Nahitaji ushauri juu ya ndoa hii niliyokuwa msimamizi

Nahitaji ushauri juu ya ndoa hii niliyokuwa msimamizi

Nimeiacha mama, ila mume kutwa kunitafuta na meseji za mapenzi sasa sijui alisahau nini. Sigombei mwanaume mimi. Maisha yenyewe mafupi haya ya nini kujipa stress toka kwa mtu mzma mwenzio.

Teh teh teh
Hilo nalo neno

Ila mwisho wa cku atarudi tu ww ndo mkewe
 
Huyo mwanamke achague, kukubali mitara au kufunga virago..

We Africans are polygamist!!
 
Mi ningekuwa huyo mke wa dar ningeshaanza;
sina kifua cha kuvumilia ujinga kama huo;

Ni moja tu kwenda kwa padri, ndoa ivunjwe nijipange na maisha mengine,

Hapo hakuna ushauri kabisa, ameshaona mke wa kwanza hamfai imetosha, mwacheni na maisha yake.

Mfano Mamndenyi ukiambiwa utoe ushari ama usuluhishe ndoa hiyo unaweza ukachukua hatua zipi kuleta amani kwa hao ndugu wawili yaani mke (Dar) na mume (Moro)
 
mwambie mke mkubwa weekend hii aende morogoro mpaka jtatu aone atalazwa sebuleni au atalaa na nani na asitoke hapo mpaka kielewe kam vipi akirudi dar na yeye aongeze houseboy

Nilitaka nikugonge like lakini hapo ulipomalizia na house boy hapo ndiyo pamegoma maana dawa ya moto siyo moto
 
Wapogolo noma, kwa mtaji huu unahitaji kutuliza akili kweli kweli la sivyo unaimaliza kabisa!


ndoa ya dini gani?

Huyo bwana harusi dini gani???? Halafu mambo ya ndoa yataka wale ambao wapo deep washaingia ndoani watu wazima sio wasimamizi na kama housegal kaolewa kwa dini bas tatizo n moja tu hajampa taarifa mkewe mkubwa bas kama n muislam lakini

Huyo Jamaa ni mshamba, sio mstaarabu na mgeni wa ngono tu..kama angekuwa mwenye busara mbona wengi tupo kwenye long distance relation na ndoa zetu lakini ratiba iko pale pale..ni suala la uvumilivu. Basi kama kaamua kuchepuka ndoa aishie uchepukoni kabisaa hajui kula na vipofu huyoo..mdada japo sio sawa lakini dawa ya moto ni maji yatauzima....fikiri chukua hatua

Aisee, hapo ni pagumu. Pole za huyo bibi harusi origino.

hebu nijuze kitu kimoja kwanza huyo mke wa kwanza aliolewa na ndugu wa pande zote mbili walikuwepo?
na kama ndiyo hiyo harusi ya housegirl ilitokea na ndugu wa pande zote mbili zikiwepo?
na kama jibu ni ndiyo kwann ndugu waliafiki ndoa bila kujua hatma ya mke wa kwanza?
ukijibu hayo nitajua tatizo lipo wapi....!!!!????

Kwani huku Dar huyu bibi arusi wa zamani hakuachiwa houseboy ampandishe nishani kisha asimike houseboy mwingine?

Si alijua weekend atapunguza ugwadu

Wandugu, msimamizi wa ndoa anaomba ushauri. Hadi hapo hamjampa ushauri.
 
Bornagain kama kweli wewe ni born again nenda na Neno badala ya maneno yako, itakuwa rahisi sana

Unajua ndugu yangu kuna kipindi kinafika maneno yanagota yaani unahitaji waota ndoto kama akina Yusuph wa kwenye biblia waje kutoa tafsiri zao.Kusema ukweli maneno na maandiko nayajua sana ila kwa hawa ndugu zangu nimechemsha ndiyo maana nikaja kuomba ushauri humu ndani maana naamini hata kama sitapata jibu kamili lakini michango ya watu wa humu ndani itanipeleke hatua nyingine mbele.Na hivi navoandika tayari kuna point watu wameshazichangia kwa hiyo walu nimeanza kupata mwanga.
Kwa taarifa yako nipo vizuri kwenye vifungu wewe cheki hapo chini

Waebrania 13.4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu
“Kwa hiyo, kile ambacho Mungu ameunganisha mtu yeyote asikitenganishe.” (Mwanzo 2:24; Mathayo 19:3-6)
Hivyo, Yehova na Yesu huona ndoa kuwa muungano wa kudumu ambao huisha wakati mwenzi mmoja anapokufa. (1 Wakorintho 7:39)
Kwa kuwa ndoa ni mpango mtakatifu, talaka haipaswi kuonwa kuwa jambo dogo. Yehova anachukia talaka ambazo hazina msingi wa Kimaandiko.—Malaki 2:15, 16.
 
