Najuta kuoa mwanamke mlokole

Najuta kuoa mwanamke mlokole

Hilo swala ni gumu kiasi ila linaweza kusuluhishika bila ya kuachana......

Kwanza,kaa chini tafakari kwa kina jinsi ulivyotoka mbali na mkeo huyo ambae ni zawadi kutoka kwa mungu paka kufikia hatua hiyo....

Pili hata siku moja usije kulaumu kwa mwenyezi mungu eti umeoa mke mlokole ni kosa kubwa, usirudie tena

Kaa chini jipange kuwa na mazungumzo ya familia ya pande mbili wazaz wa mkeo na wazaziwako, pia viongoz wa din wa upande wa mkeo mtafakari kwa kina juu ya swala husika...nadhani mnaweza kufikia suluhisho ambalo litasaidia....

Pia wewe mwenyewe kaa chini ongea na mke wako kwa upole, USIRUDIE KUMPIGA MKE WAKO, HILO NI KOSA KUBWA KULIKO ALILOANYA MKEO..

Cha muhimu tafakar zaidi njia ya kutatua bila ya kuwaza kuvunja ndoa......
 
Pole sana mkuu,
Kama wife wako ametambua kosa lake na amekubali mrudiane, kwa masilahi ya watoto unaweza bado kumpa nafasi nyingine. Hata hivyo ni lazima hiyo nafasi nyingine iendane na mashariti. Maadam tatizo lake ni kushinda kanisani, inabidi umwambie yeye mwenyewe aeleze mkakati wake namna ambavyo amejipanga kupuguza vipindi vya kwenda kanisani, na kama inawezekana aweke kwenye maandishi. Ikitokea amekiuka na kurudia Enzi zake za kushinda kanisani kila siku utalazimika kufanya maamuzi magumu! lakini siyo kumpiga!

Husiendekeze kumpiga mkeo mpaka anazimia maana kuna siku utaua na kuishia kunyea ndoo wakati wanao wanateseka. Ikishindikana kabisa kuvumiliana, talaka is the best solution kuliko kipigo!
 
Miezi miwili iliyopita nilipelekwa polisi na wazazi wa mke wangu, kwa kosa la kumpiga binti yao karibu nimuue, ndugu walikuja kunitoa

Iko hivi;
Huyu binti nilimuoa miaka miwili iliyopita na tuna mtoto mmoja, yeye na wazazi wake wote wameokoka, Hivi sasa naweza kusema kwamba mke wangu ameolewa na kanisa na si mimi.

Akitoka kazini saa kumi na moja jioni anakwenda kwenye maombi kanisani hadi saa tatu , na hii ratiba ni kila siku Monday to Friday, Jumamosi pia wanakwenda Jumapili ni kutwa nzima, wakati mwingine kuna mkesha katikati ya wiki, hali hii, imefanya ashindwe hata kupataa muda wa kumlea mtoto wetu wa mwaka alielazimika kumwachisha ziwa akiwa na miezi mitatu kutokana kubanwa na mambo ya kanisa.

Mtoto huyu ni kama amebadilishiwa mama, maana sasa analelewa na house girl wetu kwa hali na Mali
Ilifika pahala nikashindwa kuvumilia hali hii na nikamuita na kumueleza hali halisi na kumtaka abadilishe ratiba zake, akadai kwamba hana jinsi kwa kua ratiba ya kanisa kwake haina substitute , nikamwambia ni amri sio ombi

Akaendelea hivyo hivyo, kwa Mara ya kwanza nilimpa kipigo kwa kukaidi amri yangu, niliendelea kumpiga mara kwa Mara sababu ikiwa ni kanisa, kila tunapoitwa kusuluhishwa wazazi wake humtetea na kudai walikosea kunipa mm binti yao, ikawa tunagombana na wazazi wake vikaoni hadi nikaamua kuachana na vikao.

Mwanzoni mwa mwezi wa sita alidai kuna mkesha wa maombi siku hiyo na hivyo atalala huko, nikamwambia ukitoka huko utafute nyumba nyingine, baadae mama yake akanipigia kwamba kuna mkesha hivyo wote watalala church kwenye mkesha, nikamjibu haiwezekani wamruhusu wife arudi kwa kuwa ana mtoto mdogo, akakata simu

Kweli, wife hakurudi, ila kila saa alikua akinipigia simu karibu usiku kucha nami sikua napokea naiangalia tu hadi inakatika hadi saa kumi alfajiri, alikuja amesindikizwa na dada yake maana walijua nimekasirika sana

Walipofika tu niliwakamata wote wawili na kuwapa kipigo kizito sana hadi wife kuzirai, dada mtu aliniponyoka na kukimbilia main road huku nikiwa nimemtengua mbavu akapanda boda boda, saa moja wazazi wa wife wakaja nilikua nimemfungia stoo wakamchukua wakaenda nae.

Baadae wakanifuata kazini na polisi wakaniweka ndani kwa shambulio la kudhuru mwili, nilitoka kesho yake , kesi ikahamia Ustawi wa Jamii tuliitwa pale, mbele ya wazee wa pande zote, ikaamriwa kwamba binti arudi kwa wazazi wake hadi hapo baadae hali ikiwa nzuri, ila wazazi wake wakasema wanamchukua kimoja hawanihitaji tena, kwamba nisubiri taratibu za talaka, nikasema haina shida nipo tayari, tukaja nyumbani wakamchukua mtoto na hg na nguo zake wakarudi kwao

Nimeyasahau hayo naishi kwa auheni kiasi kwa sasa Ingawa bado nina msongo, surprisingly Friday wife akanifuata kazini hatukua tumeonana for two months, roho yangu iliingia kitu flani hata mtoto wangu sikutaka hata kuwa naenda kumuona ingawa pale ustawi wa jamii niliruhusiwa

Wife akaniomba tuongee, akasema anahitaji turudiane, akadai anaomba arudi home kwangu hata kesho yake ikiwezekana, kwamba ananipenda, kwamba tutarekebisha tu, nikamwambia haiwezekani simtaki tena

Wadau wana Jf, nimemwambia atafute Mme mwingine kanisani kwao ndo watawezana na sio Mimi, mke wa hivi hanifai, hata mshahara wote anapeleka huko, hilo kanisa Jumapili moja tu kuna sadaka kama 12 hivi tangu asubuhi hadi jioni, unaweza kwenda na laki mbili usirudi hata na shilingi jioni, bado katikati ya wiki, halafu wachungaji wanaishi kifajari.

Huyo mchungaji wa hilo kanisa ameshawateka akili, mimi binafsi nilikua huko nikahama kutokana na hiyo biashara ya kutakiwa kushinda huko 24/7 na pia kutumia sehemu kubwa ya mapato yangu kanisani badala ya kujenga familia, kanisa gani wanaomba hadi salary slip? Na usipowapa watakusema sana kwamba umepotea njia na kadhalika
Kanisa gani halijali ndoa za watu?

Sio kwamba sipendi mke wangu aende kanisani, aende kwa kiasi na ratiba akizingatia kuwa yeye ni mama wa familia, inapaswa kwenda kanisani unashiriki na wenzako mchana au jioni unarudi home, jumatano unakwenda kwa maombi masaa mawili, six jioni unarudi kwako, there will be nothing wrong, lakini huwezi kwenda kushinda huko 24/7. Seven days a week, inakuja kweli hiyo?

Hata dada wa mke wangu niliempiga, mumewe pia alikuja kwangu na malalamiko kama haya ya kwangu, nimeamua simtaki tena, kwanza akili yangu imeshachanganyikiwa,
Nonsense

Ni bora nirudi kwa Rachel, alinivumilia tangu chuo hadi mtaani nikamtendea vibaya nikaoa mlokole nisiemjua, kwa kweli najuta sikujua nachofanya.

najaribu kutafakari, kama sio wazee wa SHIKA NENO-TENDA NENO sijui.
 
Pole sana.
Either nawe uokoke au urudi kwa Rachel.
 
ha haha ha kauli zako SITAKI MWANAMKE ANAYEKAA BAR.... SITAKI MWANAMKE ASIYEMJUA MUNGU.... SITAKI MWANAMKE ASIYEENDA KANISANI..... nina uhakika katika maombi yako uliweka hayo kipao mbele he he he he hehe uuuuuuu nimecheka kuna mmoja hapa kitaaa atakuja na malalamiko zaidi ya ya kwako....

kwa kuwa umeamua kumwacha we mwache na kama anataka kurudiana na wewe aisee mbona bible inaeleza vyema kwamaba mtaachana na wazazi na kuambatana na mkeo,.... waazi wa mkeo na mkeo nawasi wasi nahilo kanisa wanalosali kuna jambo halipo sawa aisee........ kama unaona anafuata matwaka ya wazazi wake ujue hakujua maana ya ndoa aua anajua maana ya ndoa lakini ameamua kukaidi na kuendelea na wazazi....MWAMBIE AAMUE MOJA WAZAZI AU WEWE KAMA NI WAZAZI BASI SAWA
 
Enyway umeongea upande mmoja Wa shilingi, yaani upande wako, but hatujui upande wake anasemaje kwa yote hayo. Kama sio tungo basi ujue hapo ulifanya inshu mbaya.

Mambo ya dini kwa wenye dini zao, ukute angeolewa na MTU Wa sampuli yake muda wote wangekuwa huko kwenye misa.

Wewe unaoa mtu Wa misa ilihali wewe si MTU Wa misa wapi na wapi..!

Wawe kwenye Misa muda wote!? Kwani huko wanapewa mishahara!
 
Pole mkuu huyo ni mke wa kanisa sio wako, muepuke maana anaonekana atakusumbua yeye na wazazi wake
 
hawa kina rachel inaonekana ni watamu sana ila huwa wanachesewa na kuachwa.
huyu mtu wa tatu analeta na mkewe na kuona bora angemuoa rachel.
hata mimi nishawahi pita na rachel alikuwa mtamu balaaaa!!!
 
huwa nashangaa inakuwaje mtu unalaghaika na kanisa kiasi hicho. na wapo wengi wa hivyo, wake kwa waume.

eti unaambiwa upande mbegu hahahaaaa. si bora hiyo hela ukamsaidie muhitaji mtaani? nitatoa hela nikipenda na si kwa mtu kunishinikiza.

mkeo yuko kwenye kifungo cha imani ya hilo kanisa. kutoka huko ni kazi sana. inahitajika neema ya Mungu
 
Acha kumshauri vibaya mwenzako,
Kwanini amle housegirl? ?

anaweza akachagua mwingine badala ya hg, maneno yangu sio sheria, ila maisha mafupi sana haya usikubali mtu akupe stress
 
achene kulaumu watumishi wa Mungu wakati hata hamjui ukweli wa makanisa na kazi inayofanyika huko. wengi makanisa yenu ni JF, facebook nk. jamaa kasema yeye tu lakini hatujamsia mke wake na mnaanza kuhukumu makanisa kuwa yanaharibu watu. pia kanisani kuna sera ambayo sio rasmi. oeni wa kwenu maana mnajuana vizuri. wewe ukiwa mlokole ukaoa mkarismatic lazima kuna mambo mpishane hasa hisia zinapoanza kukata na kuanza kujitambua kama umeharisha njea ya shimo la choona maji yamekatika. ndoa sio dharura na wala sio kitu cha kukimbilia kama hujakuwa na uhakika

dini imekuwa mradi wa watu siku hizi.
 
Miezi miwili iliyopita nilipelekwa polisi na wazazi wa mke wangu, kwa kosa la kumpiga binti yao karibu nimuue, ndugu walikuja kunitoa

Iko hivi;
Huyu binti nilimuoa miaka miwili iliyopita na tuna mtoto mmoja, yeye na wazazi wake wote wameokoka, Hivi sasa naweza kusema kwamba mke wangu ameolewa na kanisa na si mimi.

Akitoka kazini saa kumi na moja jioni anakwenda kwenye maombi kanisani hadi saa tatu , na hii ratiba ni kila siku Monday to Friday, Jumamosi pia wanakwenda Jumapili ni kutwa nzima, wakati mwingine kuna mkesha katikati ya wiki, hali hii, imefanya ashindwe hata kupataa muda wa kumlea mtoto wetu wa mwaka alielazimika kumwachisha ziwa akiwa na miezi mitatu kutokana kubanwa na mambo ya kanisa.

Mtoto huyu ni kama amebadilishiwa mama, maana sasa analelewa na house girl wetu kwa hali na Mali
Ilifika pahala nikashindwa kuvumilia hali hii na nikamuita na kumueleza hali halisi na kumtaka abadilishe ratiba zake, akadai kwamba hana jinsi kwa kua ratiba ya kanisa kwake haina substitute , nikamwambia ni amri sio ombi

Akaendelea hivyo hivyo, kwa Mara ya kwanza nilimpa kipigo kwa kukaidi amri yangu, niliendelea kumpiga mara kwa Mara sababu ikiwa ni kanisa, kila tunapoitwa kusuluhishwa wazazi wake humtetea na kudai walikosea kunipa mm binti yao, ikawa tunagombana na wazazi wake vikaoni hadi nikaamua kuachana na vikao.

