Najihisi nimekuwa mraibu, Wangapi mmeweza kutumia smartphone / laptop siku nzima bila kutumia internet ?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Tangu mwaka huu uanze sikumbuki siku ambayo nilikuwa offline, Nina biashara zangu na kazi sio kwamba nipo idle.

Yani uwe na smartphone halafu ukose data waweza kuhisi unakosa mahitaji ya msingi, ukifika hii stage jijue ushaanza kuwa mraibu.

Matumizi ya data napenda kuingia Youtube kufatilia habari za Millard Ayo na channels nyingine zinazojielewa, Napenda kuiingia whatsapp kuangalia status, Twitter kufatilia habari za kimataifa, kuperuzi jamiiforums, usiku napenda kucheki tamthilia ama documentary, n.k.

TIKTOK niliitoa, ukitaka kujua maana ya kupoteza muda bila faida tumia hii app.

Wangapi mmeweza kupiga kavu siku nzima bila net
 
Mimi kila mwaka huwa natenga wiki moja sipatikani kwenye simu, situmii intaneti, sisikilizi radio wala kutazama tv. Ila huwa nakuwa mazingira fulani hivi ya kijijini. Hata kuanzia tarehe 2 hadi 8 januari napotea hewani.
Ukikaa muda huo unahisi kama akili imerelax sana, unahisi kupata uzoefu mpya ambao haujazoea.
 
Siku Ukiwa na Biashara Unayoisimamia Utakuwa Hewani tu..

Yaani Mimi Ni Mfanyabiashara wa Taa mjini na Nina Page ya Biashara Natakiwa Kupost Kila Taa Mpya Au Kifaa Kipya Na Nina Wateja Mpka Nje ya Nchi Useme Nizime Simu Week Nzima??
 
Hapo kweli mtihani. Kwa mimi huwa inawezekana kwa sababu nakuwa likizo. Hata watu ninaopiga nao mishe za kitaa huwa nawaambia naenda kijijini kwa hiyo kama kuna kazi inayohitaji uwepo wangu wanisubiri wiki.
 
Mwaka huu katikati nilijipa likizo ya mwezi mzima nje ya mtandao,nakumbuka ulikuwa ni wakati mzuri sana hata akili ya afya inakuwa stable.

Unawaona wanaokuzunguka umuhimu wa kuwepo kwao,in short kujipa likizo fupi nje ya mtandao kunasaidía mengi.

Nb:siyo uwe dalali au winga unategemea kutuma au kutumiwa picha useme na wewe unakuwa off line utakwama.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom