Najibu maswali mjadala wa Sheikh Suleiman Takadir

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,267
"Hadi asuswe na Waislamu wenzake, wana TANU na wananchi wote, bali lilikuwapo tatizo kubwa.

Hii haiwezekani ikatokea tu kama bahati mbaya, hapana."

(Kaniuliza Muulizaji)

MOHAMED SAID ANAJIBU:

"Hakika lilikuwapo tatizo kubwa

Katika mkutano uliofanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio Ukerewe Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe walipokwenda kumtaka ushauri kuhusu kumwingiza Nyerere kwenye uongozi wa juu wa TAA Hamza alishauri kuwa Nyerere achaguliwe kuwa rais na mwaka unaofuatia 1954 TANU iundwe na Nyerere aongoze harakati za kudai uhuru.

Historia hii nimeieleza mara nyingi naamini wengi wanaijua.

Nafasi ile ilitakiwa ishikwe na Mkristo ili upatikane umoja wa wananchi wote.

Harakati za siasa zilitawaliwa na Waislam na hofu ilikuwa ikiwa TANU itaundwa na kiongozi ni Muislam sura iliyokuwa imejengeka itadhihirisha kuwa harakati zile ni za Waislam.

Waingereza watatia fitna kuwashawishi Wakristo na wao wawe na chama cha siasa.

TANU walijifunza lililowafika Mohamed Ali Jinnah na Nehru kudai uhuru vyama vyao viwili vimejishikiza kwenye dini zao - Uislam na Uhindu.

Leo usiku wanapewa uhuru.
Asubuhi vita vya wenyewe kwa wenyewe vinalipuka.

TANU ilitaka kujiepusha na balaa hili.

Hili lingefanyika Tanganyika ingeingia katika kudai uhuru imegawanyika katika misingi ya dini.

Baada ya uchaguzi wa Arnautoglo baina ya Abdul Sykes na Nyerere 1953 na TANU kuundwa 1954 Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na Baraza la Wazee wa TANU chini ya uongozi wa Sheikh Suleiman Takadir wakafanya juhudi kubwa kujenga umoja wa wananchi chini ya Julius Nyerere.

Kuna historia ya kusisimua jinsi Bantu Group nayo kwa upande wake ilivyohamasisha wananchi kuwa wamoja kwa kufuta, "Salaam Aleikum Warahmatullah Wabarakatuh," kuwa mamkizi ya wanachama wa TANU.

Bantu Group akina Juma Selemani na Rashid Sisso wakaja na Salaam mpya, "Ahlan Tabu."

Hii Ahlan Tabu mimi niliiwahi na kuisikia kwa masikio yangu nikiwa na kama miaka mitano hivi.

Kibwagizo cha "Uhuru na Umoja" kilipokuja ndiyo Ahlan Tabu ikafa.

Yapo mengi na yote nimeyaeleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Sasa baada ya shutuma zile za Sheikh Suleiman Takadir dhidi ya Nyerere Waislam wote walimghadhibikia Sheikh Takadir wakamuona anasaliti msimamo uliowekwa na waasisi wenyewe wa TANU.

Hii ilikuwa 1958 na ilikuwa wazi kabisa kuwa uhuru unakaribia.

Hili ndilo tatizo kubwa lililokuwapo.

Bahati mbaya historia hii ya TANU ilifutwa na hii ndiyo sababu leo naulizwa nini lilikuwa tatizo kubwa kiasi Sheikh Suleiman Takadir apigwe pande hata na nduguze Waislam?"
 
Nzuri sana. Ila umeifupisha sana, fungua turbo, mwaga madini hayo
 
Bado hujaweka kisa cha yeye kuchukiwa mkuu?

Alikwaruzana kitu gani na Nyerere?
Yeye hakutaka Nyerere awe kiongozi? Na kwa maono yako yupi alikua sahihi!?
 
Type historia za wasio masheikh pia
Yoda,
Umekusudia niweke hapa historia ya ambao si masheikh.
Naanza na historia ya Dome Okochi Budohi:

DOME OKOCHI BUDOHI MZALENDO KUTOKA KENYA ALIYEPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
Naamini umeona hiyo video ya ufunguzi wa kumbi 12 zinazohifadhi historia ya Wakenya katika kupigania uhuru wa nchi yao.
Video hii imenitia hamu ya kumweleza Dome Okochi Budohi.
Sijui kama katika kumbi hizo kuna historia ya Wakenya walioshiriki katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kama Dome Budohi.
Historia ya Dome Okochi Budohi Mluya kutoka Kenya haiko popote katika historia ya TAA wala ya TANU.
Lakini Dome Budohi ameshiriki katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kuanzia TAA hadi TANU.
Soma hapo chini uone jinsi nilivyomweleza Dome Budohi katika kitabu cha Abdul Sykes:
''Familia yangu ilifahamiana na Dome Budohi, mmoja wa wanaharakati kutoka Kenya.
Wakati ule wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa akiishi Dar es Salaam.
Budohi alikuwa mmoja wa wazalendo walioasisi TANU na kadi yake ya uanachama ni nambari 6 aliyopewa Julai 1954.
Mwaka 1955 alikamatwa na serikali ya kikoloni kwa tuhuma ya kuwa mmoja wa askari wa Mau Mau harakati za wazalendo takriban wengi wao wakulima wadogo waliokuwa wakipigana na ukoloni wa Waingereza nchini Kenya.
Ninazo kumbukumbu nyingi za utoto nikimtembelea Budohi Kituo Cha Kati cha Polisi.
Hivi sasa jengo hilo ni Makao Makuu ya Shirika la Reli la Tanzania. Wakati huo mimi nilikuwa mtoto, si zaidi ya miaka minne hivi.
Jambo la kwanza ninalokumbuka kuhusu Budohi ni kuwa kila mara tulipokwenda kumtembelea tulimkuta anasoma gazeti.
Baadae Budohi alihamishiwa Kenya na aliwekwa kizuizini katika kisiwa cha Lamu.
Alipofunguliwa toka kizuizini mwaka wa 1963 miezi michache kabla ya uhuru wa Kenya, Budohi alikwenda Uganda na akaajiriwa na gazeti la Uganda Argus.
Hivi sasa ninaelewa kwa nini siku zile kila mara nilikuwa namkuta amezama ndani ya gazeti kila tulipokwenda kumtembelea pale rumande mjini Dar es Salaam.
Niliweza kwa msaada wa rafiki yake Maxwell aliyelowea Tanganyika, kumpata Budohi mjini Nairobi mwaka 1972.
Nilimtembelea mjini Nairobi wakati huo alikuwa akiishi Ruiru maili chache kutoka Nairobi mjini.
Budohi alikuwa ametundika picha ya Nat King Cole sebuleni kwake.
Mwaka 1974 nilimtembelea tena, safari hii katika nyumba yake ya Ngei Estate.
Budohi alikuja kuwa mtu wa kwanza kabisa kunipa habari kuhusu historia ya harakati za Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza.
Hata hivyo wakati ule nilikuwa bado sijapata hamu wala kuwa na hamu ya kuandika kitabu kuhusu uhuru wa Tanganyika.''
Picha ya pili ni Mzee Maxwell na mwandishi picha hii tulipiga katika miaka ya 1990 Mtaa wa Mafia karibu na Msikiti wa Manyema na picha ya tatu ni Dome Budohi na mwandishi, Ruiru Nairobi, 1972.

1698988058978.png

1698988127833.png

1698988169556.png
 
Back
Top Bottom