Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 8,787
- 5,535
Kuombaomba huwa mchakato wenye kumuondolea heshima yule muombaji wa misaada. Nilikuwa namsikiliza Makamu wa Rais Dr Mpango akiongelea namna utu wa kiongozi wa nchi maskini unavyodhalilika katika meza ya mkutano kati ya mawaziri wa kutoka mataifa ya dunia ya tatu na wale wa mataifa ya Ulaya na Marekani.
Wote katika chumba cha mkutano wanavaa suti mahiri na muonekano wao kwa mtu mgeni ni wa kupendeza unaozipa heshima zinazolingana pande mbili zenye kujadiliana kuhusiana na suala zima la nchi maskini kutaka ipewe pesa za kuendeshea shughuli za kimaendeleo. Lgakini ukweli ni kwamba upande mmoja unaokuwa na unyonge wakati wa kuitangaza 'njaa' inayowapeleka huko ughaibuni.
Nilimsikia Waziri wa EU mwingereza kama wiki mbili zilizopita namna alivyokuwa akitoa maagizo kwa serikali ya awamu ya sita ili iweze kupewa pesa za kuendeshea uchaguzi mkuu.
Nikaitambua fedheha aliyoisema Makamu Dr Mpango miaka kadhaa iliyopita, kwamba wanaomba pesa huku nyuso zao mkutanoni zikiwa zimejawa na unyonge.
Muingereza yule aliongea katika ukumbi wa kikao cha EU akijiamini kabisa kwamba matakwa aliyoyasema yatatimizwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ni katika muktadha huo huo wa kuondokana na unyonge wa pesa za wazungu zinazotumika katika shughuli zetu nyeti unaweza mtu kuielewa ni kwanini awamu ya sita imeamua kuukwepa unyonge tunaokutana nao mara kwa mara katika vikao na wawakilishi wa mataifa ya Ulaya na Marekani.
Naamini zipo njia nyingi halali zenye kuziwezesha serikali zetu zikaendesha uchaguzi bila ya kulazimika kukubaliana kwa shingo upande na kejeli pamoja na maagizo ya mataifa ya wazungu. Bilioni 100 ni bajeti nzima ya kila kitu kwenye uchaguzi huo.
Linaibuka suala jingine la hao wanaotoa hizo pesa, je hawawezi kuwa ni wanunuzi wa haki za msingi za walio wengi wanaoipigia kura kuiweka madarakani serikali inayotaka ridhaa yao ili imalizie ngwe ya pili?. CCM inaweza kuuweka wazi kila mtu auone na aufahamu usafi wa mazingira ya shughuli nzima iliyofanyika jana na zikapatikana bilioni 86?.
Madai ya pesa za utakatishaji kukusanywa mbele ya macho na ikawa ni ahueni ya wafanyabiashara wanaotazamwa kwa jicho baya, yamesikika kutoka kwa watu wenye mawazo huru. Nani anaweza kutumia maarifa kwa ajili ya kulifafanua suala hili kwa umma wa wapiga kura?.
Siku zote nia njema hutumika kwa lengo la kumsafisha mwenye nia hiyo mbele ya macho ya wadau wa taifa letu. Tukumbuke kuwa Mungu haufichi unafiki na Taifa hili lipo mikononi mwa mikono yake mitakatifu na salama, waombaji wanaopiga magoti huko makanisani na misikitini ni wengi na sala zao hazipotei angani bure.
Kuna siku atayaanika wazi yote yanayoweza kuwa yakifanyika kwa kigezo cha nia njema ndani ya muda huu. Mabilioni yanayokusanywa ili uchaguzi uendeshwe kwa pesa za ndani yasiwe kigezo cha wanaozitoa kutaka kujimilikishia neema zote zinazopatikana katika miaka hiyo mitano kuelekea 2030.