Kamanda
Senior Member
- Dec 5, 2007
- 150
- 176
Baada ya sakata la Richmond kumuumbua Lowassa na namna alivyohusika na ufisadi hata kuridhia kupewa zabuni kwa kampuni ya kitapeli ya kuzalisha umeme, wakati haina hata mafundi wanaojua kuchomeka bulb kwenye holder yake, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Emmanuel ole Naiko ameibuka na kudai kuwa watu wanaotoka Monduli sasa wanaonewa na kwamba wanaundiwa eti mkakati wa kuwasafisha kwenye ngazi za serikali.
Sijui ukweli wa madai yake, lakini anaonekana kuwa na uhakika anachokisema, sijui kama ametumwa na Lowassa kusema hivyo au ni yale mambo ya kujenga mkakati wa kuhakikisha Edo anakuwa rais kama anavyoota.
Madai hayo ameyatoa kwa waandishi na zaidi sana ameweka kwenye maandishi na kuishutumu vibaya sana Kamati Teule ya Bunge chini ya Dk. Mwakyembe kuwa ilikuwa na nia mbaya.
Je ana hoja au ni hatari ya kutapatapa kwa mfa maji. Nadhani naye amenusa mahali kuwa anasubiri safari ya kurejea home kwake huko huko Monduli.
Tunamfahamu Ole Naiko bwana.