Nahitaji ushauri juu ya ndoa hii niliyokuwa msimamizi

Nahitaji ushauri juu ya ndoa hii niliyokuwa msimamizi

huyu alikwenda moro kuoa sio kufanya kazi,house girl kwa kazi zipi? Mwisho atampangia chumba h/girl no 2........ushauri aache wote arudi dar kujipanga ,.He is simply a silly man :angry::angry:
 
shemeji yangu anafanya kazi mbeya, ana housegirl. Huku dar mke ana housegirl na houseboy. wanawasiliana kwa simu na kutembeleana mara 2 kwa mwezi huku baba akiendelea na juhudi za kurudi dar. kwamba anazini na housegirl huko mbeya au mwanamke mwingine hakuna ajuaye ni siri ya moyo wake. kikubwa ni kuwa yeye na mkewe wanaaminiana. tuache kubebesha wanawake mzigo waume zao wanaposhindwa kujidhibiti na kujiheshimu. unadhani huyu baba asingeenda moro asingeweza kuzini na housegirl chini ya pua ya mkewe? na unafikiri kuweka houseboy utapunguza uwezekano wa mume bazazi kuzini? ni kuomba tu neema ya mungu maana kuna watu wakiwa ndani ni waume, wakiwa nje ni mabasha. utamchunga mume na housegirl utaweza? ukiugua ukalazwa housegirl unaenda nae hospitali au unamrudisha kwao mpaka upone? ukienda kazini unaenda nae? ukiwa usingizini mumeo unamfunga pingu kwenye mkono wako ili usiku asinyate kwenda kwa housegirl?

suala hapa ni umbali uliopo ndugu nyie mnashindwa kuvumilia tofauti na sisi
 
Kwanin usimwambie mwanaume aondoke moro arudi dar kuinusuru ndoa yake.
 
Tunatofautiana aisee..my hubby amekaa na hg mwaka karibu wa nne huu...na wala sina pressure...kama mumeo anajiheshimu it doesn't matter anakaa na hg, hboy au peke yake...
Imagine huko mbali afu eti unatafuta house boy kukaa na familia kisa unaogopa mumeo kitombi...what about your kids...hujasikia story za wanachowafanyia watoto

I am about to go bck home for good...na mume wangu hajawahi kumpa mimba hg...and my assumption hajawahi kutembea na hg...

si kila mwanaume ni fisi kuwa hawezi kaa na mfupa karibu...

Kuna wanaume nawajua mabachela na wanakaa na ma house girl kwa heshima zote...hata kama ni uzinzi lazima ufanye zero grazing?

Huyu mwanaume hata kama si house girl angeoa muuza bar...tabia haina dawa...

pokea likes kibao!jamani tunapishana majukumu.hivi kwa mfano umepata scolarship au kazi uende ughaibuni utaiacha kisa mume atatembea na housegirl au ndo uweke houseboy?huyo houseboy si pia anaweza kuwa chakura ya mumeo?na mume akakuacha mazima? kama mwanaume kitombi ni kitombi tu!hata ukiwepo ndani anaweza kumega housegirl na wewe mke ukatimuliwa kweupeee! ni kuomba mungu tu!
 
ushauri rahisi, huyo mama nae atafute house boy wake wa kipogoro maisha yaendelee
 
Unajua ndugu yangu kuna kipindi kinafika maneno yanagota yaani unahitaji waota ndoto kama akina Yusuph wa kwenye biblia waje kutoa tafsiri zao.Kusema ukweli maneno na maandiko nayajua sana ila kwa hawa ndugu zangu nimechemsha ndiyo maana nikaja kuomba ushauri humu ndani maana naamini hata kama sitapata jibu kamili lakini michango ya watu wa humu ndani itanipeleke hatua nyingine mbele.Na hivi navoandika tayari kuna point watu wameshazichangia kwa hiyo walu nimeanza kupata mwanga.
Kwa taarifa yako nipo vizuri kwenye vifungu wewe cheki hapo chini

Waebrania 13.4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu
“Kwa hiyo, kile ambacho Mungu ameunganisha mtu yeyote asikitenganishe.” (Mwanzo 2:24; Mathayo 19:3-6)
Hivyo, Yehova na Yesu huona ndoa kuwa muungano wa kudumu ambao huisha wakati mwenzi mmoja anapokufa. (1 Wakorintho 7:39)
Kwa kuwa ndoa ni mpango mtakatifu, talaka haipaswi kuonwa kuwa jambo dogo. Yehova anachukia talaka ambazo hazina msingi wa Kimaandiko.—Malaki 2:15, 16.

Ohh sasa nimethibitisha kuwa unalo Neno sasa nenda na hilo wala usiwe na wasiwasi nalo liamini tu maan siy la kwako hilo hata kama akili zitakuwa hazitaki liseme tu nakuhaikikishia linaenda kuitengamanisha hiyo ndoa takatifu
 
Sasa mwanaume arudi Dar ina maana aache kazi mazima aje auze sura Dar

Nadhani cha muhimu tunaangalia kunusuru ndoa, sidhani kama huyo mwanaume akiamua kupata kazi dar hashindwi unless mchepuko umzidi nguvu
 
Mimi najua kuwa kusimamia harusi ni shughuli siyo ile ya ukumbini bali shughuli yake ni siku mambo ya hao wapendanao yanapoenda kombo maana najua wasimamizi ndiyo wanakuwa watu wa mwanzo kuelezewa kinachojiri.

Sasa kuna ndoa nimesimamia miaka miwili iliyopita yaani bwana bibi harusi na bwana harusi walipendana zaidi ya wale ndugu wa kwenye movie ya Romeo na Julieth yaani kila dakika baby umekula, baby unafanya nini sasa hivi yaani ni shida kama hujawahipita huko basi utadhani wapo peponi.

Kisa chenyewe kilianza mwezi wa kwanza mwaka huu, mwanaume alipata kazi mpya Morogoro na bi dada yeye anapiga mzigo hapa Dar.

Walikuja home kutuomba ushauri kwamba wafanyeje, mimi nikafunguka kisawasawa nikawaambia kuwa Morogoro wanaweza wakapaona ni karibu sana na Dar ila issue ya distance relationship siiungi mkono hata kidogo.

Nikashauri jamaa akomae hapahapa mjini atapata kazi nyingine tu nzuri maana familia bado changa. Ebwana kwa kuwa bado wapo mahabani bi dada akasema yeye hana shida Moro si mbali sana yupo radhi jamaa aende Moro akapige mzigo ila kwa sharti kwamba kila Ijumaa jioni mpaka Jtatu asubuhi ama Jumapili jioni ahakikishe anarudi nyumbani.

Kweli jamaa akahamia Moro na kufika Moro akatafuta house girl wa Kipogolo.To cut the story short ni kwamba jamaa sasa si weekend wala nini haji nyumbani tena ni kwamba ameoa house girl wake huyo na sasa ana house girl mwingine kumsaidia yule wa house girl wa mwanzo maana amekuwa mother house.

Sasa bwana bibi harusi amerudi nyumbani kuniomba ninusuru ndoa yake, nimewasiliana na jamaa Moro akakubali kuwa kweli amemuweka ndani house girl wake na akaniambia kuwa hana shida na mama watoto Dar maana na yeye ni mke wake na hakuna kitakachopungua.

In short watu wazima wenye ushauri wa kunisaidia kunusuru ndoa hii naombeni msaada wenu maana akili yangu imegota.

This is serious kabisa wala sitanii naombeni mwenye ushauri wa nini kifanyike anisaidie

Dahhh, kama sinema yaani!....
Ila huyo mume hana adabu, kunogewaje huko!?
 
Nadhani cha muhimu tunaangalia kunusuru ndoa, sidhani kama huyo mwanaume akiamua kupata kazi dar hashindwi unless mchepuko umzidi nguvu

Huyo jamaa hata akipata kazi Dar kazi bure, keshaonjeshwa "nyama ya mtu, ataendelea tu kuonja onja!"
 
Wote kwa ujumla nimependa michango yenu ya dhati, hata kama sitaweza kuleta mwafaka kwenye ndoa hii ila kusema ukweli nimepata mwanga sana tena sana.In short nimepata pa kuanzia na kama si pa kumalizia.Kila kitu hapa kimekuwa very clear kwa hiyo nawashukuru sana.Shukrani za dhati kabisa ziwaendee wote waliotoa mawazo yao na zaidi kabisa kwa mheshimiwa dolevaby, NANDERA, nyumba kubwa dada yangu upo vizuri sana una confidence asilimia 100% pia dada christine ibrahim upo vizuri unisaidie katika maombi yako maana inaonekana upo vizuri kwenye kupiga goti Heaven Sent na MankaM mpo vizuri nyie mnatumia formula ya zero grazing safi sana, Mamndenyi nilikuwa nakuaminia lakini hii ya leo kidogo na wewe imekuchanganya sana kama ilivonichanganya mimi

Karibu sana
Nasubiri mrejesho

Mwambie mwanamke angie kwenye maombi pia
Pamoja sn
 
Huyo jamaa hata akipata kazi Dar kazi bure, keshaonjeshwa "nyama ya mtu, ataendelea tu kuonja onja!"

Akikaa dar kidogo atakumbushwa kuliko kukaa huko moro
 
Msioaene au kuolewa kabla hamjapata kazi za kueleweka.labda kama mnategemea kujiajiri wenyewe.
 
Back
Top Bottom