Najuta kuoa mwanamke mlokole

Najuta kuoa mwanamke mlokole

pole kwa yanayokukuta. kimsingi mkeo na wakwe zako hawana akili kabisa. Imeandikwa kila jambo lifanywe kwa kiasi. Haiingii akilin mke anakesha kanisani huku akiwa ameacha mtoto mdogo kama huyo nyumbani. Hapo kuna tatizo kubwa sana
 
mwanaume kamili hapigi mke wala kulalamika. kama mtu anazingua unachukua njia yako. sioni hata haja ya kuwasema mabinti wa kilokole kwa sababu hukulazimishwa kuwa naye. kama na ameona mchungaji wake ni wa maana kuliko wewe chukua maamuzi magumu au mlowase. pia kuna ulokole na ugonjwa. ulokole hausemi mtu aharibu ndoa yake. hizo ni Imani za watu wasiojua wanachofanya. pia kisheria ukimuachisha mtoto maziwa kabla ya miezi sita unaharibu ubongo na kinga yake.
pia ungeenda kuongea na mchungaji wake. sio ustaarabu kupiga mke ambaye hulingani naye nguvu. pia hata wewe unaoneka una wenge jingi maana umempiga mke wako na kuja kumangaza hapa jf wakati yeye hawezi kujitetea. unapomsema mtu hakikisha naye yupo na anaweza kujitetea kama wewe. pia kwangu sioni tija ya ulichofanya hapa. mahusiano sio jela. mtu akizingua unajiachia kivyakooo

Sina hakika kama unauzoefu wa ndoa...kuacha is the last option.
 
mwanaume kamili hapigi mke wala kulalamika. kama mtu anazingua unachukua njia yako. sioni hata haja ya kuwasema mabinti wa kilokole kwa sababu hukulazimishwa kuwa naye. kama na ameona mchungaji wake ni wa maana kuliko wewe chukua maamuzi magumu au mlowase. pia kuna ulokole na ugonjwa. ulokole hausemi mtu aharibu ndoa yake. hizo ni Imani za watu wasiojua wanachofanya. pia kisheria ukimuachisha mtoto maziwa kabla ya miezi sita unaharibu ubongo na kinga yake.
pia ungeenda kuongea na mchungaji wake. sio ustaarabu kupiga mke ambaye hulingani naye nguvu. pia hata wewe unaoneka una wenge jingi maana umempiga mke wako na kuja kumangaza hapa jf wakati yeye hawezi kujitetea. unapomsema mtu hakikisha naye yupo na anaweza kujitetea kama wewe. pia kwangu sioni tija ya ulichofanya hapa. mahusiano sio jela. mtu akizingua unajiachia kivyakooo

Sina hakika kama unauzoefu wa ndoa...kuacha is the last option.

Hamna namna nyingine alitakiwa afunzwe tu.
 
Maradhi, ujinga, umasikini na dini Ni janja kwa waafrika walio wengi

Sisemi dini ni mbaya ila waafrica wengi wanafungwa akili na dini na kuchukulia dini kupita kiasi. Wengi wanaheshimu dini kuliko Mungu mwenyewe. Pole mkuu
 
"Wanaofanya kazi ya madhabahu, hula madhabahuni"
kama hatafunwi na mtumishi sijui tu, kipigo cha shemejio ndo kimeniacha hoi nmecheka duh
pamoja na kukuponyoka ulifanikiwa kumtengua mbavu ha ha ha ina maana asingekimbia roho ingeachana na mwili dah funny
 
Pole sana,dini ni ndani ya moyo wake na sio kukesha kanisani angeweza hata kuwa anasali akiwa nyumbani baada ya kazi zake na siku moja kwa wiki ndio angekwenda kanisani kusikiliza neno la mungu.Shida haya makanisa ya kiroho yanamafundisho yasiyo faa na yamekuwa chanzo cha kusambaratisha jamii pamoja na ndoa.Nina watu wamepotelea huko kwrnye hayo makanisa na kudhindwa kujumuika na familia au jamii
 
njoo uku kigoma uoe totoz za kituc full adabu na gemu wanaweza ataree
 
Achana naye ndoa siyo kupeana stress bhana, piga chini hakufai huyo.
 
Kwa maelezo yako na uwelewa wangu nianze na jinsi ninavyo kuona:
  • Mosi, unaelekeakuwa una wivu wa kupindukia kiasi kuwa hupendi mkeo atoke nyumbani hata kwa kwenda kanisani.
  • Pili una udikiteta fulani, ndani mwako ni amri tu hakuna mjadala (negotiation), Unalotaka ndilo linakuwa.
  • Una mapenzi ya kizamani ya kikurya ambayo yanahusisha kupigana pigana.
Ulipaswa kabla ya kuoa, uchunguze kwanza: Unataka mke wa kushinda kwenye baa au saloon ama kitchen party, maana hawa nao wapo ni wewe tu na upendeleo wako. Si rahisi kumbadilisha mtu mlevi akawa mlokole na mlokole akawa mlevi hivyo ulipaswa upate ready made kuliko kutransform. Mkeo, licha ya mapenzi yako ya kizamani ya kupigana pigana, amekusamehe, anataka mrudiane wewe hutaki. Maana yake huna roho ya msamaha. Waswahili husema 'Asiye samehe haliwezi penzi.' Kumbe wewe huwezi penzi ingawa unaweza kupanda.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa uhuru wa kila mtu kuabudu imani aitakayo, lakini wewe unataka mkeo aabudu namna unavyotaka wewe, hivyo bila kujua, unataka kuwa juu ya Katiba ambayo ndiyo sheria mama ya sheria zote nchini. Masikini nduyu yangu hata hujui kuwa kuvunja Katiba ni kosa. Unaishi katika jamii ya watu wasiostarabika, wastaarabu huheshimu sheria zilizowekwa. Ni wanyama wa porini ndiyo wanaoishi kama unavyotaka wewe na mkeo muishi.
Sijazungumzia upande wa mkeo wala wazazi wake kwa sababu sijawasikia, lakini kubwa ni wewe uliyeomba ushauri na wao hawajaomba chochote. Ndoa ni taasisi inapaswa iheshimiwe na watu wote ukiwemo wewe mwenye ndoa. Mtu yeyote aliyemo kwenye ndoa hushawishiwa wakati wote na mtu mmoja mmoja vikundi vya watu marafiki mbalimbali wakike kwa wakiume, lakini wewe mwenye ndoa unapaswa kuwa na ushawishi mkubwa kushinda makundi yote. Tunapomshawishi mke hatumshawishi kwa mabavu, tunamshawishi kwa hoja huku ukinyunyiza juu yake UPENDO usiopatikana mahala pengine popote isipokuwa kwako tu

Una ufahamu mkubwa sana wewe!!! Jamaa huyu hakuwa anajua hata anafanya nini alidhani kile alichofanya ni cha maana sana kumbe mhh!!!!!!!!!
 
Hakuna maisha yasiokua na changamoto. Kuna siku nilikua nasikiliza wimbo wa chaguo lako mpaka nikachoka. Ni chaguo lako mzee cha msingi mpotezee kwa kitambo mpaka mwenyewe ajione useless. Mwambie achague kani ya kanisa au wewe. Kila kitu too much is harmful lakini kubadili naona ni shida maana ni bora mtu uliemzoea kuliko kuanza na mtu mpya darasa la kwanza au chekechea. Fikiria pia shida atayopata mtoto wako kwa sababu ya hayo matatizo yenu. Mimi naona bora kama ndoa imekushinda ni bora usioe kabisa lakini kuoa tena naona kama ni sawa na mtu alifika chuo kikuu kurudi tena chekechea.

Hao wazazi busara zero, lakini mzee ukikumbatia sana wazazi wa mkeo watakuletea shida. Inatakiwa kuwe na kaumbali kidogo wawe na kaheshima kidogo. Maana wasijeona kama walikupa binti yao kwa kukupendelea wakati mabinti wamejaa huko mtaani wanatafuta ndoa. Inabidi uwe mkali usiingilie maisha yao nao waheshimu serikali yako.




Miezi miwili iliyopita nilipelekwa polisi na wazazi wa mke wangu, kwa kosa la kumpiga binti yao karibu nimuue, ndugu walikuja kunitoa

Iko hivi;
Huyu binti nilimuoa miaka miwili iliyopita na tuna mtoto mmoja, yeye na wazazi wake wote wameokoka, Hivi sasa naweza kusema kwamba mke wangu ameolewa na kanisa na si mimi.

Akitoka kazini saa kumi na moja jioni anakwenda kwenye maombi kanisani hadi saa tatu , na hii ratiba ni kila siku Monday to Friday, Jumamosi pia wanakwenda Jumapili ni kutwa nzima, wakati mwingine kuna mkesha katikati ya wiki, hali hii, imefanya ashindwe hata kupataa muda wa kumlea mtoto wetu wa mwaka alielazimika kumwachisha ziwa akiwa na miezi mitatu kutokana kubanwa na mambo ya kanisa.

Mtoto huyu ni kama amebadilishiwa mama, maana sasa analelewa na house girl wetu kwa hali na Mali
Ilifika pahala nikashindwa kuvumilia hali hii na nikamuita na kumueleza hali halisi na kumtaka abadilishe ratiba zake, akadai kwamba hana jinsi kwa kua ratiba ya kanisa kwake haina substitute , nikamwambia ni amri sio ombi

Akaendelea hivyo hivyo, kwa Mara ya kwanza nilimpa kipigo kwa kukaidi amri yangu, niliendelea kumpiga mara kwa Mara sababu ikiwa ni kanisa, kila tunapoitwa kusuluhishwa wazazi wake humtetea na kudai walikosea kunipa mm binti yao, ikawa tunagombana na wazazi wake vikaoni hadi nikaamua kuachana na vikao.

Mwanzoni mwa mwezi wa sita alidai kuna mkesha wa maombi siku hiyo na hivyo atalala huko, nikamwambia ukitoka huko utafute nyumba nyingine, baadae mama yake akanipigia kwamba kuna mkesha hivyo wote watalala church kwenye mkesha, nikamjibu haiwezekani wamruhusu wife arudi kwa kuwa ana mtoto mdogo, akakata simu

Kweli, wife hakurudi, ila kila saa alikua akinipigia simu karibu usiku kucha nami sikua napokea naiangalia tu hadi inakatika hadi saa kumi alfajiri, alikuja amesindikizwa na dada yake maana walijua nimekasirika sana

Walipofika tu niliwakamata wote wawili na kuwapa kipigo kizito sana hadi wife kuzirai, dada mtu aliniponyoka na kukimbilia main road huku nikiwa nimemtengua mbavu akapanda boda boda, saa moja wazazi wa wife wakaja nilikua nimemfungia stoo wakamchukua wakaenda nae.

Baadae wakanifuata kazini na polisi wakaniweka ndani kwa shambulio la kudhuru mwili, nilitoka kesho yake , kesi ikahamia Ustawi wa Jamii tuliitwa pale, mbele ya wazee wa pande zote, ikaamriwa kwamba binti arudi kwa wazazi wake hadi hapo baadae hali ikiwa nzuri, ila wazazi wake wakasema wanamchukua kimoja hawanihitaji tena, kwamba nisubiri taratibu za talaka, nikasema haina shida nipo tayari, tukaja nyumbani wakamchukua mtoto na hg na nguo zake wakarudi kwao

Nimeyasahau hayo naishi kwa auheni kiasi kwa sasa Ingawa bado nina msongo, surprisingly Friday wife akanifuata kazini hatukua tumeonana for two months, roho yangu iliingia kitu flani hata mtoto wangu sikutaka hata kuwa naenda kumuona ingawa pale ustawi wa jamii niliruhusiwa

Wife akaniomba tuongee, akasema anahitaji turudiane, akadai anaomba arudi home kwangu hata kesho yake ikiwezekana, kwamba ananipenda, kwamba tutarekebisha tu, nikamwambia haiwezekani simtaki tena

Wadau wana Jf, nimemwambia atafute Mme mwingine kanisani kwao ndo watawezana na sio Mimi, mke wa hivi hanifai, hata mshahara wote anapeleka huko, hilo kanisa Jumapili moja tu kuna sadaka kama 12 hivi tangu asubuhi hadi jioni, unaweza kwenda na laki mbili usirudi hata na shilingi jioni, bado katikati ya wiki, halafu wachungaji wanaishi kifajari.

Huyo mchungaji wa hilo kanisa ameshawateka akili, mimi binafsi nilikua huko nikahama kutokana na hiyo biashara ya kutakiwa kushinda huko 24/7 na pia kutumia sehemu kubwa ya mapato yangu kanisani badala ya kujenga familia, kanisa gani wanaomba hadi salary slip? Na usipowapa watakusema sana kwamba umepotea njia na kadhalika
Kanisa gani halijali ndoa za watu?

Sio kwamba sipendi mke wangu aende kanisani, aende kwa kiasi na ratiba akizingatia kuwa yeye ni mama wa familia, inapaswa kwenda kanisani unashiriki na wenzako mchana au jioni unarudi home, jumatano unakwenda kwa maombi masaa mawili, six jioni unarudi kwako, there will be nothing wrong, lakini huwezi kwenda kushinda huko 24/7. Seven days a week, inakuja kweli hiyo?

Hata dada wa mke wangu niliempiga, mumewe pia alikuja kwangu na malalamiko kama haya ya kwangu, nimeamua simtaki tena, kwanza akili yangu imeshachanganyikiwa,
Nonsense

Ni bora nirudi kwa Rachel, alinivumilia tangu chuo hadi mtaani nikamtendea vibaya nikaoa mlokole nisiemjua, kwa kweli najuta sikujua nachofanya.
 
Kaka pga chini na kupunguza mawazo kuna vtu vng vya kufanya wal c kuwaza mwanamke ambae hajitambui kama huyo
 
Back
Top Bottom