Najivunia kuacha chuo. Kijana mwenzangu, huhitaji shahada kufanikiwa kimaisha (to be rich)

forumyangu

JF-Expert Member
Dec 25, 2016
2,147
2,000
Moyo na akili yangu vimenisukuma kuandika haya baada ya kuona kuna uongo mkubwa katika jamii hasa kwa vijana, kuwa ukiwa na elimu kubwa ya darasani basi una uhakika wa kufanikiwa kimaisha kitu ambacho si kweli.
If a man repeats a lie over and over, he will eventually accept the lie as truth. Moreover he will believe it to be truth.

NOTE.
Naomba nieleweke kuwa sina lengo la kukosoa, kutukana, kukejeli au aina yoyote ile mbaya ila nataka kuwaonyesha vijana wenzangu upande wa pili wa shilingi (Another side of coin).

My personal story.

Mwaka 2000 nilianza elimu yangu ya msingi katika shule ya msingi X. Kusema kweli maisha ya shule yalikuwa mazuri kwa siku za mwanzo lakini kadri siku zilivyozidi, maisha yangu ya shule niliyaona magumu sana na hii ilitokana na changamoto mbalimbali hasa ya usafiri. Kwa wale waliosoma shule Dar nadhani watakuwa wamenielewa.

~Biashara yangu ya kwanza shuleni.
(My first entrepreneurial journey)

Mwaka 2004 wakati nipo darasa la 5 Mjomba angu ambaye alikuwa South Afrika alikuja Bongo, aliniletea zawadi ya baiskeli ambayo nilianza kuitumia kwenda nayo shule kila siku. Wakati nipo shuleni wanafunzi wenzangu walikuwa wanaomba baiskeli, hapa nikagundua kuwa naweza ku make money kupitia baiskeli yangu.

Ule muda wa mapumziko ya chai wanafunzi wenzangu walikuwa wananifuata nawakodisha baiskeli waendeshe alafu wanalipa pesa. Kwa wakati ule haikikuwa pesa nyingi sana kama wewe ni mtu mzima ila kwa umri ni pesa ndefu.
Nilikodisha 5 minutes kwa shilingi ishirini(Sh.20/=).kwa siku nilikuwa na uwezo wa kuingiza hadi shilingi 500~700 na kwa siku za weekend Jumamosi nilikuwa sikai nyumbani, naenda shule kupiga hela kwa kuwakodisha baiskeli wanzangu.

Naomba niwe mkweli hapa baada ya kuanzisha hiki kabiashara Kangu ka kukodisha baiskeli maisha ya shule niliyaona mazuri haina mfano. Usiku niliona unakuwa mrefu na asubuhi inachelewa muda wa kwenda shule. Ilifika hatua hadi siku ya Jumapili nilikuwa naichukia natamani Jumatatu ifike haraka nipige pesa.

Biashara iliendelea hadi namaliza elimu ya msingi. Ile siku nafanya mtihani wangu wa mwisho tu nilipofika nyumbani nilivunja kibubu changu nilichokificha chini ya uvungu wa kitanda. Sikuamini nilichokuwa nahesabu kwenye zile shillingi. Jumla nilipata kiasi cha Tsh. 326,700/=. Kusema kweli sikujuta kwenda shule.

Hapa kilipita kipindi kirefu cha kusubiri matokeo ya elimu ya msingi lakini katika kipindi hiki nilijaribu kufanya biashara kadhaa, mojawapo ile niliyokuwa nafanya mchikichini wakati naenda kupiga pindi la form one. Nilikuwa nauza zile karatasi ndefu za kufanyia mathematics kwa wale walipita kwa Aideni na Sir Mudi watakuwa wamenisoma.

MWAKA 2007
Tokeo limeshatoka na nilichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule moja maarufu hapa jijini Dar ipo katikati ya jiji(Mnazi mmoja). Nilikuwa na furaha sana kuingia sekondari lakini furaha kubwa ilikuwa kuangalia fursa gani naweza kuifanyia kazi huko shuleni.

Si Unajuwa tena ile Kinjuka njuka nafika shule mshamba mshamba wa mazingira shule ilibidi niwe mpole huku natumia macho ya tai kuangalia nini nifanye niwe napiga pesa pale shuleni.

Nilikuja kugundua fursa moja ambayo wanafunzi wengi walikuwa wanapenda sana ili kuweka kumbukumbu zao. Nilikuja kuipata karibu na siku ya graduation ya kidato cha nne ya mwaka 2007. Fursa hiyo si nyingine bali ni kuwa mpiga picha/cameraman.

Fasta nikaamua kuuza baiskeli yangu ile kwa sh.120,000/= nikaongeza kiasi kingine cha pesa, nikanunua camera mpya kabisa Kariakoo. Kazi rasmi ya kupiga picha ilianza shuleni siku ya graduation na siku zingine. Kwa kuwa nilikuwa nafanya discounts nilikamata wanafunzi wa shule yote wakawa wateja wangu. Nilinunua counterbook la 3 kwaya kwa ajili ya order za wateja.

Kuanzia shuleni kwangu, Jangwani sec, Zanaki sec, Kisutu sec, Azania sec, Benjamin sec, Dar es salaam sec nilikuwa napiga pesa ile mbaya hadi nilipata wapambe/walinzi wangu kama 7 saba hivi. Hawa walinzi ilikuwa kila nikienda shule nyingine ya jirani kupiga picha ilikuwa lazima niwachukue kwa ajili ya usalama wangu na kupata malipo yangu kwa uhakika. Kwa waliosoma Dar hasa zile shule za mjini kama vile Aza boy, Benjamin, Dar seko, Jamhuri, Kibasila na zingine wanafahamu kuwa kulikuwa na tabia za kindava sana kama mnyonge mnyonge ilikuwa lazima upate shida sana.

