Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,264
HISTORIA YA JUMBE MWINJUMA DIGOSI, SHEIKH SULEIMAN TAKADIR NA JULIUS NYERERE 1954
Inawezekana Jumbe Mwinjuma Digosi alikuwa umri huu wa sasa alionao mwanae Zakaria huyu Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kariakoo.
Naukumbuka uchaguzi wa Zakaria Digosi Jangwani kwani Kariakoo iliwaka moto kwa ushindani uliowapambanisha wana mji wenyewe wazaliwa wa Kariakoo ambao wazee wao walikuwa watu maarufu na pia wana mji.
Zakaria alikuwa anagombea kiti alichokuwa amekikalia Abdallah Faraj.
Wote hawa wawili wana watu wengi nyuma yao na wote wamekulia Kariakoo na wanajuana vyema.
Kariakoo haijapata kupoteza haiba yake katika siasa toka enzi za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kariakoo iliwaka moto wakati wa kampeni lakini mwishowe Zakaria Digosi alishinda.
Baba yake Zakaria, Mzee Mwinjuma Digosi alikuwa Jumbe katika serikali ya Muingereza.
Alikuwa na nyumba Mtaa wa Nyamwezi na nyumba hii alimpangisha Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.
Sheikh Takadir akiendesha biashara yake ya mnada kwenye nyumba hiyo.
Hapa katika huu mnada pakawa sehemu muhimu sana wana TANU wakikutana kwa biashara, mazungumzo ya siasa na kuhamasishana.
Julius Nyerere akawa hapungui kwenye barza hii.
Mnada wa Sheikh Suleiman Takadir ukawa maarufu watu wakifurika pale kwa kuuza na kununua na kwa mazungumzo.
Ukiwa humjui Nyerere unataka kumuona fika.
Rafiki yangu marehemu Mzee Kassanda anasema yeye mara ya kwanza kumtia Nyerere machoni ilikuwa pale mnadani kwa Sheikh Suleiman Takadir.
Waingereza wakamlalamikia Jumbe Digosi kuwa nyumba yake ni moja ya ngome za TANU na Julius
Nyerere anafika sana hapo kumwaga sumu.
Waingereza wakamkumbusha Jumbe Digosi kuwa yeye ni mtumishi wa Serikali ya Malkia hawezi kuwaweka wapinzani wa serikali katika nyumba yake.
Hakika huu ulikuwa mtihani mkubwa kwa Jumbe Digosi.
Vipi atamfukuza kwenye nyumba yake Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU?
Jumbe Digosi alitoa notisi kwa Sheikh Suleiman Takadir ahame nyumbani kwake akapange kwengine.
Sheikh Suleiman Takadir alihama pale Mtaa wa Nyamwezi akahamia Mtaa wa Msimbazi.
Ukoloni hakika ulikuwa na changamoto zake.
Leo mwanae Zakaria na watu wa Kariakoo wamewakumbuka wazee hawa.
PICHA: Zakaria Mwinjuma Digosi Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kariakoo kulia akiwa na Naibu Spika Mussa Zungu katika khitma ya kuwarehemu wapigania uhuru wa Tanganyika.
All reactions:
14Kheri Chomba, Kamalu Khalid and 12 others