Najuta kuoa mwanamke mlokole

Najuta kuoa mwanamke mlokole

Msafara wa mamba na kenge wamo, sasa wengi huenda kwakina kenge, kuna kanisa moja mchungaji huwafukuza watu waende nyumbani yeye hafugi watu ibada ikiisha watu warudi majumban
Kweli...hawawezi wote wakawa wabaya..lakini Wewe unaafiki afanyayo mchungaji wa kanisa hili?..mpaka kufikia hatua yakutaka kuvunja ndoa za waumi

Mimi Kuna wachungaji huwa nawasilisha kabisa japokua Mimi Ni Muisilamu.... Nasikiliza mahubiri yao.
 
mwanaume kamili hapigi mke wala kulalamika. kama mtu anazingua unachukua njia yako. sioni hata haja ya kuwasema mabinti wa kilokole kwa sababu hukulazimishwa kuwa naye. kama na ameona mchungaji wake ni wa maana kuliko wewe chukua maamuzi magumu au mlowase. pia kuna ulokole na ugonjwa. ulokole hausemi mtu aharibu ndoa yake. hizo ni Imani za watu wasiojua wanachofanya. pia kisheria ukimuachisha mtoto maziwa kabla ya miezi sita unaharibu ubongo na kinga yake.
pia ungeenda kuongea na mchungaji wake. sio ustaarabu kupiga mke ambaye hulingani naye nguvu. pia hata wewe unaoneka una wenge jingi maana umempiga mke wako na kuja kumangaza hapa jf wakati yeye hawezi kujitetea. unapomsema mtu hakikisha naye yupo na anaweza kujitetea kama wewe. pia kwangu sioni tija ya ulichofanya hapa. mahusiano sio jela. mtu akizingua unajiachia kivyakooo
Tatz mnakuwaga wabishi mpaka yawakute bnafsi niliwahi kuwa na mwanamke wa dizaini hii inahitaji moyo kuvumlia daily kanisani wachaa niishie apa
 
Channel ya Mwalimu Mwakasege huko Telegram baada ya kufunga magroup yote ya WhatsApp

 
Miezi miwili iliyopita nilipelekwa polisi na wazazi wa mke wangu, kwa kosa la kumpiga binti yao karibu nimuue, ndugu walikuja kunitoa

Iko hivi;
Huyu binti nilimuoa miaka miwili iliyopita na tuna mtoto mmoja, yeye na wazazi wake wote wameokoka, Hivi sasa naweza kusema kwamba mke wangu ameolewa na kanisa na si mimi.

Akitoka kazini saa kumi na moja jioni anakwenda kwenye maombi kanisani hadi saa tatu , na hii ratiba ni kila siku Monday to Friday, Jumamosi pia wanakwenda Jumapili ni kutwa nzima, wakati mwingine kuna mkesha katikati ya wiki, hali hii, imefanya ashindwe hata kupataa muda wa kumlea mtoto wetu wa mwaka alielazimika kumwachisha ziwa akiwa na miezi mitatu kutokana kubanwa na mambo ya kanisa.

Mtoto huyu ni kama amebadilishiwa mama, maana sasa analelewa na house girl wetu kwa hali na Mali
Ilifika pahala nikashindwa kuvumilia hali hii na nikamuita na kumueleza hali halisi na kumtaka abadilishe ratiba zake, akadai kwamba hana jinsi kwa kua ratiba ya kanisa kwake haina substitute , nikamwambia ni amri sio ombi

Akaendelea hivyo hivyo, kwa Mara ya kwanza nilimpa kipigo kwa kukaidi amri yangu, niliendelea kumpiga mara kwa Mara sababu ikiwa ni kanisa, kila tunapoitwa kusuluhishwa wazazi wake humtetea na kudai walikosea kunipa mm binti yao, ikawa tunagombana na wazazi wake vikaoni hadi nikaamua kuachana na vikao.

Mwanzoni mwa mwezi wa sita alidai kuna mkesha wa maombi siku hiyo na hivyo atalala huko, nikamwambia ukitoka huko utafute nyumba nyingine, baadae mama yake akanipigia kwamba kuna mkesha hivyo wote watalala church kwenye mkesha, nikamjibu haiwezekani wamruhusu wife arudi kwa kuwa ana mtoto mdogo, akakata simu

Kweli, wife hakurudi, ila kila saa alikua akinipigia simu karibu usiku kucha nami sikua napokea naiangalia tu hadi inakatika hadi saa kumi alfajiri, alikuja amesindikizwa na dada yake maana walijua nimekasirika sana

Walipofika tu niliwakamata wote wawili na kuwapa kipigo kizito sana hadi wife kuzirai, dada mtu aliniponyoka na kukimbilia main road huku nikiwa nimemtengua mbavu akapanda boda boda, saa moja wazazi wa wife wakaja nilikua nimemfungia stoo wakamchukua wakaenda nae.

Baadae wakanifuata kazini na polisi wakaniweka ndani kwa shambulio la kudhuru mwili, nilitoka kesho yake , kesi ikahamia Ustawi wa Jamii tuliitwa pale, mbele ya wazee wa pande zote, ikaamriwa kwamba binti arudi kwa wazazi wake hadi hapo baadae hali ikiwa nzuri, ila wazazi wake wakasema wanamchukua kimoja hawanihitaji tena, kwamba nisubiri taratibu za talaka, nikasema haina shida nipo tayari, tukaja nyumbani wakamchukua mtoto na hg na nguo zake wakarudi kwao

Nimeyasahau hayo naishi kwa auheni kiasi kwa sasa Ingawa bado nina msongo, surprisingly Friday wife akanifuata kazini hatukua tumeonana for two months, roho yangu iliingia kitu flani hata mtoto wangu sikutaka hata kuwa naenda kumuona ingawa pale ustawi wa jamii niliruhusiwa

Wife akaniomba tuongee, akasema anahitaji turudiane, akadai anaomba arudi home kwangu hata kesho yake ikiwezekana, kwamba ananipenda, kwamba tutarekebisha tu, nikamwambia haiwezekani simtaki tena

Wadau wana Jf, nimemwambia atafute Mme mwingine kanisani kwao ndo watawezana na sio Mimi, mke wa hivi hanifai, hata mshahara wote anapeleka huko, hilo kanisa Jumapili moja tu kuna sadaka kama 12 hivi tangu asubuhi hadi jioni, unaweza kwenda na laki mbili usirudi hata na shilingi jioni, bado katikati ya wiki, halafu wachungaji wanaishi kifajari.

Huyo mchungaji wa hilo kanisa ameshawateka akili, mimi binafsi nilikua huko nikahama kutokana na hiyo biashara ya kutakiwa kushinda huko 24/7 na pia kutumia sehemu kubwa ya mapato yangu kanisani badala ya kujenga familia, kanisa gani wanaomba hadi salary slip? Na usipowapa watakusema sana kwamba umepotea njia na kadhalika
Kanisa gani halijali ndoa za watu?

Sio kwamba sipendi mke wangu aende kanisani, aende kwa kiasi na ratiba akizingatia kuwa yeye ni mama wa familia, inapaswa kwenda kanisani unashiriki na wenzako mchana au jioni unarudi home, jumatano unakwenda kwa maombi masaa mawili, six jioni unarudi kwako, there will be nothing wrong, lakini huwezi kwenda kushinda huko 24/7. Seven days a week, inakuja kweli hiyo?

Hata dada wa mke wangu niliempiga, mumewe pia alikuja kwangu na malalamiko kama haya ya kwangu, nimeamua simtaki tena, kwanza akili yangu imeshachanganyikiwa,
Nonsense

Ni bora nirudi kwa Rachel, alinivumilia tangu chuo hadi mtaani nikamtendea vibaya nikaoa mlokole nisiemjua, kwa kweli najuta sikujua nachofanya.
Pole sana mkuu naona ulikurupuka na ndo ujue sasa kwamba sio kila aitae bwana atarithi ufalme wa Mungu
 
Kweli...hawawezi wote wakawa wabaya..lakini Wewe unaafiki afanyayo mchungaji wa kanisa hili?..mpaka kufikia hatua yakutaka kuvunja ndoa za waumi

Mimi Kuna wachungaji huwa nawasilisha kabisa japokua Mimi Ni Muisilamu.... Nasikiliza mahubiri yao.
Kufikia kuwashindisha watu kanisani hapana, mie mwenyewe nikiwa kanisani muda ukipita wakawaida hukosa amani kabisa , sipendi imani yangu kumkwaza mwingine, habari za mikesha nawaachia huko wengine, ndiyo maana Bible inasema mtumikie MUNGU ungali kijana ukiingia maisha ya ndoa mmm nimtihani mwingine!
 
Back
Top Bottom