Kusema kweli maisha yangu ya sekondari yalikuwa mazuri sana sana, pesa ilikuwa haipigi chenga ilikuwa ya kutosha, wapembe walikuwepo wa kutosha lakini kizuri zaidi nilikula sana mademu.

Mwaka 2009 wakati nipo kidato cha 3, Anko wangu alikuja Bongo akitokea SA safari hii alikuja na academic books, vitabu vingi sana vya science akiamini napenda sana hayo masomo. Nakumbuka niliwahi kumwambia wakati nipo S/M kuwa ndoto yangu ni kuwa daktari Muhimbili. Hii ndoto ilizidi kupotea wakati nipo sekondari kwani hata masomo nilichukua ya mchepuo wa biashara.

MWAKA 2010:
Nilifanya mtihani wangu wa kidato cha nne. Nashukuru Mungu tokeo lilitoka nimefaulu nimechaguliwa advance Benjamin Sekondari.

Hapa Benjamin Sec ni uwanja wa nyumbani kwanza nilikuwa nakuja kupiga picha lakini hapakuwa mbali na shule yangu ya O level.

Nilifanya biashara kadhaa shuleni lakini kutokana na ugumu wa masomo ya advance niliamua kuacha kwa muda biashara na kuongeza umakini katika masomo.

Nilikuja kushtuka nipo kidato cha sita, kusema ule ukweli kabisa licha ya kuwa nilikuwa nipo busy na masomo lakini moyoni akili ilikuwa inawaza nini nifanye ili niwe naiingiza hela.

Kwa kipindi hiki wakati nipo kidato cha sita nilikuwa sifanyi biashara yoyote shuleni lakini uswahilini nilikuwa nafanya biashara ya kuuza opening shoes hasa za kike pale Buguruni chama.

Nilikuwa na Brother Ommy Aka Tembo, goli lilifunguliwa kuanzia saa 10 au 11 jioni hadi saa 5-6 Usiku. Kwa siku kuingiza laki 2-4 ni kawaida.

Mchana brother Tembo anaenda kuchukua mzigo Kariakoo ndani ndani huko kwa Wachina kwa 1200-1500 akirudii anajifungia ndani kutwa kufanya marekebisho madogo madogo jioni tunaingia mzigoni.

MWAKA 2012
Nilimaliza elimu yangu ya Advance, niliingia kitaa rasmi kufanya biashara. Niwe mkweli ile miaka miwili ya advance niliiona mingi sana na inanichelewesha kuingia in business world.

Nilipo kuwa kidato cha 5 na 6 nilikuwa najiuliza maswali mengi sana kuhusu aina ya elimu tuliyokuwa tunapata pale shuleni, tunasoma masomo ya biashara lakini mbona hatufundishwi namna kufanya biashara na kuingiza pesa.
Kusema kweli sikukuwa napenda kile tulichokuwa tunafundishwa shuleni.

Hivyo kumaliza elimu ya advance nilifurahi sana kwani ilikuwa inanichelewesha kuingia rasmi katika biashara.
Wakati nipo kidato cha sita mwisho mwisho nilijiapiza ya kuwa sitaendelea na elimu ya chuo kama nitachaguliwa kwa kuwa sitaendelea elimu ya chuo kikuu, haina shida kama sitajiunga na JKT.

Kwahyo nili drop chuo na JKT, kwani nilichaguliwa kujiunga na elimu ya juu lakini nilishakataa kusoma chuo kikuu.

INAENDELEA

MWAKA 2013

Maisha baada ya kudrop chuo.

Mara baada ya kuwambia wazazi kuwa sitaendelea na elimu ya juu(chuo kikuu) walinisema sana na kuona kuniona kama nimepotea njia lakini kwa kuwa nilijua ninachotaka katika maisha yangu hayanipa shida sana kelee zao.

Kwa kuwa nilishatangaza rasmi msimamo wangu kuhusu elimu ya chuo, anko aliyopo SA alinitumia nauli niweze kwenda kukaa huko. Nilienda SA.

Nilipofika katika ardhi ya watu sikutaka kujiingiza katika biashara, muda mwingi niliutumia kusoma vitabu mbalimbali.

Kusema kweli kwa kuwa nilijuwa kuwa naingia katika dunia ya biashara nikirudi Tanzania basi muda nwingi niliutumia kusoma vitabu mbalimbali vya Personal Development, Financial Education, Human psychology, Human relation, Negotiation, Books of Biograph, na vingine vingi.

Hapa ndipo niliwasoma ma Guru katika biashara.
Kama Andrew Carnegie.

MWAKA 2014
Nilirudi bongo Tanzania sasa rasmi kuingia katika biashara bila kikwazo cha aina yoyote ile. Kwangu kusoma kulikuwa kikwazo sana katika kufanikiwa katika Maisha yangu. Nakumbuka wakati narudi Tanzania nilikuwa na akiba ya Tsh 380000/= ambayo niliingia katika Kuanza biashara sasa.

Nashukuru kwa kuwa viji biashara nilianza kitambo, machimbo mengi ya hapa mjini hayakunipa shida, niliongea na brother Tembo akanipa taarifa zote namna ya kuingia mzigoni. Tarehe 12/6/2014 niliingia Karikaoo kununua mali(mzigo), nguo za ndani za wadada, taiti, bra na opening shoes nikawa namwaga zangu Buguruni chama.

Kwa kuwa nilikuwa na ndoto za kuwa mfanya biashara mkubwa nilihakikisha sicheki na kima katika kipato ninachopata kwa kuziba mianya yote ya kuchukua ngawira zangu. Nakumbuka nilikuwa nakula milo miwili tu, sometime hata mmoja ili niweze kuweka akiba.
Baada ya mwaka mmoja nilikuza msingi wa biashara kutoka Sh 380,000/=hadi Mil.2 640,200//=. Kwangu Haya yalikuwa mafanikio makubwa sana.

Hakuna mtu aliyefanikiwa kwa kuwa na chanzo kimoja cha mapato ndani ya huo nilianzisha kufuga kuku View attachment 1408551

Licha ya kuwa kulikuwa na changamoto katika kuwatunza nilihakikisha natoa hadi tone la mwisho la damu ili nifaulu vizuri kwenye kuku.
Na kusema ukweli nilifanikiwa licha ya changamoto kadhaa. Nikawa nauza na wengine nachomesha mwenyewe kwa kutafuta kijana wa kufanya kazi hiyo.

Mwaka 2015 uliisha kwa mafanikio makubwa sana nilivuka malengo yangu, hivyo nilijipanga kuingia mwaka 2016 kwa kashindo kikubwa.

MWAKA 2016

Safari ya kwenda kusini mwa Tanzania. Ndani ya mwaka 2016 niliweka malengo makubwa sana ikiwa pamoja na kukuza kipato changu na kuanzisha miradi mingine kama miwili hivi. Nikiweka malengo sina tabia ya mapenzi, huwa natupa kule.

Brother Tembo ni mtu wa kusini(Mtwara) Kwa hiyo mara inapofika msimu wa korosho huwa anapeleka bidhaa mbalimbali huko, sasa huu mwaka nilimwambia na mimi nataka twende pamoja Mtwara. Nilijiandaa golini kwangu Buguruni nilimuweka mwanangu mmoja hivi ambaye amemaliza degree yake na hana mbele wala nyuma.

Ilipofika mwezi wa 11 tulizama Kusini/Mtwara sana, nikiwa nimefunga mzigo wa Sh.Mil 9 kuanzia Sandroz za kiume, boksa, bra, open shoes, tyt, Madela, mikoba, jeans na vingine kibao.

Mtwara kipindi cha msimu kunakuwa na pesa jamani. Japokuwa ulikuwa msimu wangu wa kwanza kwenda Mtwara ila hadi msimu unaisha nilitoboa tobo la maana sana. Nilianza na mil.9 lakini hadi msiimu unaisha nina mil.17 na lupea kadhaa. Wamakonde wakiwa na hela wananunua tena bila kuomba punguzo hata kidogo.

Mwenyeji wangu alinisadia sana kupata ka fresh ambacho nilikodi kwa muda mfupi tu, lakini kutokana na ucheshi wangu nilipata marafiki wengi sana huko pia nilinunua mashamba kadhaa ya mikorosho huko kusini. Mmoja ya watu ambao nilikutana nao na nashukuru sana kufahamiana nae nini Boss Msham, huyu jamaa aliinipa madini yote kuanzia Mtwara(korosho), Lindi-liwale, kilwa(Ufuta) na Masasi Mbaazi. Jamani watu wanapiga pesa huko mikoani.

Baada ya msimu kuisha nilirudi zangu Dar kupumzika kwa siku kadhaa kisha nikaaingia tena zangu Buguruni kwenye goli langu nililomwachia jamaaa. Nilikuta bado anapiga vitu fresh tu, kwenye hii ofisi nikamwacha yeye mimi nikafungua ofisi nyingine.

Ile pesa niliyopata kule kwenye korosho haikuchezewa kwani Boss Msham alinipanga kuwa mwezi wa 4-5 Kusini hasa mkoani Lindi kuna anza kuvunwa ufuta. Kwa hiyo kwa kupitia jamaa niliweka ahadi ya kununua na mimi. Kwa kuwa jamaa alikuwa mzoefu nilipanga kumtumia na mimi niingie katika kununua mazao huko kwao.

MWAKA 2017
Nilirudi rasmi kusini katika mkoa wa Lindi kwa ajili ya kununua zao la ufuta. Niliingia na mtaji wangu mdogo tu wa mil 15, nasema mdogo kwa sababu kuna wafanyabiashara wa huko wakubwa wenye mitaji ya mil.100-300 wana nunua ufuta, lakini pia kuna wahindi kibao hawa wa Kariakoo wanajazana huko kusini kwa ajili ya kununua ufuta.

Kusema kweli bahati ilikuwa upande wangu kupitia jamaa alinipatia badhii ya brokers wake huko vijijini na mimi walinunulia ufuta hadi pesa yangu ilipoisha.
 
feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
5,364
2,000
Hongera kwa kuwa umefikiria nje ya boksi japo hatuwezi lingana kwenye mipango na maono.

Sasa mkuu hebu tuambie mpaka sasa una kipi ambacho ni mafanikio kwako si lazima iwe nyumba na gari nahitaji kujua maendeleo ya unachokifanya na unafanya hicho hicho ulichotuambia au una kingine?

Pia kwenye stori nzima hatujasikia changamoto yoyote uliyowahi kukutana kwenye biashara zako mbali na hizo za shule kukubana je, hukuwahi kupata? Na kama ulipata ulitatuaje?

Tueleze yale tusiyojua kwa ufupi kwenye biashara mfano unakuta mtu anakwambia nilianza na lita 10 za petrol ndani ya mwaka mmoja nikawa na petrol station bila ya kutuambia mchakato ulikuaje?

