ambayo ni more incriminatory out there.

Angalia, mpaka namba ya mtu ya simu ameandika. This guy is really bogus. Hata maswala ya ulinzi na usalama wake hayajui achilia mbali kulinda chama.

Hakufanya hata vetting ya watu aliokuwa anaongea nao na anawapa maelekezo nyeti kama haya. Mpaka note yake amewapatia.

kuna watu watakataa kuwa huu siyo mwandiko wake, lakini kugundua hand writing ni rahisi sana zaidi ya sauti ya mtu.
Kwenye hili nakubaliana na wewe, kumchunguza mtu sio vibaya kwa kazi yake, lakini kaifanya kizembe sana! Kuna kila dalili kwamba lwakatare alimuamini kupita kiasi huyo Bukoba boy, asijue mwenzake keshachukua vipande vya fedha.

Mimi namfahamu vizuri lwakatare najua ni yeye kwenye issue nzima kuendelea kupinga ni kujiumiza kichwa, hatahivyo nadhani kuna vipande vimeungwa ungwa ili kutengeneza na kuiboresha move, kwa mfano pale pa moro na anapotaja igunga havihusiani na havikuwa muhimu kwenye habari inayozungumzwa, lakini nadhani ni somo pia kwamba hapa duniani jiamini wewe tu na roho yako!
 
Mojawapo ya sifa ya uongozi bora ni kutatua matatizo yanayoonekana kana kwamba hayana mlango wa kutokea.

Hata wao ccm wanajifunza mengi juu ya matukio wanayotuletea CHADEMA na namna tunavyoyatatua.
Kwa tatizo hili la Lwakatare na jinsi litakavyotatuliwa, itakuwa ni uthibitisho mwingine mbele ya jamii kwamba CHADEMA inao uwezo wa kushika uskani wa Taifa hili na kukabili matukio na kuyatatua.........

Hiki ni kipimo bora cha kuwaonyesha wananchi uwezo CHADEMA ilio nao wa kung'amua mambo ya sirini na kuyadhibiti na nchi ikawa salama.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom