Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
MBUNGE NDAISABA AIBUA SAKATA LA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) MBELE YA NAIBU WAZIRI MKUU DKT. BITEKO
Mbunge wa Jimbo la Ngara Ndaisaba Ruholo amelalamikia kuwepo kwa unyanyasaji kwa wananchi juu ya upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa hali inayopelekea wananchi wengi kukosa haki yao ya msingi
Akiongea mbele ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko wakati wa hafla ya uwashaji umeme katika kijiji cha Ntanga Ruholo amesema kuwa wananchi wake wananyimwa haki ya kupata vitambulisho kwa sababu tu ya majina yao.
Amemuomba Dkt. Biteko kuwasaidia wananchi wa wilaya ya Ngara na maeneo mengine ya mipakani kwakuwa wamekuwa wakihangaika kupata huduma muhimu kwa kukosa kitambulisho cha Taifa.
Dkt. Biteko amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Ngara na maeneo mengine ya mipakani kuwa wale wenye uhalali wa kupata vitambulisho hivyo watavipata na wala wasihukumiwe kwa majina yao.
Aidha amezionya taasisi zinazohusika na vitambulisho kuacha ukiritimba na urasimu badala yake watumie sharia na taratibu zinazo takiwa na wananchi wenye sifa basi wapatiwe vitambulisho vyao.
Sambamba na hilo amewataka wananchi kuwa wazalendo na kutoa ushirikiano pale wanapoona mtu ambaye hana sifa wala sio mtanzania anataka kupata kitambulisho basi wakamripoti kwenye mamlaka husika ili wale wenye haki yao waipate.