Naibu Spika aliesema ofisi yake haina taarifa ya wanaoitwa wa CHADEMA kuvuliwa Uanachama, kumbe alikuwa muongo?

Kabla ya hii barua ya kufutwa uanachama kwa hawa 19, ambayo speaker anasema haina vithibitisho, je uthibitisho wa kuteuliwa kwao hao Covid 19 ulikua na "vithibitisho" ambavyo bunge na tume ya uchaguzi waliridhika? Tuanzie hapo kwanza.
Kwani we ujuavyo barua hiyo huambatana na vitu gani?

Pia kuna pingamizi lolote lilitolewa hawa 19 kutokuapishwa?
 
Siku chache zilizopita, Naibu Spika, Tulia alisiika akisema Bunge halina taarifa rasimi ya wanaoitwa Wabunge wa CHADEMA kuvuliwa uanachama, akimanisha wao kama Bunge hawajapata barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ya kuwavua uanachama.

Sasa kauli tata ya Spika ya leo ya kutaka vithibitisho kuwa CHADEMA walifuata taratibu za kuwavua uanachama si ni uthibitisho kuwa ofisi ya Spika ilipokea barua kutoka CHADEMA?

Ama kweli njia ya muongo ni fupi!
Tatizo hapa ni kuwa Mwendazake kaondoka na nguvu yao imepungua. Kinachofanyika kwa Sasa ni Sarakasi ili kupoteza muda. Kwa Sasa hakuna mwenye nguvu ile... Ile nguvu ni personality ya mtu. Huwezi kuicopy and paste.
 
Yeye kama Spika kama barua zilikuwa hazijitoshelezi alitakiwa awajibu sio kukaa kimya na kuleta malumbano yasio na msingi
Mkuu serikali haifanyi kazi kwa mihemko kwa kuwa mambo ya kufanya kila siku ni mengi sana. Kama wao wanalumbana hayo ni matatizo yao binafsi
 
Back
Top Bottom