Naibu Waziri Kakunda: Binti hatoolewa bila 'leaving certificate' ya form four

Hivi amekosa mikakati ya kuboresha elimu mpaka ahangaike vitu vya kitoto hv? Mawaziri huenda hawana kaz za kufanya.
 
Yaani mimi namsamehe bure maana yeye tu kwanza hajitambui na hajielewi!! Hata hafai kujadiliw humu!! Tumuache amebahatisha kupataunaibu waziri acha apambane na hali yake.....anaona amemaliza ujinga tu umemjaa....
 
Ni wa kuwasamehe hawa jamaa

Yaani living certificate anadhani ni kama vitumbua kwamba kila mtanzania anayo

Hawa jamaa naona kama tumewaazima mahali au nchi fulani. Hawajui uhalisia wa maisha ya watanzania kabisa
Wanashindwa kupambana na hali ya Wanafunzi wanao shindwa kuendelea na Masomo kwa kukosa nauli ya Daladala kuifikia Shule....!

Kuna mabinti wanalazimika kupanda magari mawili kuifikia Shule, ukiwatazama wanatoka katika familia Duni (Masikini)

Wapo wazazi wanajitahidi kuwasomesha hivyohivyo kwa nauli za kuungaunga, unafika muda mzazi anamwambia Mtoto wake kuwa ni bora akae/abaki Nyumbani...!!

Haya yapo/yako mtaani huku tunayashuhudia na sio kusimuliwa..

Ni vyema Serikali ikachukua hatua, kwa kuwapeleka wanafunzi wote wanaofaulu, katika Mashule ama yaliyo jirani na Shule wanazotoka au katika Mashule wanayo chagua wenyewe, wakati wa kujaza fomu.!

Mbali na hapo tusipangiane Maisha.
 
Kuna:Management by walking around..MBWA
Kuna :Leading by examples
Kuna:Management by objectives.
Kuna ile ya mpigaji Zumari pia.
Katika zote hizo,ni ipi ya kuweza kutuvusha hapa tulipo.
 
Huyu mzee nimemuelewa anadhamira ya dhati juu ya kukomesha tatizo la mimba lakini approach yake sio nzuri ni wakati wa kuweka sheria zinazoeleweka.
 
Ikiwa kwa mapenzi yako baba kikombe hiki cha vichekesho na mihemko..kituepuke sisi watanzania... Mungu tumekukosea nn sisi wanyonge hadi hv vituko ndio vinatuongoza sisi dah! Si ajabu huyo ni dr flan
 
Back
Top Bottom