Du! Dereva kama angekuwa na jimbo!!!!!!
Tumbi hakuna x-ray hii nchi tunatia aibu sana...sijui vipaumbele vyetu ni vipi kama tunashindwa kuwekeza kwenye afya za walipa kodiwakati wa ajali inatokea nyuma kulikuwa na gari ya waziri wa mambo ya nje mhebMembe na ndio alitoa msaada wa kusaidia kuokoa majeruhi na mali kwenye gari.Mhe naibu waziri yupo salama....ni dereva wake alieumia vibaya kichwani.Sasa dereva anapelekwa muhimbili kutoka tumbi.
Mbona hamna ajali ni bust tu ilitokea gari ikaacha njia na kugonga mpapai
REPEAT - INVISIBLE kaisha weke hii habari toka mapema sana asubuhiAnaitwa Abdullah Juma Abdalla Saddallah na familia yake kupata ajali mbaya eneo la Tumbi Kibaha wakati akitoka Bungeni na familia yake.
Ajali hiyo mbaya ilitokea majira ya jioni hii wakati naibu waziri huyo akitokea Bungeni kuelekea jijini D'salaam akiwa na mkewe pamoja na watoto wake wawili na a dereva wake ambaye aliumia vibaya na kukimbizwa hospital yaTumbi-KibahaMashuhuda wa ajali hiyo akiwemno Abdulaziz Video amedai kuwa chanzo cha ajali hiyo inasemekana alikuwa analikwepa Lori alilokuwa akipishana nalo na hivyo gari lake kuhama njia na kupinduka .
Imeelezwa baada ya ajali hiyo umati wa wananchi wakiwemo vibaka walifika eneo hilo kutaka kupora mali mbali mbali ila hawakuweza kufanikiwa baada ya raia wema kusaidia kuepusha hali hiyo .Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo baada ya kuhojia na mwandishi wa habari hizi na kuwa hali ya naibu waziri huyo si mbaya sana zaidi ya dereva wake ambaye ameumia kichwani.". Chanzo: Francis Godwinblog.
mungu ni mwingi wa huruma na neema atawaponya amina.
tumbi hakuna x-ray hii nchi tunatia aibu sana...sijui vipaumbele vyetu ni vipi kama tunashindwa kuwekeza kwenye afya za walipa kodi
Mungu awatie nguvu wapone ili waendelee na kazi ya kulijenga taifa letu.
Poleni sana Mheshimiwa na familia yako!! Mpone haraka na kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa!!
Kujenga au kulitafuna? kuna nini unachosema eti waendelee kulijenga taifa letu
Mkuu ukifikiria sana kihivyo utakuwa stressed bure na kujikuta unaongea peke yako barabara! Just smile n walk away huku ukitafuta mbinu ya kuwatoa hawa wakoloni weusi. Mhe kapata ajali, tumtakie kheri ya kupona haraka ili ashuhudie mabadiliko yanayokuja.Ujenzi wa taifa gan? mbona mnanichanganya?
walikuwa wanawahi kwenda kudalalia ardhi ya tanzania kwa muwekezaji.Nini sababu ya ajali?
Mkuu ukifikiria sana kihivyo utakuwa stressed bure na kujikuta unaongea peke yako barabara! Just smile n walk away huku ukitafuta mbinu ya kuwatoa hawa wakoloni weusi. Mhe kapata ajali, tumtakie kheri ya kupona haraka ili ashuhudie mabadiliko yanayokuja.