Najuta kuoa mwanamke mlokole

Najuta kuoa mwanamke mlokole

But life is a very interesting game, MTU akioa mke anayetulia home analalamika oo mywifewangu golikipaflan ivi, kujibwetekea sake home, akioa mcharuko basi kila siku analalama kaibiwa, akioa chapombe basi ndo usiseme, akioa mfanyakazi analalamika all time yuko ofisini, wengi humu vihoro juu wakihofia wake zao kuchepukia kwa mabosi wao.

Basi Dunia vurugu, ukioa mpenda Dini ndo hivi Tena. Kwanini mnaoa si mkae tu msioe.?

Haya mambo we yasikie kwa mwenzako tu kaka
 
Mfyuuuuuuuu dume zima utajisifiaje kumpiga mke???
Wakati unamuoa hukujua ni mlokole

Yaani wewe ufungwe tu
 
But life is a very interesting game, MTU akioa mke anayetulia home analalamika oo mywifewangu golikipaflan ivi, kujibwetekea sake home, akioa mcharuko basi kila siku analalama kaibiwa, akioa chapombe basi ndo usiseme, akioa mfanyakazi analalamika all time yuko ofisini, wengi humu vihoro juu wakihofia wake zao kuchepukia kwa mabosi wao.

Basi Dunia vurugu, ukioa mpenda Dini ndo hivi Tena. Kwanini mnaoa si mkae tu msioe.?
kila kitu kwa kiasi amesema hapingi yeye kusali lakini kusali kusifanye ukose muda wa kukaa na family
 
Mpaka sasa umesha control situation kwa 75%.
Huna haraka. Mpe second chance yenye masharti makali. Sharti namba moja ni kuwa asiende tena kwenye hilo kanisa. Sharti la pili ni kuwa asitumie zaidi ya masaa 3 kanisani kwa wiki. Yani kwa siku zote za wiki akijumuisha mda aliokaa kanisani usizidi masaa 3. Na uwe kati ya saa 2 asbh na saa 10 jioni...

Na kuwa utamrudishia uhuru wake wa kutumia muda kanisani baadae
 
Mimi nakuahauri msamehe mrudiane ila kwa mikakati m ipya na makubaliano maalumu!
 
Vijana wa siku hizi wanasema.

"Temana naye."
 
Miezi miwili iliyopita nilipelekwa polisi na wazazi wa mke wangu, kwa kosa la kumpiga binti yao karibu nimuue, ndugu walikuja kunitoa

Iko hivi;
Huyu binti nilimuoa miaka miwili iliyopita na tuna mtoto mmoja, yeye na wazazi wake wote wameokoka, Hivi sasa naweza kusema kwamba mke wangu ameolewa na kanisa na si mimi.

Akitoka kazini saa kumi na moja jioni anakwenda kwenye maombi kanisani hadi saa tatu , na hii ratiba ni kila siku Monday to Friday, Jumamosi pia wanakwenda Jumapili ni kutwa nzima, wakati mwingine kuna mkesha katikati ya wiki, hali hii, imefanya ashindwe hata kupataa muda wa kumlea mtoto wetu wa mwaka alielazimika kumwachisha ziwa akiwa na miezi mitatu kutokana kubanwa na mambo ya kanisa.

Mtoto huyu ni kama amebadilishiwa mama, maana sasa analelewa na house girl wetu kwa hali na Mali
Ilifika pahala nikashindwa kuvumilia hali hii na nikamuita na kumueleza hali halisi na kumtaka abadilishe ratiba zake, akadai kwamba hana jinsi kwa kua ratiba ya kanisa kwake haina substitute , nikamwambia ni amri sio ombi

Akaendelea hivyo hivyo, kwa Mara ya kwanza nilimpa kipigo kwa kukaidi amri yangu, niliendelea kumpiga mara kwa Mara sababu ikiwa ni kanisa, kila tunapoitwa kusuluhishwa wazazi wake humtetea na kudai walikosea kunipa mm binti yao, ikawa tunagombana na wazazi wake vikaoni hadi nikaamua kuachana na vikao.

Mwanzoni mwa mwezi wa sita alidai kuna mkesha wa maombi siku hiyo na hivyo atalala huko, nikamwambia ukitoka huko utafute nyumba nyingine, baadae mama yake akanipigia kwamba kuna mkesha hivyo wote watalala church kwenye mkesha, nikamjibu haiwezekani wamruhusu wife arudi kwa kuwa ana mtoto mdogo, akakata simu

Kweli, wife hakurudi, ila kila saa alikua akinipigia simu karibu usiku kucha nami sikua napokea naiangalia tu hadi inakatika hadi saa kumi alfajiri, alikuja amesindikizwa na dada yake maana walijua nimekasirika sana

Walipofika tu niliwakamata wote wawili na kuwapa kipigo kizito sana hadi wife kuzirai, dada mtu aliniponyoka na kukimbilia main road huku nikiwa nimemtengua mbavu akapanda boda boda, saa moja wazazi wa wife wakaja nilikua nimemfungia stoo wakamchukua wakaenda nae.

Baadae wakanifuata kazini na polisi wakaniweka ndani kwa shambulio la kudhuru mwili, nilitoka kesho yake , kesi ikahamia Ustawi wa Jamii tuliitwa pale, mbele ya wazee wa pande zote, ikaamriwa kwamba binti arudi kwa wazazi wake hadi hapo baadae hali ikiwa nzuri, ila wazazi wake wakasema wanamchukua kimoja hawanihitaji tena, kwamba nisubiri taratibu za talaka, nikasema haina shida nipo tayari, tukaja nyumbani wakamchukua mtoto na hg na nguo zake wakarudi kwao

Nimeyasahau hayo naishi kwa auheni kiasi kwa sasa Ingawa bado nina msongo, surprisingly Friday wife akanifuata kazini hatukua tumeonana for two months, roho yangu iliingia kitu flani hata mtoto wangu sikutaka hata kuwa naenda kumuona ingawa pale ustawi wa jamii niliruhusiwa

Wife akaniomba tuongee, akasema anahitaji turudiane, akadai anaomba arudi home kwangu hata kesho yake ikiwezekana, kwamba ananipenda, kwamba tutarekebisha tu, nikamwambia haiwezekani simtaki tena

Wadau wana Jf, nimemwambia atafute Mme mwingine kanisani kwao ndo watawezana na sio Mimi, mke wa hivi hanifai, hata mshahara wote anapeleka huko, hilo kanisa Jumapili moja tu kuna sadaka kama 12 hivi tangu asubuhi hadi jioni, unaweza kwenda na laki mbili usirudi hata na shilingi jioni, bado katikati ya wiki, halafu wachungaji wanaishi kifajari.

Huyo mchungaji wa hilo kanisa ameshawateka akili, mimi binafsi nilikua huko nikahama kutokana na hiyo biashara ya kutakiwa kushinda huko 24/7 na pia kutumia sehemu kubwa ya mapato yangu kanisani badala ya kujenga familia, kanisa gani wanaomba hadi salary slip? Na usipowapa watakusema sana kwamba umepotea njia na kadhalika
Kanisa gani halijali ndoa za watu?

Sio kwamba sipendi mke wangu aende kanisani, aende kwa kiasi na ratiba akizingatia kuwa yeye ni mama wa familia, inapaswa kwenda kanisani unashiriki na wenzako mchana au jioni unarudi home, jumatano unakwenda kwa maombi masaa mawili, six jioni unarudi kwako, there will be nothing wrong, lakini huwezi kwenda kushinda huko 24/7. Seven days a week, inakuja kweli hiyo?

