Najuta kufundisha lugha ya Kiingereza

DREAMBOY

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
2,114
1,358
Habari wadau wa elimu!

Mimi ni mwalimu ambaye ninafundisha lugha hii muhimu ya biashara,utawala na diplomasia ktk mojawapo ya shule ya sekondari nchini.
Kwanini nimekuja na bandiko hili, ukweli ni kuwa pamoja na ualimu kuwa kazi yenye maslahi hafifu bado ni kazi muhimu kwa mno; Mimi ni Mkuu wa idara ya somo hili hapa yanayonikuta mpaka najuta ni haya.

Walimu wezangu under my department are very poor in speaking ,hebu fikiria Mwalimu hawezi maliza dakika tatu akiwa anazungumza kiingereza halafu tunahimiza watoto wazungumze English from morning to departure time, to be honest this is a joke. Halafu Mkuu wa idara unasimama unasisitiza wanafunzi wazungumze English kwa motisha na mikwara kibao.

Toka nimeajiriwa sijawahi kumsikia Mkuu wa shule akiwahutubia wanafunzi kwa lugha hii which means naye inamtatiza.. Ukienda madarasa ni ukalimani ndo unaendelea , sasa najiuliza how will I fulfill the desired out comes Kama sio kunichafulia CV . Na nyinyi colleges and universities mnawezaje kumqualify mtu asiyeweza kuongea lugha Fulani akawe Mwalimu wa lugha hiyo.? Ushauri: Tufundishe kwa lugha yetu ya kiswahili na English iwe optional subject kuliko haya maigizo yanayoendelea huku kwenye field.

NB; I have brought this with constructive conscience.
Nawasilisha.
 
You should have expected the unexpected. Walimu wengi wanasingizia kuwa watoto hawatawaelewa wakiwafundisha kwa kiingereza. The big question is, WHEN WILL THESE STUDENTS BE ABLE TO UNDERSTAND INSTRUCTIONS GIVEN IN ENGLISH IF THEY ARE NOT GIVEN THE OPPORTUNITY OF PRACTISING IT?
Hata mimi ninakumbana na tatizo hilo hilo.
Nilikuwa mkuu wa idara ya Kimombo... ni shiiida.
Kuhusu mkuu wa shule hajiwezi, huwa naogopa hata kumsalimia kwa kiingereza asije akaumbuka.
Walimu wenzangu wa kiingereza nao chali.
Kwa sasa niko ofisi ya taaluma. huko ndo majanga zaidi. Utagombana na wangapi?
Nilichoamua ni kuishi kwa principles zangu.
Mwanafunzi akija kwangu lazima ajipange kuzungumza kiingereza.
Wengi wao huwa wananikwepa na kwenda kwa walimu wengine.
 
Ingependeza sana ungeleta huu uzi kwa lugha unayofundishia ...ili tujiridhishe na the the zako kama mkuu wa idara kwanza..
Ni kweli kabisa sina perfection kama binadamu ila haya majukumu yangu naya umudu, Mimi nikisisima nikaongea kingereza kama haunioni unaweza hisi kunamwekezaji kutoka ughaibuni amekutembeleeni. Asante mungu nimesomea shule hohehahe lakini waliopitia private hawaniachi mbali aisee
 
Hata mreta mada ni jipu,anajinasibu kwa kuwakandia wenzake,kaandika "this a joke" instead of "this is a joke".english is an elephant's meet,every one cuts to his/her size.
do you think, speaking English fluently is the issue of errors avoidance.? errors and mistakes ktk lugha yoyote kitu cha kawaida kabisa. Kuhusu hiyo "is" iliyo omitiwa,do you think is not into my lexicon wakati present umbo hili orthographically. kama umosoma lugha jikumbushe psycholinguistics. utajua tu. halafu tofautisha speaking skills and writing skills.
 
Kiswahili tabu
English shidaaaaaa eti kililetwa kwa pipa.
Kazi sana.
Nilisisitiza sana kutumia hii lugha ya kufundishia mwaka 2012 wakati nimeajiriwa,mwisho nilikata tamaa,mwaka 2013 nikaamua kujichanganya mtaani kufanya biashara zangu Kariakoo,sasa kipindi changu tu ndio kinanipeleka kazini,huwezi kufanikiwa ni kujipa shida isiyokuwa na faida
 
Nilisisitiza sana kutumia hii lugha ya kufundishia mwaka 2012 wakati nimeajiriwa,mwisho nilikata tamaa,mwaka 2013 nikaamua kujichanganya mtaani kufanya biashara zangu Kariakoo,sasa kipindi changu tu ndio kinanipeleka kazini,huwezi kufanikiwa ni kujipa shida isiyokuwa na faida
Mi bado nasisitiza kutumia lugha hii ingawa nina mambo mengine pia.
Hata watoto wanajua kuwa nje au ndani ya darasa siongei nao kiswahili, labda mtoto awe na shida ya kiafya inayohitaji msaada haraka.
Wanafunzi wameshanizoa kiasi kwamba hata nikiwa na walimu wenzangu, salamu hutenganishwa. Napewa ya kiigereza, wenzangu ya kiswahili.
 
Nilikua kiranja wa taaluma O-level, pamoja na mambo mengine nilitakiwa kusimamia wanafunzi wote kuongea kiingereza, ilikua shida watu waligeuka mabubu. Nikilegeza mwalimu ananishushia rungu mimi nikakaza watoto wa watu wanatia huruma, Ni shida. Mungu Mkubwa leo natema yai si haba.
 
Mi bado nasisitiza kutumia lugha hii ingawa nina mambo mengine pia.
Hata watoto wanajua kuwa nje au ndani ya darasa siongei nao kiswahili, labda mtoto awe na shida ya kiafya inayohitaji msaada haraka.
Wanafunzi wameshanizoa kiasi kwamba hata nikiwa na walimu wenzangu, salamu hutenganishwa. Napewa ya kiigereza, wenzangu ya kiswahili.
Hongera,mimi nilishindwa na kuna mwingine aliajiriwa mwaka jana naona alikuwa anahimiza sasa kaamua kutulia na kufanya mambo yake
Mji wa Dar shule zote huwezi kufanikiwa
 
Back
Top Bottom