Nisaidie au tusaidie mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Liverpool_Jr

JF-Expert Member
Sep 7, 2019
1,222
2,000
Moyo na akili yangu vimenisukuma kuandika haya baada ya kuona kuna uongo mkubwa katika jamii hasa kwa vijana,kuwa ukiwa na elimu kubwa ya darasani basi una uhakika wa kufanikiwa kimaisha kitu ambacho si kweli.
If a man repeats a lie
over and over,he will eventually accept the lie as truth.Moreover he will believe it to be truth.

NOTE.
Naomba nieleweke kuwa sina lengo la kukosoa,kutukana,kukejeli au aina yoyote ile mbaya ila nataka kuwaonyesha vijana wenzangu upande wa pili wa shilingi(Another side of coin).

My personal story.

Mwaka 2000 nilianza elimu yangu ya msingi katika shule ya msingi x.Kusema kweli maisha ya shule yalikuwa mazuri kwa siku za mwanzo lakini kadri siku zilivyozidi ,maisha yangu ya shule niliyaona magumu sana na hii ilitokana na changamoto mbalimbali hasa ya usafiri.Kwa wale waliosoma shule Dar nadhani watakuwa wamenielewa.

~Biashara yangu ya kwanza shuleni.
(My first entrepreneur journey)

Mwaka 2004 wakati nipo darasa la 5 Mjomba angu ambaye alikuwa South Afrika alikuja Bongo,aliniletea zawadi ya baiskeli ambayo nilianza kuitumia kwenda nayo shule kila siku.
Wakati nipo shuleni wanafunzi wenzangu walikuwa wanaomba baiskeli ,hapa nikagundua kuwa naweza ku make money kupitia baiskeli yangu.

Ule muda wa mapumziko ya chai wanafunzi wenzangu walikuwa wananifuata nawakodisha baiskeli waendeshe alafu wanalipa pesa. Kwa wakati Ule haikikuwa pesa nyingi sana kama wewe ni mtu mzima ila kwa umri ni pesa ndefu.
Nilikodisha 5 minutes kwa shilingi ishirini(Sh.20/=).kwa siku nilikuwa na uwezo wa kuingiza hadi shilingi 500~700,Na kwa siku za weekend jumamosi nilikuwa sikai nyumbani,naenda shule kupiga hela kwa kuwakodisha baiskeli wanzangu

Naomba niwe mkweli hapa.Baada ya kuanzisha hiki kabiashara Kangu ka kukodisha baiskeli maisha ya shule niliyaona mazuri haina mfano.Usiku niliona unakuwa mrefu na asubuhi inachelewa muda wa kwenda shule.
Ilifika hatua hadi siku ya jumapili nilikuwa naichukia Natamani jumatatu ifike haraka nipige pesa.

Biashara iliendelea hadi namaliza elimu ya msingi.Ile siku nafanya mtihani wangu wa mwisho tu nilipofika nyumbani nilivunja kibubu changu nilichokificha chini ya uvungu wa kitanda. Sikuamini nilichokuwa nahesabu kwenye zile shillingi,Jumla nilipata kiasi cha Tsh. 326,700/=. Kusema kweli sikujuta kwenda shule.

Hapa kilipita kipindi kirefu cha kusubiri matokeo ya elimu ya msingi lakani katika kipindi hiki nilijaribu kufanya biashara kadhaa,mojawapo ile niliyokuwa nafanya mchikichini wakati naenda kupiga pindi la form one.
Nilikuwa nauza zile karatasi ndefu za kufanyia mathematics kwa wale walipita kwa Aideni na Sir Mudi watakuwa wamenisoma.

Mwaka 2007.

Tokeo limeshatoka na nilichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule moja maarufu hapa jijini Dar ipo katikati ya jiji(Mnazi mmoja).

Nilikuwa na furaha sana kuingia sekondari lakini furaha kubwa ilikuwa kuangalia fursa gani naweza kuifanyia kazi huko shuleni.
Si Unajuwa tena ile Kinjuka njuka nafika shule mshamba mshamba wa mazingira shule ilibidi niwe mpole huku natumia macho ya tai kuangalia nini nifanye niwe napiga pesa pale shuleni.

Nilikuja kugundua fursa moja ambayo wanafunzi wengi walikuwa wanapenda sana ili kuweka kumbukumbu zao.Nilikuja kuipata karibu na siku ya graduation ya kidato cha nne ya mwaka 2007. Fursa hiyo si nyingine bali ni kuwa mpiga picha/cameraman.

Fasta nikaamua kuuza baiskeli yangu ile kwa sh.120,000/= nikaongeza kiasi kingine cha pesa, nikanunua camera mpya kabisa kariakoo.Kazi rasmi ya kupiga picha ilianza shuleni siku ya graduation na siku zingine.Kwa kuwa nilikuwa nafanya discounts nilikamata wanafunzi wa shule yote wakawa wateja wangu.Nilinunua counterbook la 3 kwaya kwa ajili ya order za wateja.

Kaunzia shuleni kwangu, Jangwani sec,Zanaki sec,Kisutu sec,Azania sec,Benjamin sec,Dar es salaam sec nilikuwa napiga pesa ile mbaya hadi nilipata wapambe/walinzi wangu kama 7 saba hivi.Hawa walinzi ilikuwa kila nikienda shule nyingine ya jirani kupiga picha ilikuwa lazima niwachukue kwa ajili ya usalama wangu na kupata malipo yangu kwa uhakika.Kwa waliosoma Dar hasa zile shule za mjini kama vile Aza boy,Benjamin,Dar seko,Jamhuri,kibasila, na zingine wanafahamu kuwa kulikuwa na tabia za kindava sana,kama mnyonge mnyonge ilikuwa lazima upate shida sana.

Kusema kweli maisha yangu ya sekondari yalikuwa mazuri sana sana,Pese ilikuwa haipigi chenga ilikuwa ya kutosha,wapembe walikuwepo wa kutosha lakini kizuri zaidi nilikula sana mademu.

Mwaka 2009 wakati nipo kidato cha 3,Anko wangu alikuja bongo akitokea SA safari hii alikuja na academic books,vitabu vingi sana vya science akiamini napenda sana hayo masomo,nakumbuka niliwahi kumwambia wakati nipo S/m kuwa ndoto yangu ni kuwa daktari Muhimbili. Hii ndoto ilizidi kupotea wakati nipo sekondari kwani hata masomo nilichukua ya mchepuo wa biashara.

Mwaka 2010:
Nilifanya mtihani wangu wa kidato cha nne. Nashukuru Mungu tokeo lilitoka nimefaulu nimechaguliwa advance Benjamin sekondari.

Hapa Benjamin sec ni uwanja wa nyumbani kwanza nilikuwa nakuja kupiga picha lakini hapakuwa mbali na shule yangu ya O level.

Nilifanya biashara kadhaa shuleni lakini kutokana na ugumu wa masomo ya advance niliamua kuacha kwa muda biashara na kuongeza umakini katika masomo.

Nilikuja kushtuka nipo kidato cha sita,kusema ule ukweli kabisa licha ya kuwa nilikuwa nipo busy na masomo lakini moyoni akili ilikuwa inawaza nini nifanye ili niwe naiingiza hela.

Kwa kipindi hiki wakati nipo kidato cha sita nilikuwa sifanyi biashara yoyote shuleni lakini uswahilini nilikuwa nafanya biashara ya kuuza opening shoes hasa za kike pale Buguruni chama.

Nilikuwa na Brother Ommy Aka Tembo goli lilifunguliwa kuanzia saa 10 au 11 jioni hadi saa 5-6 Usiku.Kwa siku kuingiza laki 2-4 ni kawaida.

Mchana brother Tembo anaenda ku chukua mzigo kariakoo ndani ndani huko kwa wachina kwa 1200-1500 akirudii anajifungia ndani kutwa kufanya marekebisho madogo madogo jioni tunaingia mzigoni.

Mwaka 2012.
Nilimaliza elimu yangu ya Advance,niliingia kitaa rasmi kufanya biashara.Niwe mkweli ile miaka miwili ya advance niliiona mingi sana na inanichelewesha kuingia in business world.

Nilipo kuwa kidato cha 5 na 6 nilikuwa najiuliza maswali mengi sana kuhusu aina ya elimu tuliyokuwa tunapata pale shuleni,tunasoma masomo ya biashara lakini mbona hatufundishwi namna kufanyaa biashara na kuingiza pesa.
Kusema kweli siku kuwa Napenda kile tulichokuwa tunafundishwa shuleni.

Hivyo kumaliza elimu ya advance nilifurahi sana kwani ilikuwa inanichelewesha kuingia rasmi katika biashara.
Wakati nipo kidato cha sita mwisho mwisho nilijiapiza ya kuwa sitaendelea na elimu ya chuo kama nitachaguliwa,kwa kuwa sitaendedelea elimu ya chuo kikuu haina shida kama sitajiunga na JKT.

Kwahyo nili drop chuo na Jkt,kwani nilichaguliwa kujiunga na elimu ya juu lakini nilishakataa kusoma chuo kikuu.
Nakupinga..
Binafsi nimejiajiri ila hii fursa niliipata wakati nasoma Masters..

#YNEA

Wrote from Anfield..!!
 
6321

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
429
1,000

Hiyo advance ulipata grade gan? Naomba ushahid wa picha ukinionyesha Cheti chako ficha vingine vyoote acha grade na Jina la shule, 2. Mafanikio kwako unaya tafsiri vip?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
forumyangu

JF-Expert Member
Dec 25, 2016
2,147
2,000
Mwaka 2013.

Maisha baada ya kudrop chuo.

Mara baada ya kuwambia wazazi kuwa sitaendelea na elimu ya juu(chuo kikuu) walinisema sana na kuona kuniona kama nimepotea njia.Lakini kwa kuwa nilijuwa ninachotaka katika maisha yangu hayanipa shida sana kelee zao.

Kwa kuwa nilishatangaza rasmi msimamo wangu kuhusu elimu ya chuo,anko aliyopo SA alinitumia nauli niweze kwenda kukaa huko.Nilienda SA.

Nilipofika katika ardhi ya watu sikutaka kujiingiza katika biashara,muda mwingi niliutumia kusoma vitabu mbalimbali.

Kusema kweli kwa kuwa nilijuwa kuwa naingia katika dunia ya biashara nikirudi TZ basi muda nwingi niliutumia kusoma vitabu mbalimbali vya Personal Development,Financial Education,Human psychology,Human relation,Negotiation,Books of Biograph, na vingine vingi.

Hapa ndipo niliwasoma ma Guru katika biashara.
Kama Andrew Carnegie.

Mwaka 2014.
Nilirudi bongo TZ sasa rasmi kuingia katika biashara bila kikwazo cha aina yoyote ile.Kwangu kusoma kulikuwa kikwazo sana katika kufanikiwa katika Maisha yangu.
Nakumbuka wakati narudi TZ nilikuwa na akiba ya Tsh 380000/= ambayo niliingia katika Kaunza biashara sasa.
Nashukuru kwa kuwa viji biashara nilianza kitambo machimbo mengi ya hapa mjini haya kunipa shida,niliongea na brother Tembo akanipa taarifa zote namna ya kuingia mzigoni.Tarehe 12/6/2014 niliingia karikaoo kununua mali(mzigo),nguo za ndani za wadada,taiti,bra na opening shoes nikawa namwaga zangu buguruni chama.

Kwa kuwa nilikuwa na ndoto za kuwa mfanya biashara mkubwa nilihakikisha sicheki na kima katika kipato ninachopata kwa kuziba mianya yote ya kuchukua ngawira zangu.Nakumbuka nilikuwa nakula milo miwili tu,sometime hata mmoja ili niweze kuweka akiba.
Baada ya mwaka mmoja nili kuza msingi wa biashara kutoka Sh 380000/=hadi Hadi Mil.2 640,200//=.Kwangu Haya yalikuwa mafanikio makubwa sana.

Hakuna mtu aliyefanikiwa kwa kuwa na chanzo kimoja cha mapato ndani ya huo nilianzisha kufuga kuku
IMG_2686.JPG
Licha ya kuwa kulikuwa na changamoto katika kuwatunza nilihakikisha natoa hadi tone la mwisho la damu ili nifaulu vzr kwenye kuku.
Na kusema ukweli nilifanikiwa licha ya changamoto kadhaa.
Nikawa nauza na wengine nachomesha mwenyewe kwa kutafuta kijana wa kufanya kazi hiyo.

Mwaka 2015 uliisha kwa mafanikio makubwa sana nilivuka malengo yangu,hivyo nilijipanga kuingia mwaka 2016 kwa kashindo kikubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MSUKUMA02

Senior Member
Dec 12, 2011
164
250
Sasa mkuu mbona hukuwa umedrop O level au A level ili upate hayo mafanikio ya biashara zako alafu unaleta uzi wa habari za kudrop chuo

Naona unataka kuwalisha matango pori vijana waachane na chuo unashindwa kuelewa huyo atakaye drop chuo huenda hatma yake ipo huko kwenye elimu alafu wewe unavutia upande wako

Alafu pili kiufupi wewe umeacha tu chuo lakini una elimu tosha maana umesoma kuanzia primary hadi kidato cha sita

Cha mwisho acha kuwadanganya madogo wapige chini chuo wafuate upuuzi huu maana hujaelezea ni mafanikio gani uliyoyapata hadi hii leo na umesaidia nini katika jamii inayokuzunguka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
6321

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
429
1,000
Moyo na akili yangu vimenisukuma kuandika haya baada ya kuona kuna uongo mkubwa katika jamii hasa kwa vijana,kuwa ukiwa na elimu kubwa ya darasani basi una uhakika wa kufanikiwa kimaisha kitu ambacho si kweli.
If a man repeats a lie
over and over,he will eventually accept the lie as truth.Moreover he will believe it to be truth.

NOTE.
Naomba nieleweke kuwa sina lengo la kukosoa,kutukana,kukejeli au aina yoyote ile mbaya ila nataka kuwaonyesha vijana wenzangu upande wa pili wa shilingi(Another side of coin).

My personal story.

Mwaka 2000 nilianza elimu yangu ya msingi katika shule ya msingi x.Kusema kweli maisha ya shule yalikuwa mazuri kwa siku za mwanzo lakini kadri siku zilivyozidi ,maisha yangu ya shule niliyaona magumu sana na hii ilitokana na changamoto mbalimbali hasa ya usafiri.Kwa wale waliosoma shule Dar nadhani watakuwa wamenielewa.

~Biashara yangu ya kwanza shuleni.
(My first entrepreneur journey)

Mwaka 2004 wakati nipo darasa la 5 Mjomba angu ambaye alikuwa South Afrika alikuja Bongo,aliniletea zawadi ya baiskeli ambayo nilianza kuitumia kwenda nayo shule kila siku.
Wakati nipo shuleni wanafunzi wenzangu walikuwa wanaomba baiskeli ,hapa nikagundua kuwa naweza ku make money kupitia baiskeli yangu.

Ule muda wa mapumziko ya chai wanafunzi wenzangu walikuwa wananifuata nawakodisha baiskeli waendeshe alafu wanalipa pesa. Kwa wakati Ule haikikuwa pesa nyingi sana kama wewe ni mtu mzima ila kwa umri ni pesa ndefu.
Nilikodisha 5 minutes kwa shilingi ishirini(Sh.20/=).kwa siku nilikuwa na uwezo wa kuingiza hadi shilingi 500~700,Na kwa siku za weekend jumamosi nilikuwa sikai nyumbani,naenda shule kupiga hela kwa kuwakodisha baiskeli wanzangu

Naomba niwe mkweli hapa.Baada ya kuanzisha hiki kabiashara Kangu ka kukodisha baiskeli maisha ya shule niliyaona mazuri haina mfano.Usiku niliona unakuwa mrefu na asubuhi inachelewa muda wa kwenda shule.
Ilifika hatua hadi siku ya jumapili nilikuwa naichukia Natamani jumatatu ifike haraka nipige pesa.

Biashara iliendelea hadi namaliza elimu ya msingi.Ile siku nafanya mtihani wangu wa mwisho tu nilipofika nyumbani nilivunja kibubu changu nilichokificha chini ya uvungu wa kitanda. Sikuamini nilichokuwa nahesabu kwenye zile shillingi,Jumla nilipata kiasi cha Tsh. 326,700/=. Kusema kweli sikujuta kwenda shule.

Hapa kilipita kipindi kirefu cha kusubiri matokeo ya elimu ya msingi lakani katika kipindi hiki nilijaribu kufanya biashara kadhaa,mojawapo ile niliyokuwa nafanya mchikichini wakati naenda kupiga pindi la form one.
Nilikuwa nauza zile karatasi ndefu za kufanyia mathematics kwa wale walipita kwa Aideni na Sir Mudi watakuwa wamenisoma.

Mwaka 2007.

Tokeo limeshatoka na nilichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule moja maarufu hapa jijini Dar ipo katikati ya jiji(Mnazi mmoja).

Nilikuwa na furaha sana kuingia sekondari lakini furaha kubwa ilikuwa kuangalia fursa gani naweza kuifanyia kazi huko shuleni.
Si Unajuwa tena ile Kinjuka njuka nafika shule mshamba mshamba wa mazingira shule ilibidi niwe mpole huku natumia macho ya tai kuangalia nini nifanye niwe napiga pesa pale shuleni.

Nilikuja kugundua fursa moja ambayo wanafunzi wengi walikuwa wanapenda sana ili kuweka kumbukumbu zao.Nilikuja kuipata karibu na siku ya graduation ya kidato cha nne ya mwaka 2007. Fursa hiyo si nyingine bali ni kuwa mpiga picha/cameraman.

Fasta nikaamua kuuza baiskeli yangu ile kwa sh.120,000/= nikaongeza kiasi kingine cha pesa, nikanunua camera mpya kabisa kariakoo.Kazi rasmi ya kupiga picha ilianza shuleni siku ya graduation na siku zingine.Kwa kuwa nilikuwa nafanya discounts nilikamata wanafunzi wa shule yote wakawa wateja wangu.Nilinunua counterbook la 3 kwaya kwa ajili ya order za wateja.

Kaunzia shuleni kwangu, Jangwani sec,Zanaki sec,Kisutu sec,Azania sec,Benjamin sec,Dar es salaam sec nilikuwa napiga pesa ile mbaya hadi nilipata wapambe/walinzi wangu kama 7 saba hivi.Hawa walinzi ilikuwa kila nikienda shule nyingine ya jirani kupiga picha ilikuwa lazima niwachukue kwa ajili ya usalama wangu na kupata malipo yangu kwa uhakika.Kwa waliosoma Dar hasa zile shule za mjini kama vile Aza boy,Benjamin,Dar seko,Jamhuri,kibasila, na zingine wanafahamu kuwa kulikuwa na tabia za kindava sana,kama mnyonge mnyonge ilikuwa lazima upate shida sana.

Kusema kweli maisha yangu ya sekondari yalikuwa mazuri sana sana,Pese ilikuwa haipigi chenga ilikuwa ya kutosha,wapembe walikuwepo wa kutosha lakini kizuri zaidi nilikula sana mademu.

Mwaka 2009 wakati nipo kidato cha 3,Anko wangu alikuja bongo akitokea SA safari hii alikuja na academic books,vitabu vingi sana vya science akiamini napenda sana hayo masomo,nakumbuka niliwahi kumwambia wakati nipo S/m kuwa ndoto yangu ni kuwa daktari Muhimbili. Hii ndoto ilizidi kupotea wakati nipo sekondari kwani hata masomo nilichukua ya mchepuo wa biashara.

Mwaka 2010:
Nilifanya mtihani wangu wa kidato cha nne. Nashukuru Mungu tokeo lilitoka nimefaulu nimechaguliwa advance Benjamin sekondari.

Hapa Benjamin sec ni uwanja wa nyumbani kwanza nilikuwa nakuja kupiga picha lakini hapakuwa mbali na shule yangu ya O level.

Nilifanya biashara kadhaa shuleni lakini kutokana na ugumu wa masomo ya advance niliamua kuacha kwa muda biashara na kuongeza umakini katika masomo.

Nilikuja kushtuka nipo kidato cha sita,kusema ule ukweli kabisa licha ya kuwa nilikuwa nipo busy na masomo lakini moyoni akili ilikuwa inawaza nini nifanye ili niwe naiingiza hela.

Kwa kipindi hiki wakati nipo kidato cha sita nilikuwa sifanyi biashara yoyote shuleni lakini uswahilini nilikuwa nafanya biashara ya kuuza opening shoes hasa za kike pale Buguruni chama.

Nilikuwa na Brother Ommy Aka Tembo goli lilifunguliwa kuanzia saa 10 au 11 jioni hadi saa 5-6 Usiku.Kwa siku kuingiza laki 2-4 ni kawaida.

Mchana brother Tembo anaenda ku chukua mzigo kariakoo ndani ndani huko kwa wachina kwa 1200-1500 akirudii anajifungia ndani kutwa kufanya marekebisho madogo madogo jioni tunaingia mzigoni.

Mwaka 2012.
Nilimaliza elimu yangu ya Advance,niliingia kitaa rasmi kufanya biashara.Niwe mkweli ile miaka miwili ya advance niliiona mingi sana na inanichelewesha kuingia in business world.

Nilipo kuwa kidato cha 5 na 6 nilikuwa najiuliza maswali mengi sana kuhusu aina ya elimu tuliyokuwa tunapata pale shuleni,tunasoma masomo ya biashara lakini mbona hatufundishwi namna kufanyaa biashara na kuingiza pesa.
Kusema kweli siku kuwa Napenda kile tulichokuwa tunafundishwa shuleni.

Hivyo kumaliza elimu ya advance nilifurahi sana kwani ilikuwa inanichelewesha kuingia rasmi katika biashara.
Wakati nipo kidato cha sita mwisho mwisho nilijiapiza ya kuwa sitaendelea na elimu ya chuo kama nitachaguliwa,kwa kuwa sitaendedelea elimu ya chuo kikuu haina shida kama sitajiunga na JKT.

Kwahyo nili drop chuo na Jkt,kwani nilichaguliwa kujiunga na elimu ya juu lakini nilishakataa kusoma chuo kikuu.
Hiyo advance ulipata grade gan? Naomba ushahid wa picha ukinionyesha Cheti chako ficha vingine vyoote acha grade na Jina la shule, 2. Mafanikio kwako unaya tafsiri vip?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dr Dre

JF-Expert Member
May 23, 2015
1,571
2,000
Sasa mkuu mbona hukuwa umedrop O level au A level ili upate hayo mafanikio ya biashara zako alafu unaleta uzi wa habari za kudrop chuo

Naona unataka kuwalisha matango pori vijana waachane na chuo unashindwa kuelewa huyo atakaye drop chuo huenda hatma yake ipo huko kwenye elimu alafu wewe unavutia upande wako

Alafu pili kiufupi wewe umeacha tu chuo lakini una elimu tosha maana umesoma kuanzia primary hadi kidato cha sita

Cha mwisho acha kuwadanganya madogo wapige chini chuo wafuate upuuzi huu maana hujaelezea ni mafanikio gani uliyoyapata hadi hii leo na umesaidia nini katika jamii inayokuzunguka

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kuwa negative kihivyo mkuu, wapi amesema watu waache chuo
 
forumyangu

JF-Expert Member
Dec 25, 2016
2,147
2,000
Mwaka 2016.

Safari ya kwenda kusini mwa Tz.
Ndani ya mwaka 2016 niliweka malengo makubwa sana ikiwa pamoja na kukuza kipato changu na kuanzisha miradi mingine kama miwili hivi.
Nikiweka malengo sina tabia ya mapenzi,huwa natupa kule.

Brother Tembo ni mtu wa kusini(Mtwara) Kwahy mara inapofika msimu wa korosho huwa anapeleka bidhaa mbalimbali huko,sasa huu mwaka nilimwambia na mimi nataka twende pamoja Mtwara.
Nilijiandaa golini kwangu Buguruni nilimuweka mwanangu mmoja hivi ambaye amemaliza degree yake na hana mbele wala nyuma.

Ilipofika mwezi wa 11 tulizama kusini/Mtwara sana,nikiwa nimefunga mzigo wa Sh.Mil 9 kuanzia Sandroz za kiume,boksa,bra,open shoes,tyt,Madela,mikoba,jeans na vingine kibao.
Mtwara kipindi cha msimu kuna kuwa na pesa jamani.Japo kuwa ulikuwa msimu wangu wa kwanza kwenda mtwara ila hadi msimu unaisha nilitoboa tobo la maana sana.Nilianza na mil.9 lakini hadi msiimu unaisha nina mil.17 na lupea kadhaa.
Wamakonde wakiwa na hela wananunua tena bila kuomba punguzo hata kidogo.

Mwenyeji wangu alinisadia sana kupata ka fresh ambacho nilikodi kwa muda mfupi tu,lakini kutokana na ucheshi wangu nilipata marafiki wengi sana huko,pia nilinunua mashamba kadhaa ya mikorosho huko kusini.
Mmoja ya watu ambao nilikutana nao na Nashukur sana kufahamiana nae nini Boss Msham,huyu jamaa aliinipa madini yote kuanziia mtwara(korosho),Lindi-liwale,kilwa(Ufuta) na Masasi Mbaazi.Jamani watu wanapiga pesa huko mikoani.

Baada ya msimu kuisha nilirudi zangu Dar ku pumzika kwa siku kadhaa kisha nikaaingia tena zangu Buguruni kwenye goli langu nililomwachia jamaaa.
Nilikuta bado anapiga vitu fresh tu,kwenye hii ofisi nikamwacha yeye mimi nikafungua ofisi nyingine.

Ile pesa niliyopata kule kwenye korosho haikuchezewa kwani Boss Msham alinipanga kuwa mwezi wa 4-5 kusini hasa mkoani Lindi kuna anza kuvunwa ufuta.Kwahiyo kwa kupitia jamaa niliweka ahadi ya kununua na mimi.
Kwa kuwa jamaa alikuwa mzoefu nilipanga kumtumia na mimi niingie katika kununua mazao huko kwao.

Mwaka 2017.
Nilirudi rasmi kusini katika mkoa wa lindi kwa ajili ya kununua zao la ufuta.
Niliingia na mtaji wangu mdogo tu wa mil 15,nasema mdogo kwa sababu kuna wafanya biashara wa huko wakubwa wenye mitaji ya mil.100-300 wana nunua ufuta,lakini pia kuna wahindi kibao hawa wa kariakoo wanajazana huko kusini kwa ajili ya kununua ufuta.
Kusema kweli bahati ilikuwa upande wangu kupitia jamaa alinipatia badhii ya brokers wake huko vijijini na mimi walinunulia ufuta hadi pesa yangu ilipoisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
2,941
2,000
Elimu ni silaha mojwapo ya kutafuta ukwasi,
Hata kama Mbunge Mh Mkulima hana elimu ya chuo kikuu,na amekuwa tajiri,tusisahau elimu ilipomfikisha mzee Mengi,elimu ndio ilimpa uzoefu mpaka akaanzisha makampuni yake,
Mzee Mfuruki,alisoma ujerumani,akafanya kazi kiwanda cha Benzi,akarudi nyumbani kuanzisha kampuni yake,je angebaki kijijini akichunga ng'ombe,Angeupata utajiri kama wa Mh msukuma?ur guess is as good as mine,no one can tell for sure,
Elimu ni muhimu,kama huna zipo njia nyingine za kupata ukwasi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom