SoC03 Umuhimu wa utabiri wa siku zijazo katika kuendeleza dira ya taifa

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
124
66
Kwa hakika ni jambo la kukatisha tamaa kwa siku za hivi karibuni kutazama mikutano ya vyama vya siasa nchini Tanzania yenye hoja zilezile za kizamani na zisizodumu . Hakuna ujasiri, hakuna ari na hakuna ujumbe wenye nguvu zaidi ya sentensi chache kwa wakati mmoja zenye porojo nyingi.

Dira husaidia kufafanua vigezo vya maendeleo ya binadamu, kijamii na kiuchumi. Dira kwa ajili ya nchi humaanisha kufafanua hali tunayotaka kuishi katika wakati ujao ambayo ni bora zaidi katika nyanja mbalimbali za maisha ya kila siku kuliko hali tunayoishi leo.

Maendeleo ya Taifa ni mchakato ambapo jamii hubadilika, uwezo na mtaji wake hujengeka, na taasisi hubadilika . Kwahiyo, mkakati wa maendeleo ni mchakato wa mabadiliko ndani ya maono ya jumla kushughulikia vikwazo vya mabadiliko na kutambua mageuzi muhimu kwa mafanikio ya taifa.

Dira ni sharti la maendeleo. uwezekano wa mkakati wa maendeleo wa nchi huongezeka kulingana na ushiriki na kujitolea kwa wadau wake wote wa kijamii na kisiasa. Dira ya pamoja ya siku zijazo kati ya wadau wakuu wa kijamii na kisiasa nchini ni rasilimali ya kitaifa.Na vijana wana umuhimu sana katika ushiriki wa uundwaji wa dira ya nchi .

Ni muhimu sana kuwa na dira ya kitaifa katika enzi hizi za utandawazi, wakati faida ya ushindani ya nchi inajengwa na haipatikani bure, na wakati mabadiliko yanayohitajika ni ya kimuundo na kwa hivyo ni ya muda mrefu.

Katika dira yoyote ipo haja kuwashirikisha vijana na kuwapa uhuru kushiriki vile ambavyo vinawafaa wenyewe,wazee na vizazi vijavyo.

KWANINI VIJANA WANA UMUHIMU KATIKA MAONO YA TAIFA:-
Vijana hupigania maendeleo kote Tanzania na ulimwenguni , lakini ingawa wanaunda nusu ya Watanzania wote, hawawakilishwi na hawathaminiwi ipasavyo katika maeneo ambayo maamuzi hufanywa na ambapo nguvu iko.

Wamekuwa waoga na wana fursa chache na zilizozuiliwa za kufanya kazi kupitia taasisi rasmi kuunda sera ambazo huathiri moja kwa moja maisha yao.

Vijana wa kike na wanawake, na vijana kutoka makundi yaliyotengwa, wanakabiliwa na ubaguzi uliokita mizizi na vikwazo vya juu zaidi vya ushiriki. wengi wao wamekuwa mfano wa kuigwa kwa ushiriki katika kuijenga Tanzania bora kama wanaharakati katika jamii zetu. Lakini wanapopinga kwa amani, wanapuuzwa, kudharauliwa, au kukandamizwa - mara nyingi kwa ukali.

Haishangazi kwamba vijana wengi wako ndani ya kukatishwa tamaa na walio madarakani na wengine wanapoteza matumaini kwa siku zijazo.

YAFUATAYO YANAHITAJIKA IKIWA VIONGOZI WATATIMIZA AHADI ZAO ZA KUWASIKILIZA NA KUFANYA KAZI PAMOJA NA VIJANA ILI KUJIFUNZA KWA KULETA MABADILIKO:

1. Kutoka kukosekana kwa usawa, ubaguzi, na unyanyasaji hadi kupatikana kwa haki kwa vijana na kuthaminiwa.

2. Kutoka kuwalazimisha kuwa wafuasi hadi kukumbatia matakwa na ndoto zao

3. Kutoka kudhibiti hatima zao hadi kuwapa nafasi ili kuzijenga siku zijazo

4. Kutoka kuwaacha pembeni hadi kuwashirikisha katika kila hatua ya kufanya maamuzi.

YAFUATAYO NI YA KUFANYIA MAANANI:-
• Vijana kupewa ufikiaji wa haki kwa wakati na pale ambapo wenzao wanakuwa waathirika wa matendo yao au shida kisheria zinapowakumba au wanapokuwa na shida kipesa, madeni, kodi, huduma za umma, au changamoto ndani ya familia au jamii zao wanapaswa waeleweke na wenye maamuzi kuingia katika jamii zao wanapoishi na sio kuwahukumu na kuwapeleka mojakwamoja mahakamani au kuwachukulia sheria mkononi kwa kuwaadhibu.

