Najivunia kuacha chuo. Kijana mwenzangu, huhitaji shahada kufanikiwa kimaisha (to be rich)

mkuu umedanganya huwez maliza 2012 ikiwa umeanza 2000 futilia taarifa zako
 
Acha kujidanganya ndugu.
Maisha yana fomula kama huko chuo ndo mnaambiwa hivyo basi ilikuwa kwangu sahihi kabisa ku drop chuo


Sent using Jamii Forums mobile app
Maisha kutokuwa na formula..maana Yake Sio wote tutatumia Pythagoras Theorem kufika solution sahisi..Bali kila mtu atatumia njia yake ambayo yeye anaona inafaa kufikia mafanikio.
 
Kufuata unacho amini sio tatizo , lakini shida inakuja pale unapotumia nguvu kubwa kuwalizimisha watu wakufuate , go ur self....wasomi ndio wanotuendeshea dunia hii
 
Nashukuru sana.

Mafanikio yapo kwani nilipoanza sio sawa na hapa nilipo sasa.Haya kwangu ni mafanikio makubwa sana.
Tangu nipo shule ya msingi nilikuwa napenda nifanye kitu/kutatua tatzo ili nipate pesa lakini mimi nimesaidia tatizo hilo,kwahy nimewasaidia wengi sana katika umri wangu huu niliokuwa nao.

Nimefakiwa kuajiri watu kama 12 hadi saa directy.Katika hao 12,5 wanafamilia zao ambao zinawategemea kwa kila kitu.Hii kwangu ni mafanikio.

Ila nina mtandao mkubwa sana wa kupata taarifa mbalimbali za biashara ambazo zinanisaidia kutambua fursa wapi ilipo na namna ya ku achiev hiyo fursa.

Ila kikubwa nilikuwa napenda niwe na freedom katika maisha yangu hasa financial freedom Nashukuru nimepata uhuru ninao utaona.

Mafanikio yapo mengi sana


Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo biashara ya mazao, mfano ufuta, wewe unakiwa ni middle man?
 
fikra za kijinga kabisa hizi tena mawazo na akili kama hizi wanazo waarabu, ndiyo maana pamoja na utajili wao walionao bado wanatawaliwa na wamarekani na waisrael
 
Mwaka 2020.
Mafanikio yangu.

Licha ya changamoto kadhaa nilizopitia katika safiri ambayo bado sija fika mwisho,nimepata mafanikio mengi sana tena sana.

1~Nimepata connections na watu wengi ambao ni productive na Money maker.

2~Nimepata knowledge kubwa sana ambao hauwez kupatikana darasani hata ukisoma miaka 20.Lakini knowledge hii unaipata ukiwa unapambana na maisha.

3~ukiacha materials thing(Nyumba kadhaa,usafiri,n.k) naweza kwenda bank na kuchukua hata mil 150-200 kitu ambacho ni wasomi wachache na wafanyakazi ambao wanaweza kukopesheka kiasi hicho cha pesa.

Hapa mwezi huu nimepanga nizame bank nikachukue mil.80 kwa ajili ya kununua ufuta huko Lindi.




Sent using Jamii Forums mobile app
SITAKI KUKUKOSOA ila nataka mikupe ufahamu mmoja ili uache kufanya reference kwa wasomi kwenye vitu vinavyohusu mafanikio ya kimaisha.

Mkuu..ili ufanikiwe kuna njia nyingi, kama vile biashara, elimu, mziki, mpira, uigizaji, n.k...Hizi zote ni njia halali kabisa na zenye lengo moja la kutoboa kimaisha...Ukishindwa nia moja unaenda njia nyingine tena fresh kabisa...Kwamfano wewe hapo, plan A yako ilikuwa ni elimu ila ukaona haifai ukajaribu plan B then ime work out na umetoboa..HONGERA SANA.

Lakini usisahau kuwa kuna mtu sasa hivi ana historia kama yako, plan A yake ilikuwa Biashara ila pengine ilifeli akaamua kurudi shule (plan B) na akatoboa....

HOJA yangu ni kwamba, kwanini jamii inamuona mtu aliyesoma na kufeli maisha kama LOOSER tofauti na aliyefanya mziki/biashara na kufeli maisha...kwanini hukumu kubwa inakuja kwa huyu msomi aliyefeli tofauti na mfanyabiashara/mziki aliyefeli wakati zote hizi ni Plan A za maisha?

Hakuna sehemu ilipoandikwa kuwa kila anaesoma au anefanya biashara lazima afanikiwe..Kuna watu elimu zinawapa ufahari, kuna watu elimu wanazichukia jinsi zilivyowafanya at the same time kuna watu biashara zinawapa ufahari wakati wengine hawataki hata kuzisikia kwa jinsi zilivyowapa hasara kwenye maisha.

HITIMISHO:
Plan zote kwenye maisha ni sawa, hakuna iliyobora zaidi ya nyingine..zote zinaweza kukupa maisha au kukunyima maisha..kikubwa plan A ikifeli jaribu plan B ila sio vizuri kuhisi kila mafanikio yako lazima yalinganishwe na mtu ambae plan A yake ni elimu.. Kuna watu wengi wanafanya biashara kama wewe na HAWAKOPESHEKI mda huo huo kuna wasomi wengi tu wanakopesheka...No plan is better than the other...ukweli ni kuwa, hatma zetu zinaamuliwa toka siku ya kwanza tunapozaliwa..

FOHADI: Focus Hardwork Discipline​
 
Kabla sijamaliza kusoma hio laki tatu ni kamba...na mwaka huo kuuza baskeli et laki na 20 ni ya aina gani...maana baskeli mpya dukani tulinunua elf 85 mountain 21speed wewe baskeli ichezewe na wenzio uuze laki 😁😁
Hongera kwa kuwa umefikiria nje ya boksi japo hatuwezi lingana kwenye mipango na maono.

Sasa mkuu hebu tuambie mpaka sasa una kipi ambacho ni mafanikio kwako si lazima iwe nyumba na gari nahitaji kujua maendeleo ya unachokifanya na unafanya hicho hicho ulichotuambia au una kingine?

Pia kwenye stori nzima hatujasikia changamoto yoyote uliyowahi kukutana kwenye biashara zako mbali na hizo za shule kukubana je, hukuwahi kupata? Na kama ulipata ulitatuaje?

Tueleze yale tusiyojua kwa ufupi kwenye biashara mfano unakuta mtu anakwambia nilianza na lita 10 za petrol ndani ya mwaka mmoja nikawa na petrol station bila ya kutuambia mchakato ulikuaje?

Nisaidie au tusaidie mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom