Nahitaji ushauri: Nimechoka kukaa ukweni

Nahitaji ushauri: Nimechoka kukaa ukweni

hahaa wi ni bora asepe tu huyu.........kila kitu kiko wazi

unajuaje labda halipi kodi ndo maana ameamua kutulia.
Si ajabu anapenda kula vinono ukweni.
Ukweni kuna raha zake bhana ila hapafai kulowea.
Inavyoonekana jamaa amenunua uraia kabisa
Tehe tehe tehe..........
 
Siafadhali angekua anamnunulia mwanae tu! Kunasiku alininunulia suti, mpaka leo ipo tu ndani sajawahi kuivaa.

Ingekuwa umeamua kukaa ukweni ili ubane matumizi kwa kuwa unajenga ningekuelewa ila sasa nazidi kujiuliza
 
Moja ya mitihani ninayo kumbana nayo kwenye ndoa yangu ni mazingira ninayo ishi. Nimevumilia sana lakini sinabudi kusema basi, liwalo naliwe lakini siwezi kukubali kuendelea kuishi ktk nyumba ambayo ni mali ya familia ya mke wangu (Ukweni) Siokwamba nyumba ni mbovu au maeneo ni yakishamba hapana, tatizo nashindwa kujitawala ndani ya ndoa yangu. Nashindwa kufanya maamuzi ya kiume ndani ya ndoa yangu sina kauli kabisa kisa naishi kwenye nyumba yao, nyumba ambayo imejazana kaka na dada wa mkewangu. Siwezi hata kumkata makofi mkewangu pindi aniudhipo kiufupi nipo ndani ya ndoa isiyo nafuraha kwaupande wangu . Hiiyote ilitokana na mimi kukubali kumuoa binti yao. Hiifamilia ni yakibabe sana uwezi amini. Nilipo jitokeza nakutangaza niayangu yakumposa binti yao sharti kubwa nililopewa nikua binti yao hawezi kwenda kuishi mbali nao Kwahoja bado ni mdogo kiumri hivyo anaitaji uwangalizi kutoka kwao. Hivyo ikaamuliwa kama nahitaji kumuoa binti yao basi nikubari tuishi wote hapo kwao hivyo nikakabidhiwa chumba ambacho naona kama ndio kinacho nitesa kwasasa. Nimevumilia dharau kutoka kwa kaka na dada zake kwamuda wamiaka minne sasa ila imefikia hatua nasema nimechoka bola kama mke nikose kuliko kuendelea kuonekana ----. Kama kuzaa tumesha zaa natayari mtoto keshakua. Kama nyuma ninayo tena siyo ya urithi kama mtoto wao walisema bado hajakua sasa teyari ameshakua ushahidi ni huyu mtoto tulie nae hapana bola nikose mke kuliko kuendelea kuonekana ----. Inafikia hatua mpaka mkewangu ambeye ndiye mtoto wao ananionea huruma jinsi ninavyo buruzwa na familia yake? hapa bola niendezangu nyumbani wazazi wangu wanashindwa kujitawala pindi wakija kunitembelea wanakosa uhuru Kabbisa wa kupanga mambo mbalimbali na mimi mtoto wao kisa niko ukweni? Ukowapi utamu wa ndoa ikiwa kilakitu anapanga baba mkwe? Chakula anunue mpaka nguo za mke wangu pia?

Still bado unaweza kuedit post hii kwa kuweka punctuations mkuu.
Hebu fanza hivyo bhana
 
unajuaje labda halipi kodi ndo maana ameamua kutulia.
Si ajabu anapenda kula vinono ukweni.
Ukweni kuna raha zake bhana ila hapafai kulowea.
Inavyoonekana jamaa amenunua uraia kabisa
Tehe tehe tehe..........

sa yote hayo ndo yanamponza..........

kudharauliwa na mashemeji bora asepe tu......
 
Wazee wa busara ndio zao! Shtuka fasta. Mnakaa kama mizikule bwana. Ukichelewa yatakukuta mambo ya w bush.
Mkuu, naweza amini usemacho, huyu mzee wenda ni mchawi, kwani ndani ya hii nyumba sipo pekeyangu niishio hapo. Hata dada zake pia wameolewa lakini wote wakohapo na waume zao. Chaajabu yupo mwenzangu nimemkuta hapo, anamika kama7 na hajawahi kudai kupewa rukhsa ya kuhama na mkewe. Chingine kinacho nifanya nihoji ni kwanini tuishi mfumo wa familia moja? (yani woote kama tupo kwa baba yetu mzazi) Nyumba hii Chakula kinapikwa chungu kimoja, sahani ni tatu yani moja barazani (wanaume watupu) nyingine uwani (wanawake watupu) na moja ni yawatoto.
 
