Msandawe Halisi
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 647
- 351
Wana viwembe waleMwenge kituoni hapafai kabisa!
Mi huwa nikifika hapo nasimama kimachalemachale tayari kumpa mtu upper cuts.
Wana viwembe wale
Jana katika mizunguko yangu, nimetoka banana Ukongo mida ya jioni kuelekea Bunju. Kufika Mwenge kukawa na usafiri wa shida sana. Mara gari ya Bunju hiyo. Abaria tukaanza kufanya mahaba ya kuikumbatia gari toka lango la kungilia mpaka karibu na yanapo paki mabasi ya Tegeta, Bunju ndani ya kituo cha mwenge, sababu konda aligoma kufungua mlango tupande pale yanapo ingilia mabasi. Baada ya mlango kufunguliwa likatokea purukushani la kufa mtu kuakikisha kila moja anawahi siti. Ile kufika ndani tu najikagua mifukoni Simu yangu holaa, nikaseach mpaka mifuko ya nyuma holaaa. Najiangalia mfuko mwingine elfu hamsini hola. Nikachoka ghafla nikafa kiumee kimya kimya huku nikapata upweke wa kukosa kuperusi JF. kwa bahati nzuri mfuko wa shati kulikuwa na ATM card na elfu mbili.
Ndugu zangu, Naaaaaaaajuuuuuuuuuutttttaaaa kuuuuuuuuiiiifahammuuuu Mweengeee Stand.
Mi huwa natembea na bisbis...
Hujawahi kuibiwa dogo...........watakuibia siku hadi utawapongeza na halafu ukajichoma yako bisbis kujilaumu!
Mi huwa natembea na bisbis...
Njoo Rio Quality Gym & Spa .. Hapa tunajifunza kuwa fit mpaka karate ..bisibisi za nini mkuu wangu ..!!
Mi huwa natembea na bisbis...
nyani bana we tunachekeshana mbele za wakwe bana, wahahahhaaa!
Hahah mwana wa abajato acha woga. Mimi toka mwana 2012 huwa nikipanda daladala nina i phone 4 nai pa na sijawahi kuibiwa . Sijisifii manake najua wanaweza kuniotea kama walivyoweza kunipiga passport ila hii ya kupanda dala dala na pp kijiti manake unawaogopa na mbinu zao huzijuiAh wapi! Mi mtoto wa town wewe. Mwana Abajaro wa zamani. Nimezipiga sana na Kiboko Msheli.
Mbinu zote wanazozitumia nazijua. Sipandi daladala na chochote cha thamani zaidi ya pipi kijiti.
Kipindi nasoma, kuna siku nimetoka menge naenda Ubungo, mfukoni nina elfu tatu bajeti ya nauli kula na maji. Ile karibu nafika Mlimani city mifuko miupeeee.
Uzuri wake konda alikuwa hajaanza kukusanya nauli, ikabidi nimwombe kazi ya kuita abiria hadi Ubungo ili nisilipe nauli.
Uzuri wake konda alikuwa mwelewa kwa sababu aliona ninavyojisachi baada ya kuchezewa chezo na watoto wa mujini.
So nikachapa mzigo hadi Ubungo na nikaachiwa na sh. 1000 na konda kama mshahara halali.
Chuma nimeanza kupiga in earnest tokea 1993 pale Gerezani. Rio gym ya watoto mayai.