• Serikali lazima wajitahidi kuwafunza/kuwazuia polisi na watendaji wengine wa haki wasiwatusi vijana bali washirikiane nao zaidi ili kupambana na “yale yenye kuleteleza upotofu na uharibifu na kupelekea kuchochea uendelevu wa rushwa,mmomonyoko wa maadili na umasikini”.Kwamfano,Malala Yousafzai alipigwa risasi ya kichwa alipozungumzia kuhusu haki ya wasichana kusoma. Alipopata fahamu, aliendelea na msimamo wa kukataa kunyamazishwa.Leo hii ni mfano wa kuigwa kwa wasichana na wanawake kote duniani.

• Lakini mara nyingi jamii haitazami, wanaharakati wachanga mara nyingi huchukuliwa kama tishio, badala ya kuthaminiwa kwa uwezo wao na mawazo yao mazuri ya kubadilisha jamii, bali wanaonekana kama wachochezi na wavunja misingi iliyowekwa na jamii.

• Wanaharakati vijana wengi wao ni waathirika kihisia na kimwili , na wengine hata wamekuwa walemavu wakudumu na wengine wamepoteza maisha kabisa. Hawapaswi kuadhibiwa kwa sababu ya kusema na kujitetea haki zao. Gonjwa hilo haliwezi kuwa kisingizio cha kuwanyamazisha au kuwadhuru na kuwapoteza. Jamii inapaswa Kukomesha mashambulizi dhidi ya watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari na vijana wengine ambao wana ari ya kujenga Tanzania bora.Watu hawa wanapaswa kulindwa,kupewa nafasi na kutetewa.

• Kuwezesha ushirikiano kati ya mashirika ya kijamii, huduma za kiafya za mitaa ,mataasisi, shule na vyuo mbalimbali kwa pamoja wanapaswa kuwasaidia vijana wetu wawe salama kimwili na ustahimilivu wa kiakili wakati wakishiriki mambo ya kijamii;

• Suala la kuweka salama nafasi kwa vijana ni kazi ya pamoja, na kutoa upatikanaji wa ushauri nasaha ili kushughulikia makuzi salama na maadili mazuri ni mambo ya msingi kuzingatiwa na kutiliwa maanani.

• Vijana wanaendesha harakati za kijamii zinazosukuma mabadiliko , na wanaongoza katika juhudi kupinga dhidi ya machafuzi ya hali ya hewa, ukosefu wa haki ,ubaguzi wa kibinadamu,usawa wa kijinsia, na demokrasia.

• Lakini vijana wanahitaji maeneo salama ya kukusanyika, kuweka ajenda za siku zijazo, na kuhamasisha utekelezaji wake ,nafasi hizi lazima ziwe huru na zipatikane katika mitandao na nje ya mitandao ya kijamii na katika ulimwengu wa kweli, Lakini kama mtandao bado haupatikani kwa watu wengi, ipo haja.

• kuibua nguvu za jamii za vijijini nakujenga uhusiano kati ya vijana ndani na nje ya nchi.Ni muhimu viongozi kuwa na mamlaka ya kukutana na vijana pale walipo, badala ya kutarajia vijana kuwa wageni kila wakati kwenye majukwaa yao.

• Mawasiliano hayapaswi kuwa ya upendeleo kwa upande mmoja ,wakitutaka wanatupata ila tukiwataka inakuwa mlolongo mrefu mpaka haki inaminywa na kukatisha tamaa.

• Jamii inapaswa Kutunga sheria kusisitiza usalama wa mtandao kama haki ya binadamu na kuhusisha vijana kimaana katika mazungumzo kuhusu utawala wa mtandao ili waweze kuwa salama kujieleza mtandaoni
MWISHO.

Lazima sote kujitahidi kuwa mabingwa kwa vizazi vijavyo ,Umuhimu kimaadili wa kulinda maslahi ya vizazi vijavyo huangukia kwa kila mtu, bila kujali jinsia wala umri . Lakini kuna hisa maalum yakuwekeza katika kesho.

Baadhi yetu tutaishi kuona mwisho wa karne hii na watoto wetu na wajukuu wataweza kuishi mbali katika inayofuata. Hivyo ipo haja, kuzungumzia siku zijazo, kuhakikisha matendo yetu hayadhuru vizazi vijavyo. Tujenge urithi Wa Mtanzania ambao tutajivunia na kujipiga vifua kila iitwayo leo.
 
Back
Top Bottom