Najuta kuoa mwanamke mlokole

Najuta kuoa mwanamke mlokole

Miezi miwili iliyopita nilipelekwa polisi na wazazi wa mke wangu, kwa kosa la kumpiga binti yao karibu nimuue, ndugu walikuja kunitoa

Iko hivi;
Huyu binti nilimuoa miaka miwili iliyopita na tuna mtoto mmoja, yeye na wazazi wake wote wameokoka, Hivi sasa naweza kusema kwamba mke wangu ameolewa na kanisa na si mimi.

Akitoka kazini saa kumi na moja jioni anakwenda kwenye maombi kanisani hadi saa tatu , na hii ratiba ni kila siku Monday to Friday, Jumamosi pia wanakwenda Jumapili ni kutwa nzima, wakati mwingine kuna mkesha katikati ya wiki, hali hii, imefanya ashindwe hata kupataa muda wa kumlea mtoto wetu wa mwaka alielazimika kumwachisha ziwa akiwa na miezi mitatu kutokana kubanwa na mambo ya kanisa.

Mtoto huyu ni kama amebadilishiwa mama, maana sasa analelewa na house girl wetu kwa hali na Mali
Ilifika pahala nikashindwa kuvumilia hali hii na nikamuita na kumueleza hali halisi na kumtaka abadilishe ratiba zake, akadai kwamba hana jinsi kwa kua ratiba ya kanisa kwake haina substitute , nikamwambia ni amri sio ombi

Akaendelea hivyo hivyo, kwa Mara ya kwanza nilimpa kipigo kwa kukaidi amri yangu, niliendelea kumpiga mara kwa Mara sababu ikiwa ni kanisa, kila tunapoitwa kusuluhishwa wazazi wake humtetea na kudai walikosea kunipa mm binti yao, ikawa tunagombana na wazazi wake vikaoni hadi nikaamua kuachana na vikao.

Mwanzoni mwa mwezi wa sita alidai kuna mkesha wa maombi siku hiyo na hivyo atalala huko, nikamwambia ukitoka huko utafute nyumba nyingine, baadae mama yake akanipigia kwamba kuna mkesha hivyo wote watalala church kwenye mkesha, nikamjibu haiwezekani wamruhusu wife arudi kwa kuwa ana mtoto mdogo, akakata simu

Kweli, wife hakurudi, ila kila saa alikua akinipigia simu karibu usiku kucha nami sikua napokea naiangalia tu hadi inakatika hadi saa kumi alfajiri, alikuja amesindikizwa na dada yake maana walijua nimekasirika sana

Walipofika tu niliwakamata wote wawili na kuwapa kipigo kizito sana hadi wife kuzirai, dada mtu aliniponyoka na kukimbilia main road huku nikiwa nimemtengua mbavu akapanda boda boda, saa moja wazazi wa wife wakaja nilikua nimemfungia stoo wakamchukua wakaenda nae.

Baadae wakanifuata kazini na polisi wakaniweka ndani kwa shambulio la kudhuru mwili, nilitoka kesho yake , kesi ikahamia Ustawi wa Jamii tuliitwa pale, mbele ya wazee wa pande zote, ikaamriwa kwamba binti arudi kwa wazazi wake hadi hapo baadae hali ikiwa nzuri, ila wazazi wake wakasema wanamchukua kimoja hawanihitaji tena, kwamba nisubiri taratibu za talaka, nikasema haina shida nipo tayari, tukaja nyumbani wakamchukua mtoto na hg na nguo zake wakarudi kwao

Nimeyasahau hayo naishi kwa auheni kiasi kwa sasa Ingawa bado nina msongo, surprisingly Friday wife akanifuata kazini hatukua tumeonana for two months, roho yangu iliingia kitu flani hata mtoto wangu sikutaka hata kuwa naenda kumuona ingawa pale ustawi wa jamii niliruhusiwa

Wife akaniomba tuongee, akasema anahitaji turudiane, akadai anaomba arudi home kwangu hata kesho yake ikiwezekana, kwamba ananipenda, kwamba tutarekebisha tu, nikamwambia haiwezekani simtaki tena

Wadau wana Jf, nimemwambia atafute Mme mwingine kanisani kwao ndo watawezana na sio Mimi, mke wa hivi hanifai, hata mshahara wote anapeleka huko, hilo kanisa Jumapili moja tu kuna sadaka kama 12 hivi tangu asubuhi hadi jioni, unaweza kwenda na laki mbili usirudi hata na shilingi jioni, bado katikati ya wiki, halafu wachungaji wanaishi kifajari.

Huyo mchungaji wa hilo kanisa ameshawateka akili, mimi binafsi nilikua huko nikahama kutokana na hiyo biashara ya kutakiwa kushinda huko 24/7 na pia kutumia sehemu kubwa ya mapato yangu kanisani badala ya kujenga familia, kanisa gani wanaomba hadi salary slip? Na usipowapa watakusema sana kwamba umepotea njia na kadhalika
Kanisa gani halijali ndoa za watu?

Sio kwamba sipendi mke wangu aende kanisani, aende kwa kiasi na ratiba akizingatia kuwa yeye ni mama wa familia, inapaswa kwenda kanisani unashiriki na wenzako mchana au jioni unarudi home, jumatano unakwenda kwa maombi masaa mawili, six jioni unarudi kwako, there will be nothing wrong, lakini huwezi kwenda kushinda huko 24/7. Seven days a week, inakuja kweli hiyo?

Hata dada wa mke wangu niliempiga, mumewe pia alikuja kwangu na malalamiko kama haya ya kwangu, nimeamua simtaki tena, kwanza akili yangu imeshachanganyikiwa,
Nonsense

Ni bora nirudi kwa Rachel, alinivumilia tangu chuo hadi mtaani nikamtendea vibaya nikaoa mlokole nisiemjua, kwa kweli najuta sikujua nachofanya.
Kwa kweli hapafai kwenda:nono::nimekataa
 
Too much of anything is harmful! Jambo la msingi ni kuwa na kiasi kwa kila kitu tunachofanya.
 
mi pia mlokokole ishu sio ulokole ishi ni ufahamu kichwani...........usidhani jina ulokole ndio pona ukioa unaoa mke yani mtu na tabia flani....sasa nyie hamuendani yani umeoa mtu ambaye sijui kama anajua wajibu wake kwa mume na familia......Bilblia inasema uwe na kiasi....sasa masaa yote kanisani ndio kusema yupo kiroho sana au....noooo

We nawe unampiga ili uiweje tena utafungwa kwa upuuzi wako....kupiga sio suluhu,...tafuta suluhu uliingia ndoa kwa shida na raha........so tumia busara na sio kuvunja watu viuno....

Ndoa ndoano hakuna formula kuwa ukiona mlokole sijui nini kwanza ishu si hilo jina....ishu ni mkristo anayemuamini Mungu thru Jesus...chunga sana waowaji...ndoa sio ulokole

pole sana mwishoni duuu kazi unayo mke wa hivo binafsi tutashindwana tuuu
 
walokole wanaoana wenyewe kwa wenyewe bana, kama umehama ulokole huwezi ishi na huyo binti.
 
I wish i could talk to your wife. Ni pm tafadhali na uniambie hilo ni kanisa gani?
 
Rachel fast huku, nafasi iko wazi kwa ajili yako
 
Pole sana mkuu cha msingi kama hapo umepanga fanya utaratibu uombe tranfer uhamie mkoa mwngne upunguze shari haya makanisa cku hiz n balaaaaa😏
 
Nlishasema mm..kuna makanisa matatu tu! KKKT, KATORIKI na ANGLIKAN,,, hawa utaratibu wao wa ibada ni mzuri sana, imani yako ndio inayo kuponya,,hata ukioa mke katika makanisa haya hutasikia upuuzi wa kwenda kanisani kila siku,,..sio hawa wanajiita walokole....
 
Nlishasema mm..kuna makanisa matatu tu! KKKT, KATORIKI na ANGLIKAN,,, hawa utaratibu wao wa ibada ni mzuri sana, imani yako ndio inayo kuponya,,hata ukioa mke katika makanisa haya hutasikia upuuzi wa kwenda kanisani kila siku,,..sio hawa wanajiita walokole....

Mkuu katoriki ndo kanisa gani?
 
Pole sana ndugu yangu. Kimsingi kama unavomwona anakukosea, ujue naye anakuona umepotoka, na sababu kubwa ni kwamba mnatumikia mabwana wawili tofauti hivyo ni lazima utumishi utofautiane, ratiba zitofautiane, mitazamo itofautiane........... nk.
Neno linasema watu wawili hawawezi tembea pamoja wasipopatana.
ni kweli mkuu,nakubaliana na wewe kwa hili.
 
Sasa wewe hufai kabisa huyo mke anafaa maana anamtumikia Mungu na wewe anakuombea shida yako nini kwani unyumba hupati? kama unyumba hupati hapo short. Lakini usimpe Talaka eti sababu anasali sana hapo unakosea

Ushauri wa bure tafuta spare wa kukusaidia kwa siku anazoenda kulala kanisani hapo utakuwa umemaliza shida zote
 
Enyway umeongea upande mmoja Wa shilingi, yaani upande wako, but hatujui upande wake anasemaje kwa yote hayo. Kama sio tungo basi ujue hapo ulifanya inshu mbaya.

Mambo ya dini kwa wenye dini zao, ukute angeolewa na MTU Wa sampuli yake muda wote wangekuwa huko kwenye misa.

Wewe unaoa mtu Wa misa ilihali wewe si MTU Wa misa wapi na wapi..!

Umenena ukwel, ila tatzo jngne ni kwmba kaka e2 huyu, mke wke anafny kaz, hvyo mshahara unaishia huko kansani, pesa y jamaa huyu ndo ina2mika, so km wangekuw wote wa2 wa hvyo unafkr wangekuw na nn ? Mwsho wakafa maskn wenzao wanatajrka, tatzo la walokole hawajielewi, nawaurumia sn jnc wanavoibiw pesa na mali zao, they av 2 change, ckatai ibada, ibada wafanye ila inshu ya kutoa hela tena nyng kla cku mh, iyo namashaka nayo, ibada inanunuliwa, ata iwe sadaka ndo kw cku utoe lak 5 afu familia itaishje ? sadak toa kiasi kdogo, inatosha ili naww uweze kuish, sio unatoa yt, kesho km huna utatoa nn ?
Walokole badlken, msiwe km chama tawala!!!
 
Back
Top Bottom