Mimi najua kuwa kusimamia harusi ni shughuli siyo ile ya ukumbini bali shughuli yake ni siku mambo ya hao wapendanao yanapoenda kombo maana najua wasimamizi ndiyo wanakuwa watu wa mwanzo kuelezewa kinachojiri.

Sasa kuna ndoa nimesimamia miaka miwili iliyopita yaani bwana bibi harusi na bwana harusi walipendana zaidi ya wale ndugu wa kwenye movie ya Romeo na Julieth yaani kila dakika baby umekula, baby unafanya nini sasa hivi yaani ni shida kama hujawahipita huko basi utadhani wapo peponi.

Kisa chenyewe kilianza mwezi wa kwanza mwaka huu, mwanaume alipata kazi mpya Morogoro na bi dada yeye anapiga mzigo hapa Dar.

Walikuja home kutuomba ushauri kwamba wafanyeje, mimi nikafunguka kisawasawa nikawaambia kuwa Morogoro wanaweza wakapaona ni karibu sana na Dar ila issue ya distance relationship siiungi mkono hata kidogo.

Nikashauri jamaa akomae hapahapa mjini atapata kazi nyingine tu nzuri maana familia bado changa. Ebwana kwa kuwa bado wapo mahabani bi dada akasema yeye hana shida Moro si mbali sana yupo radhi jamaa aende Moro akapige mzigo ila kwa sharti kwamba kila Ijumaa jioni mpaka Jtatu asubuhi ama Jumapili jioni ahakikishe anarudi nyumbani.

Kweli jamaa akahamia Moro na kufika Moro akatafuta house girl wa Kipogolo.To cut the story short ni kwamba jamaa sasa si weekend wala nini haji nyumbani tena ni kwamba ameoa house girl wake huyo na sasa ana house girl mwingine kumsaidia yule wa house girl wa mwanzo maana amekuwa mother house.

Sasa bwana bibi harusi amerudi nyumbani kuniomba ninusuru ndoa yake, nimewasiliana na jamaa Moro akakubali kuwa kweli amemuweka ndani house girl wake na akaniambia kuwa hana shida na mama watoto Dar maana na yeye ni mke wake na hakuna kitakachopungua.

In short watu wazima wenye ushauri wa kunisaidia kunusuru ndoa hii naombeni msaada wenu maana akili yangu imegota.

This is serious kabisa wala sitanii naombeni mwenye ushauri wa nini kifanyike anisaidie

Bornagain. Inaonekana mume anatambua kuwa yuko ndani ya ndoa na ninaona wazi anampenda mkewe. Kosa alilofanya ni kujaribu mpango kando na kwa bahati mbaya ametekwa. Hilo ni funzo kubwa kwa wanandoa.

USHAURI WANGU
Nashauri kuwa mke aombe likizo kazini na ahamie Moro kwa mumewe kwa muda wote wa likizo; na ahilakikishe anapampana kikweli. Kama house girl aliyegeuka mke anajua kuwa jamaa ana mke huenda atapoteza ujasiri wa kumbana jamaa. Kwa kuwa mume anaonekana bado anamtambua mkewe lkn amebanwa, ninaamini hataweza kumkimbia mkewe atakapomfuata Moro na kukaa naye kwa kipindi chote cha likizo na kwa jinsi hiyo huenda wakaiokoa ndoa yao.

Ikiwa likizo ya mke itashindikana, ni afadhali mke aache kazi na amfuate mumewe kama kweli ana nia ya dhati kuipigania na kuiokoa ndoa yake. Asisubiri mumewe azae na housegirl, ndoa yao itakuwa ngumu zaidi.
 
