Malipo kwamungu
JF-Expert Member
- Mar 12, 2012
- 574
- 86
Samweli Sita alikuwa spika wa viwango haitakaa itokee
Mheshimiwa uliona wapi Kaka akamuadhibu Mdogo wake. Ingekuwa Jirani ungeona mpaka JW safari hii wangehusika kumtoa mtu nje ya ukumbi.cuf si walifanya vurugu jaba awape adhabuu sasa tuone
Naibu Spika wa Bunge,Ndugu Job Ndugai amesema kuwa kuanzia sasa hatamwadhibu Mbunge yeyote anayeleta vurugu Bungeni kwakuwa amechoka lawama. Akihojiwa na Redio One Stereo katika kipindi cha Kumepambazuka asubuhi hii,Ndugai amesema kuwa yeye amechoka kuitwa mzembe,zezeta na goigoi na vyombo vya habari.
Ndugai amesema kuwa hata kwa Wabunge waliosababisha tafrani Bungeni jana, hata mmoja kuichana Nyaraka za Bunge,hawatachukuliwa hatua yoyote. Kila Mbunge anayeadhibiwa na Kiti cha Spika anaonekana Shujaa. Sisi tunamuona mtovu wa nidhamu,wananchi wanamuona shujaa.Siko tayari tena kwa hilo.'alisema Ndugai
Kuhusu uandalizi wa Bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani na kama hupitiwa kabla ya kusomwa Bungeni,Ndugai amesema kuwa Bajeti hizo zinapaswa kujadili mafungu ya Bajeti husika ya Serikali na si vinginevyo. Kwanza,hawa wenzetu wanatoka na Bajeti zao nyumbani moja kwa moja na kuja kuzisoma pale.Hawapaswi kutunga za kwao.Wanatakiwa kujadili mafungu ya Bajeti ya Wizara husika tu. Wakati mwingine,mtu mmoja anajiandikia tu Bajeti ya Upinzani wenzake hawawezi kumkana Bungeni alisema kwa hasira Ndugai.
Alipoulizwa kuhusu kutenda haki kwa kuwaadhibu na Wabunge waCCM,Ndugai alikwepa na kuanza kufoka kuhusu Wabunge wa CHADEMA kuwa hawana nidhamu na hatowagusa tena. Watanzania si ndivyo watakavyo .sawa,na sisi tutawaacha ili wasiwe mashujaa! alisisitiza Ndugai.
Mimi : Waungwana wenzangu watanzania, tutegemeee nini Bungeni kutokana na kauli hii ya Naibu Spika? Naibu Spika ndiyo amesusa? Basi awapishe wengine kwakuwa hakuna maana ya kuwa naye tena kama Naibu Spika
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
unapoacha kufuata kanuni na kufanya maamuzi kwa kufuata hisia matokeo yake huwa si mazuri hata kidogo'
Mkeo hata kama akikuudhi vipi hadharani huwa hapigwi hadharani, mume bora anafahamu wapi pa kwenda kumrekebisha.Kwa sababu wamefanya vurugu wale walio funga ndao ndoa ccm B ndo maana hachukui hatua.
Mkeo hata kama akikuudhi vipi hadharani huwa hapigwi hadharani, mume bora anafahamu wapi pa kwenda kumrekebisha.
Wabunge wa chadema majanga tupu.
Huyu bwana sio kuwa kasusa, hizo ni mbinu tu za kukwepa kuwawajibishwa wabunge wa CCM na CUF ambao jana na hata huko nyuma (hasa wa CCM) walionyesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu.Naibu Spika wa Bunge,Ndugu Job Ndugai amesema kuwa kuanzia sasa hatamwadhibu Mbunge yeyote anayeleta vurugu Bungeni kwakuwa amechoka lawama. Akihojiwa na Redio One Stereo katika kipindi cha Kumepambazuka asubuhi hii,Ndugai amesema kuwa yeye amechoka kuitwa mzembe,zezeta na goigoi na vyombo vya habari.