Hahahahahahahaaaaaaaaaaa. Wewe hukujua tangu mwanzo kuwa Raha ya ndoa usikae UKWENI. Timuka haraka sana, beba mkeo akigoma, mpe notisi ya miezi mitatu akufuate vinginevya mtangazie kuwa utaoa mwingine. Kitabu cha Mungu kimeelekeza kuwa Mtaachana na Wazazi wenu kwenda kuunda nyumba yenu nanyi mtakuwa mwili mmoja.
 
Una bahati wewe sio kakangu. Ungetukanwa ukweni afu na mie nakuita mahali naagiza nyama choma nakusimanga weeeeeeh! Ulcers zingekuhusu.
 
Mkuu, na huo msosi ananunua nani na kupika nani?
Mkuu, naweza amini usemacho, huyu mzee wenda ni mchawi, kwani ndani ya hii nyumba sipo pekeyangu niishio hapo. Hata dada zake pia wameolewa lakini wote wakohapo na waume zao. Chaajabu yupo mwenzangu nimemkuta hapo, anamika kama7 na hajawahi kudai kupewa rukhsa ya kuhama na mkewe. Chingine kinacho nifanya nihoji ni kwanini tuishi mfumo wa familia moja? (yani woote kama tupo kwa baba yetu mzazi) Nyumba hii Chakula kinapikwa chungu kimoja, sahani ni tatu yani moja barazani (wanaume watupu) nyingine uwani (wanawake watupu) na moja ni yawatoto.
 
Huyu ni mume wa ajabu,na wazazi wa ajabu pia,zinduka kijana,kaanzishe mji wako na huko ndo kukua kwenyewe,hujachelewa mkuu.
 
Jamaniiii kwaiyo nyie kila siku game ni chumbani tu! Hamjawahi kujaribu bafuni...jikoni....sebuleni...???/ Unasikitisha sana bro....

Duh!
 
Mkuu, na huo msosi ananunua nani na kupika nani?
Babamkwe ndie mnunuzi wa kila kitu ndani ya nyumba hii. Kuhusu Chakula, kinapikwa kwa zamu. Leo akipika mkewangu kesho anapika wifi yake (mke wa kaka yake) siku inayofuata anapika dada mtu, zamu inakwenda hiyo mpa inarudi tena kwa mkewangu.
 
Jamaniiii kwaiyo nyie kila siku game ni chumbani tu! Hamjawahi kujaribu bafuni...jikoni....sebuleni...???/ Unasikitisha sana bro....

Duh!
Kwahiyo kumbe wenzangu munafanya mpaka JIKONI? aah munafaidi kweli.
 
Jamaniiii kwaiyo nyie kila siku game ni chumbani tu! Hamjawahi kujaribu bafuni...jikoni....sebuleni...???/ Unasikitisha sana bro....

Duh!

kutakuwa kuna matatizo mengine mbona kila kitu wazi!
wacha nimwombee kidogo!
 
Jipange ndugu, maisha ni uchaguzi. Simamia kile ambacho nafsi yako inahitaji
Mkuu, hakika ninahitaji uhuru ulio ambatana na heshima ndani ya ndoa yangu. Inafikia hatua naombea huyu mzee wenda(babamkwe) afe, wenda nitapata fursa ya kuhama hii nyumba.
 
kwa hiyo baba mkwe anawalisha familia nzima, na haulipi umeme wala maji. na hauna gharama hata ya hausigelo. usihame bwana. wewe vumilia, kama mnalishwa kama watoto hapo:A S-confused1:
Babamkwe ndie mnunuzi wa kila kitu ndani ya nyumba hii. Kuhusu Chakula, kinapikwa kwa zamu. Leo akipika mkewangu kesho anapika wifi yake (mke wa kaka yake) siku inayofuata anapika dada mtu, zamu inakwenda hiyo mpa inarudi tena kwa mkewangu.
 
kwa hiyo baba mkwe anawalisha familia nzima, na haulipi umeme wala maji. na hauna gharama hata ya hausigelo. usihame bwana. wewe vumilia, kama mnalishwa kama watoto hapo:A S-confused1:
Naweza sema kua hii nyumba kilakitu kikochini ya babamkwe kuanzia Chakula, umeme, maji mpa inafikia hatua ananunua nguo kwa wote (watoto wake na sisi wakweze) yani kama tuko kwa baba yetu vilee!. Lakini hivyo Vyote havina thama kama uhuru niutakao. Nahitaji niwe huru niwe nasauti ndani ya ndoa yangu, niwe nauwezo wakuamua chochote kuusiana na mustakabbali wa ndoa yangu bila kuhofu mtu.
 
Back
Top Bottom