Elections 2010 Nakaaya ana hali gani?

Im feeling so pitty for Naakaya, she wanted to go back home (CCM), there she is now...... next time think twice before u start kutangatanga woman......
:israel:
 
Kwa kweli huyu sister ni zamu yake ya kuona MABADILIKO aliyokuwa akiyaimba kwa muda mrefu katika wimbo wake wa Mr POLITICIAN.
 
Huyo nakaaya kazoea kudanganywa. Jamaa wa mkataba wa sony alikula akapiga chini. Ccm nao wamekula na watampiga chini. Wasanii na mashabiki wake nao wamtose akafie mbele

Nadhani ni mmoja kati ya waliochangia kuporomoka kwa ccm this time!...kwa hapa JF nina imani kabisa kuwa amechangia sana kuwafanya watu wengi sana waichukie ccm, hasa pale alipotangaza kukihama CHADEMA!...Mimi binafsi siku hiyo ndipo nilipofanikiwa kumshawishi mke wangu kuwachana na matapeli hawa, na nikafanikiwa!
 
hivi yule mzee wake kule arumeru mashariki atamaliza miaka 5? amechoka mbaya..

Kuhusu Naakaya achaneni naye ila msishangae akapewa Ukuu wa wilaya..
 
Najaribu kuwaza Nakaaya Sumari atakuwa na hali gani kwa sasa, hasa baada ya kuanza kushuhudia kwa macho yake maana halisi ya Peoples Power, nakushuhudia mabesti zake almost wote aliowatelekeza wakiingia mjengoni!!
Si hivyo tu, lakini pia anavyoshuhudia baba yake Jeremiah Sumari akipelekwa puta na kijana mdogo wa miaka 24 mwanafunzi wa chuo kikuu huko Arumeru Magharibi.
Namhurumia sana huyu dada masikini jamani...tujaribu kuwasiliana naye, labda atakuwa anahitaji TOBA!

Wajua Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza sasa yeye amepalamia makuti mchan kweupe bila hata kuuliza iseje ikawa ndio kama zile stories tulizokuwa twapashwa jana kutoka majimboni kuwa CCM wanataka kuwapa pesa wagombea wa chadema waachie majimbo na halikufanikiwa hilo zoezi.

Sasa kwa Nakaaya ndio hili sasa limemkuta either alisogezewa kitu kidogo kwani fika CCM walijuwa Binti anagonga au anatinga mjengoni kwa tiketi ya CHADEMA waka mrubuni kwa kijana kama yule kweli ni mfurukutwa anahamia chama tu basi huku alikuwa anapigania haki ya wanyonge na vijana wengi walitegemea akazibe lile pengo la Amini Chifupa kule khaaaa.

Siku nikimwona mdogo wake nikija huko arusha ntamwambia kabisa Dada yako nae kashemka mchana kweupe unajua hizi siasa kuna baadhi ya vijana hawajui ni nini wakafanye kwenye siasa ni wanajitupia tuuu basi ili waonekane wako kwa siasa.

Kawaabisha wadada hapo Arusha kwa kweli, Ukipitia CCM kuwa mbunge uwe na roho ngumu kama jiwe hivi kwani CCM hawataki kupingwa na kukosolewa mfn Shibuda aliwaambia kweli wakamfanyia fitna na akenda CHADEMA na amerudi mjengoni.

 
Nadhani anaitaji msaaada kwani alikuwa hajui alifanyalo. Nasikitika kusema kuwa wimbo wa Mr Politician alikuwa anaimba lakini halikuwa aelewi maana yake, na atakuwa anajisikitikia sana kuimba huu wimbo kwani unamgeukia na yeye mwenyewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom