Nahusishwa kutumiwa na CHADEMA shuleni

Nahusishwa kutumiwa na CHADEMA shuleni

Kama waewe ni mwalimu uliyepangiwa kufundisha somo la history na badala yake unatumia muda mwingi kuongelea masuala ya siasa/ unafundisha siasa kwenye vipindi vya historia je mwalimu wa uraia/ civics/ general studies atafundisha nini? Je wanafunzi wako wata-cover all topics included in the syllabus? Pole sana mwalimu - Pole Sana Wanafunzi!
 
watu wa aina hii mkuu ni hatari sana kwa taifa letu. yeye amesoma, amepata kazi sasa anaharibu watoto wa watu, ni muhimu sana kumshughulikia hadi ajitambue na aheshimu mipaka ya utumishi na siasa

Naona wa.ji.nga mnajibizana (chating) nyie kwa nyie kama vile nyie ndo wenye nchi. Ujinga mwingine bwana!

cc. Lizaboni.
 
unatafuta umaarufu wa chee halafu unajichanganya mwenyewe. wewe una nini hasa cha maana hadi utafutwe, kwanza huna maadili maana mipango ya kuzini na wananfunzi wako ni utovu mkubwa wa nidhamu na maadili ya uongozi na kukosa uadilifu

akili ndogo angekuwa ccm mngemfuata
 
mbaya zaidi ni mzinzi, kumbe huwa anavizia siku za kufunga shule anawachukua wanafunzi wake anaenda kuzini nao moshi mjini. ameiga tabia za mbowe na slaa huyu

akili ndogo za lumumba utazijua wamejawa na mahaba ya usukule zaidi jibuni hoja
 
kwa hiyo aendelee kuharibu mind za watoto?? bahati nzuri hafahamiki lakini atafahamika tu
Acha kutisha watu na Pumzi yako ya Deni na kila unapopumua unalipa deni.na ili uishi utakwepa hewa ya Mungu.Na ata usiku wa leo Mungu anaweza kuitaka roho yako.
 
LUZaboni wacha matusi na dharau, labda huna unalojua kuhusu TISS!!
Huyo bwn kaomba ushauri, asaidiwe, sio atukanwe tabia mbaya hiyo, heshimu wenzio!!
 
Last edited by a moderator:
Ni kawaida sana hata watumishi wa dini wanafuatwa sana. CCM haitaki kuondoka madarakani. Jambo linalotakiwa ni kuiweka demokrasia imee na isiwe na uhusiano na chama bali na matakwa ya wannachi. Hao TISS yafaa wawepo CDM na kwenye vyama vingine ili kila hila mbaya itambulike na sio kuua vyama . Hatuwezi kujiita tuna vyama vingi na demokrasia huku tunaendelea kukumbatia mawazo mgando ya chama kimoja na wengine kuwaona wakosaji na waharibu amani kwa ajili ya mawazo yao. Ningependa leo hii itokee tume inyang'anye mali zote za CCM na kuunda vyama vipya vijipambanie kwa sera sio historia..

Kuna ukweli fulani katika uzi huu. Mm walihonga mahouse girl wakaniibia electroni device zangu na wakajidai kukata dirisha ionekane kuwa ni majambazi walivamia wakatupa dawa ya usingizi.... Kuna makosa walifanya sehem nikagundua mbinu yote waliyotumia. Any way walichoshindwa kuelewa ni kuwa mtu yeyote makini na mzalendo hawezi kuhujumu usalama wa nchi yake. Kama ni kufanya tufatumia njia za wazi na kidemokrasia....

Kama kweli usalama wa Taifa watumiwa ku intimidate raia wanaset precedence mbaya sana na kama ndivyo basi wao ndiyo watakao haribu amani ya nchi hii maana watu wakijisikia kutokuwa salama watatafuta jinsi ya kujihami na hatimaye kutaanza kuwa na makundi ya kimafia....Chonde chonde ndugu zangu kila mtu anawajibu wa kuilinda nchi hii maana hatuna kwetu kwingine. Kila mtu anahaki ya kulindwa na kujisikia yupo salama ila tu pale anapovunja sheria ya nchi.
 
Kamanda wewe piga kazi
nje ya darasa piga cdm ndani ya darasa fundisha historia. Wakikuuliza maswali ya siasa waambie wangoje kipindi cha civics. Hofu ondoa kabisa hata kama utangplewa meno bila ganzi ukitafut haki hayo maumivu hutayasikia. Kila mtu na imani yake asikulazimishe mtu kupenda kitu ambacho roho yako haikubali! Sema kweli daima fitina kwako iwe mwiko. Mwombe sana Mungu ili kila wakitegesha mtego wajinase wenyewe. VIVA CDM. TUNAJIVUNIA NGUVU YA UMMA.
 
Ndugu wanajamvi napenda kuwasalimu kama ishara ya upendo kwenu. Baada ya salamu naomba nilirudi kwenye suala la msingi lililonifanya niandike uzi huu.

Mimi ni mwalimu kwa taaluma na nafundisha katika shule moja hapa wila ya Mwanga mkoani Kilimanjaro. Nisingependa kuitaja shule hiyo siyo kwa sababu ya woga bali kwa sababu zangu binafsi ambazo nazo ni za Msingi sana.

Msingi wa hoja yangu ni haya mauza uza ninayofanyiwa hapa shuleni wakati mwengine hata nje ya shule. Ambayo kwangu mimi kuna kila sababu ya kuamini watu wa usalama wapo nyuma ya hili.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikihusishwa kutumiwa na CHADEMA katika masuala mbalimbali hapa shule na hata katika jamii ninapoishi kitu ambacho nitakitolea ufafanuzi hapo mwisho.

Miongoni mwa mambo ambayo nahusishwa nayo ni pamoja na kushawishi wanafunzi katika kufanikisha malengo ya CHADEMA ya mabadiliko katika taifa hili. Kutoa hotuba za chuki kwa wanafunzi ninapokuwa nafundisha darasani zenye lengo la kuiharibia CCM na kuipa mtaji CHADEMA (Katika hili siwezi kukanusha wala kukubali kutokana na somo ninalofundisha). Ila ninachopinga ni kuhusianisha ninachofundisha na kuinadi CHADEMA na kuikandamiza CCM. Mimi sifanyi siasa shuleni ila ninayofundisha yanahusisha siasa pia ambayo msingi wake ni Past events, present and their results on future respectively ambayo yanahusu all aspects of life including siasa.

Nafundisha somo la Historia ambalo about 70% percent ya somo la historia ni world's politics. Lakini pamoja na hivyo sifundishi siasa nafundisha matukio ya kihistoria ambayo yanahusisha pia matukio ya kisiasa kama ambavyp yameelekezwa kwenye syllabus.

Lakini pamoja na yote hayo mimi ni mwanachama wa CHADEMA, nilijiunga na CHADEMA mwaka 2011 nikiwa chuo. Kwa wakati wote nikiwa chuo niliweza kufanya kazi kwa karibu na katibu mwenezi wa tawi la CHADEMA lililofunguliwa karibu na chuo chetu. Niliweza pia kuwa katibu mwenezi katika ngazi ya msingi mtaani kwetu mara tu baada ya kuhitimu chuo.

Sio lengu langu kuzungumzia uanachama wangu au kuzungumzia kazi zangu za ufundishaji ninapokuwa shule, ambazo nimeshakili hapo juu sizifanyi kisiasa bali nazifanya kwa uhalisi kama tunavyoelekezwa katika mikataba ya utumishi.

Lengo langu ni kuzungumzia mauza uza ninayokutana nayo katika maeneo yangu ya kazi hata nje ya kazi.

Baada ya kuhusishwa kwa muda mrefu kutumika na CHADEMA nikaanza kufuatiliwa kwa namna ya kuhalibiwa na kuchafuliwa ili nionekane ni mtovu wa maadili.

Kwa mfano: Mnamo mwezi September mwaka 2013, kuna mwalimu ambaye ni rafiki yangu mkubwa sana alinipa taarifa ambayo ilinishtua sana.

Mwalimu huyo alinialika kwenda kufanya starehe na wanafunzi wa kike wa kidato cha sita mjini Moshi. Kwa mujibu wake ni kwamba, wanafunzi hao walimwomba mwalimu juu ya mwaliko huo. Hivyo mwalimu nae akaniomba niungane nae katika tukio hilo kwani wanafunzi waliomwomba kufanya tukio hilo walikuwa wawili na hivyo ingekuwa busara walimu nao tukiwa wawili.

Awali taarifa hizo alinitumia kwa njia ya sms, ambazo zilinishangaza kidogo. Lakini kwa sababu nilikuwa na hisia za muda mrefu kuwa kuna watu wananifuatilia nikaamua kumkubalia mwalimu ambaye ni rafiki yangu: Malengo ya kukubali yalikuwa kama ifuatavyo:-

1. Kwanza nilielewa ni mtego ambao unapangwa ili mwisho wa siku wanikamate kama mtovu wa maadili ya kazi kwa kutembea na wanafunzi. Nilifahamu tangu siku ya kwanza tu nilipopokea taarifa ile. Lakini niliamini zaidi pale mwalimu alieniomba nishiriki nae katika hili aliponionyesha business card ya Lodge ambayo alishaiandaa kwa ajili ya kwenda kufanya starehe na wanafunzi.

2. Niliamua kukubali ili mwisho wa siku waliopanga mipango ile nije niwachezee Turn Around Game. Nije niwageuzie kibao ambapo mwisho wa siku ukweli ungejulikana. Katika hili kuna mipango ambayo niliiandaa binafsi, ikiwemo kuwasiliana na waandishi wa habari na kuwapa picha ya tukio zima pamoja na kuwaeleza siku ya tukio jenyewe. Lengo hapa lilikuwa siku ya tukio mwalimu yule ambae aliandaa mpango ule atiwe nguvuni katika mazingira yale ya starehe akiwa na wanafunzi ili mwisho wa siku angekamatwa na ukweli ungefahamika (Niliamini angesema aliyemtuma kwani asingekubali kuadhilika). Tulipanga kuanda askali polisi na waandishi wa habari, na mipango yote nilishaanza kuifanya kwa kushirikiana na waandishi wa habari. Tulijadili mikakati ya kuifanya ili siku ya tukio mimi niwapige chenga wale wanafunzi pamoja na mwalimu ili wao pekee wabaki na wanafunzi then mtego wetu uwakamate.

Ikumbukwe kwamba wanafunzi wale hawakishirikishwa kwa namna yoyote juu ya huo mchezo, mwalimu aliwadanganya kama kwenda kuwapa ofa mjini Moshi. Kwahiyo hawakuwa wanajua chochote lile juu ya mpango huo. Kutokana na hilo mimi nika take advantage ya kuwashirikisha wanafunzi wale na kuwaeleza nia nzima ya yule mwalimu. Lengo ilikuwa ni kuwapanga wawe upande wangu na tushirikiane katika mipango niliyokuwa naipanga. Ilikuwa ngumu kunielewa lakini mwisho walikubali na wakaniahidi kuwa upande wangu hivyo nikataka wakubaliane na kila jambo ambalo yule mwalimu aliwataka wafanya kuelekea siku ya tukio.

3. Kwakuwa nilifahamu mchezo mchafu unaopangwa kufanyika na kwa kuwa niliamini njia bora ya kumshinda adui yako ni kumfahamu yeye pamoja na mbinu anazotumia nikana ni bora niingie kwenye kile nilichokiona mtego wa adui ninaoufahamu. Niliamua kukubali nikiamini kuwa kupitia mtego huo nitafichua huo uovu, na kama ningejifanya kuufahamu na hivyo kuutupilia mbali kwa maana ya kukataa ofa ile ya mwalimu basi maana yake kungeandaliwa mtego mwengine ambapo pengine nisingeufahamu hivyo ningenasa. Hivyo ningenasa na wangefurahi kutimiza malengo yao. Niliamua kukubali ili niwaumbue kwenye mtego wao wa mwanzao kabisa.

