bornagain
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 3,383
- 1,360
Mimi najua kuwa kusimamia harusi ni shughuli siyo ile ya ukumbini bali shughuli yake ni siku mambo ya hao wapendanao yanapoenda kombo maana najua wasimamizi ndiyo wanakuwa watu wa mwanzo kuelezewa kinachojiri.
Sasa kuna ndoa nimesimamia miaka miwili iliyopita yaani bwana bibi harusi na bwana harusi walipendana zaidi ya wale ndugu wa kwenye movie ya Romeo na Julieth yaani kila dakika baby umekula, baby unafanya nini sasa hivi yaani ni shida kama hujawahipita huko basi utadhani wapo peponi.
Kisa chenyewe kilianza mwezi wa kwanza mwaka huu, mwanaume alipata kazi mpya Morogoro na bi dada yeye anapiga mzigo hapa Dar.
Walikuja home kutuomba ushauri kwamba wafanyeje, mimi nikafunguka kisawasawa nikawaambia kuwa Morogoro wanaweza wakapaona ni karibu sana na Dar ila issue ya distance relationship siiungi mkono hata kidogo.
Nikashauri jamaa akomae hapahapa mjini atapata kazi nyingine tu nzuri maana familia bado changa. Ebwana kwa kuwa bado wapo mahabani bi dada akasema yeye hana shida Moro si mbali sana yupo radhi jamaa aende Moro akapige mzigo ila kwa sharti kwamba kila Ijumaa jioni mpaka Jtatu asubuhi ama Jumapili jioni ahakikishe anarudi nyumbani.
Kweli jamaa akahamia Moro na kufika Moro akatafuta house girl wa Kipogolo.To cut the story short ni kwamba jamaa sasa si weekend wala nini haji nyumbani tena ni kwamba ameoa house girl wake huyo na sasa ana house girl mwingine kumsaidia yule wa house girl wa mwanzo maana amekuwa mother house.
Sasa bwana bibi harusi amerudi nyumbani kuniomba ninusuru ndoa yake, nimewasiliana na jamaa Moro akakubali kuwa kweli amemuweka ndani house girl wake na akaniambia kuwa hana shida na mama watoto Dar maana na yeye ni mke wake na hakuna kitakachopungua.
In short watu wazima wenye ushauri wa kunisaidia kunusuru ndoa hii naombeni msaada wenu maana akili yangu imegota.
This is serious kabisa wala sitanii naombeni mwenye ushauri wa nini kifanyike anisaidie