Natumai u mzima wa afya njema, nimesoma ujumbe wako nimesikia kuumia sana moyoni,!
La Princesa,najaribu kuitazama hali ya mama yangu kule kijijini,halafu akose mtu wa kumsaidia ilhali yeye hana uwezo wa kujitafutia pesa ya kujikimu,roho inauma sana
Lakini vipi shemeji umejaribu kuongea naye juu ya jambo hilo? Na kwanini akuwekee mazingira magumu wewe kwenda kumuona mama? Kwa vyovyote vile,huyo ni mzazi wako na kama hana msaada mwingine zaidi ya wewe,usikubali kumuacha mama akateseka,(ni mama kama alivyo mama wa mumeo)
Sikushauri kuvunja ndoa yako hata kidogo,lakini ni muhimu kutafuta namna zozote zinazowezekana kuhakikisha mama anapata angalau kiasi kidogo cha kumuwezesha kupata mahitaji yake
Dada,mimi ni mwanaume,najua wakati fulani si rahisi sana kushauriwa na mwanaume namna ninavyokushauri
Kwanza ukiona hali imekuwa ngumu sana kupata pesa,bana hata ya matumizi ya nyumbani,mtumie mama,(mf kama anakupa bajeti ya sh.15000 kwa siku,hakikisha hapo angalau 7000 unaiweka pembeni,kwa wiki nzima mtumie mama) maisha yaendelee
Ukweli kuacha kazi haukuwa uamuzi mzuri,hasa ukizingatia nature ya mume wako,lakini haupaswi kujutia tu,ni lazima uchukue hatua,bora ukala maharage,dagaa kwa angalau wiki moja,umsapoti mama!
Pole sana,kwa mapito hayo magumu..