Waheshimiwa habari za mida
Mimi ni IT specialist kwenye shirika moja lisilo la kiserikali mshahara wangu ni Wa kati si mkubwa sana wala si mdogo sana
Lakini pia Mimi ni lecturer part time nafundisha jioni wafanyakazi katika chuo kimoja hapa DSM
Nimeoa na Nina watoto wawili
Huyu mke wangu ni chotara Wa kiarabu
Wakati tumeanza tumeanza kudate hakuniambia kama ana mtoto na kwa kweli alivyo mzuri sikutilia shaka kama ana mtoto maana hata nyonyo zake zilikuaa zimesimama kama mtoto anaebalehe
Baadae mapenzi yaliponoga ndipo akaniambia kuwa ana mtoto alie darasa la kwanza yupo kwa mama mzazi yaani bibi Wa mtoto
Kwa kuwa nilikua tayari nimezama kwenye mahaba mazito ikabidi nikubali tu maana by that time nilishatangaza ndoa ilikua ni point of no return
Ila mchumba alianihakikishia kuwa mtoto wake hatakua kikwazo kwenye ndoa yetu na kwamba huduma zote za malezi ikiwa ni pamoja na shule, malazi,maradhi na mengineyo yatakua chini ya baba Wa mtoto
Huo ndio ukawa mkataba wetu na kwamba mtoto ataishi kwa bibi na baadae atahamia kwa baba mzazi ambae ni Mwarabu mwenzie
Akabadli dini kuja ukristo tukafunga ndoa haikua shida maana mama ake pia ni mkristo baba ndio muislam na aliwatelekeza siku nyingi
Miezi sita baada ya ndoa akamleta mtoto kwetu kuishi permanent kinyume na mkataba wetu, anyway nikawa na roho ya utu nikasema haina shida kuepusha Shari
Mtoto wake alipofika darasa LA NNE wakampeleka boarding sisi hapo tuna watoto wawili mapacha Wa miaka minne kasoro nadhani
Mimi ndie nililipa ada ya boarding
Siku moja katikati ya wiki nilibeba mahitaji kadhaa nikampelekea yule mtoto shuleni niliomba wakaniruhusu kuingia pale
Surprisingly matron akaniambia huyo mtoto mbona ana vitu vya kutosha mama ake na baba ake walikua hapa juzi siku tano hivi zimepita.
Akaniuliza kwan we nani Wa mtoto nikamweleza
Akashangaa akaniambia mbona walikua wamekaa na mtoto kama ni familia inayoishi pamoja akanipa kama umbea flani hivi
Nilishangaa kwa kuwa mke wangu hakuniambia kama alienda kwa mtoto na mzazi mwenzie alikuwepo
Visiting day moja nikaenda na watoto wangu kumuona mwenzao, mke wangu aliondoka mapema akatangulia tulipofika pale tukakuta jamaa nae yupo wamekaa na mtoto na wife, Mshikaji akaaga bila kunisalimia akaondoka zake
Nilishindwa kumwelewa nikazuga tukaendelea na mengine
Hatimae yule mtoto akamaliza LA saba, Mama ake akamtafutia shule nzuri sana yenye matokeo mazuri kila mwaka
Kimbembe kikaja kwenye ada, Mimi nikamwambia mwisho wangu ilikua ni LA saba sasa walipe wenyewe maana watoto wangu pia wameanza shule ya ma padre Lieberman ada wote wawili ni million sita kwa mwaka
Bado Nina mdogo wangu Wa kike anasoma chuo nalipa Mimi ingawa ana mkopo asilimia ishirini
Bado gharama za uendeshaji familia za kila siku, hivyo nikamwambia sitaweza kulipa, ni vema babaake ajipange kulipa
Wakuu kwa kauli yangu hiyo ulizuka mgogoro mkubwa Huduma zote muhimu nilisitishiwa pamoja na za chumbani
Akaondoka akarudi kwao kwa mwezi mzima baada ya kusuluhishwa akarudi mm nikashikilia msimamo kuwa silipi ada
Hivi karibuni wakati hayupo nimeingia kwenye mapenzi na mdada Jirani yangu amepanga upande anaish na ndugu
Wife amerudi sina hamu nae tena, huyu demu Jirani nimekua nikimpa lift asubuhi kwa muda mrefu sasa na ndipo tukaelewana na anajua matatizo yetu
Alikua akitusaidia sana nyumbani wakati wife ameondoka
Nimedhamiria kumuacha wife mazima nimeshachoka
Juzi baba amekuja akaniambia nilikushangaa ulipojifanya mjuaji kuoa mwanamke mwenye mtoto tukakuzuia ukalazimisha sasa umeyaona?
Wakuu nipo njia panda ?
Nifanyeje?