Naishukuru JF, nimepata mchumba!

Status
Not open for further replies.
Be care,wakati mwingine mbwa huwageukia wanaowatunza!!
 
Hongera sana mkuu! Kila la kheri kwenye maandalizi ya harusi.
 
kililili yuko wifi yetu aje hapa tumuone yu wapi eeeeeeeeeeeeeh nakumbuka mbaliiiiiiiii
 
Binafsi mfumo uliopo si mzuri na pengine unafanya wanaotafuta kweli wachumba kuona aibu namna ya kuwasiliana. Wangejaribu kuboresha namna bora zaidi, maana yake hapa mchumba apatikane kwa kujadiliana na watu wengi?
 
Hivi inawezekana ukampata mchumba ndani ya miezi 3
ukamuita mchumba bora na kutangaza kumuoa
hata mwaka haujaisha? Unataka kutuambia
mmeshachunguzana vema na mkaridhiana kitabia au
wote mmekutana mkiwa na matatizo yenu mkaazimia kuoana gafla? Hata hiyo miezi 6 umesema haitoshi take your time kuchungazana,kwa sasa jiiteni marafiki na sio wachumba.
Ndoa ni maisha ndugu sio kama kununua matunda sokoni
kumbuka ni maagano ya maisha tahadhari usije kujuta baaadae.
Kazi kwako kila la kheri.
 
Habari wakuu,
Kama mtakumbuka mnamo tarehe 10 mwezi mei mwaka huu mnamo saa tisa na dakika 50 nilipost thread ya kutafuta mchumba. Ingawa zoezi lilikuwa gumu sana lakini napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipatie mchumba bora. Taratibu zote kwa mujibu wa mila nimezifuata na napenda kusema kuwa tutafunga ndoa katika kipindi cha miezi sita ijayo.
Napenda kuishukuru JF kwa kuniwezesha kupata mchumba bora ambaye natarajia atakuwa mke bora.
Nawashukuru wadau wote walionipa ushauri kupitia jamvini humu na wale waliojitokeza kutaka niwe mume mtarajiwa wao.
Mwisho: Mitandao ya kijamii ni mitandao inayoweza kuleta mapinduzi makubwa sana katika nchi yetu. Tuitumie vema ili tupate maendeleo na tupinge kwa nguvu zetu zote ubeberu wa aina yoyote wenye lengo la kuifungia au kuiwekea vikwazo mitandao ya kijamii, na hapa nazungumzia JAMII FORUM.
Nawasilisha.

Kaka miezi miwili tu ushatangaza ndoa..!!!. Kakulambisha nini huyo binti....??? Nina wasi wasi na hii thread naona imejaa uongo wa kutosha.
 
ukishaoa uje tena tukupe maushauri namna bora ya kuishi na mwanamke
 
Habari wakuu,
Kama mtakumbuka mnamo tarehe 10 mwezi mei mwaka huu mnamo saa tisa na dakika 50 nilipost thread ya kutafuta mchumba. Ingawa zoezi lilikuwa gumu sana lakini napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipatie mchumba bora. Taratibu zote kwa mujibu wa mila nimezifuata na napenda kusema kuwa tutafunga ndoa katika kipindi cha miezi sita ijayo.
Napenda kuishukuru JF kwa kuniwezesha kupata mchumba bora ambaye natarajia atakuwa mke bora.
Nawashukuru wadau wote walionipa ushauri kupitia jamvini humu na wale waliojitokeza kutaka niwe mume mtarajiwa wao.
Mwisho: Mitandao ya kijamii ni mitandao inayoweza kuleta mapinduzi makubwa sana katika nchi yetu. Tuitumie vema ili tupate maendeleo na tupinge kwa nguvu zetu zote ubeberu wa aina yoyote wenye lengo la kuifungia au kuiwekea vikwazo mitandao ya kijamii, na hapa nazungumzia JAMII FORUM.
Nawasilisha.

Hongera ila Utulie sasa.. Na Huyu Chema nadhani nae atajitokeza tu Tu Tumfahamu nae...Sijui atakuwa ni cacico au Kongosho Muweke Historia Mpya ya Maisha Yenu hata Mkiulizwa Njiani mseme hamkukutana Barabarani kama JK na EL
 
Last edited by a moderator:
We mtu mi Nkafikir umepata Familia..kumbe mchumba..long way to Go

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom