Naishi naye ndio, Lakini...

Naishi naye ndio, Lakini...

Usiishi na mwanamke usiyempenda eti kisa umezaa naye, Mwandalie Mazingira mazuri mama na mwanao halafu muoe haraka mwanamke wa ndoto zako ili uishi kwa furaha, Usitishwe na maneno hakuna revenge wala kisasi
Mnamchanganya sana jamaa
 
humpendi mwanamke.. unakaa nae nyumbani kwako miaka mitatu!!??? unamwonea huyo mwanamke!? au kisa ni mnyonge!? au kisa ni mwanamke!? bro umekosea.. tena sana!! kama humpend ungemwacha mapema nae ajue anenda kuishije... umemzalisha si kosa sana.. umekaa nae kwako miaka mitatu.. unafikiri hapo mtaani kuna mtu atamwoa!??
.
.
kwakwel hapo amua wewe mwenyewe! mimi kila ninapowaza navaa viatu vyake.. nakuta nagota!!
 
Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia. Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile. Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu. Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami. Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo. Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro. Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini. Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu. Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.. Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana. Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo. Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
Acha uenda WAZIMU,
Huyo unaye na aliye kuzalia myoto NDIYE MKEO, ACHANA NA HUYO UNAYE MWITA mchumba wako .....!

MAMBO MENGI MEMA NA MAZURI MARA NYINGI HUJA ACCIDENTALLY NA BAADAE NDIO HUWA YA KWELI.

nakuambia kuwa ukimwacha huyo ukaona na huyo unaye MWITA mchumba wako na mna malengo makubwa Sana!
UTAJUTA MAISHANI MWAKO YOTE.

nautaikumbuka hii comment yangu.......!

KAMILISHA NDOA NA UPIYE ZAA NAYE, huyo mchumba wako KAFICHA MAKUCHA, mwache uliye mzalisha utalia na kusaga meno.
 
Ulivyochepuka bila kutumia kinga ulitegemea nini?, mimi binafsi nampongeza huyu mama mtoto kajua kujishikilia haswaa ,ulipaswa umwambie siku ile ile kuwa humpendi sio kumtumia miaka yote hiyo alafu uje umuache tuu na hajakukosea chochote hakika karma haitakuacha salama
AMINA, SIO KARMA TU, MUNGU ATAKUHUKUMU KWA HUO UFEDHULI UNAOTAKA KUUFANYA.
HUYO MCHUMBA WAKO KUKUSAMEHE ISIWE NDIO SABABU YA KUMUACHA BINTI WA WATU.
UNASEMA HUNA HISIA NAYE?, UMEMZALISHA, UMEKAA NAYE ZAIDI YA MIAKA 3 LEO UNASEMA HUNA HISIA NAYE? WEWE AKILI ZAKO ZIPO SEHEMU GANI? MAKALIONI? NA UKIMUACHA HUYO DADA ULIYEMZALISHA ANA HAKI YA KUKUROGA AU KUKUFANYA KITU CHOCHOTE KIBAYA.
 
Kosa la kifundi ni wewe kuruhusu kuzaa na mtu ambaye huna mpango nae, na mbali ya hapo kukaa nae kama mke. Chakushangaza zaidi mpaka leo uko nae na unaendelea kumla eti unajizuia kuzaa nae, wakati huo huo unasema una mwanamke eti mna mipango mikubwa.
Nakushauri kama umeweza kuishi nae huyu miaka yote hii na umejiridhisha anakupenda, huyu ndio mkeo, huyo mbaye inaonekana wewe unampenda , yeye hakupendi mpaka kukuruhusu uishi na mke mwingine akijua kabisa mnakutana kimwili, ana malengo tu fulani na wewe.
Oa huyu mzazi mwenzako akupendaye.
Ukweli kabisa.
 
Hizi mada nazipenda sana maana yaliyonikuta ni makubwa mno. Siku nikijua kubadilisha jina kwenye Ac yangu ya jf ntafunguka,nimazito sana.
Nikushauri tu kua hakuna mwanamke anaeweza kukusamehe kosa kama hilo,as long as bado unaishi na huyo,kwaio oa mwenye mtoto wako na najua unampenda ndomana uko nae hadi leo, saivi unajiona huna hisia naye kwasababu upo nae apo,lkn siku akukutoka utaona ni jinsi gani ulivyokua unampenda. Your bloodly connected.
 
Umeshazaa nae huyo ni mkeo ,hebu acha mawazo mengine ya kijinga
 
Hili ndio kosa ulilofanya just imagine mtu mnalala na kuamka kwa number of years then ghafla anakwambia hana malengo na wewe does it make sense?
Si ndo hapo jamani.bora baby mama wake tu.sasa hivi hatoelewa nini namaanisha.lakini akimrudia sijui mchumba wakeee atakuja k-u-j-u-t-a-,,,,
 
Sikiliza wewe kijana. Acha kuchezea wanawake utakuja kujuta. Nitakupa kisa fulani kidogo tu. Kuna rafiki yangu fulani aliajiriwa huko kanda ya ziwa. Baada ya kuona maisha ya kupika ni taabu akajipatia house girl wa kisukuma tena mkubwa tu na wakati huo alikuwa na mchumba wake aliyekuwa akija kumtembelea. House girl naye hakuwa mjinga kwani kwa ushawishi wa wapambe aliweza kumtega jamaa mpaka akawa anagonga vitu. Zoezi hilo liliendelea kwa muda mrefu tu. Shida ilikuja pale alipomwambia arudi kwao kwani kipindi cha kufunga ndoa na mchumba wake kimekaribia. Ndani ya wiki hiyohiyo jamaa aliugua kwikwi mfululizo ambayo ilimuondoa duniani. Hakuna mwenye uhakika kama binti yule alihusika au la. Hivyo chukua tahadhali kijana. Acha kucheza na hisia za wanawake.
Kuna mmoja musoma nae alikuwa player sana, siku moja akaingia chaka km kawaida akapiga hlf akakimbia. Kilichomkuta asb alijikuta anakuwa na kasauti ka kike hlf jamaa alikuwa bonge la bwana. Kahangaika na ile sauti km miaka miwili, siku alivyopona alifunga na ndoa na akaacha hiyo tabia.
 
" nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu"

"Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami"

"Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake]"

"nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa"

"sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu"

Nia ya huu uzi ni kututafutia wengine ban tu! Tunaotaka kuporomosha mitusi tunakomenti wapi jameni
 
Tatizo ni hisia.. Hisia zangu haziko kwake hata kidogo. Awali nilidhani kuwa, baada ya muda huenda ningeweza kujifunza kumpenda, lakini naona hali inazidi kuwa mbaya siku hadi siku
Ouky Kama hauna hisia nae mtengenezee mama yake (mzazi mwenzio ) maisha ili aweze kumuhudumia mtoto pale utakapo muacha.... Huwezi kulazimishwa kumpenda mtuu ila jali damu yako mgungulie biashara au mtafutie kazi then muachie nyumba mnayokaa uondoke na nguo zako tuu uende kwa uyo mchumba ako wa zamani
 
" nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu"

"Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami"

"Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake]"

"nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa"

"sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu"

Nia ya huu uzi ni kututafutia wengine ban tu! Tunaotaka kuporomosha mitusi tunakomenti wapi jameni

Naomba unitukane Mimi please
 
Usiishi na mwanamke usiyempenda eti kisa umezaa naye, Mwandalie Mazingira mazuri mama na mwanao halafu muoe haraka mwanamke wa ndoto zako ili uishi kwa furaha, Usitishwe na maneno hakuna revenge wala kisasi
Una undugu na uyo mchumba anayependwa au ndo wewe???
 
" nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu"

"Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami"

"Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake]"

"nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa"

"sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu"

Nia ya huu uzi ni kututafutia wengine ban tu! Tunaotaka kuporomosha mitusi tunakomenti wapi jameni
Hahaha best umechukia
 
Sikiliza wewe kijana. Acha kuchezea wanawake utakuja kujuta. Nitakupa kisa fulani kidogo tu. Kuna rafiki yangu fulani aliajiriwa huko kanda ya ziwa. Baada ya kuona maisha ya kupika ni taabu akajipatia house girl wa kisukuma tena mkubwa tu na wakati huo alikuwa na mchumba wake aliyekuwa akija kumtembelea. House girl naye hakuwa mjinga kwani kwa ushawishi wa wapambe aliweza kumtega jamaa mpaka akawa anagonga vitu. Zoezi hilo liliendelea kwa muda mrefu tu. Shida ilikuja pale alipomwambia arudi kwao kwani kipindi cha kufunga ndoa na mchumba wake kimekaribia. Ndani ya wiki hiyohiyo jamaa aliugua kwikwi mfululizo ambayo ilimuondoa duniani. Hakuna mwenye uhakika kama binti yule alihusika au la. Hivyo chukua tahadhali kijana. Acha kucheza na hisia za wanawake.
Duuuh!!!!
 
Back
Top Bottom