Hata dada wa mke wangu niliempiga, mumewe pia alikuja kwangu na malalamiko kama haya ya kwangu, nimeamua simtaki tena, kwanza akili yangu imeshachanganyikiwa,
Nonsense

Ni bora nirudi kwa Rachel, alinivumilia tangu chuo hadi mtaani nikamtendea vibaya nikaoa mlokole nisiemjua, kwa kweli najuta sikujua nachofanya.
Hahahaaa hayo ndo malipo ya kumtenda ubaya Rachel.Mkipataga wanawake wapya mnakuwaga na maneno ya shombo. Mwenyewe ulidhani umepata kumbe umepatikana.
 
Pole sana.Hakika kweli umechanganyikiwa.kama imefikia stage hata mwanao huna huruma nae.
 
Ndoa za Kikristo hazina TALAKA labda kwa wachungaji uchwara pekee!
Kama amejirudi yeye mwenyewe mpokee ila kwa sharti la kusali weekend tu na kutoshiriki mikesha.
Waweza kumbadilishia kanisa pia maana makanisa ya kilokole yapo mengi bila shaka.
 
ulikosea kumpiga. why?
sio kila kanisa wanamuabudu MUNGU wa kweli. mengine ni makanisa ya shetani. (ndoa na iheshimiwe na watu wote)
mkeo amesahau kuwa "watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa"
 
Pole sanaa Bro. Nakuelewa sanaaa. Hawa walokole wanashida sanaaa. Huyo mkeo ana elimu gan ??

Kuna watu shule haijawakomboa kabisaa.
 
Pole sana ndugu yangu. Kimsingi kama unavomwona anakukosea, ujue naye anakuona umepotoka, na sababu kubwa ni kwamba mnatumikia mabwana wawili tofauti hivyo ni lazima utumishi utofautiane, ratiba zitofautiane, mitazamo itofautiane........... nk.
Neno linasema watu wawili hawawezi tembea pamoja wasipopatana. Anyway.... binafsi najua na nimepitia changamoto kama zako, lakini nimeamua kuvumilia tu nikiamini bado Mungu anayomipango bora kwangu na kwa mke wangu.
Ushauri wa bure kwenu ambao hamjaoa/ kuolewa: kuoa/ kuolewa na mtu asiye wa imani yako, utakuja kujuta. Najua wengine mpo mbioni kuoa/ kuolewa na watu wa imani tofauti, na huenda usinielewe ninachokisema hapa, au alichosema mtoa mada. Ndugu nawasihi mtafakari upya uamuzi huo. Usiombe kuwa mhanga, wacha tu uyasikie.
 
aliyeleta ulokole duniani alikosea Sana, tatizo kubwa linalonkera kuhusu wao ni viburi na kujiona wamemaliza kila kitu
yani Walokole wana maudhiiiiiiii uwiii!!
 
Brother pole sana najua unapitia kipindi kigumu sana hasa kwa kuwa binadamu yeyote hupenda kwenda kwa mipango.Jambo moja napenda kujua kutoka kwako je wampenda kwa dhati au unasubiria kupata sababu ya kumwacha kama bado unampenda mpe nafasi ongea naye kwa upendo ukimweleza tatizo la kanisa hilo bila kutumia hasira na ukiweza mkae sehemu nzuri mkiwa na mtoto wenu sehemu tulivu,ongea taratibu na kwa kina naamini atajirudi zaidi ya yote hata ukimwacha haitasaidia kama ulimpenda kwa dhati.Pole sana
 
Usiseme walokole. Ni akili ya mtu tu. Kama ameokoka na hatunzi familia biblia inasema huyo ni mbaya kuliko yule asieamini uwepo wa Mungu. Rudiana nae ili mtoto asidhurike na matatizo yenu ila mpe masharti ya kutokaa kanisani siku nzima. Aende kwa kiasi khaaa na pengine uchunguze hilo kanisa sio bure huduma kam hizo za kukaa siku nzima ni za vijana...na si wamama wala wababa...Pole sana kwa hilo mkuu. Rudisha moyo.
 
Back
Top Bottom