Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,918
- 30,259
HISTORIA FUPI YA BIBI TITI NILIYOZUNGUMZA UWANJA WA UJAMAA KATIKA KILELE CHA BIBI TITI FESTIVAL
Nilifungua kwa kusema kuwa Bibi Titi hana mfanowe.
Rufiji ina historia ya pekee katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
TANU ilipoundwa kazi ya usajili walipewa Mwalimu Julius Nyerere, TANU Territorial President, Kadi ya TANU No. 1, Abdul Sykes Kadi No. 3 na Ally Sykes Kadi No. 2.
Msajili Mwingereza akakataa kuisajili TANU kwa kuwa Nyerere hakuwa na orodha ya wanachama wala kadi za TANU.
Alipofikisha taarifa hii kwa wenzake, Abdul akasema aitwe Said Chamwenyewe.
Said Chamwenyewe akakabidhiwa rejesta na kadi za TANU aende Rufiji akalete wanachama wa TANU.
Hivi ndivyo TANU ilivyosajiliwa November 1954.
TANU ilikuwa na wazungumzaji hodari watatu: Julius Nyerere, Sheikh Suleiman Takadir na Bibi Titi.
Bibi Titi amehutubia mikutano miwili Viwanja Vya Mnazi Mmoja hajapata kumuona Nyerere.
Siwezi kukuambieni kati ya Nyerere nani kamzidi mwengine kwa kuwa nyie hapa mmemsikia Nyerere hamjapata kumsikia Bibi Titi.
Lakini kwa kuwa inajengwa Maktaba ya Bibi Titi Dodoma, pale zitawekwa hotuba za Bibi Titi na mtamsikia Bibi Titi na mtaamua wenyewe nani kamzidi mwenzie.
Lakini Abbas Sykes amepata kuniambia kuwa kulikuwa na wakati Nyerere anaishiwa na la kusema na akimuomba Bibi Titi azungumze.
Kutoka hotuba ya Bibi Titi Mwalimu Nyerere atapata maneno ya kusema.
Bibi Titi hakunyanyua kalamu kuandika maisha yake lakini kabla ya kufariki kwake alimweleza Leila Sheikh historia yote ya maisha yake.
Leila kafariki hakujaaliwa kuandika historia ya Bibi Titi.
Zifanyike juhudi historia ya Bibi Titi iandikwe ili kitabu kiwepo katika Maktaba ya Bibi Titi itakapofunguliwa.