Najihisi nina tatizo nisaidieni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Najihisi nina tatizo nisaidieni

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by cheusimangala, Apr 9, 2012.

 1. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  As salam aleykum wapendwa wangu.
  Natumai pasaka imekua yenye furaha kwenu.

  Wapendwa kwa asili mim ni mtu mwenye kupenda utani na mtu ambaye ni vigumu saaana kukasirika.Hakuna binadamu asiyekasirika lakini kwa kweli mimi Cheusie nikikasirika lazima hilo jambo litakuwa kubwa mara nyingi mim ni mtu wakufurahi na mwingi wa tabasamu usoni mwangu.

  Lakini wapendwa sijui ni nini kimenipata siku za hivi karibuni,yaani ninaweza kuamka nikiwa nimejawa na hasira bila hata kuudhiwa na mtu yeyote.Yaani siku hiyo shemeji yenu nimpendae kupita maelezo kila atakaloongea nitaona linanitibua,akijaribu kujitetea kuwa hajamaanisha kitu kibaya ndio anakua kaharibu kila kitu.Yaani siku za kuamka na hasira na kuwa sijisikii kuongea na mtu yeyote.Siku kama hizi hata JF siingii sababu nikiingia naweza kujibizana na mtu vibaya nikaishia kuwa banned.

  Ajabu ni kwamba kuna siku nyingine tena naamka moyo wangu unakua umejaa furaha ya ajabu,furaha ambayo sijui hata inatokea wapi.

  Kuna siku naweza nikaamka nikiwa nina huzuni ya ajabu,huzuni ambayo siwezi kuelezea imesababishwa na nini.Siku hiyo naweza kujikuta najisikia kulia,kama niko nyumbani nitajitupa zangu kitandan machozi yatanitoka nitalia wee huku nikisikia huzuni kubwa moyoni mwangu.

  Shemeji yenu,marafiki,wanafunzi na wafanyakazi wenzangu nahisi wamegundua kuwa siku hizi siko normal,naona wanakua kama wananisoma kwanza kuona kama leo Cheusie kaamka na mood gani,nikiwa na mood ya furaha basi wataongea na mim kama tulivyozoea siku zote,nikiwa na mood ya hasira au huzuni naona wanakua makini wakati wakuongea na mimi.

  Kiukweli nahisi something is not right with me,sijui ni nini kinanisumbua,lakini najijua mimi hii sio kawaida yangu.
  Je hii ndio Depression au ndio dalili za stress? Au hii ni nini jamani..

  Niko serious,naombeni kama kuna mpendwa yeyote humu ndani ameshawahi kutokewa na kitu kama hiki aniambie au kama kuna wataalam mnaojua hii inasababishwa na nini mnisaidie.

  Natanguliza shukrani zangu kwa mtakaonichukulia serious na kujaribu kunisaidia.
  Asante.

  Cheusie.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Apr 9, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Go get your thyroid checked...
   
 3. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,459
  Trophy Points: 280
  umeanza kuwa misllaneous na ni jambo baya mtu ambaye anakuwa hivi anakera na inakuwa vigumu kumdetermine atakuwa katika hali gani.
  Inawezekana labda una msongo wa mawazo au tatizo flani linalo kusumbua ambalo hujalipatia ufumbuzi.
  Sitaki ongea mengi kwakuwa mimi si mwana psychology(ia)
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  sasa nimekuelewa, kuna ziku huwa unanshangaza tu.

  sea Cliff hotel, kuna wataalam wa ushauri wa mambo hayo, ni wellness program.

  Au AAR head quater pale Chato Street/ally Hassan Mwinyi.

  Kama uko serious utaniPM nikupe namba ya mhusika wa program hiyo.
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kwa waafrika unaweza kuwa na tatizo la 'kutokwenda kutambika' kwenu kwa mda mrefu....

  but kizungu nashauri utazame afya yako kiujumla
  hebu kapime 'hormones zako' ina sound kama
  kuna mvurugiko wa homones au depression au 'mzunguko wa siku zako'
  au dalili ya ugonjwa mwingine
   
 6. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  mie nahisi ni bipolar disorder hio,ndio inakuwaga hivyo highs and lows...muone mtaalamu..lol
   
 7. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Pole kwa hali hiyo.
  ila kama uko katika hali hiyo katika avatar yako(mjamzito) hiyo ni hali ya kawaida.
  Inasababishwa na mabadiliko/ongezeko la hormones katika mwili wako.
  Pia sio ajabu kwa wajawazito(nisamehe kama sio mjamzito) kuwa na depression.
  Hata hivyo ni vuzuri ukawaona wataalam ili wajue kiini cha hali hii hasa kama huna ujauzito.
  Kama wewe ni mjamzito jitahidi usiwe unakasirika kasirika sana maana utamstress mtoto wako aliye tumboni.
  Mungu ni mwema atakusaidia urudie katika ile hali yako ya zamani uliyoielezea.
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ohhhh kumbe ndio maana ulikuja vile juzi?

  Nwy kama wewe ni mtarajiwa kama avatar yako inavyoonyeshaga(pole kama nimekuchanganya na mwingine) basi waambie wakuvumilie tu maana hizo mood swings hua.zinawasumbua kweli baadhi ya watu wenye ujauzito. Kama sio tafuta msaada wa kisaikolojia na kifizikia maana inawezekana kinachokosumbua kikawa kichwani au mwilini kwa ujumla (stress/hormones/depression n.k). Ila zaidi jitahidi kutoruhusu hisia zako hizo zinyime watu wengine raha.
   
 9. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
 10. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,932
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160
  Sorry lakini naomba kuuliza!

  Hiyo Avatar yako inaonyesha kama uko mjamzito ... je kwa sasa ni mjamzito? ... kama ndio basi nafikiri hizi mood swings zitakuwa zinatokana na hiyo hali.

  If you are pregnant or are supporting someone through pregnancy, you probably have had some experience with mood swings. You are not alone; mood swings are common during pregnancy. You may be excited about being pregnant, but you can also be stressed or overwhelmed.

  Mood changes during pregnancy can be caused by physical stresses, fatigue, changes in your metabolism, or by the hormones estrogen and progesterone.

  Significant changes in your hormone levels can affect your level of neurotransmitters, which are brain chemicals that regulate mood. Mood swings are mostly experienced during the first trimester between 6 to 10 weeks and then again in the third trimester as your body prepares for birth.
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  hiyo avatar ni miaka miwili now
  sio ujauzito itakuwa some disease...for sure

  ushauri wangu muone dokta fasta
   
 12. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  thanx kongosho,ila siko Dar ila nitatafuta wataalam huku nilipo.
   
 13. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Thanx kwa ushauri,kwetu ninakwenda bila shida ila siamini katika matambiko.
  Ila hayo mengine uliyonishauri nitayazingatia.
   
 14. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  namshukuru Mungu leo nimemka moyo wangu umejaa furaha maana...
  Ila labda mwaya maana hata hao wenye bipolar hawakuomba kuwa hivyo na yeyote anaweza kuwa hivyo au kuzaa mtoto wa hivyo(God forbid).
   
 15. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Juzi nilikua kawaida tu sikua na shida yeyote,nilitoa tu mtizamo wangu.

  Asante kwa ushauri mzuri,nitautendea kazi.
  Kusema kweli huwa sometimes nashindwa kuact normal japo najua kwa mfano ninapoamua kutoongea na mtu, huyo mtu anajisikia vibaya.
   
 16. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
 17. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #17
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ushauri wa kumuona dokta naupokea ila hayo mengine mmmh.
  Boss sijui kwa nini unanichukia lol
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Apr 9, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mtizamo mtizamo haswa!!!

  Nwy. . .Kila la kheri...angalia watu wasije wakakukimbia.
   
 19. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #19
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kwani mbona ni vitu vingi naandika lakini sielewi kwanini ile ya juzi imekugusa namna hiyo.
  anyway my dear,watu hawatanikimbia,huwezi kuamini huko mtaani watu wananipenda sana,sema tu nikinuna wanamiss ucheshi wangu.Na mtu ukishagundua una tatizo basi ni mwanzo wa tiba wa hilo tatizo.Ushauri mnaonipatia mpaka dakika umenisaidia kwa kiasi kikubwa tu na Mungu awabariki kwa hilo na ninashukuru.
   
 20. Mayasa

  Mayasa JF-Expert Member

  #20
  Apr 9, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 587
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  avata inajieleza, ukijifungua hali hiyo itatoweka.
   
Loading...