ledada
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 17,460
- 67,429
Kama uliezaa naye hana shida zaidi ya kutokuwa na hisia naye, nakushauri usimuache na ogopa sana mwanamke mkimya,usifikiri hana mdomo mpe heshima yake,fanya yako na huyo mchumba wako japo naamini mwisho wake ni mbaya zaidi hasa utakapojichanganya ukamuacha mzazi mwenzio,na kama ni hisia kapige pombe zako lazima hisia zitasoma tu,kama zilivyosoma hapo mwanzo

Kwamba apige gambe hisia zisome tena...

Kama hukumpenda why udinye bila ndomu??? Alafu kizembe tu unampa mimbaa..bora bhasi upate dhambi ya kutoa kuliko kumpa mateso mwanao na huyo mwanamkee...Usiishi na mwanamke usiyempenda eti kisa umezaa naye, Mwandalie Mazingira mazuri mama na mwanao halafu muoe haraka mwanamke wa ndoto zako ili uishi kwa furaha, Usitishwe na maneno hakuna revenge wala kisasi
Yaani ujue nimeshindwa kumuelewa huyo mchumba wake
Ama kweli watu tunatofautiana.

mchumba anamlia timing tuu. Mkuu umenichekesha sana unavyong'ang'ana kwamba una malengo makubwa wakati mimi sioni kama una lengo lolote kubwa![]()
Wewe bwana hapo ndio umeshaoa cha maana we endelea kujenga maisha na mkeo na mtoto wenu. Sio kila ndoa ina matarumbeta mkuu. Miaka minne yote mi nafikiri huyo ulie nae ndani ndio mkeo. Hizo nyingine ni ndoto tuu kama mimi navyoota kujenda ghorofa

Ndoto za Kuwa kama Mengi

woiiii ndotoni labda

Habari wana jamvi...
Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia. Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile. Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.
Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu. Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami. Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.
Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo. Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.
Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro. Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.
Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini. Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu. Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.
Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.. Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana. Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo. Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.
Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
Na kweli, ukute ana mishe zake hivyo jamaa hampi stress maana yupo wa kumpa faraja.mchumba anamlia timing tuu.
Au pengine mchumba yupo na mambo yake na hakuwa na time na jamaa.
Duh unamtihani mzito kaka ila tu nakushaur muulize anaweza kufanya biashara gani MPE mtaji usimwache hivi hivi naungana na ww mapenz yanajengwa na hisia pia poleHabari wana jamvi...
Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia. Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile. Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.
Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu. Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami. Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.
Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo. Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.
Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro. Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.
Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini. Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu. Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.
Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.. Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana. Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo. Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.
Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
Aisee itakuwa alimlogaa walahii.. Kwikwi inamuuaje mtu????Sikiliza wewe kijana. Acha kuchezea wanawake utakuja kujuta. Nitakupa kisa fulani kidogo tu. Kuna rafiki yangu fulani aliajiriwa huko kanda ya ziwa. Baada ya kuona maisha ya kupika ni taabu akajipatia house girl wa kisukuma tena mkubwa tu na wakati huo alikuwa na mchumba wake aliyekuwa akija kumtembelea. House girl naye hakuwa mjinga kwani kwa ushawishi wa wapambe aliweza kumtega jamaa mpaka akawa anagonga vitu. Zoezi hilo liliendelea kwa muda mrefu tu. Shida ilikuja pale alipomwambia arudi kwao kwani kipindi cha kufunga ndoa na mchumba wake kimekaribia. Ndani ya wiki hiyohiyo jamaa aliugua kwikwi mfululizo ambayo ilimuondoa duniani. Hakuna mwenye uhakika kama binti yule alihusika au la. Hivyo chukua tahadhali kijana. Acha kucheza na hisia za wanawake.
Umemaliza hapaKosa la kifundi ni wewe kuruhusu kuzaa na mtu ambaye huna mpango nae, na mbali ya hapo kukaa nae kama mke. Chakushangaza zaidi mpaka leo uko nae na unaendelea kumla eti unajizuia kuzaa nae, wakati huo huo unasema una mwanamke eti mna mipango mikubwa.
Nakushauri kama umeweza kuishi nae huyu miaka yote hii na umejiridhisha anakupenda, huyu ndio mkeo, huyo mbaye inaonekana wewe unampenda , yeye hakupendi mpaka kukuruhusu uishi na mke mwingine akijua kabisa mnakutana kimwili, ana malengo tu fulani na wewe.
Oa huyu mzazi mwenzako akupendaye.
Sijui labda ni "coincidence" tu, ila tahadhari ni muhimu.Aisee itakuwa alimlogaa walahii.. Kwikwi inamuuaje mtu????