Najivunia kuacha chuo. Kijana mwenzangu, huhitaji shahada kufanikiwa kimaisha (to be rich)

Ushauri wangu........Elimu ni Taa ya kuondoa Ujinga na Giza, na Elimu si ya kujitajirisha kimapeni bali kufungua Ubongo....Naomba watu waelewe sana.

Zamani tukiambiwa, tusome kwa biddi tupate kazi nzuri, ndio lakini lengo kubwa ni kuwa mwerevu ki dunia!!!!
 
Moyo na akili yangu vimenisukuma kuandika haya baada ya kuona kuna uongo mkubwa katika jamii hasa kwa vijana,kuwa ukiwa na elimu kubwa ya darasani basi una uhakika wa kufanikiwa kimaisha kitu ambacho si kweli.
If a man repeats a lie over and over, he will eventually accept the lie as truth.Moreover he will believe it to be truth.

NOTE.
Naomba nieleweke kuwa sina lengo la kukosoa,kutukana,kukejeli au aina yoyote ile mbaya ila nataka kuwaonyesha vijana wenzangu upande wa pili wa shilingi (Another side of coin).

My personal story.

Mwaka 2000 nilianza elimu yangu ya msingi katika shule ya msingi X. Kusema kweli maisha ya shule yalikuwa mazuri kwa siku za mwanzo lakini kadri siku zilivyozidi, maisha yangu ya shule niliyaona magumu sana na hii ilitokana na changamoto mbalimbali hasa ya usafiri.Kwa wale waliosoma shule Dar nadhani watakuwa wamenielewa.

~Biashara yangu ya kwanza shuleni.
(My first entrepreneurial journey)

Mwaka 2004 wakati nipo darasa la 5 Mjomba angu ambaye alikuwa South Afrika alikuja Bongo,aliniletea zawadi ya baiskeli ambayo nilianza kuitumia kwenda nayo shule kila siku. Wakati nipo shuleni wanafunzi wenzangu walikuwa wanaomba baiskeli, hapa nikagundua kuwa naweza ku make money kupitia baiskeli yangu.

Ule muda wa mapumziko ya chai wanafunzi wenzangu walikuwa wananifuata nawakodisha baiskeli waendeshe alafu wanalipa pesa. Kwa wakati Ule haikikuwa pesa nyingi sana kama wewe ni mtu mzima ila kwa umri ni pesa ndefu.
Nilikodisha 5 minutes kwa shilingi ishirini(Sh.20/=).kwa siku nilikuwa na uwezo wa kuingiza hadi shilingi 500~700,Na kwa siku za weekend jumamosi nilikuwa sikai nyumbani,naenda shule kupiga hela kwa kuwakodisha baiskeli wanzangu

Naomba niwe mkweli hapa.Baada ya kuanzisha hiki kabiashara Kangu ka kukodisha baiskeli maisha ya shule niliyaona mazuri haina mfano.Usiku niliona unakuwa mrefu na asubuhi inachelewa muda wa kwenda shule. Ilifika hatua hadi siku ya Jumapili nilikuwa naichukia natamani Jumatatu ifike haraka nipige pesa.

Biashara iliendelea hadi namaliza elimu ya msingi.Ile siku nafanya mtihani wangu wa mwisho tu nilipofika nyumbani nilivunja kibubu changu nilichokificha chini ya uvungu wa kitanda. Sikuamini nilichokuwa nahesabu kwenye zile shillingi,Jumla nilipata kiasi cha Tsh. 326,700/=. Kusema kweli sikujuta kwenda shule.

Hapa kilipita kipindi kirefu cha kusubiri matokeo ya elimu ya msingi lakani katika kipindi hiki nilijaribu kufanya biashara kadhaa,mojawapo ile niliyokuwa nafanya mchikichini wakati naenda kupiga pindi la form one. Nilikuwa nauza zile karatasi ndefu za kufanyia mathematics kwa wale walipita kwa Aideni na Sir Mudi watakuwa wamenisoma.

Mwaka 2007.

Tokeo limeshatoka na nilichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule moja maarufu hapa jijini Dar ipo katikati ya jiji(Mnazi mmoja). Nilikuwa na furaha sana kuingia sekondari lakini furaha kubwa ilikuwa kuangalia fursa gani naweza kuifanyia kazi huko shuleni.

Si Unajuwa tena ile Kinjuka njuka nafika shule mshamba mshamba wa mazingira shule ilibidi niwe mpole huku natumia macho ya tai kuangalia nini nifanye niwe napiga pesa pale shuleni.

Nilikuja kugundua fursa moja ambayo wanafunzi wengi walikuwa wanapenda sana ili kuweka kumbukumbu zao.Nilikuja kuipata karibu na siku ya graduation ya kidato cha nne ya mwaka 2007. Fursa hiyo si nyingine bali ni kuwa mpiga picha/cameraman.

Fasta nikaamua kuuza baiskeli yangu ile kwa sh.120,000/= nikaongeza kiasi kingine cha pesa, nikanunua camera mpya kabisa kariakoo.Kazi rasmi ya kupiga picha ilianza shuleni siku ya graduation na siku zingine.Kwa kuwa nilikuwa nafanya discounts nilikamata wanafunzi wa shule yote wakawa wateja wangu.Nilinunua counterbook la 3 kwaya kwa ajili ya order za wateja.

Kaunzia shuleni kwangu, Jangwani sec,Zanaki sec,Kisutu sec,Azania sec,Benjamin sec,Dar es salaam sec nilikuwa napiga pesa ile mbaya hadi nilipata wapambe/walinzi wangu kama 7 saba hivi.Hawa walinzi ilikuwa kila nikienda shule nyingine ya jirani kupiga picha ilikuwa lazima niwachukue kwa ajili ya usalama wangu na kupata malipo yangu kwa uhakika.Kwa waliosoma Dar hasa zile shule za mjini kama vile Aza boy,Benjamin,Dar seko,Jamhuri,kibasila, na zingine wanafahamu kuwa kulikuwa na tabia za kindava sana,kama mnyonge mnyonge ilikuwa lazima upate shida sana.

Kusema kweli maisha yangu ya sekondari yalikuwa mazuri sana sana, pesa ilikuwa haipigi chenga ilikuwa ya kutosha, wapembe walikuwepo wa kutosha lakini kizuri zaidi nilikula sana mademu.

Mwaka 2009 wakati nipo kidato cha 3, Anko wangu alikuja Bongo akitokea SA safari hii alikuja na academic books, vitabu vingi sana vya science akiamini napenda sana hayo masomo. Nakumbuka niliwahi kumwambia wakati nipo S/M kuwa ndoto yangu ni kuwa daktari Muhimbili. Hii ndoto ilizidi kupotea wakati nipo sekondari kwani hata masomo nilichukua ya mchepuo wa biashara.

Mwaka 2010:
Nilifanya mtihani wangu wa kidato cha nne. Nashukuru Mungu tokeo lilitoka nimefaulu nimechaguliwa advance Benjamin Sekondari.

Hapa Benjamin Sec ni uwanja wa nyumbani kwanza nilikuwa nakuja kupiga picha lakini hapakuwa mbali na shule yangu ya O level.

Nilifanya biashara kadhaa shuleni lakini kutokana na ugumu wa masomo ya advance niliamua kuacha kwa muda biashara na kuongeza umakini katika masomo.

Nilikuja kushtuka nipo kidato cha sita, kusema ule ukweli kabisa licha ya kuwa nilikuwa nipo busy na masomo lakini moyoni akili ilikuwa inawaza nini nifanye ili niwe naiingiza hela.

Kwa kipindi hiki wakati nipo kidato cha sita nilikuwa sifanyi biashara yoyote shuleni lakini uswahilini nilikuwa nafanya biashara ya kuuza opening shoes hasa za kike pale Buguruni chama.

Nilikuwa na Brother Ommy Aka Tembo, goli lilifunguliwa kuanzia saa 10 au 11 jioni hadi saa 5-6 Usiku. Kwa siku kuingiza laki 2-4 ni kawaida.

Mchana brother Tembo anaenda kuchukua mzigo Kariakoo ndani ndani huko kwa Wachina kwa 1200-1500 akirudii anajifungia ndani kutwa kufanya marekebisho madogo madogo jioni tunaingia mzigoni.


Mwaka 2012.
Nilimaliza elimu yangu ya Advance, niliingia kitaa rasmi kufanya biashara.Niwe mkweli ile miaka miwili ya advance niliiona mingi sana na inanichelewesha kuingia in business world.

Nilipo kuwa kidato cha 5 na 6 nilikuwa najiuliza maswali mengi sana kuhusu aina ya elimu tuliyokuwa tunapata pale shuleni, tunasoma masomo ya biashara lakini mbona hatufundishwi namna kufanyaa biashara na kuingiza pesa.
Kusema kweli siku kuwa napenda kile tulichokuwa tunafundishwa shuleni.

Hivyo kumaliza elimu ya advance nilifurahi sana kwani ilikuwa inanichelewesha kuingia rasmi katika biashara.
Wakati nipo kidato cha sita mwisho mwisho nilijiapiza ya kuwa sitaendelea na elimu ya chuo kama nitachaguliwa,kwa kuwa sitaendedelea elimu ya chuo kikuu haina shida kama sitajiunga na JKT.

Kwahyo nili drop chuo na JKT, kwani nilichaguliwa kujiunga na elimu ya juu lakini nilishakataa kusoma chuo kikuu.
Acha tamaa.

Acha kukurupukia maisha kila kitu kina wakati wake.
 
Ushauri wangu........Elimu ni Taa ya kuondoa Ujinga na Giza, na Elimu si ya kujitajirisha kimapeni bali kufungua Ubongo....Naomba watu waelewe sana.

Zamani tukiambiwa, tusome kwa biddi tupate kazi nzuri, ndio lakini lengo kubwa ni kuwa mwerevu ki dunia!!!!
 
Ushauri wangu........Elimu ni Taa ya kuondoa Ujinga na Giza, na Elimu si ya kujitajirisha kimapeni bali kufungua Ubongo....Naomba watu waelewe sana.

Zamani tukiambiwa, tusome kwa biddi tupate kazi nzuri, ndio lakini lengo kubwa ni kuwa mwerevu ki dunia!!!!
 
Hongera kwa kuwa umefikiria nje ya boksi japo hatuwezi lingana kwenye mipango na maono.

Sasa mkuu hebu tuambie mpaka sasa una kipi ambacho ni mafanikio kwako si lazima iwe nyumba na gari nahitaji kujua maendeleo ya unachokifanya na unafanya hicho hicho ulichotuambia au una kingine?

Pia kwenye stori nzima hatujasikia changamoto yoyote uliyowahi kukutana kwenye biashara zako mbali na hizo za shule kukubana je,hukuwahi kupata? Na kama ulipata ulitatuaje?

Tueleze yale tusiyojua kwa ufupi kwenye biashara mfano unakuta mtu anakwambia nilianza na lita 10 za petrol ndani ya mwaka mmoja nikawa na petrol station bila ya kutuambia mchakato ulikuaje?

Nisaidie au tusaidie mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app

Nashukuru sana.

Mafanikio yapo kwani nilipoanza sio sawa na hapa nilipo sasa.Haya kwangu ni mafanikio makubwa sana.
Tangu nipo shule ya msingi nilikuwa napenda nifanye kitu/kutatua tatzo ili nipate pesa lakini mimi nimesaidia tatizo hilo,kwahy nimewasaidia wengi sana katika umri wangu huu niliokuwa nao.

Nimefakiwa kuajiri watu kama 12 hadi saa directy.Katika hao 12,5 wanafamilia zao ambao zinawategemea kwa kila kitu.Hii kwangu ni mafanikio.

Ila nina mtandao mkubwa sana wa kupata taarifa mbalimbali za biashara ambazo zinanisaidia kutambua fursa wapi ilipo na namna ya ku achiev hiyo fursa.

Ila kikubwa nilikuwa napenda niwe na freedom katika maisha yangu hasa financial freedom Nashukuru nimepata uhuru ninao utaona.

Mafanikio yapo mengi sana


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chuo ndo kuna fursa sasa kama kweli ww ni mfanya biashara. Ila njia yoyote uliyoichagua lazima utobe maana unaonekana ww ni mbishi.
 
Bro emu angalia jicho la tatu hapo we unaongelea una ndugu SA maana yake capital ipo tu je mimi mbulukenge wa mwigumbi ata baba yangu hajawahi fika dalesalama unanishauri niache chuo kweli nikazibe pancha za baiskeli na baba still tutoboe #for what i know kila mtu ana njia yake yakutokea.
Refer Bible mwenye nacho ataongezewa na kina mbulukenge tutapunguziwa .
Wote hatuwezi kufanikiwa dunia itafika mwisho acha tu tukomae na engineering drawing zetu.


Sent using Jamii Forums mobile app

Kama umeanza kusoma tangu mwanzo umepata vitu vingi tofauti na SA.

Nimefanya biashara nyingi ambazo haikuhitaji mkubwa sana kwa kijana yoyote angeweza kufanya.
Ila tatizo ni mindset na elimu ya shule


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana. Kila siku rafiki yangu ananiimbia wimbo njoo mtwara uangalie fursa za kibiashara.

Sent using Fly in any Weather.

KAKA nimeandika kwa herufi kubwa.

Mtwara kuna fursa nyingi sana nakuhakikishia.Mfano mwaka jana msimu wa korosho,korosho unannunua Sh.1500-2000 kwa mkulima alf wewe unapeleka ghalani na kuuza kwa Sh.3300/=
Faiid 1700-1300


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom