Naiko adai wanaotoka Monduli wanaonewa, watapambana

Kamanda

Senior Member
Dec 5, 2007
150
176
Baada ya sakata la Richmond kumuumbua Lowassa na namna alivyohusika na ufisadi hata kuridhia kupewa zabuni kwa kampuni ya kitapeli ya kuzalisha umeme, wakati haina hata mafundi wanaojua kuchomeka bulb kwenye holder yake, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Emmanuel ole Naiko ameibuka na kudai kuwa watu wanaotoka Monduli sasa wanaonewa na kwamba wanaundiwa eti mkakati wa kuwasafisha kwenye ngazi za serikali.

Sijui ukweli wa madai yake, lakini anaonekana kuwa na uhakika anachokisema, sijui kama ametumwa na Lowassa kusema hivyo au ni yale mambo ya kujenga mkakati wa kuhakikisha Edo anakuwa rais kama anavyoota.

Madai hayo ameyatoa kwa waandishi na zaidi sana ameweka kwenye maandishi na kuishutumu vibaya sana Kamati Teule ya Bunge chini ya Dk. Mwakyembe kuwa ilikuwa na nia mbaya.

Je ana hoja au ni hatari ya kutapatapa kwa mfa maji. Nadhani naye amenusa mahali kuwa anasubiri safari ya kurejea home kwake huko huko Monduli.

Tunamfahamu Ole Naiko bwana.
 
Baada ya sakata la Richmond kumuumbua Lowassa na namna alivyohusika na ufisadi hata kuridhia kupewa zabuni kwa kampuni ya kitapeli ya kuzalisha umeme, wakati haina hata mafundi wanaojua kuchomeka bulb kwenye holder yake, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Emmanuel ole Naiko ameibuka na kudai kuwa watu wanaotoka Monduli sasa wanaonewa na kwamba wanaundiwa eti mkakati wa kuwasafisha kwenye ngazi za serikali.

Sijui ukweli wa madai yake, lakini anaonekana kuwa na uhakika anachokisema, sijui kama ametumwa na Lowassa kusema hivyo au ni yale mambo ya kujenga mkakati wa kuhakikisha Edo anakuwa rais kama anavyoota.

Madai hayo ameyatoa kwa waandishi na zaidi sana ameweka kwenye maandishi na kuishutumu vibaya sana Kamati Teule ya Bunge chini ya Dk. Mwakyembe kuwa ilikuwa na nia mbaya.

Je ana hoja au ni hatari ya kutapatapa kwa mfa maji. Nadhani naye amenusa mahali kuwa anasubiri safari ya kurejea home kwake huko huko Monduli.

Tunamfahamu Ole Naiko bwana.

Hii Hoja,

Ina maana moja tu! nayo ni TIC kuchafu kunahitaji kusafishwa, hii ni pre-emtive defence trick !!! Mwambieni kama aliingia kwa mrengo wa ki-monduli style; then, yes time is almost up! He should get prepared with immediate effect.
 
Mwisho wao (MAFISADI) umefika and lazma heshima ya serikali irudi.
 
aise hayo maneno mazito sana na yanatakiwa yachambuliwe kwa umakini hebu tupatieni nakala ya hayo maelezo ya huyo middleman wa wawekezaji (wezi)ili yawepo kwenye kumbukumbu za JF halafu tuangalie jinsi ya kumuadhibu kwa kutukejeli watanzania kupitia Mwakyembe
 
In my Opinion, Naiko can say anything . . . He can look into the matter in a positive or negative way.

He can only see sense if he look the matter into balanced way. Huwezi kumzuia mtu kusema. Mdomo ni mali yake.
 
Unajua kuwa mzee Naiko ninamtilia shaka sana kwenye utendaji wake. Ktk safari zote anazomsindikiza Muungwana nje yeye huwa hata hajishughulishi kutafuta aawekezaji wa kweli kuja nchini badala yake amekuwa mkia wa Muungwana kila aendapo. Walah huyu jamaa ni mzigo haswa.

Sijawahi kuona au kusikia akiandaa forums au mikutano ya kuhamasisha uwekezaji akiwa ktk safari zote za nje. Huyu jamaa ni mtalii na anatalii kwelikweli. Ni busara arudi monduli akachunge ng'ombe na kuhimiza uwekezaji ngazi ya kata.
 
In my Opinion, Naiko can say anything . . . He can look into the matter in a positive or negative way.

He can only see sense if he look the matter into balanced way. Huwezi kumzuia mtu kusema. Mdomo ni mali yake.

Labda yana sense ila kwa kiongozi wa ngazi za juu kama yeye kuamua kusema-sema kupitia media mambo ambayo yataamsha chuki ktk jamii ni dalili ya kukosa maadili na ina maana ahjui njia na ngazi za kufuata ili kufikisha madai yake.

Pia ieleweke kuwa kuikosoa kamati teule ya Bunge ambayo mapendekezo yake yaliungwa mkono na Bunge zima ni sawa na kulidharau Bunge ambapo ni mfano mbaya kwa kiongozi wa stahili yake.

Pia huyu bwana anataka kutupeleka kusiko na hili suala likishabikiwa basi tutambue tunaurudisha ukabila kwa mlango wa nyuma. (Mwenye akili na afahamu)
 
kamanda umeitoa wapi hiyo habari?

...anyhow Ole Naiko he is another guy who has TO GO.......ni jinsi gani waliipitisha pitisha RDC itabidi watueleze vizuri.

....kama ni kweli hayo ni maneno yake...........basi sisi tunamwambia aache kutapa tapa na kulia wanaonewa.........hivi wananchi wanaokufa kila siku kwa kukosa huduma muhimu (kutokana na kupitisha uozo wa mafisadi) nao wasemeje

.....acha kutapatapa Ole Naiko.......we are coming to you!!
 
..inawezekana maneno yake yana ukweli. hapa jamboforums tumeshuhudia chuki dhidi ya wachaga kwasababu Mramba na Mama Mkapa wanatokea Kilimanjaro.

..katika chuki hizo hizo wapare nao wakaunganishwa ktk jamii inayojulikana hapa jamboforums kama "wakilimanjaro" kwasababu Msuya naye yumo!! rejea topic ya TRA.

..hata kama sikubaliani na Ole Naiko, lakini kwa mambo niliyoyashuhudia hapa jamboforums, nalazimika kutokumpuuza moja kwa moja.

..tahadhari hapa ni kwamba tuwatofautishe wananchi wa kawaida na viongozi wanaotoka ktk maeneo hayo.
 
Inawezekana kabisa katika politics za kubebana Lowassa alimbeba Naiko katika kupata ile kazi na sasa Naiko anataka kuonyesha loyalty yake kwa Lowassa.

Otherwise atueleze watu wa Monduli wanaoonewa ni kina nani (watu ni plural) na wameonewa vipi.
 
Ikishafikia hatua ya mtu kutumia ukabila wake ili kung'ang'ania madaraka kwa kutafuta huruma za watu, basi huyo mtu mjue kabisa amefilisika kisiasa na kiutendaji na anatakiwa kuondoka au kuondolewa kwa nguvu. Ni hatari sana huyu.Tena ni kati ya uchafu serikalini ulioachwa na Mkapa. Unatakiwa kusafishwa mara moja.

Pinda anza kazi sasa baba! hakuna kulala, mpaka wote waishe, hata kama ni kutoka kilimanjaro, monduli, wafipa...hakuna kuangalia. Uozo ni uozo tu hauna kabila wala jimbo, ni lazima kuusafisha mara moja kabla haujazidi kuenea sehemu nyingi zaidi na kuleta madhara makubwa kwa nchi yetu. Huyu lowassa sasa anatafuta gereza, apelekwe mahakamani jamani, tunasubiri nini?
 
Kamanda tunaomba ufafanuzi zaidi,

Je yeye Naiko anaongea ktk capacity kama nani? Mkurugenzi TIC? Mtu wa Monduli?

Je anamtetea Lowassa? Yeye kama nani? Najua sii mwanasiasa..ila naskitika watu wataanza to question his credibility over usafi wa TIC ktk nchi hii!

Kama anapenda yuko huru kwenda kugombea ubunge ili kama akipata aongee kama mwanasiasa!
 
Huyu Jamaa Kwa Namna Moja Au Nyingine Nae Ni Fisadi.haiwezekan Kuwa Upande Wa Fisadi Kama Wewe Sio Fisadi.yeye Anadai Wanamonduli Wanaonewa Kwa Lipi Au Kwa Kuitwa Richmond?wanamonduli Ni Watanzania,na Kama Ikatokea Wamepata Madaraka Serikalin Basi Wayatumie Vizuri,wakilite Mambo Yao Ya Kifisadi Jf Wapo Tutaangusha Mbuyu Tu,mwisho Naomba Kamanda Ulete Hapa Hiyo Nakala Ya Huyo Naiko Ili Tuijadiri Yawezekana Nae Yupo Kwa Vile Alipigiwa Debe Na Richlowasa.
 
Huyu Jamaa Kwa Namna Moja Au Nyingine Nae Ni Fisadi.haiwezekan Kuwa Upande Wa Fisadi Kama Wewe Sio Fisadi.yeye Anadai Wanamonduli Wanaonewa Kwa Lipi Au Kwa Kuitwa Richmond?wanamonduli Ni Watanzania,na Kama Ikatokea Wamepata Madaraka Serikalin Basi Wayatumie Vizuri,wakilite Mambo Yao Ya Kifisadi Jf Wapo Tutaangusha Mbuyu Tu,mwisho Naomba Kamanda Ulete Hapa Hiyo Nakala Ya Huyo Naiko Ili Tuijadiri Yawezekana Nae Yupo Kwa Vile Alipigiwa Debe Na Richlowasa.

Nafasi ile na watu wanamna yake wote waliipata kwa kifua cha Mzee mamvi.Sasa linakuja Tsunami kuanzia kule waliko akina Mkwasa hadi yeye Naiko watajua kwamba kubebana si kitu kizuri hata mara moja .Nangoja yule Mkuu wa Wilaya moja kule Mbeya alimpiga mwenyekiti wa Kijiji mbele za watu na waziri akiwepo.Yeye cheo alipewa tu na Rais lakini alimpiga mtu mwenye mandate ya wananchi .Pinda sijui uko kundi gani lakini nakumulika kwa taa zote nikuone vyema .
 
Kwa kiongozi unapotoa maneno ya kibaguzi ni hatari sana kwa jamii unayoitumikia. Kwa wapenzi wa soka mtakumbuka wiki iliyopita Kocha wa arsenal alitoa maneno makali sana juu ya mchezaji wa aliyemvunja Edwardo mguu,akagundua maneno yake yalikuwa siyo ya kiungwana akaomba radhi.
Ole Naiko,kwa maneno yake haya makali sana na yenye ubaguzi na ukabila ndani yake,anastahili kuwaomba radhi watanzania. Kwangu mimi nalazimika kuamini ofisi ya TIC imejaa ubaguzi wa kikabila na naamini ofisi hii imejaa wamasai na hasa wale wanaotoka monduli. kama hili halitashughulikiwa,basi ndiyo tunaanza kubaguana kiaina.
 
Oh come on Mr Ole Naiko

Adam Lusekelo said:

Daily News; Tuesday,February 26, 2008 @20:02

THE Tanzanian Investment Centre (TIC) supremo, Emmanuel Ole Naiko, has been having nightmares. He has suggested that there may be a deliberate and systematic campaign to remove people of Maasai ethnicity from top government positions.

Eti, following the exit of former premier Ted Lowassa over the Richmond corruption scandal. Ethnic cleansing! Strong words, Mr Ole Naiko. But I am sure that Bwana Ole Naiko has only been having hallucinations. Well, anyone is allowed to hallucinate. It's not against the law. I once hallucinated that I was holding this curvaceous binti who was kissing me like nobody's business and pouring chilled champagne into my glass.

And then-damn! I woke up to reality. Some people dream of being presidents, some to be star footballers, some of being Miss Tanzania. We all hallucinate. But after that, keep it in the head and enjoy it. Methinks there are vestiges of tribalism in the claims of "ethnic cleansing". How come we haven't heard the Bahaya make noises about the cleansing the ethnic group from top positions in government or companies after Nazir Karamagi resigned from the ministry of energy and minerals!

And how come we haven't heard noises from the Wazaramo. After all, one of their jewel scholars, Dr Ibrahim Msabaha, had to go. So he resigned. Any Mzaramo who has been ethnically cleansed should come to our offices, post-haste and we will forward it to the necessary authorities. I mean Tanzanians might be poor and we are robbed dizzy by some guys who rule us. But we are not uncouth. We are not that unrefined. We are treated like children by thugs in suits. But we are not a bunch of savages.

I think Mr Ole Naiko is trying do some 'ndogo ndogo' for Ted Lowassa. Read it as a campaign to rehabilitate Ted. Mr Ole Naiko implies that Ted Lowassa is equal to all Maasai! Touch Ted and the entire Maasai ethnic group is vilified? Frankly, that is a load of rubbish! Rubbish and dangerous thinking.

I have lived and travelled in Arusha Region for more than 10 years. I have fond memories and fast friends among the Maasai, both men and 'nditos'. They are a very proud people and when you become their friend, you don't have to look over your shoulders. They cherish the word 'trust'. But I don't think that any right thinking Tanzanian should stereotype anyone. It is just not right! Is any Muslim wearing a beard and in a kanzu a suicide bomber? Are all Kuryas soldiers? I know one who is a priest!

Ted Lowassa could be a Mmasai. But he definitely is not Wamaasai. Most of them don't even know about the Richmond scandal. There is a lot of Wamaasai out there who are not called Lowassa. Why should any bum want to harm the Maasais?

Ole Naiko ni hatari kwa jamii, anatakiwa aangaliwe vizuri yeye mwenyewe, Je, amekaa pale muda gani? Je, amefanikisha mangapi au na yeye ndiye FISADI mwingine? Hatutauonea uvivu uvundo kwenye vyombo vya serikali ambavyo jukumu lake ni kuwakwamua WTZ kutoka kwenye umasikini.

Bravo Adam for this artical and many more which you write.
 
Oh come on Mr Ole NaikoOle Naiko ni hatari kwa jamii, anatakiwa aangaliwe vizuri yeye mwenyewe, Je, amekaa pale muda gani? Je, amefanikisha mangapi au na yeye ndiye FISADI mwingine? Hatutauonea uvivu uvundo kwenye vyombo vya serikali ambavyo jukumu lake ni kuwakwamua WTZ kutoka kwenye umasikini.

Bravo Adam for this artical and many more which you write.

Achaneni na tapeli mwingine. Hebu kamuulizeni Ole Naiko kama yeye ni mmasai. Wazazi wake ni Wasonjo, na swahiba wake Lowassa ni Mmeru. Leo ndio wanakuwa watetezi wa Wamasai? Walahi Sokoine akifufuka atakufa tena kwa kihoro. We Lowassa na Naiko, acheni ukabila- nyinyi wenyewe mmeyakana makabila yenu

Asha
 
Ole Naiko ajitetea kuhusu ukabila

na Mobini Sarya

BAADA ya kujikuta katika mashambulizi makali kutokana na kauli zake za hivi karibuni, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Emmanuel ole Naiko, amekana kujaribu kuhusisha ukabila katika sakata la Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond.
Ole Naiko alikuwa akitoa ufafanuzi kuhusiana na mashambulizi yanayoelekezwa kwake kutokana na kunukuliwa akisema kuwa watu wanaolishikia bango sakata hilo wana lengo la kuwaandama watu wanaotoka katika Wilaya ya Monduli.

Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Ole Naiko alivilalamikia baadhi ya vyombo vya habari, akidai kuwa vimebadili nia yake njema ya kutoa ufafanuzi kuhusiana na mkataba huo na kuifanya kuwa kinyume na alivyokusudia.

Ole Naiko, ambaye awali alikuwa amekataa kuzungumza na gazeti hili kwa maelezo kuwa hataki malumbano, alikanusha taarifa zinatolewa kuwa alitoa tamko la hatari, akionya wale wanaoelekeza suala la mkataba wa Richmond kuwa wanawaandama watu wanaotokea Monduli.

Akifafanua kauli yake hiyo, alisema kuwa hawezi kutumia ukabila hata siku moja, kwani hata mke wake ni Mpare kutoka Usangi, ambaye imani yake ni ya Kiislamu, na yeye ni Mmasai wa Monduli, ambaye imani yake ni Mkristo wa Kanisa la Kilutheri, kwa hiyo watoto wake hawana kabila zaidi ya Utanzania.

“Sijui mimi nitakuwa nimerukwa na akili niseme mambo ya ukabila,” alisema Ole Naiko na kuongeza kuwa kuna watu walikuwa wanamtafutia sababu na sasa wanatumia suala hilo kumkandamiza ili aonekane ni mbaguzi.

Kwa kubainisha kuwa hakuhusisha suala hilo na ukabila, alisema kuwa yeye binafsi hakutajwa katika ripoti hiyo ya kamati teule ya Bunge kuwa alihusika na mkataba huo, bali taasisi anayoiongoza, yaani TIC.

Alisema alilazimika kutoa taarifa kwa vyombo vya habari baada ya kuona baadhi ya magazeti yameanza kuandika yakipindisha ukweli kwa kuonyesha kuwa TIC ilikuwa na makosa.

Alisema anashangazwa na baadhi ya magazeti (ambayo hakuyataja), yamekuwa mstari wa mbele kushikia bango suala la yeye kutumia ukabila wakati alipowaalika waandishi wake wakati anatoa ufafanuzi, hawakuhudhuria.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa awali aliamua kuitisha mkutano na waandishi wa habari, ili kujibu tetesi zilizokuwa zinatolewa na vyombo vya habari zikielekezwa TIC, ambayo yeye ni mkubwa wake, kuwa vigogo wake walihusika kutoa ushahidi wa uongo kwenye kamati ya Bunge iliyokuwa inachunguza kashfa ya Richmond.

“Kuna watu wanaokota okota nyaraka kisha wanakwenda kuzichapisha kuwa Ole Naiko amesema hivi… mimi niliita waandishi wa habari baada ya kuona lawama nyingi za Richmond zinaelekezwa TIC kama taasisi na si kama mtu binafsi. Kwa mfano, kuna gazeti moja katika toleo lake la Januari 2 liliandika ‘Vigogo wazidi kuanikwa.’

“Ukisoma ile habari inasema baadhi ya mashahidi walibainika kusema uongo katika kamati ya Bunge na walipoitwa mara ya pili wakakiri kusema uongo, mmoja wao ni kigogo wa ngazi za juu wa Kituo cha Uwekezaji (TIC),” alinukuu gazeti hilo na kuongeza kuwa baada ya kuona hivyo akaamua kuitisha mkutano kama mkuu wa kituo na kutoa tamko kuwa kituo chake hakihusiki kwa namna yoyote ile na mkataba wa Richmond, kwani si kazi yao kushughulikia mikataba na wala hakuna kiongozi kutoka TIC aliyebainika kutoa ushahidi wa uongo kwenye kamati.

“Mimi najua hili suala linapikwa tu kwa makusudi lakini nikifikishwa kokote kule nitasema yote jinsi suala hili linavyolengwa kupotoshwa, ili ionekane TIC tulihusika, kwa hiyo tuchukuliwe hatua ambayo haikupendekezwa na kamati ya Bunge,” alisema.

Alisema katika njama hizo, wapo watu ambao wanaeneza hata maneno mengine yasiyohusiana na jambo lolote kama vile kueleza kuwa yeye ni rafiki wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Akizungumzia tuhuma za kutumia ukabila kwenye mkataba huo, alisema kuwa yeye alitoa tu angalizo akimnukuu mmoja wa maaskofu aliyetahadharisha watu wasihusishe suala la Richmond na watu wanaotoka Monduli kwa kuwaita Richmonduli.

Source: Tanzania Daima
 
Wewe Ole Naiko uliamua kum-"Xerox" Laizer.........kwa kuwa unatoka Monduli.......hivi kabla ya hapo ni wapi katika UVUNDO huu ambapo watu walihusisha watu wa Monduli zaidi ya kumtaja EL pekee na kundi lake...........sasa Askofu mzima kajiingiza kichwa kichwa kupokea fisadi...........na wewe umeingia kichwa kichwa kum-Xerox Askofu............kwa hiyo by virtue of the logic na wewe.....indirectly (at least for now)........unatetea uovu!!.

Ole Naiko una part yako ume-play kuingiza hasara nchi yetu, kuna thread hapa JF inaonyesha hivo.........................na nyie waandishi mnaotaka kusafisha hawa mafisadi..........please please.....huu mziki wa JF hamuuwezi
 
Back
Top Bottom