Naibu Spika: Sitamgusa Mbunge yeyote

Naibu Spika: Sitamgusa Mbunge yeyote

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Naibu Spika wa Bunge,Ndugu Job Ndugai amesema kuwa kuanzia sasa hatamwadhibu Mbunge yeyote anayeleta vurugu Bungeni kwakuwa amechoka lawama. Akihojiwa na Redio One Stereo katika kipindi cha Kumepambazuka asubuhi hii,Ndugai amesema kuwa yeye amechoka kuitwa mzembe,zezeta na goigoi na vyombo vya habari.

Ndugai amesema kuwa hata kwa Wabunge waliosababisha tafrani Bungeni jana, hata mmoja kuichana Nyaraka za Bunge,hawatachukuliwa hatua yoyote. ' Kila Mbunge anayeadhibiwa na Kiti cha Spika anaonekana Shujaa. Sisi tunamuona mtovu wa nidhamu,wananchi wanamuona shujaa'.Siko tayari tena kwa hilo.'alisema Ndugai

Kuhusu uandalizi wa Bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani na kama hupitiwa kabla ya kusomwa Bungeni,Ndugai amesema kuwa Bajeti hizo zinapaswa kujadili mafungu ya Bajeti husika ya Serikali na si vinginevyo. ' Kwanza,hawa wenzetu wanatoka na Bajeti zao nyumbani moja kwa moja na kuja kuzisoma pale.Hawapaswi kutunga za kwao.Wanatakiwa kujadili mafungu ya Bajeti ya Wizara husika tu. Wakati mwingine,mtu mmoja anajiandikia tu Bajeti ya Upinzani wenzake hawawezi kumkana Bungeni' alisema kwa hasira Ndugai.

Alipoulizwa kuhusu kutenda haki kwa kuwaadhibu na Wabunge waCCM,Ndugai alikwepa na kuanza kufoka kuhusu Wabunge wa CHADEMA kuwa hawana nidhamu na hatowagusa tena. ‘Watanzania si ndivyo watakavyo….sawa,na sisi tutawaacha ili wasiwe mashujaa!' alisisitiza Ndugai.

Mimi : Waungwana wenzangu watanzania, tutegemeee nini Bungeni kutokana na kauli hii ya Naibu Spika? Naibu Spika ndiyo amesusa? Basi awapishe wengine kwakuwa hakuna maana ya kuwa naye tena kama Naibu Spika

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Wakifanya hawa, anachukua hatua, wakifanya wale, anasema hatachukua hatua tena. Huu mtindo wa kusema "kuanzia leo ...." una maana hakuna kanuni zinazoeleweka bungeni, au kanuni zinapindishwa ili kuwaadhibu baadhi na kuwakwepeshea adhabu baadhi. Usishangae kesho Ndugai akasema "kuanzia leo mbunge atakayetukana namwitia askari", halafu akawa anasikilizia ni nani atafanya kosa hilo ili either achukue hatua au abatilishe kanuni!
 
Naibu Spika wa Bunge,Ndugu Job Ndugai amesema kuwa kuanzia sasa hatamwadhibu Mbunge yeyote anayeleta vurugu Bungeni kwakuwa amechoka lawama. Akihojiwa na Redio One Stereo katika kipindi cha Kumepambazuka asubuhi hii,Ndugai amesema kuwa yeye amechoka kuitwa mzembe,zezeta na goigoi na vyombo vya habari.

Ndugai amesema kuwa hata kwa Wabunge waliosababisha tafrani Bungeni jana, hata mmoja kuichana Nyaraka za Bunge,hawatachukuliwa hatua yoyote. ' Kila Mbunge anayeadhibiwa na Kiti cha Spika anaonekana Shujaa. Sisi tunamuona mtovu wa nidhamu,wananchi wanamuona shujaa'.Siko tayari tena kwa hilo.'alisema Ndugai

Kuhusu uandalizi wa Bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani na kama hupitiwa kabla ya kusomwa Bungeni,Ndugai amesema kuwa Bajeti hizo zinapaswa kujadili mafungu ya Bajeti husika ya Serikali na si vinginevyo. ' Kwanza,hawa wenzetu wanatoka na Bajeti zao nyumbani moja kwa moja na kuja kuzisoma pale.Hawapaswi kutunga za kwao.Wanatakiwa kujadili mafungu ya Bajeti ya Wizara husika tu. Wakati mwingine,mtu mmoja anajiandikia tu Bajeti ya Upinzani wenzake hawawezi kumkana Bungeni' alisema kwa hasira Ndugai.

Alipoulizwa kuhusu kutenda haki kwa kuwaadhibu na Wabunge waCCM,Ndugai alikwepa na kuanza kufoka kuhusu Wabunge wa CHADEMA kuwa hawana nidhamu na hatowagusa tena. ‘Watanzania si ndivyo watakavyo….sawa,na sisi tutawaacha ili wasiwe mashujaa!' alisisitiza Ndugai.

Mimi : Waungwana wenzangu watanzania, tutegemeee nini Bungeni kutokana na kauli hii ya Naibu Spika? Naibu Spika ndiyo amesusa? Basi awapishe wengine kwakuwa hakuna maana ya kuwa naye tena kama Naibu Spika

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Umekuwa msemaji wa ndugai siku hizi auni personal secretary wake au umejisikia tu kuleta hiki ulicho leta.
 