Mwanzoni mwa mwezi wa sita alidai kuna mkesha wa maombi siku hiyo na hivyo atalala huko, nikamwambia ukitoka huko utafute nyumba nyingine, baadae mama yake akanipigia kwamba kuna mkesha hivyo wote watalala church kwenye mkesha, nikamjibu haiwezekani wamruhusu wife arudi kwa kuwa ana mtoto mdogo, akakata simu

Kweli, wife hakurudi, ila kila saa alikua akinipigia simu karibu usiku kucha nami sikua napokea naiangalia tu hadi inakatika hadi saa kumi alfajiri, alikuja amesindikizwa na dada yake maana walijua nimekasirika sana

Walipofika tu niliwakamata wote wawili na kuwapa kipigo kizito sana hadi wife kuzirai, dada mtu aliniponyoka na kukimbilia main road huku nikiwa nimemtengua mbavu akapanda boda boda, saa moja wazazi wa wife wakaja nilikua nimemfungia stoo wakamchukua wakaenda nae.

Baadae wakanifuata kazini na polisi wakaniweka ndani kwa shambulio la kudhuru mwili, nilitoka kesho yake , kesi ikahamia Ustawi wa Jamii tuliitwa pale, mbele ya wazee wa pande zote, ikaamriwa kwamba binti arudi kwa wazazi wake hadi hapo baadae hali ikiwa nzuri, ila wazazi wake wakasema wanamchukua kimoja hawanihitaji tena, kwamba nisubiri taratibu za talaka, nikasema haina shida nipo tayari, tukaja nyumbani wakamchukua mtoto na hg na nguo zake wakarudi kwao

Nimeyasahau hayo naishi kwa auheni kiasi kwa sasa Ingawa bado nina msongo, surprisingly Friday wife akanifuata kazini hatukua tumeonana for two months, roho yangu iliingia kitu flani hata mtoto wangu sikutaka hata kuwa naenda kumuona ingawa pale ustawi wa jamii niliruhusiwa

Wife akaniomba tuongee, akasema anahitaji turudiane, akadai anaomba arudi home kwangu hata kesho yake ikiwezekana, kwamba ananipenda, kwamba tutarekebisha tu, nikamwambia haiwezekani simtaki tena

Wadau wana Jf, nimemwambia atafute Mme mwingine kanisani kwao ndo watawezana na sio Mimi, mke wa hivi hanifai, hata mshahara wote anapeleka huko, hilo kanisa Jumapili moja tu kuna sadaka kama 12 hivi tangu asubuhi hadi jioni, unaweza kwenda na laki mbili usirudi hata na shilingi jioni, bado katikati ya wiki, halafu wachungaji wanaishi kifajari.

Huyo mchungaji wa hilo kanisa ameshawateka akili, mimi binafsi nilikua huko nikahama kutokana na hiyo biashara ya kutakiwa kushinda huko 24/7 na pia kutumia sehemu kubwa ya mapato yangu kanisani badala ya kujenga familia, kanisa gani wanaomba hadi salary slip? Na usipowapa watakusema sana kwamba umepotea njia na kadhalika
Kanisa gani halijali ndoa za watu?

Sio kwamba sipendi mke wangu aende kanisani, aende kwa kiasi na ratiba akizingatia kuwa yeye ni mama wa familia, inapaswa kwenda kanisani unashiriki na wenzako mchana au jioni unarudi home, jumatano unakwenda kwa maombi masaa mawili, six jioni unarudi kwako, there will be nothing wrong, lakini huwezi kwenda kushinda huko 24/7. Seven days a week, inakuja kweli hiyo?

Hata dada wa mke wangu niliempiga, mumewe pia alikuja kwangu na malalamiko kama haya ya kwangu, nimeamua simtaki tena, kwanza akili yangu imeshachanganyikiwa,
Nonsense

Ni bora nirudi kwa Rachel, alinivumilia tangu chuo hadi mtaani nikamtendea vibaya nikaoa mlokole nisiemjua, kwa kweli najuta sikujua nachofanya.

Duh. Hatare. Kama ni ishu ya kweli ni basi braza ana stress kweli kweli. Hebu fikiria unaoa mke halafu anakuacha usiku unapigwa na baridi anaenda kwenye mkesha. Ni bora abaki kwa wazazi.
 
Real men don't beat on women. Tafuta mwingine, usije ukapata Kesi ya mauaji. Huo sio ulokole wakuto kumsikiliza mume wako.
 
Back
Top Bottom