Ngoja nikwambie kitu msimamizi

Km mwanaume mkimuuliza ana adimit yaani anakubali kuwa ni kweli hapo c akili yake ni nguvu za giza zinahusika!

Ss basi huyu mke asithubutu kwenda kufanya vurugu wala eti kumtoa huyo dada kwa.nguvu atafukuzwa na hyo mwanaume na hataamini macho yake!

Kwanza mpaka amekushirikisha,ameshawahi kwenda huko moro kabla hajakwambia?...if nt y?
If yes, ilikuwaje?

Ss amrudie Mungu,aombe Toba na maombi ya Rehema apige goti ht hapa kwetu namkaribisha....kwa.maombi tu ya.kuita hyo nafsi ,manaake hyo nafsi imeshikwa ndo maana anakubali c akili yake. .. mwanaume mwenyewe atarudi kuomba msamaha.

Ila akijifanya kwenda kimwili cjui kibabe uchawi hauaiangalii hilo ataishia kuharibu kabisa.

Biblia inasema ' Bwana ameumba jambo jipya mwanamke atamlinda mwanaume (mume) wake '

Hapo kosa ni la mke!
Wadada tupunguze kuongea bali Tuombee sn familia
Huyu mke wa jamaa alikuwa anakwenda Morogoro kama kawaida na anamkuta house girl pale akifanya majukumu ya house girl na kusema ule ukweli kwa jinsi alivokuwa anamuamini mume wake yaani dada wa watu alijua kuwa house girl anafanya majukumu ya uhouse girl tu na siku za mwanzo mwanzo hakukuwa na dalili zozote za kimahusiano.Baada ya muda kidogo alivorudi Moro akakuta kama kuna mabadiliko kiasi maana house girl hakuwa na adabu kama mwanzo anasema kuna muda alikuwa anaingia chumbani kwa mumewe kama mtu ambae ameshapozoea.Na katika kupekuapekua chumbani kwa mumewe ndo akakutana na vyupi na kanga chumbani kwa mumewe.So alivomuuliza mumewe akakiri kuwa ni kweli sasa hivi anajisevia house girl.Dada alichosema ni kwamba alikuwa disparate and the same day akarudi Dar maana hakutaka tena kulala Morogoro.Mimi nilivoambiwa nikampigia jamaa apange safari aje Dar tuzungumze, kweli nilizungumza nae akakiri kuwa anatembea na housegirl wake ila akasema kuwa bado anampenda mke wake na anaheshimu ndo yake.Nikamuuliza kumpenda yawezekana kweli unampenda mke wako lakini sasa heshima iko wapi.Akasema alipitiwa tu ila atajirekebisha.Sasa juzi kati mama akarudi Moro kwa kustukiza nakuambia alichokutana nacho ni aibu maana mume wake kaleta house girl mpya na yule house girl original ni mother house.Yaani jamani nyie wanawake hamna huruma kabisa yaani kweli mke wa jamaa unamjua vizuri ila wewe unanataka kitibua ndoa yake kweli jamani.Naamini kwa wanaume ni kesi ndogo sana za namna hii eti kuchukua mke wa mtu jumla ilihali mumuwe yupo
 
Bornagain. Inaonekana mume anatambua kuwa yuko ndani ya ndoa na ninaona wazi anampenda mkewe. Kosa alilofanya ni kujaribu mpango kando na kwa bahati mbaya ametekwa. Hilo ni funzo kubwa kwa wanandoa.

USHAURI WANGU
Nashauri kuwa mke aombe likizo kazini na ahamie Moro kwa mumewe kwa muda wote wa likizo; na ahilakikishe anapampana kikweli. Kama house girl aliyegeuka mke anajua kuwa jamaa ana mke huenda atapoteza ujasiri wa kumbana jamaa. Kwa kuwa mume anaonekana bado anamtambua mkewe lkn amebanwa, ninaamini hataweza kumkimbia mkewe atakapomfuata Moro na kukaa naye kwa kipindi chote cha likizo na kwa jinsi hiyo huenda wakaiokoa ndoa yao.

Ikiwa likizo ya mke itashindikana, ni afadhali mke aache kazi na amfuate mumewe kama kweli ana nia ya dhati kuipigania na kuiokoa ndoa yake. Asisubiri mumewe azae na housegirl, ndoa yao itakuwa ngumu zaidi.

Mke anasema yeye kama yeye kurudi Morogoro kubeba fedheha hawezi kamwe,anasema yeye kurudi kwake Moro ni pale tu atakapohakikishiwa kuwa hakuna tena uhusiano kati ya mumewe na huyo house girl.Infact anataka house girl wote watoweke nyumbani kwa mumewe
 
Kweli kuishi kwingi kuona mengi. Weye unasema ati kafunga ndoa na H/girl. Kafungia wapi na sherehe ilikuwa wapi? Yaani weye kufungia ndoa kitandani tu tayari weye umeona hiyo nayo ni ndoa halal? Hata ya kipagani haifungwi hivyo. Lazima mahari na vilambio viwepo.
Mwambie shem hapo Dar, atulize manyanga. Amkaribishe mzee home na ajiandae vyema kumpokea. Kama wana mtoto, ahakikishe anapata mdogo wake haraka. Kama bado, hapo tena imekula kwake.
Mzee akija, asianze kelele za Oh! Nikija Moro naua leleleleeee. Hapana, amsifu mke mwenza sana na kwamba angetamani ka wangekuja Dar na mzee one day.
Mzee akiona hajamzingua, ataanza kuona kuwa alikuwa juha. Taratib, atajirudi na kurudi home. Kelele hazitamrudisha mzee home. Pia akijidai naye anapendwa ataishia kujiua na Ukimwi bure. Akimtishia mzee hata huyo h/girl wa h/girl naye atakuwa mke wa 3 sasa hivi. Dawa ya kichaa wa mapenzi si kelele ni utulivu na maombi sana.

unashauri kitu ambacho hata wewe unaweza kukifanya? Unawezaje kumshauri mke amkaribishe vyema mumewe ahakikishe anapata na mtoto haraka? VVU je? Labda VVU tuache pembeni. Anabebaje hiyo mimba na stress? Analeaje huyo mtoto na baba aliye na makao kwa mpogolo moro? ingekuwa mimi ningefanya moja kati ya haya mawili: kutaliki /kutengana au kusamehe kutakakoambatana na masharti.
 
Huyu mke wa jamaa alikuwa anakwenda Morogoro kama kawaida na anamkuta house girl pale akifanya majukumu ya house girl na kusema ule ukweli kwa jinsi alivokuwa anamuamini mume wake yaani dada wa watu alijua kuwa house girl anafanya majukumu ya uhouse girl tu na siku za mwanzo mwanzo hakukuwa na dalili zozote za kimahusiano.Baada ya muda kidogo alivorudi Moro akakuta kama kuna mabadiliko kiasi maana house girl hakuwa na adabu kama mwanzo anasema kuna muda alikuwa anaingia chumbani kwa mumewe kama mtu ambae ameshapozoea.Na katika kupekuapekua chumbani kwa mumewe ndo akakutana na vyupi na kanga chumbani kwa mumewe.So alivomuuliza mumewe akakiri kuwa ni kweli sasa hivi anajisevia house girl.Dada alichosema ni kwamba alikuwa disparate and the same day akarudi Dar maana hakutaka tena kulala Morogoro.Mimi nilivoambiwa nikampigia jamaa apange safari aje Dar tuzungumze, kweli nilizungumza nae akakiri kuwa anatembea na housegirl wake ila akasema kuwa bado anampenda mke wake na anaheshimu ndo yake.Nikamuuliza kumpenda yawezekana kweli unampenda mke wako lakini sasa heshima iko wapi.Akasema alipitiwa tu ila atajirekebisha.Sasa juzi kati mama akarudi Moro kwa kustukiza nakuambia alichokutana nacho ni aibu maana mume wake kaleta house girl mpya na yule house girl original ni mother house.Yaani jamani nyie wanawake hamna huruma kabisa yaani kweli mke wa jamaa unamjua vizuri ila wewe unanataka kitibua ndoa yake kweli jamani.Naamini kwa wanaume ni kesi ndogo sana za namna hii eti kuchukua mke wa mtu jumla ilihali mumuwe yupo

Ok

Ss kosa alilolifanya ni baada ya kuona yale@first na kumuuliza mumewe na alipokiri akachukua hatua ya kurudi dar!

Ilitakiwa palepale amfukuze huyo HG

Na nakuhakikishia HG alijua hyo ni mme wa.mtu na.kitendo cha.mke kuondoka akamaliza kabisa yaani ushirikina unahusika asilimia kubwa sn.

Ndo maana nakwambia akienda kwa sshv atachemka vby sn
 
Mke anasema yeye kama yeye kurudi Morogoro kubeba fedheha hawezi kamwe,anasema yeye kurudi kwake Moro ni pale tu atakapohakikishiwa kuwa hakuna tena uhusiano kati ya mumewe na huyo house girl.Infact anataka house girl wote watoweke nyumbani kwa mumewe

Atasubiri sn kuhakikishiwa instead of kuomba Mungu.

Na hyo ndoa ataisikia kwenye bomba
Yaani inshort itabaki story alifungaga ndoa mume akaondoka na Hg
 
Hahahaaaa mume akae na hausi gelo ndani ni utata mtupu jaman mambo ya kujitakia haya

shemeji yangu anafanya kazi mbeya, ana housegirl. Huku dar mke ana housegirl na houseboy. wanawasiliana kwa simu na kutembeleana mara 2 kwa mwezi huku baba akiendelea na juhudi za kurudi dar. kwamba anazini na housegirl huko mbeya au mwanamke mwingine hakuna ajuaye ni siri ya moyo wake. kikubwa ni kuwa yeye na mkewe wanaaminiana. tuache kubebesha wanawake mzigo waume zao wanaposhindwa kujidhibiti na kujiheshimu. unadhani huyu baba asingeenda moro asingeweza kuzini na housegirl chini ya pua ya mkewe? na unafikiri kuweka houseboy utapunguza uwezekano wa mume bazazi kuzini? ni kuomba tu neema ya mungu maana kuna watu wakiwa ndani ni waume, wakiwa nje ni mabasha. utamchunga mume na housegirl utaweza? ukiugua ukalazwa housegirl unaenda nae hospitali au unamrudisha kwao mpaka upone? ukienda kazini unaenda nae? ukiwa usingizini mumeo unamfunga pingu kwenye mkono wako ili usiku asinyate kwenda kwa housegirl?
 
Wandugu, msimamizi wa ndoa anaomba ushauri. Hadi hapo hamjampa ushauri.

unajua sio kisa vibonyezo vipo karibu basi unaandika andika tu bila kufatilia chunguza conversation ilipoanzia ndugu!!!
cheki hapa halafu edit utumbo wako!!!

hebu nijuze kitu kimoja kwanza huyo mke wa kwanza aliolewa na ndugu wa pande zote mbili walikuwepo?
na kama ndiyo hiyo harusi ya housegirl ilitokea na ndugu wa pande zote mbili zikiwepo?
na kama jibu ni ndiyo kwann ndugu waliafiki ndoa bila kujua hatma ya mke wa kwanza?
ukijibu hayo nitajua tatizo lipo wapi....!!!!????


anhaaa!!! sasa ni hivi huwez jua kilitokea nn kwa huyo housegirl mpaka akaamua kuropoka wazi...!!!!
kwani walijenga nyumba na wamefanikiwa mtoto hata mmoja!!!!?


tatizo dogo sana hilo ampigie simu amwambie anampa mwisho weekend hii awe amefika kuzungumzia suala hilo akishindwa basi atamkuta mtoto wake kwa wazazi wake na sehemu waliyojenga anauza na asije akamtafuta kwani atakuwa ni mke wa bwana mwingine tena!!!!
na ahakikishe kama hakuja hampigii simu wala chochote auchune kimya bila kikomo na akipigiwa simu akate na azime........ afanye hivyo!!!!
sisi wanaume tunafika kipindi tunaumiza kichwa, kitakachotokea uje kutuarifu hapa!!!
 
Wandugu, msimamizi wa ndoa anaomba ushauri. Hadi hapo hamjampa ushauri.

Msimamizi mwenyewe ameshaana kummezea mate shemejie hapa anaomba tu baraka za wajumbe wee unaona hatukumshauri? Wee ushauri wako ukoje!
 
Back
Top Bottom