Hajielewi kabisa huyo......anamsusia nani?kama pamemshinda hapo ang'oke.Hata Jenista anamshinda.!!!!!watu wakuwekwawekwa wana matatizo sana.....waliowapandikiza hapo ww na Madam Senkyu waliwaona nyinyi ndo mtawanyamazisha wapinzani sasa hivi Mmesanda.
 
unapoacha kufuata kanuni na kufanya maamuzi kwa kufuata hisia matokeo yake huwa si mazuri hata kidogo'
 
Nimemsikia redio one kumbe huwa yanamfikia haya maneno kuwa ni zezeta,bora kakata tamaa saizi anataka wapelekewe hotuba halafu wao wanazipeleka kwa kina mtela mwampamba wacha wakutane na mawe hivyohivyo!!!!!!!!!
 
Haya sasa ni maajabu!!
Bunge linapaswa kuongozwa na kanuni na wala sio kwa utashi wa kiti cha spika.
Spika ni msimamizi wa kanuni za bunge, sasa kama anashindwa kusimamia kanuni, kuna haja gani kwa yeye kuendelea kukalia kiti cha spika?

Hana lolote huyo ndugai.
Yeye anajua kuwaadhibu wabunge wa CHADEMA tu tena pasipo kosa lolote.
Mbunge wa CCM au CUF akikosea haadhibiwi wala haonywi, mfano ni fujo za jana bungeni, ilipaswa wale wabunge wa CUF na CCM waadhibiwe, lakini kanywea.

Kiti cha spika kimeliharibu kabisa bunge.
 
Ndugai ukiacha uccm bunge utaliweza lkn umeonyesha udhifu mkubwa.eti hautachukua hatua tena tunajua kafu ni ccm b ndio maana
 
Zile hila za kumnyofoa mh.Sitta sasa zinawatokea puani. Kama wangefata kanuni kwa haki tangu awali wasingeliharibu bunge namna hii. Achia kiti ama fata KANUNI kwa haki.
 
Wapinzani wakisema ukweli wanaonekana wachochezi na wavunjaji wa kanuni za bunge. Hauhitaji kuwa msomi sana kujua kwamba bunge linaendeshwa kwa misingi ya kukandamiza wapinzani na kuibeba serikali ya CCM hata pale inapofanya madudu ya wazi kabisa
 
mhhhh wonders never end aisee!

yaani huyu bwana ndugai ana tatizo kubwa sana la ufahamu na kutojiamini.

Ameamua kukosa au kujitoa UFAHAMU kwa makusudi kwa sababu sisi wananchi tunachotaka ni haki na weledi katika kusimamia bunge na sio vinginevyo. Kama mbunge wa CCM amevunja kanuni au kaonesha utovu wa nidhamu basi aadhibiwe na kiti cha spika exactly kama ambavyo mbunge wa upinzani angeadhibiwa, tena kwa kufuata taratibu na kanuni zilizopo.

Impartiality au upendeleo katika maamuzi ya kiti cha spika kwa chama tawala na serikali yake ndicho kinachowa-cost hadi tunawaona hawana weledi au ufahamu, au yupo pale si kwa ajili ya kuongoza bunge na wenzake ili watimize wajibu na haki yao ya kuikosoa, kuishauri na kuisimamia serikali kwa umakini BADALA yake kuilinda na kuitetea serikali hata katika mambo ya ovyo kabisa.

KUTOJIAMINI kwake ni kwa sababu alitegemea kwamba alichofanya angesifiwa na kuonekana shujaa. Mtu anayejiamini hana wasiwasi na maamuzi yake especially kama anafuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa. Kama haufuati hayo then unategemea public support huko ndiko tunaita kutojiamini na kutafuta cheap popularity.

Kwa sasa namshauri mh ndugai aachane kabisa na wazo la kutafuta public sympathy bali asimamie kuhakikisha kwamba kiti cha spika kinaongozwa kwa weledi kwa hali ya juu bila kusahau kuweka mbele maslahi ya kitaifa na siyo ya chama.

Mungu ibariki Tanzania
 
wabunge wa awamu hii wamesahau kilichowapeleka bungeni(mambumbumbu)

mi naona maspika ndio wamesahau kilichowapeleka bungeni, kwa wabunge ni very simple kanuni, haki na sheria tu zingefuatwa na viongozi wa bunge kusingekuwa na utata. Sasa wao wanapenda kukiadhibu chama kimoja tu, na ndio maana wanakwama
 
Naibu Spika, ameshindwa kazi ukiwa kama kiongozi unatakiwa ufate sheria na kanuni zinazokulinda wewe na kuongoza idara husika katika kutekeleza majukumu yake hata kama jamii itakuchulia vipi lakini hupaswi kupishindisha sheria zilizowekwa kwa kuogopa kuwa jamii itakuchukuliaje, huo ni udhaifu wa wazi, kwa watu wanaofikiria sana wataona huo ni upendeleo kwa CCM na CUF kwani wao ndio jana wameanzisha vurugu na hata kuchana nyaraka za bunge.

Swali je kama ingekuwa wabunge wa chadema ndio wamefanya hizo fujo jana angevumilia? kazi kama imemshinda akae pembeni apishe watu wanaoweza kuliongoza na kuliendesha bunge kwa kufata sheria na siyo maono au hisia za watu, mtu au kikundi cha watu fulani
 
alidhani sitting allowance ya bure, hayo ndiyo malipo take, ndugai asijifanye haelewi anacho ambiwa, muhimu ahache kutumika na chama cha mafisadi
 
Back
Top Bottom