Najivunia kuacha chuo. Kijana mwenzangu, huhitaji shahada kufanikiwa kimaisha (to be rich)

Nimewahi tu siti kungojea part ingine

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
 
Mwaka 2016.

Safari ya kwenda kusini mwa Tz.
Ndani ya mwaka 2016 niliweka malengo makubwa sana ikiwa pamoja na kukuza kipato changu na kuanzisha miradi mingine kama miwili hivi.
Nikiweka malengo sina tabia ya mapenzi,huwa natupa kule.

Brother Tembo ni mtu wa kusini(Mtwara) Kwahy mara inapofika msimu wa korosho huwa anapeleka bidhaa mbalimbali huko,sasa huu mwaka nilimwambia na mimi nataka twende pamoja Mtwara.
Nilijiandaa golini kwangu Buguruni nilimuweka mwanangu mmoja hivi ambaye amemaliza degree yake na hana mbele wala nyuma.

Ilipofika mwezi wa 11 tulizama kusini/Mtwara sana,nikiwa nimefunga mzigo wa Sh.Mil 9 kuanzia Sandroz za kiume,boksa,bra,open shoes,tyt,Madela,mikoba,jeans na vingine kibao.
Mtwara kipindi cha msimu kuna kuwa na pesa jamani.Japo kuwa ulikuwa msimu wangu wa kwanza kwenda mtwara ila hadi msimu unaisha nilitoboa tobo la maana sana.Nilianza na mil.9 lakini hadi msiimu unaisha nina mil.17 na lupea kadhaa.
Wamakonde wakiwa na hela wananunua tena bila kuomba punguzo hata kidogo.

Mwenyeji wangu alinisadia sana kupata ka fresh ambacho nilikodi kwa muda mfupi tu,lakini kutokana na ucheshi wangu nilipata marafiki wengi sana huko,pia nilinunua mashamba kadhaa ya mikorosho huko kusini.
Mmoja ya watu ambao nilikutana nao na Nashukur sana kufahamiana nae nini Boss Msham,huyu jamaa aliinipa madini yote kuanziia mtwara(korosho),Lindi-liwale,kilwa(Ufuta) na Masasi Mbaazi.Jamani watu wanapiga pesa huko mikoani.

Baada ya msimu kuisha nilirudi zangu Dar ku pumzika kwa siku kadhaa kisha nikaaingia tena zangu Buguruni kwenye goli langu nililomwachia jamaaa.
Nilikuta bado anapiga vitu fresh tu,kwenye hii ofisi nikamwacha yeye mimi nikafungua ofisi nyingine.

Ile pesa niliyopata kule kwenye korosho haikuchezewa kwani Boss Msham alinipanga kuwa mwezi wa 4-5 kusini hasa mkoani Lindi kuna anza kuvunwa ufuta.Kwahiyo kwa kupitia jamaa niliweka ahadi ya kununua na mimi.
Kwa kuwa jamaa alikuwa mzoefu nilipanga kumtumia na mimi niingie katika kununua mazao huko kwao.

Mwaka 2017.
Nilirudi rasmi kusini katika mkoa wa lindi kwa ajili ya kununua zao la ufuta.
Niliingia na mtaji wangu mdogo tu wa mil 15,nasema mdogo kwa sababu kuna wafanya biashara wa huko wakubwa wenye mitaji ya mil.100-300 wana nunua ufuta,lakini pia kuna wahindi kibao hawa wa kariakoo wanajazana huko kusini kwa ajili ya kununua ufuta.
Kusema kweli bahati ilikuwa upande wangu kupitia jamaa alinipatia badhii ya brokers wake huko vijijini na mimi walinunulia ufuta hadi pesa yangu ilipoisha.


Sent using Jamii Forums mobile app
Msham (kingomega)?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2017.
Msimu wa ufuta

Kusema ile kweli.Ufuta unalipa tena vizuri sana sisi chochoma tulikuwa tuna nunua kwa wakulma wadogo kwa sh 1500-2000 alafu sisi tuliuza kwa Sh.3000 kwa wastani.
Nilinunua ufuta nikauza,nikalipwa pesa zangu na kuingia tena chaka kununua tena ufuta,nilifanya huu mchezo kama mara 3 hivi.
Kuna kipindi hadi nilikuwa naogopa lakini Boss Msham Ali niamby kama unataka kupiga pesa basi uoga weka kisogoni.
Hadi msimu wa ufuta unakata Lindi nilikuwa na kiasi cha Sh mil.26.
Kusema ukweli kuna wakati tulikuwa tunawakaanga vibaya sana wakulima.Jamaa alinifundisha michezo ya ki ninja katika kununua mazoa,mwanzo nilikuwa muoga ku play hiyo michezo ila baada ya muda nilikuwa Ninja master katika kutumia kanuni za kununua mazao.

Baada ya. Msimu nilirudi Dar nikiwa na furaha usoni.Kwani niliingiza pesa Nzuri tu lakini pia miradi yangu ilikuwa inaenda fresh tu.
Ukiacha pesa cash,biashara zangu zote zilikuwa na thamani ya Sh.Mil kama 9-11 kwa maono yangu mwenyewe.
Niwe muwazi kwa jinsi mambo yangu yalikuwa yanaenda fresh,jamaa zangu kibao wa skuli niliwapiga gape tena kubwa.

Nimefanya biashara nyingi sana mara baada ya boss Msham kunifungua macho katika biashara ya mazao.Hii biashara ina pesa kama ukiweza kwenda na upepo fresh.
Nilinunua mazao kama vile(Michele,maharage,viazi,vitunguu,n.k)na kuleta Dar.
Kusema kweli maisha si magumu licha ya changamoto za wakati ulipo,lakini nikijilinganisha na marafiki zangu wengi kama sio wote nimewaacha mbali.

Kwa umri wangu huu nilikuwa nao ni mafanikio makubwa sana.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale mtakao pitia uzi huu kama ukifanikiwa kupata nafasi ya kusoma soma..kuna watu elimu imebadilisha maisha yao na pia kuna watu ambao hajafanikiwa kuwa hivyo.

Kikubwa katika maisha kila mtu ananjia yake ya kufikia mafanikio kama wewe ulivyofanikiwa kupitia biashara. Natoa pongezi nyingi kwako endelea kupush gurudumu

NB: kwa utakae soma uzi huu chukua tahadhari nasisitiza


It is never to late to begin. Start now
 
Mwaka 2020.
Mafanikio yangu.

Licha ya changamoto kadhaa nilizopitia katika safiri ambayo bado sija fika mwisho,nimepata mafanikio mengi sana tena sana.

1~Nimepata connections na watu wengi ambao ni productive na Money maker.

2~Nimepata knowledge kubwa sana ambao hauwez kupatikana darasani hata ukisoma miaka 20.Lakini knowledge hii unaipata ukiwa unapambana na maisha.

3~ukiacha materials thing(Nyumba kadhaa,usafiri,n.k) naweza kwenda bank na kuchukua hata mil 150-200 kitu ambacho ni wasomi wachache na wafanyakazi ambao wanaweza kukopesheka kiasi hicho cha pesa.

Hapa mwezi huu nimepanga nizame bank nikachukue mil.80 kwa ajili ya kununua ufuta huko Lindi.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha tunatofautiana mtoa mada hakupenda shule ila shule ilimpenda na pesa ikampenda pia.
Binafsi japo sikufika mbali kielimu ila mwanzo suala la kutokufika mbali lilinitesa sana kisaikolojia ila nikiangalia maisha ya wasomi wengi nabaki kusema kuwa MUNGU alikuwa na makusudi na maisha yangu.
Nachoweza kusema ni kwamba kila kitu hutokea kwa sababu ambazo MUNGU kakupangia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bro emu angalia jicho la tatu hapo we unaongelea una ndugu SA maana yake capital ipo tu je mimi mbulukenge wa mwigumbi ata baba yangu hajawahi fika dalesalama unanishauri niache chuo kweli nikazibe pancha za baiskeli na baba still tutoboe #for what i know kila mtu ana njia yake yakutokea.
Refer Bible mwenye nacho ataongezewa na kina mbulukenge tutapunguziwa .
Wote hatuwezi kufanikiwa dunia itafika mwisho acha tu tukomae na engineering drawing zetu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ulivyosoma huo uzi wewe umeona mleta uzi ana lengo lipi na kwa maaneno hayo unaona kalenga kuwashauri nini vijana?


Sent using Jamii Forums mobile app
sijui ni kukurupuka au ni elimu uliyonayo haijakusaidia.yani kuna haja gani sasa ya wewe kuitetea elimu wakati kuelewa tu mada kama hii imekushinda.sina haja ya kubishana na mtu ambaye hata hoja nyepesi kama hii imekushinda kuielewa
 
Back
Top Bottom