Nahitaji Wafanyakazi 50 Kiwandani- Kibaha

Nahitaji Wafanyakazi 50 Kiwandani- Kibaha

Waajiri kama hawa tukiwaacha ndiyo wananyonya wenzao kisha wanajitajirisha tu.

Sasa laki 2 utaishi ishi vipi? Condition ukae kibaha utalipa kodi kiasi gani? Nauli ya kwenda na kurudi? Kula/maji/umeme/mawasiliano?
Mkuu kwa hali ya sasa na mambo yalivyo magumu ni hora huyu anayetoa kidogo ajira kuliko yule ambaye hakuna anachotoa
 
Ndio mkuu kwa mshahara wa elf sabini tu wakisikia Kuna mshahara wa laki mbili watapiga shangwe na watajiona walichelewa sana

Tuwaombee sana
Kuna jamaa angu analipwa elfu therathin kwa mwezi
 
Vijana huku msiende mtaacha ndala.
Ideas mbona zipo nyingi sana haziitaji mtaji?
Mfano kuwa tu humu JF tayari ni fursa.
Kama kijana upo humu utakubali kwenda kuhenyeka kwaajili ya 200k wewe lazima utakufa masikini
 
Mkuu jambo jema sana na Mungu akubariki sana kwa kuwakumbuka vijana. Kama unavyojua ajira hakuna kwa MASKINI ila zipo kwa wanaojiweza (konekshen)...

Ila Sasa mkuu ,Kiwango cha chini cha mshahara katika sekta ya viwanda nchini Tanzania ni TZS 358,322 kwa mwezi. Kima hiki kipya kilianza kutumika rasmi tarehe 1 Januari 2026 kufuatia ongezeko la asilimia 33.4 lililotangazwa na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu.

Naomba jitahidi uongeze ili angalau kupunguza ukali wa maisha. Nikutakie kila la heri.
 
Mkuu kwa hali ya sasa na mambo yalivyo magumu ni hora huyu anayetoa kidogo ajira kuliko yule ambaye hakuna anachotoa
Kwani hizo ajira hakuna? Watu hawataki kwasababu ya maslahi finyu ,hizo kazi zipo kibao unalipwa elfu 6 kwa siku.
 
Ndiyo fikiria elfu 6 kwa siku utaitumia vipi ,navyojua huko kibaha lazima utumie boda boda kwenda sehemu ya kazi....

Na hiyo inaoenekana ni kazi ya kutumia nguvu means inatakiwa ule milo mitatu ya kushiba.
Mmmh we jamaaa umefikilia deep sana aiseee.. duu hii ni kweli kazi ngumu plas lazima ule daaah 6000 ndogo mkuu kweli kabisa ..

Hapa nimeona why umepingna na jamaaa hawa ni wanyonyaji
 
Mmmh we jamaaa umefikilia deep sana aiseee.. duu hii ni kweli kazi ngumu plas lazima ule daaah 6000 ndogo mkuu kweli kabisa ..

Hapa nimeona why umepingna na jamaaa hawa ni wanyonyaji
Mkuu nawajua hao waajiri ,wanapata faida kubwa sana ,wanachofanya wanatumia udhaifu wa ukosefu wa ajira kulipa vijana ujira mdogo.

Hawezi kupata watu wa kufanya ,akipata mtu atafanya mwezi mmoja wa kujibana atimize lengo lake asepe.
 
Na ndio maana hizi kazi si mara ya kwanza wanakuja kuomba watu humu..

Unakuta mtu anasema anaenda kukomaa mwezi mmoja tu amalize asepe
 
Na ndio maana hizi kazi si mara ya kwanza wanakuja kuomba watu humu..

Unakuta mtu anasema anaenda kukomaa mwezi mmoja tu amalize asepe
NI mtu anayeenda ni yule amekwama kabisa kwahiyo akienda anahakikisha anajibana kweli kweli apokee hiyo hela apate msingi wa kwenda kujifanyia umachinga mjini.

Hauwezi kupata watu wa kudumu na ndiyo maana ukienda tu kiwandani asubuhi kwa hao matajiri unapata kazi fresh tu unaondoka na elfu 7 yako.
 
Dah ,maisha haya ila poa Mimi kwenye factor yangu silipi mtu Kwa Mwezi, nalipa Kwa siku ,kadri kijana anavyojituma ndivyo anavyotoka na pesa ,kuna muda mtu anafikisha laki mbili per day.

Napenda maendeleo yangu na ya wengine , vijana wangu karibu wote kila mtu anaishi kwake,vyumba viwili,vitatu ni kawaida mradi tu hadaiwi Kodi
 
Back
Top Bottom