Nakala ya Hukumu ya Kesi ya Felix Mkosamali

Wanabodi,
Nimeipitia hukumu hii neno kwa neno na kuilinganisha na ile hukumu ya Arusha dhidi ya G.J. Lema na kujiuliza maswali mengi sana pasipo majibu.
Kimsingi, hukumu hii imeonyesha aina ya majaji tulionao na uwezo wao katika kushambua, kutafsiri sheria na kutoa maoni yao ya kisheria.Kwamba tuhuma zilizokuwa zinamkabili Mkosamali na Lema, walau zinafanana - kutoa maneno ya kashfa - na namna shauri lenyewe lilivyosikilizwa, ushahidi na mashahidi waliotumika, unapata mashaka sana na uwezo wa chombo hichi muhimu katika kutoa haki.
1. Imeelezwa wazi kuwa Burden of proof, anaibeba mlalamikaji(mshtaji) na lazima atoe ushahidi wa kuthibitika, pasi na mashaka yeyote.Baadhi ya wasomi wa sheria waliokuwa hapa, wali-dispute dhana hii katika kesi ya Lema kwa kusema kwamba kesi za uchaguzi(nadhani walimaanisha za madai) hakuhitajiki kuthibitisha pasi na shaka yeyote ushahidi wako, bali kwa kile kinachoitwa kisheria on balance of probabilities.

2.Na kwamba ushahidi unatakiwa ujitosheleze na usiwe na shaka(doubt) na pia uwe consistent.Yaani kama ni tuhuma imetolewa kwa kusema ulimsikia mgombea katika kampeni akiongea neno la kashfa, basi usiwe peke yako, bali uwepo wa mtu mwingine kuku-support kwamba alikusikia.

3. Ushahidi wa kusema kwamba mashahidi wako wa upande wa mlalamikaji lazima wawe watu wa kawaida(common citizen) peke yake haujitoshelezi kwani katika mazingira ya siasa na uchaguzi, pale mtu anaposhindwa, lazima atajitokeza mtu anayepinga ushindi, hata kama hana manufaa na kesi yenyewe.

Ukilinganisha shauri hili lililotolewa uamuzi na Jaji Sumari na ukaulinganisha na wa kesi ya Lema, utaona mapungufu, pamoja na mambo mengine, yafuatayo:

1. Upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yao.Kwamba kwa kusema tu, tulimsikia mgombea akisema msimchague Buriani kwa kuwa ni mwanamke, mwislamu, mzanzibari na ana mimba ya Mh. E. L. haikutosheleza kuthibitisha kwamba kweli Lema alisema hivyo.Walipaswa kuleta ushahidi wa sauti, video au hata kwenye diary zao au notebooks kuonyesha kuwa walirekodi/nakili maneno hayo ya kashfa.

2. Kwamba ushahidi lazima uwe consistent.Katika Kesi ya Lema, tuliona mmu mmoja mmoa aliyehudhuria mkutano wa hadhara wa kampeni, akisema kuwa alimsikia Lema akitoa maneno ya kashfa - mwingine Sokoni 1,mwingine Kwa Mrefu, Mwingine Mbauda etc.Hata wale mashahidi wengine walishindwa kuthibitisha ni wapi walisikia maneno hayo yakitamkwa.Kwa kuwa ule ni mkutano wa hadhara na ulifanyika kwa kuhudhuriwa na watu wengi, tulitegemea wangejitokeza mashahidi wengi zaidi na kuelezea kuwa walimsikia Lema akitamka maneno hayo ya kashfa.

3.Katika hukumu yake, mwanzoni kabisa, judge Rwakibarila alielezea wasifu wa baadhi ya mashahidi muhimu ambao alizingatia ushahidi wao.Alimtaka mama muuza mitumba na mkulima ambaye alikuwa askari mstaafu wa JWTZ.Alisema kuwa aliuzingatia ushahidi wa watu hawa kwa kuwa wao walikuwa wananchi wa kawaida na hawakuwa na interest katika shauri lile.Jaji alikosea na alisahau kuwa " katika uchaguzi na mshindi anapopatikana, hutokea mtu yeyote tu akaupinga ule ushindi na kutoa ushahidi wa uongo "..out of victorty...."
Jaji ali-dismiss ushahidi wa viongozi wa CHADEMA kwa kusema wana maslahi na ile kesi, na akasahau hata mshtaki alikuwa ana maslahi na ile keshi(Refer. Juma Mkanga, historia yake, nafasi zake za kisiasa, tuhuma alizokabiliwa nazo akiwa mwanasiasa etc)

Tusubiri na hukumu ya Mahanga tuipate, tuisome na tuone Jaji Profesa Juma alitoa hukumu PASI YA SHAKA YEYOTE au ni hukumu ambayo iko shaky na imeacha maswali mengi nyuma yake.
 
Kuandika hukumu kwa Kikoloni ni dalili ya kuendeleza utumwa. Kwani ni lazima hukumu iandikwe kwa English?? hukumu yenyewe imejaa quotes kibao za Kiswahili
 
Say what?

EMT na Pasco, hebu njoo mtufafanulie; hivi hawa majaji wetu kwanini wasiombe ujaji badala ya kuteuliwa tu?

Ndo maana watanzania hawana imani na mahakama!

Mkuu Invisible hata majaji wa zamani kama akina Lugakingira, Samata, Mwakasendo, Mwalusanya, na wengineo walikuwa wanateuliwa lakini walikuwa wanakata issues kwenye hukumu zao. Ukisoma hukumu zao nyingi ni nzuri na mtu unajifunza mengi. Kwa mfano, hukumu za Mwalusanya kama ile DPP v Daudi Pete ni desa tosha kwa sheria za bail sio Tanzania bali pia kwa nchi nyingine za Afrika, Commonwealth and duniani kwa ujumla. Ni nadra sana kwa hukumu kama ile kutolewa na majaji wa siku hizi. Tena imagine wakati huo wala tulikuwa hatuna demokrasia tulitonayo sasa.

Kwa hukumu za siku hizi hata Pasco atakubaliana nami kuwa inakuwa ngumu kidogo kwa mwanafunzi wa sheria ku-refer kama "In the celebrated judgment of....." They are not celebrated judgements anymore.

Lakini hata hiyo kuna umuhimu wa kuangalia hili suala kwa mapana zaidi. Inawezekana labda kwa ujumla fani ya sheria imeshuka kiwango? Uzuri wa hukumu ya jaji inategemea pia na submissions za mawakili wa pande zote mbili. Je, mawakili wa siku hizi huwa wanakata shule ya kutosha na ku-submit strong and well supported arguments mahakani kiasi cha kumfanya jaji nae akakate shule?

Kama mawakili wanasubmit arguments nyepesi nyepesi unafikiri kweli jaji atahangaika kuumiza kichwa? Sisi tunatumia adversarial system ambapo jaji anakuwa kama referee tuu. Mchezo wote unachezwa na mawakili wa pande zote mbili. Kama mawakili wako shallow, kuna uwezekano mkubwa pia hukumu ikawa shallow hata kama jaji ni nzuri.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom