Najuta kuoa mwanamke mwenye mtoto

Najuta kuoa mwanamke mwenye mtoto

Unaweza kunisaidia mawazo kuhusu tatizo sugu la ada ya mtoto maana ndilo tatizo lililonileta hapa kuomba ushauri
Hilo la uzinzi lina ngazi ya familia na wazee walishahusika nalo
Kama ingekua ni uzinzi pekee nisingekuja hapa lina mahala pake

Hili LA mtoto ndio limeondoa amani ya nyumba na limeshindikana kwenye ngazi zote
Watu wengi wananipa ushauri kwa jambo ambalo sijaomba ushauri (uzinzi) na ambalo Nina suluhisho tayari
Wanaacha kichwa cha somo husika ambacho ndio kimebeba dhana nzima ya somo hili

acha upopoma na wewe bwana.. we umetuwekea stori nyingi mpaka kuwa tayari una mtu mwingine unataka sie hilo somo kuu tulielewe vipi? au unataka tuanze kukupa ushauri wa kijinga?,,, by the way nilisahau kukuuliza hicho kichwa cha somo kina upara au ni kirasta???
 
pole sana mkuu,ila kiukweli hapo mkewako unasaidiwa hadi mengine na uyo baba wa zamani,waarabu wanawezana na waarabu wenzao.kama baba yake yupo na shule anaenda kwa nn hamlipii ada mwanae?.mkeo mtaalamu anapiga kona yeye na kichwa anafungwa mwenyewe.pole sana
 
Ninavyoelewa, mwanamke mwenye mtoto ni shida kwani bado yule mzazi mwenzie anahusika nae katika kulea mtoto ikiwa ni pamoja na kupata haki ya penzi. Na ni rahis kumpa nafasi hiyo kama nija ya kupata matumizi ya mtoto. Na wakati mwingine mzazi mwenzie anatumia kigezo cha matumizi ya mtoto kulazimisha tendo la ndoa.

labda wanawake golikeepa aisee yaan vijisent vya matumiz kwa mtoto vinifanye nijiuze? kama kama bila kumpa hatoi matumizi nikujiuza huko. ndo maana hawa viumbe ukizaa naye akitaka kumtunza mtoto atunze asipotaka atajiju siwez fanya ujinga huo mimi nimeolewa najirudisha ili mtoto atunzwe kwani huyo mtoto mmoja anakula kiasi gani shule za ada ya milion moja zipo kibao
 
Unaweza kunisaidia mawazo kuhusu tatizo sugu la ada ya mtoto maana ndilo tatizo lililonileta hapa kuomba ushauri
Hilo la uzinzi lina ngazi ya familia na wazee walishahusika nalo
Kama ingekua ni uzinzi pekee nisingekuja hapa lina mahala pake
Hili LA mtoto ndio limeondoa amani ya nyumba na limeshindikana kwenye ngazi zote
Watu wengi wananipa ushauri kwa jambo ambalo sijaomba ushauri (uzinzi) na ambalo Nina suluhisho tayari
Wanaacha kichwa cha somo husika ambacho ndio kimebeba dhana nzima ya somo hili
WEWE SASA UMECHANGANYIKIWA
ada ya mtoto inakuhusu nini wakati umeshaambiwa wenzako wanaenda
tumekuambia hata huyo mtoto akikua ni wa Kiarabu HATAKUJALI

kina GHIBUU wamekwambie mfyeke miguu huyo kesharudi kwenye zinaa
ww unatuambia tunapotoka kukushauri kulipa ADA kumbe unalo jibu ENDELEA
Tunakubaliana na wewe tu kuwa kuzini angezini tu, hapa umeleta tatizo la mtoto, lakini tatizo tulilo liona sisi sio mtoto, kuna kamchezo unachezwa,
kwanza kumfumania au kupata taarifa kuwa anakwenda kumuona mtoto bila ya taarifa yako,
pili kwenda pamoja na baba yake mtoto shuleni bila ya kuwapo wewe.
Tatu kulazimishwa wewe umlipie ada mtoto mtoto.
Jee wewe binafsi haya masuala unayo majibu gani?
Toka uwanze kulipa ada ni miaka mingapi? Una jua hao watu washaonana mara ngapi bila ya wewe kujua?
Suala moja tu la kutoka kwako kwenda kuonana na haram yake ni kosa kubwa kwako na kwa Allah.
Sisi waislam suala hilo ni kubwa sana, mi naweza vunja n guu yake na red card juu
 
Unaweza kunisaidia mawazo kuhusu tatizo sugu la ada ya mtoto maana ndilo tatizo lililonileta hapa kuomba ushauri
Hilo la uzinzi lina ngazi ya familia na wazee walishahusika nalo
Kama ingekua ni uzinzi pekee nisingekuja hapa lina mahala pake

Hili LA mtoto ndio limeondoa amani ya nyumba na limeshindikana kwenye ngazi zote
Watu wengi wananipa ushauri kwa jambo ambalo sijaomba ushauri (uzinzi) na ambalo Nina suluhisho tayari
Wanaacha kichwa cha somo husika ambacho ndio kimebeba dhana nzima ya somo hili

To be honest mimi sioni swala la ada kama ni kubwa sana as long as huyo ni mke wako just asume ni sawa ambavyo wewe unaweza kumsaidia ndugu yako wewe na mke asilalamike mimi nadhani ungeilipa kama hilo ndio tatizo litakwisha na maisha yataendelea.kama ambavyo umesema kuna mdogo wako unamsaidia like wise unakila sababu za kubeba ilo jukumu la mkeo otherwise muwezeshe afanye biashara ili amsaport mwanae .
 
labda wanawake golikeepa aisee yaan vijisent vya matumiz kwa mtoto vinifanye nijiuze? kama kama bila kumpa hatoi matumizi nikujiuza huko. ndo maana hawa viumbe ukizaa naye akitaka kumtunza mtoto atunze asipotaka atajiju siwez fanya ujinga huo mimi nimeolewa najirudisha ili mtoto atunzwe kwani huyo mtoto mmoja anakula kiasi gani shule za ada ya milion moja zipo kibao
Hongera yako maana wengine unakuta alipoolewa mtoto hatakiwi hivyo atapelekwa kwa bibi mzaa mama nahuko matunzo yanatakiwa. Ili ayapate lazima atoe something!
 
acha upopoma na wewe bwana.. we umetuwekea stori nyingi mpaka kuwa tayari una mtu mwingine unataka sie hilo somo kuu tulielewe vipi? au unataka tuanze kukupa ushauri wa kijinga?,,, by the way nilisahau kukuuliza hicho kichwa cha somo kina upara au ni kirasta???

Mkuu kwa mfano nikikwambia suala la usaliti nimeshali address utasema nn?
Hili suala la baba Wa mtoto kwenda kumuona akiwa na mama mtu lilitokea mtoto akiwa darasa la nne, leo tunagombana kuhusu up keep na education cost ya mtoto na mtoto yupo form one sasa
Kwa Maneno mengine mambo ya uzinzi yameshatatuliwa miaka na yaliisha
Mnataka kuanzia mtoto akiwa LA NNE nianze kuadisia line to line kwamba LA tano ikawa ivi then la sita n.k
Read carefully and understand
 
Jamaa kani pm ujumbe huu
Mnamwelea huyu mtu kweli?
 
Hahahah pale pale kwenye Point of no return ndo ulipocheza mistaje.. Ulitakiwa umpige chini kwa.sababu tayari alikudanganya...

Then huyo mdada kimsing alikuwa analiwa.mzgo kama kawaida
 
To be honest mimi sioni swala la ada kama ni kubwa sana as long as huyo ni mke wako just asume ni sawa ambavyo wewe unaweza kumsaidia ndugu yako wewe na mke asilalamike mimi nadhani ungeilipa kama hilo ndio tatizo litakwisha na maisha yataendelea.kama ambavyo umesema kuna mdogo wako unamsaidia like wise unakila sababu za kubeba ilo jukumu la mkeo otherwise muwezeshe afanye biashara ili amsaport mwanae .

Tatizo ni kwamba mdada huyo anayoa mxgo kwa x wake kama kawaida.. Huo ndo ukweli ndo mana akienda kumchek mtoto anaenda bila kuaga.. Anaenda kukutana.na baba mtoto.. Unadhan kuna cha maana hapo
 
Unaweza kunisaidia mawazo kuhusu tatizo sugu la ada ya mtoto maana ndilo tatizo lililonileta hapa kuomba ushauri
Hilo la uzinzi lina ngazi ya familia na wazee walishahusika nalo
Kama ingekua ni uzinzi pekee nisingekuja hapa lina mahala pake

Hili LA mtoto ndio limeondoa amani ya nyumba na limeshindikana kwenye ngazi zote
Watu wengi wananipa ushauri kwa jambo ambalo sijaomba ushauri (uzinzi) na ambalo Nina suluhisho tayari
Wanaacha kichwa cha somo husika ambacho ndio kimebeba dhana nzima ya somo hili

Kama ni hivyo mbona easy sasa, acha kumlipia huyo mtoto ada and then sikilizia reaction ya mama yake. Kama atataka muachane kwa sababu umekataa kumlipia mwanae ada hapo sasa sikilizia moyo wako unasemaje. Kama uko poa aondoke basi mwache aende zake, ila kama moyo wako unampenda basi mwambie utakuwa unachangia nusu na baba mtoto atamalizia nusu inayobaki
 
Waheshimiwa habari za mida,

Mimi ni IT specialist kwenye shirika moja lisilo la kiserikali mshahara wangu ni wa kati si mkubwa sana wala si mdogo sana. Lakini pia mimi ni lecturer part time nafundisha jioni wafanyakazi katika chuo kimoja hapa DSM, Nimeoa na nina watoto wawili, huyu mke wangu ni chotara wa Kiarabu.

Wakati tumeanza kudate hakuniambia kama ana mtoto na kwa kweli alivyo mzuri sikutilia shaka kama ana mtoto maana hata nyonyo zake zilikua zimesimama kama mtoto anaebalehe.Baadae mapenzi yaliponoga ndipo akaniambia kuwa ana mtoto alie darasa la kwanza yupo kwa mama mzazi yaani bibi wa mtoto.

Kwa kuwa nilikua tayari nimezama kwenye mahaba mazito ikabidi nikubali tu maana by that time nilishatangaza ndoa ilikua ni point of no return. Ila mchumba alinihakikishia kuwa mtoto wake hatakua kikwazo kwenye ndoa yetu na kwamba huduma zote za malezi ikiwa ni pamoja na shule, malazi, maradhi na mengineyo yatakua chini ya baba wa mtoto.

Huo ndio ukawa mkataba wetu na kwamba mtoto ataishi kwa bibi na baadae atahamia kwa baba mzazi ambae ni Mwarabu mwenzie. Akabadli dini kuja ukristo tukafunga ndoa haikua shida maana mama ake pia ni mkristo baba ndio muislam na aliwatelekeza siku nyingi.

Miezi sita baada ya ndoa akamleta mtoto kwetu kuishi permanent kinyume na mkataba wetu, anyway nikawa na roho ya utu nikasema haina shida kuepusha shari. Mtoto wake alipofika darasa la nne wakampeleka boarding sisi hapo tuna watoto wawili mapacha wa miaka minne kasoro nadhani mimi ndie nililipa ada ya boarding.

Siku moja katikati ya wiki nilibeba mahitaji kadhaa nikampelekea yule mtoto shuleni, niliomba wakaniruhusu kuingia pale Surprisingly Matron akaniambia huyo mtoto mbona ana vitu vya kutosha. Mama yake na baba yake walikua hapa juzi siku tano hivi zimepita. Akaniuliza kwani wewe ni nani wa mtoto nikamweleza, akashangaa akaniambia mbona walikua wamekaa na mtoto kama ni familia inayoishi pamoja.

Akanipa kama umbea flani hivi nilishangaa kwa kuwa mke wangu hakuniambia kama alienda kwa mtoto na mzazi mwenzie alikuwepo. Visiting day moja nikaenda na watoto wangu kumuona mwenzao, mke wangu aliondoka mapema akatangulia tulipofika pale tukakuta jamaa nae yupo wamekaa na mtoto na wife.

Mshikaji akaaga bila kunisalimia akaondoka zake nilishindwa kumwelewa, nikazuga tukaendelea na mengine hatimae yule mtoto akamaliza la saba. Mama yake akamtafutia shule nzuri sana yenye matokeo mazuri kila mwaka kimbembe kikaja kwenye ada, mimi nikamwambia mwisho wangu ilikua ni la saba.

Sasa walipe wenyewe maana watoto wangu pia wameanza shule ya Mapadre Lieberman ada wote wawili ni million sita kwa mwaka bado nina mdogo wangu wa kike anasoma chuo nalipa mimi ingawa ana mkopo asilimia ishirini. Bado gharama za uendeshaji familia za kila siku, hivyo nikamwambia sitaweza kulipa, ni vema babaake ajipange kulipa.

Wakuu kwa kauli yangu hiyo ulizuka mgogoro mkubwa, Huduma zote muhimu nilisitishiwa pamoja na za chumbani akaondoka akarudi kwao kwa mwezi mzima baada ya kusuluhishwa akarudi mimi nikashikilia msimamo kuwa silipi ada.

Hivi karibuni wakati hayupo nimeingia kwenye mapenzi na mdada jirani yangu amepanga upande anaishi na ndugu, wife amerudi sina hamu nae tena. Huyu mdada jirani nimekua nikimpa lift asubuhi kwa muda mrefu sasa na ndipo tukaelewana na anajua matatizo yetu, alikua akitusaidia sana nyumbani wakati wife ameondoka.

Nimedhamiria kumuacha wife mazima nimeshachoka, juzi baba amekuja akaniambia nilikushangaa ulipojifanya mjuaji kuoa mwanamke mwenye mtoto tukakuzuia ukalazimisha sasa umeyaona.

Wakuu nipo njia panda, ushauri tafadhali

Pole sana ndugu! haya matatizo kwa %100 husababishwa na wanawake haswa wanao zaa kabla ya kuolewa,maana pia huwa husema ukweli baadae sana, na pia kwasisi wanaume huwa tuna makosa,kwani hupenda kuahidi kulea watoto wawatu ilmradi tu ufanikiwe kuwa na huyo mwanamke wakati kiasilia ni ngumu kwa %50. mara nyingi wanapopata ujauzito familia zao pamoja na marafiki, majirani ndio hujitokeza kuwa washauri wao wakuu na wakosoaji wa kuu, na hasa anayehukumiwa kwa wakati ule ni mwanaume aliyempatia ujauzito. nilisha wahi kushuhudia mdada ana PHD ya KENTY UNIVERSITY UK amezaa na rafiki yangu na walikuwa na mpango mzuri tu wa kuishi pamoja na walikuwa wanaheshimiana sana! sasa baada ya kujifungua sarakasi zilianza pale washauri wakuu walipoanza kumkosoa baba wa mtoto kisa ni form four! hatimaye wameachana tena kwa kashfa! ila uhakika penzi haliwezi kufa kwa baba wa mtoto japo hasira zipo na ugomvi ulikuwepo! sasa anapokutana na mtu mwingine huwa anadhani amepata ufumbuzi wa tatizo la moyo wake hususani kimapenzi! tatizo linapotokea au mkikwaruzana kidogo humkumbuka baba wa mtoto wake aka mzazi mwenzie na hofu ya kukuheshimu inatoweka maana si anauhakika kuna mahali anapenda na anapendwa nyie mlikutana tu wakati wa maafa!! na ukumbuke baba wa mtoto lazima atakuwa na sauti kuliko wewe kwa kipindi kirefu labda itokee alimbaka huyo binti na kumpatia ujauzito, lakini kama walianza kwa kuelewana na hadi kufikia kuzaa ujue kuna msingi mzuri kati yao.
Ushauri wangu kwatu sisi vijana! tupende kuwa na subira ili tuyaanze maisha na we wa ujana wetu! kuishi au kuoa na kuolewa na mume/mke aliyekwisha zaa na mwingine nikujivurugia system ya kufurahia mapenzi ndani ya ndoa.
 
Back
Top Bottom