Kwa bahati mbaya tukio hilo halikuweza kutokea, wanafunzi niliokuwa nafanya nao ile mipango, katika tukio ambalo lilikuwa lifanyike siku ya kufanga shule. Wanafunzi wale ilikuwa wafuatwe na wazazi wao kwa ajili ya kwenda majumbani hivyo kukosa nafasi ya kwenda Moshi. Waliniambia juu ya hilo namimi sikuwa na ubishi nikawaelewa hivyo mipango yote kukwama.

Pamoja na yote hayo nimekuwa nikifuatwa sana. Kwa mfano mnano tarehe 26 na 27 mwezi Oktoba mwaka 2013 nilienda Arusha kubudhulia kongamano la CHADEMA na wadau wa kanda ya kaskazini lililofanyika Corido Spring hotel. Kwa hakika sikumuaga mtu juu ya kwenda huko lakini cha kushangaza kuna watu wanataarifa kuwa nilikuwa kwenye kongamano.

Nilihudhuria pia mkutano wa Kiongozi kamanda mpambanaji Henry Kilewo uliofanyika Oktoba 12 2013 mjini Mwanga. Pamoja na kwamba sikukutana na mtu anaenifahamu pale lakini taarifa zangu pia zilisambaa kuwa nilikuwa kwenye mkutano.

Siku ile niliongozana na Henry Kilewa mpaka maeneo ya Angela Inn Hotel ambapo ndipo alipofikia kisha tulirudi wote maeneo ya stendi ya Mwanga tukiwa kwenye gari aina ya Jeep nyeusi. Henry Kilewo hakuwa ananifahamu, lakini wakati wa kuagana niliomba namba yake ya simu na alinipatia.

Siku ile niliweza kuwasiliana nae usiku nikamueleza mengi tu juu yangu na mazingira halisi ya ninapofanya kazi na jinsi ninavyoandamwa.

Kilewo hakuonekana kujali sana pengine kwasababu hakuwa ananiamini sana labda alidhani mimi ni Spy. Kubwa zaidi aliniambia hapendi kujadili siasa kwa njia ya simu hasa kwa mtu ambae hamfahamu. Nilimpongeza kwa hilo na nikaamua kuachana nae.

Kuna tukio jingine ambalo naona linapikwa na bado nalifanyia kazi, nikilipatia uthibitisho nitarudi tena hapa kuliweka.

Lakini leo tarehe 24/01/2014 kuna rafiki yangu ambae nae ni mwalimu amenipa taarifa fulani. Aliniambia kuwa amepokea simu kutoka kwa mtu aliejitambulisha kuwa ni mwenyekiti wa walimu CCM kwa upande wa vijana kutoka moshi akimtaka ampe taarifa zangu. Alinitaja kwa majina yote na kwamba akamueleza kuwa eti mimi natumika na CHADEMA. Mwalimu huyo alinifuata leo na kunipa taarifa ile, nikamshukuru kwa taarifa lakini nilichomwambia ni kuwa kazi hii ya ualimu ninayoifanya siiogopi bali naiheshimu hivyo nipo tayari kwa chochote. Lakini kubwa zaidi nikamwambia mimi sifanyi siasa shule kwani ni kinyume na mkataba wangu wa ajira, ila hiko wanachokitafsiri siasa ni mwendelezo wa majukumu yangu ya kawaida ya kufundisha somo la historia kama mwalimu.

Ninachotaka kutolea ufafanuzi juu ya kutumika na CHADEMA ni kwamba, mimi situmwi na yoyete CHADEMA, sifahamiki na yeyote CHADEMA kuanzia mwwnyekiti mpaka viongozi wa kanda, mimi hawanifahamu hivyo kuniambia kama natumika ni kuweweseka na vuguvugu la mabadiliko.

Ninachotaka kuwaeleza ni kwamba uahiriki wangu kwenye makongamano au mikutano ya hadhala ya CHADEMA ni shauku ya kutaka kufahamu mikakati ya kiukombozi ya taifa letu, na hii ni kwa sababu I love Tanzania deeply, I love CHADEMA and I care so strongly about its future.

Mizengwe yoyote ambayo ninafanyiwa inaniongezea ujasili.

Naomba kuwasilisha.


Wewe ni kamanda wala usiogope chochote, maliza elimu yako vizuri na ukiona wanaendelea kukusumbua omba mzazi/mlezi akuhamishe hapo.
 
Wewe ni kamanda wala usiogope chochote, maliza elimu yako vizuri na ukiona wanaendelea kukusumbua omba mzazi/mlezi akuhamishe hapo.

akili za kushikiwa hizi
yani mtu na kazi yake ategemee mzazi amuamishee? gongo mbaya
 
Tanzania tunalalamika kuwa hakuna ajira lakini kuna watu ambao wanaweza kutengeneza script na kuuza hata magwiji wa sinema kama Hollywood.

Hii story ukiisoma ina mashimo mengi ili ifaulu kuingia kwenye ukweli.

Kuna mtu analengwa kwenye promotion kwa faida ya kisiasa huko mbele ya safari.

Siasa kwa sasa zimepata wenyewe!

Mpaka Uchaguzi Mkuu ufike, tutaona na kusikia mengi sana.
 
Tiss hawana muda mchafu

Hakuna taasisi ndani ya nchi hii iliyokosa kazi za kufanya kama TISS! Wameacha majukumu yao yaliyowekwa kwenye makabrasha yao wanafanya mambo ambayo hata mgambo hawezi kubali kuyafanya. Hebu jiulize ni madudu mangapi yanafanyika nji hïi bila hatua yoyote ya kuweza kuyafichua? Mi huwa nahisi tiss alikufa nayo nyerere.
 
Pole kamanda ila songa mbele

kamanda nakutahadharisha mpango wako wa kutaka kugombea ubunge jimbo la mwanga kwa tiketi ya chadema henry kilewo anaujua. jiandae kumwagiwa tindikali maana kilewo ana kutafuta sana
 
Inaweza ikawa ni Hofu ama ni njia pekee ya makusudi uliyoamua kuitumia kujinadi ili TISS wakujue uko wapi au CHADEMA na CCM wakujue ili iwe Rahisi kwako kufanya Deal na upande wowote utakao kujia.

Anyway! wewe umeamua kuwa nani hasa katikati ya Jamii? Mwalimu au Mwanasiasa! Unaweza kucheza nafasi zote bila ya kuleta madhara kwa taaluma yako (Hapa itategemeana sana na uwezo wa Kichwa chako kubeba mambo ya utu uzima).

Nina Rafiki yangu ni Mwalimu masomo ya Sayansi akiwafundisha madent lazima wafaulu tu.

Shuleni hakuna anayemjua kama ni MWANA CHADEMA ila ukimkuta kwenye anga za siasa ni hatari kuliko maelezo ninayoyatoa. TIMIZA WAJIBU WAKO UTAKUWA SALAMA.
 
Wewe MM3 pa kuweka r hujui wala pakuweka l hujui. Hivi Mwalim kama wewe si majanga tu. Ndio maana Tanzania mijitu mijinga inazidi kuwa mingi, ikiwa Mwalim ni wewe tena wa history, hao wanafunzi watajuwa kuwa Vasco alipotua pwani yetu alikuta tumeendelea kuliko nchi nyingi za Europe?

Hivi wewe nae wa kutafutwa? Kwa lipi zaidi?

Nakushauri ukaonane na madaktari wa wagonjwa wa akili, una tatizo kubwa sana la akili.

Kwanza jifundishe kuandika, ni aibu mwalim wa historia kutokujuwa kuandika.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom